Genesis 49 (BOKCV)

1 Ndipo Yakobo akawaita wanawe na kusema: “Kusanyikeni kunizunguka ili niweze kuwaambia lile litakalowatokea siku zijazo. 2 “Kusanyikeni na msikilize, enyi wana wa Yakobo,msikilizeni baba yenu Israeli. 3 “Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza,nguvu zangu, tunda la kwanza la nguvu zangu,umepita kwa heshima, umepita kwa uwezo. 4 Usiyezuiwa kama maji, basi hutakuwa mkuu tena,kwa kuwa ulipanda kwenye kitanda cha baba yako,kwenye kitanda changu na kukinajisi. 5 “Simeoni na Lawi ni wana ndugu:panga zao ni silaha za jeuri. 6 Mimi na nisiingie katika baraza lao,nami nisiunganike katika kusanyiko lao,kwa kuwa wamewaua watu katika hasira yao,walikata mishipa ya miguu ya mafahalikama walivyopenda. 7 Hasira yao na ilaaniwe, kwa kuwa ni kali mno,nayo ghadhabu yao ni ya ukatili!Nitawatawanya katika YakoboNa kuwasambaza katika Israeli. 8 “Yuda, ndugu zako watakusifu;mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako;wana wa baba yako watakusujudia. 9 Ee Yuda, wewe ni mwana simba;unarudi toka mawindoni, mwanangu.Kama simba hunyemelea na kulala chini,kama simba jike: nani athubutuye kumwamsha? 10 Fimbo ya ufalme haitaondoka kwa Yuda,wala fimbo ya mtawala kati ya miguu yake,hadi aje yeye ambaye milki ni yake,ambaye utii wa mataifa ni wake. 11 Atamfunga punda wake katika mzabibu,naye mwana-punda wake kwenye tawi lililo bora zaidi;atafua mavazi yake katika divai,majoho yake katika damu ya mizabibu. 12 Macho yake yatakuwa mekundu kwa divai,meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa. 13 “Zabuloni ataishi pwani ya baharina kuwa bandari za kuegesha meli;mpaka wake utapanuka kuelekea Sidoni. 14 “Isakari ni punda mwenye nguvuambaye amelala kati ya mizigo yake. 15 Aonapo palivyo pazuri mahali pake pa kupumzikana jinsi nchi yake inavyopendeza,atainamisha bega lake kwenye mzigona kujitolea kwa ajili ya kazi ngumu. 16 “Dani atahukumu watu wake kwa hakikama mmoja wa makabila ya Israeli. 17 Dani atakuwa nyoka kando ya barabara,nyoka mwenye sumu kando ya njia,yule aumaye visigino vya farasiili yule ampandaye aanguke chali. 18 “Ee BWANA, nautafuta wokovu wako. 19 “Gadi atashambuliwa ghafula na kundi la washambuliaji,lakini yeye atawageukia na kuwashinda kabisa. 20 “Chakula cha Asheri kitakuwa kinono,naye atatoa chakula kitamu kimfaacho mfalme. 21 “Naftali ni kulungu jike aliyeachiwa huruazaaye watoto wazuri. 22 “Yosefu ni mzabibu uzaao,mzabibu uzaao ulio kando ya chemchemi,ambao matawi yake hutanda ukutani. 23 Kwa uchungu wapiga mshale walimshambulia,wakampiga mshale kwa ukatili. 24 Lakini upinde wake ulibaki imara,mikono yake ikatiwa nguvu,na mkono wa Mwenye Nguvu wa Yakobo,kwa sababu ya Mchungaji, Mwamba wa Israeli, 25 kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia,kwa sababu ya Mwenyezi, yeye anayekubarikikwa baraka za mbinguni juu,baraka za kilindi kilichoko chini,baraka za matitini na za tumbo la uzazi. 26 Baraka za baba yako ni kubwakuliko baraka za milima ya kale,nyingi kuliko vilima vya kale.Baraka hizo zote na zikae juu ya kichwa cha Yosefu,juu ya paji la yule mkuu miongoni mwa ndugu zake. 27 “Benyamini ni mbwa mwitu mlafi mwenye njaa kuu;asubuhi hurarua mawindo yake,jioni hugawa nyara.” 28 Haya yote ndiyo makabila kumi na mawili ya Israeli, na hivi ndivyo baba yao alivyowaambia alipowabariki, akimpa kila mmoja baraka inayomfaa. 29 Ndipo alipowapa maelekezo haya: “Mimi niko karibu kukusanywa kwa watu wangu. Mnizike pamoja na baba zangu kwenye pango katika shamba la Efroni, Mhiti, 30 pango lililoko katika shamba la Makpela, karibu na Mamre huko Kanaani, ambalo Abrahamu alinunua kwa ajili ya mahali pa kuzikia kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba. 31 Huko ndiko Abrahamu na Sara mkewe walikozikwa, huko akazikwa Isaki na Rebeka mkewe, na huko nilimzika Lea. 32 Shamba hilo na pango lililoko ndani yake lilinunuliwa kutoka kwa Wahiti.” 33 Baada ya Yakobo kumaliza kutoa maelekezo hayo kwa wanawe, akarudisha miguu yake kitandani, akapumua pumzi ya mwisho, na akakusanywa kwa watu wake.

In Other Versions

Genesis 49 in the ANGEFD

Genesis 49 in the ANTPNG2D

Genesis 49 in the AS21

Genesis 49 in the BAGH

Genesis 49 in the BBPNG

Genesis 49 in the BBT1E

Genesis 49 in the BDS

Genesis 49 in the BEV

Genesis 49 in the BHAD

Genesis 49 in the BIB

Genesis 49 in the BLPT

Genesis 49 in the BNT

Genesis 49 in the BNTABOOT

Genesis 49 in the BNTLV

Genesis 49 in the BOATCB

Genesis 49 in the BOATCB2

Genesis 49 in the BOBCV

Genesis 49 in the BOCNT

Genesis 49 in the BOECS

Genesis 49 in the BOGWICC

Genesis 49 in the BOHCB

Genesis 49 in the BOHCV

Genesis 49 in the BOHLNT

Genesis 49 in the BOHNTLTAL

Genesis 49 in the BOICB

Genesis 49 in the BOILNTAP

Genesis 49 in the BOITCV

Genesis 49 in the BOKCV2

Genesis 49 in the BOKHWOG

Genesis 49 in the BOKSSV

Genesis 49 in the BOLCB

Genesis 49 in the BOLCB2

Genesis 49 in the BOMCV

Genesis 49 in the BONAV

Genesis 49 in the BONCB

Genesis 49 in the BONLT

Genesis 49 in the BONUT2

Genesis 49 in the BOPLNT

Genesis 49 in the BOSCB

Genesis 49 in the BOSNC

Genesis 49 in the BOTLNT

Genesis 49 in the BOVCB

Genesis 49 in the BOYCB

Genesis 49 in the BPBB

Genesis 49 in the BPH

Genesis 49 in the BSB

Genesis 49 in the CCB

Genesis 49 in the CUV

Genesis 49 in the CUVS

Genesis 49 in the DBT

Genesis 49 in the DGDNT

Genesis 49 in the DHNT

Genesis 49 in the DNT

Genesis 49 in the ELBE

Genesis 49 in the EMTV

Genesis 49 in the ESV

Genesis 49 in the FBV

Genesis 49 in the FEB

Genesis 49 in the GGMNT

Genesis 49 in the GNT

Genesis 49 in the HARY

Genesis 49 in the HNT

Genesis 49 in the IRVA

Genesis 49 in the IRVB

Genesis 49 in the IRVG

Genesis 49 in the IRVH

Genesis 49 in the IRVK

Genesis 49 in the IRVM

Genesis 49 in the IRVM2

Genesis 49 in the IRVO

Genesis 49 in the IRVP

Genesis 49 in the IRVT

Genesis 49 in the IRVT2

Genesis 49 in the IRVU

Genesis 49 in the ISVN

Genesis 49 in the JSNT

Genesis 49 in the KAPI

Genesis 49 in the KBT1ETNIK

Genesis 49 in the KBV

Genesis 49 in the KJV

Genesis 49 in the KNFD

Genesis 49 in the LBA

Genesis 49 in the LBLA

Genesis 49 in the LNT

Genesis 49 in the LSV

Genesis 49 in the MAAL

Genesis 49 in the MBV

Genesis 49 in the MBV2

Genesis 49 in the MHNT

Genesis 49 in the MKNFD

Genesis 49 in the MNG

Genesis 49 in the MNT

Genesis 49 in the MNT2

Genesis 49 in the MRS1T

Genesis 49 in the NAA

Genesis 49 in the NASB

Genesis 49 in the NBLA

Genesis 49 in the NBS

Genesis 49 in the NBVTP

Genesis 49 in the NET2

Genesis 49 in the NIV11

Genesis 49 in the NNT

Genesis 49 in the NNT2

Genesis 49 in the NNT3

Genesis 49 in the PDDPT

Genesis 49 in the PFNT

Genesis 49 in the RMNT

Genesis 49 in the SBIAS

Genesis 49 in the SBIBS

Genesis 49 in the SBIBS2

Genesis 49 in the SBICS

Genesis 49 in the SBIDS

Genesis 49 in the SBIGS

Genesis 49 in the SBIHS

Genesis 49 in the SBIIS

Genesis 49 in the SBIIS2

Genesis 49 in the SBIIS3

Genesis 49 in the SBIKS

Genesis 49 in the SBIKS2

Genesis 49 in the SBIMS

Genesis 49 in the SBIOS

Genesis 49 in the SBIPS

Genesis 49 in the SBISS

Genesis 49 in the SBITS

Genesis 49 in the SBITS2

Genesis 49 in the SBITS3

Genesis 49 in the SBITS4

Genesis 49 in the SBIUS

Genesis 49 in the SBIVS

Genesis 49 in the SBT

Genesis 49 in the SBT1E

Genesis 49 in the SCHL

Genesis 49 in the SNT

Genesis 49 in the SUSU

Genesis 49 in the SUSU2

Genesis 49 in the SYNO

Genesis 49 in the TBIAOTANT

Genesis 49 in the TBT1E

Genesis 49 in the TBT1E2

Genesis 49 in the TFTIP

Genesis 49 in the TFTU

Genesis 49 in the TGNTATF3T

Genesis 49 in the THAI

Genesis 49 in the TNFD

Genesis 49 in the TNT

Genesis 49 in the TNTIK

Genesis 49 in the TNTIL

Genesis 49 in the TNTIN

Genesis 49 in the TNTIP

Genesis 49 in the TNTIZ

Genesis 49 in the TOMA

Genesis 49 in the TTENT

Genesis 49 in the UBG

Genesis 49 in the UGV

Genesis 49 in the UGV2

Genesis 49 in the UGV3

Genesis 49 in the VBL

Genesis 49 in the VDCC

Genesis 49 in the YALU

Genesis 49 in the YAPE

Genesis 49 in the YBVTP

Genesis 49 in the ZBP