Isaiah 41 (BOKCV)

1 “Nyamazeni kimya mbele zangu, enyi visiwa!Mataifa na wafanye upya nguvu zao!Wao na wajitokeze, kisha waseme,tukutane pamoja mahali pa hukumu. 2 “Ni nani aliyemchochea mmoja kutoka mashariki,akimwita katika haki kwa utumishi wake?Huyatia mataifa mikononi mwake,na kuwatiisha wafalme mbele zake.Huwafanya kuwa mavumbi kwa upanga wake,huwafanya makapi yapeperushwayo na upepo kwa upinde wake. 3 Huwafuatia na kuendelea salama,katika njia ambayo miguu yake haijawahi kupita. 4 Ni nani aliyefanya jambo hili na kulitimiliza,akiita vizazi tangu mwanzo?Mimi, BWANA, ni wa kwanzanami nitakuwa pamoja na wa mwisho:mimi BWANA ndiye.” 5 Visiwa vimeliona na kuogopa,miisho ya dunia inatetemeka.Wanakaribia na kuja mbele, 6 kila mmoja humsaidia mwinginena kusema kwa ndugu yake, “Uwe hodari!” 7 Fundi humtia moyo sonara,yeye alainishaye kwa nyundohumhimiza yeye agongeaye kwenye fuawe,Humwambia yeye aunganishaye, “Ni kazi njema.”Naye huikaza sanamu kwa misumari ili isitikisike. 8 “Lakini wewe, ee Israeli, mtumishi wangu,Yakobo, niliyemchagua,ninyi wazao wa Abrahamu rafiki yangu, 9 nilikuchukua toka miisho ya dunia,nilikuita kutoka pembe zake za mbali.Nilisema, ‘Wewe ni mtumishi wangu’;nimekuchagua, wala sikukukataa. 10 Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe;usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako.Nitakutia nguvu na kukusaidia;nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu. 11 “Wote walioona hasira dhidi yakohakika wataaibika na kutahayarika,wale wakupingaowatakuwa kama vile si kitu, na kuangamia. 12 Ingawa utawatafuta adui zako,hutawaona.Wale wanaopigana vita dhidi yakowatakuwa kama vile si kitu kabisa. 13 Kwa maana Mimi ndimi BWANA, Mungu wako,nikushikaye mkono wako wa kuumena kukuambia, Usiwe na hofu,nitakusaidia. 14 Usiogope, ee Yakobo uliye mdudu,ee Israeli uliye mdogo,kwa kuwa Mimi mwenyewe nitakusaidia,” asema BWANA,Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. 15 “Tazama, nitakufanya chombo cha kupuria,kipya na chenye makali, chenye meno mengi.Utaipura milima na kuipondana kuvifanya vilima kuwa kama makapi. 16 Utaipepeta, nao upepo utaichukua,dhoruba itaipeperushia mbali.Bali wewe utajifurahisha katika BWANAna katika utukufu wa yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. 17 “Maskini na wahitaji wanatafuta maji,lakini hayapo,ndimi zao zimekauka kwa kiu.Lakini Mimi BWANA nitawajibu,Mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha. 18 Nitaifanya mito itiririke juu ya vilima vilivyo kame,nazo chemchemi ndani ya mabonde.Nitaligeuza jangwa liwe mabwawa ya maji,nayo ardhi iliyokauka kuwa chemchemi za maji. 19 Katika jangwa nitaoteshamwerezi, mshita, mhadasi na mzeituni.Nitaweka misunobari, mivinje na misandukupamoja huko nyikani, 20 ili kwamba watu wapate kuona na kujua,wapate kufikiri na kuelewa,kwamba mkono wa BWANA umetenda hili,kwamba yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli ndiye alilifanya.” 21 BWANA asema, “Leta shauri lako.Toa hoja yako,” asema Mfalme wa Yakobo. 22 “Leteni sanamu zenu zituambieni nini kitakachotokea.Tuambieni mambo ya zamani yalikuwa nini,ili tupate kuyatafakarina kujua matokeo yake ya mwisho.Au tutangazieni mambo yatakayokuja, 23 tuambieni ni nini kitakachotokea baadaye,ili tupate kujua kuwa ninyi ni miungu.Fanyeni jambo lolote zuri au baya,ili tupate kutishika na kujazwa na hofu. 24 Lakini ninyi ni zaidi ya bure kabisa,na kazi zenu hazifai kitu kabisa;yeye awachaguaye ni chukizo sana. 25 “Nimemchochea mtu mmoja kutoka kaskazini,naye yuaja, mmoja toka mawio ya jua aliitaye Jina langu.Huwakanyaga watawala kana kwamba ni matope,kama mfinyanzi akanyagavyo udongo wa kufinyangia. 26 Ni nani aliyenena hili tokea mwanzoni, ili tupate kujua,au kabla, ili tuweze kusema, ‘Alikuwa sawa’?Hakuna aliyenena hili,hakuna aliyetangulia kusema hili,hakuna yeyote aliyesikia maneno kutoka kwenu. 27 Nilikuwa wa kwanza kumwambia Sayuni,‘Tazama, wako hapa!’Nilimpa Yerusalemu mjumbe wa habari njema. 28 Ninatazama, lakini hakuna yeyote:hakuna yeyote miongoni mwao awezaye kutoa shauri,hakuna yeyote wa kutoa jibu wakati ninapowauliza. 29 Tazama, wote ni ubatili!Matendo yao ni bure;vinyago vyao ni upepo mtupu na machafuko.

In Other Versions

Isaiah 41 in the ANGEFD

Isaiah 41 in the ANTPNG2D

Isaiah 41 in the AS21

Isaiah 41 in the BAGH

Isaiah 41 in the BBPNG

Isaiah 41 in the BBT1E

Isaiah 41 in the BDS

Isaiah 41 in the BEV

Isaiah 41 in the BHAD

Isaiah 41 in the BIB

Isaiah 41 in the BLPT

Isaiah 41 in the BNT

Isaiah 41 in the BNTABOOT

Isaiah 41 in the BNTLV

Isaiah 41 in the BOATCB

Isaiah 41 in the BOATCB2

Isaiah 41 in the BOBCV

Isaiah 41 in the BOCNT

Isaiah 41 in the BOECS

Isaiah 41 in the BOGWICC

Isaiah 41 in the BOHCB

Isaiah 41 in the BOHCV

Isaiah 41 in the BOHLNT

Isaiah 41 in the BOHNTLTAL

Isaiah 41 in the BOICB

Isaiah 41 in the BOILNTAP

Isaiah 41 in the BOITCV

Isaiah 41 in the BOKCV2

Isaiah 41 in the BOKHWOG

Isaiah 41 in the BOKSSV

Isaiah 41 in the BOLCB

Isaiah 41 in the BOLCB2

Isaiah 41 in the BOMCV

Isaiah 41 in the BONAV

Isaiah 41 in the BONCB

Isaiah 41 in the BONLT

Isaiah 41 in the BONUT2

Isaiah 41 in the BOPLNT

Isaiah 41 in the BOSCB

Isaiah 41 in the BOSNC

Isaiah 41 in the BOTLNT

Isaiah 41 in the BOVCB

Isaiah 41 in the BOYCB

Isaiah 41 in the BPBB

Isaiah 41 in the BPH

Isaiah 41 in the BSB

Isaiah 41 in the CCB

Isaiah 41 in the CUV

Isaiah 41 in the CUVS

Isaiah 41 in the DBT

Isaiah 41 in the DGDNT

Isaiah 41 in the DHNT

Isaiah 41 in the DNT

Isaiah 41 in the ELBE

Isaiah 41 in the EMTV

Isaiah 41 in the ESV

Isaiah 41 in the FBV

Isaiah 41 in the FEB

Isaiah 41 in the GGMNT

Isaiah 41 in the GNT

Isaiah 41 in the HARY

Isaiah 41 in the HNT

Isaiah 41 in the IRVA

Isaiah 41 in the IRVB

Isaiah 41 in the IRVG

Isaiah 41 in the IRVH

Isaiah 41 in the IRVK

Isaiah 41 in the IRVM

Isaiah 41 in the IRVM2

Isaiah 41 in the IRVO

Isaiah 41 in the IRVP

Isaiah 41 in the IRVT

Isaiah 41 in the IRVT2

Isaiah 41 in the IRVU

Isaiah 41 in the ISVN

Isaiah 41 in the JSNT

Isaiah 41 in the KAPI

Isaiah 41 in the KBT1ETNIK

Isaiah 41 in the KBV

Isaiah 41 in the KJV

Isaiah 41 in the KNFD

Isaiah 41 in the LBA

Isaiah 41 in the LBLA

Isaiah 41 in the LNT

Isaiah 41 in the LSV

Isaiah 41 in the MAAL

Isaiah 41 in the MBV

Isaiah 41 in the MBV2

Isaiah 41 in the MHNT

Isaiah 41 in the MKNFD

Isaiah 41 in the MNG

Isaiah 41 in the MNT

Isaiah 41 in the MNT2

Isaiah 41 in the MRS1T

Isaiah 41 in the NAA

Isaiah 41 in the NASB

Isaiah 41 in the NBLA

Isaiah 41 in the NBS

Isaiah 41 in the NBVTP

Isaiah 41 in the NET2

Isaiah 41 in the NIV11

Isaiah 41 in the NNT

Isaiah 41 in the NNT2

Isaiah 41 in the NNT3

Isaiah 41 in the PDDPT

Isaiah 41 in the PFNT

Isaiah 41 in the RMNT

Isaiah 41 in the SBIAS

Isaiah 41 in the SBIBS

Isaiah 41 in the SBIBS2

Isaiah 41 in the SBICS

Isaiah 41 in the SBIDS

Isaiah 41 in the SBIGS

Isaiah 41 in the SBIHS

Isaiah 41 in the SBIIS

Isaiah 41 in the SBIIS2

Isaiah 41 in the SBIIS3

Isaiah 41 in the SBIKS

Isaiah 41 in the SBIKS2

Isaiah 41 in the SBIMS

Isaiah 41 in the SBIOS

Isaiah 41 in the SBIPS

Isaiah 41 in the SBISS

Isaiah 41 in the SBITS

Isaiah 41 in the SBITS2

Isaiah 41 in the SBITS3

Isaiah 41 in the SBITS4

Isaiah 41 in the SBIUS

Isaiah 41 in the SBIVS

Isaiah 41 in the SBT

Isaiah 41 in the SBT1E

Isaiah 41 in the SCHL

Isaiah 41 in the SNT

Isaiah 41 in the SUSU

Isaiah 41 in the SUSU2

Isaiah 41 in the SYNO

Isaiah 41 in the TBIAOTANT

Isaiah 41 in the TBT1E

Isaiah 41 in the TBT1E2

Isaiah 41 in the TFTIP

Isaiah 41 in the TFTU

Isaiah 41 in the TGNTATF3T

Isaiah 41 in the THAI

Isaiah 41 in the TNFD

Isaiah 41 in the TNT

Isaiah 41 in the TNTIK

Isaiah 41 in the TNTIL

Isaiah 41 in the TNTIN

Isaiah 41 in the TNTIP

Isaiah 41 in the TNTIZ

Isaiah 41 in the TOMA

Isaiah 41 in the TTENT

Isaiah 41 in the UBG

Isaiah 41 in the UGV

Isaiah 41 in the UGV2

Isaiah 41 in the UGV3

Isaiah 41 in the VBL

Isaiah 41 in the VDCC

Isaiah 41 in the YALU

Isaiah 41 in the YAPE

Isaiah 41 in the YBVTP

Isaiah 41 in the ZBP