James 4 (BOKCV)

1 Ni kitu gani kinachosababisha mapigano na ugomvi miongoni mwenu? Je, haya hayatokani na tamaa zenu zinazoshindana ndani yenu? 2 Mnatamani lakini hampati, kwa hiyo mwaua. Mwatamani kupata lakini hampati vile mnavyotaka, kwa hiyo mnajitia katika magomvi na mapigano. Mmepungukiwa kwa sababu hammwombi Mungu. 3 Mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya, ili mpate kuvitumia hivyo mtakavyopata kwa tamaa zenu. 4 Ninyi wanaume na wanawake wazinzi, hamjui ya kwamba urafiki na dunia ni uadui na Mungu? Kwa hiyo mtu yeyote anayetaka kuwa rafiki wa dunia hufanyika adui wa Mungu. 5 Au mwadhani kwamba Andiko lasema bure kuwa huyo Roho ambaye Mungu amemweka ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu? 6 Lakini yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Andiko husema:“Mungu huwapinga wenye kiburi,lakini huwapa wanyenyekevu neema.” 7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia. 8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu ninyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu ninyi wenye nia mbili. 9 Huzunikeni, ombolezeni na kulia. Kicheko chenu na kigeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni. 10 Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainua. 11 Ndugu, msineneane mabaya ninyi kwa ninyi. Mtu yeyote anayesema mabaya dhidi ya ndugu yake au kumhukumu anasema dhidi ya sheria na kuihukumu. Unapoihukumu sheria, basi huishiki sheria bali umekuwa hakimu wa kuihukumu hiyo sheria. 12 Yuko Mtoa sheria mmoja tu na yeye peke yake ndiye Hakimu, ndiye awezaye kuokoa au kuangamiza. Lakini wewe ni nani hata umhukumu jirani yako? 13 Basi sikilizeni ninyi msemao, “Leo au kesho tutakwenda katika mji huu ama ule tukae humo mwaka mmoja, tufanye biashara na kupata faida.” 14 Lakini hamjui hata litakalotukia kesho. Maisha yenu ni nini? Ninyi ni ukungu ambao huonekana kwa kitambo kidogo kisha hutoweka. 15 Badala yake, inawapasa kusema, “Kama Bwana akipenda, tutaishi na kufanya hili ama lile.” 16 Kama ilivyo sasa, mnajisifu na kujigamba. Kujisifu kwa namna hiyo ni uovu. 17 Basi mtu yeyote anayejua jema limpasalo kutenda, lakini asilitende, mtu huyo anatenda dhambi.

In Other Versions

James 4 in the ANGEFD

James 4 in the ANTPNG2D

James 4 in the AS21

James 4 in the BAGH

James 4 in the BBPNG

James 4 in the BBT1E

James 4 in the BDS

James 4 in the BEV

James 4 in the BHAD

James 4 in the BIB

James 4 in the BLPT

James 4 in the BNT

James 4 in the BNTABOOT

James 4 in the BNTLV

James 4 in the BOATCB

James 4 in the BOATCB2

James 4 in the BOBCV

James 4 in the BOCNT

James 4 in the BOECS

James 4 in the BOGWICC

James 4 in the BOHCB

James 4 in the BOHCV

James 4 in the BOHLNT

James 4 in the BOHNTLTAL

James 4 in the BOICB

James 4 in the BOILNTAP

James 4 in the BOITCV

James 4 in the BOKCV2

James 4 in the BOKHWOG

James 4 in the BOKSSV

James 4 in the BOLCB

James 4 in the BOLCB2

James 4 in the BOMCV

James 4 in the BONAV

James 4 in the BONCB

James 4 in the BONLT

James 4 in the BONUT2

James 4 in the BOPLNT

James 4 in the BOSCB

James 4 in the BOSNC

James 4 in the BOTLNT

James 4 in the BOVCB

James 4 in the BOYCB

James 4 in the BPBB

James 4 in the BPH

James 4 in the BSB

James 4 in the CCB

James 4 in the CUV

James 4 in the CUVS

James 4 in the DBT

James 4 in the DGDNT

James 4 in the DHNT

James 4 in the DNT

James 4 in the ELBE

James 4 in the EMTV

James 4 in the ESV

James 4 in the FBV

James 4 in the FEB

James 4 in the GGMNT

James 4 in the GNT

James 4 in the HARY

James 4 in the HNT

James 4 in the IRVA

James 4 in the IRVB

James 4 in the IRVG

James 4 in the IRVH

James 4 in the IRVK

James 4 in the IRVM

James 4 in the IRVM2

James 4 in the IRVO

James 4 in the IRVP

James 4 in the IRVT

James 4 in the IRVT2

James 4 in the IRVU

James 4 in the ISVN

James 4 in the JSNT

James 4 in the KAPI

James 4 in the KBT1ETNIK

James 4 in the KBV

James 4 in the KJV

James 4 in the KNFD

James 4 in the LBA

James 4 in the LBLA

James 4 in the LNT

James 4 in the LSV

James 4 in the MAAL

James 4 in the MBV

James 4 in the MBV2

James 4 in the MHNT

James 4 in the MKNFD

James 4 in the MNG

James 4 in the MNT

James 4 in the MNT2

James 4 in the MRS1T

James 4 in the NAA

James 4 in the NASB

James 4 in the NBLA

James 4 in the NBS

James 4 in the NBVTP

James 4 in the NET2

James 4 in the NIV11

James 4 in the NNT

James 4 in the NNT2

James 4 in the NNT3

James 4 in the PDDPT

James 4 in the PFNT

James 4 in the RMNT

James 4 in the SBIAS

James 4 in the SBIBS

James 4 in the SBIBS2

James 4 in the SBICS

James 4 in the SBIDS

James 4 in the SBIGS

James 4 in the SBIHS

James 4 in the SBIIS

James 4 in the SBIIS2

James 4 in the SBIIS3

James 4 in the SBIKS

James 4 in the SBIKS2

James 4 in the SBIMS

James 4 in the SBIOS

James 4 in the SBIPS

James 4 in the SBISS

James 4 in the SBITS

James 4 in the SBITS2

James 4 in the SBITS3

James 4 in the SBITS4

James 4 in the SBIUS

James 4 in the SBIVS

James 4 in the SBT

James 4 in the SBT1E

James 4 in the SCHL

James 4 in the SNT

James 4 in the SUSU

James 4 in the SUSU2

James 4 in the SYNO

James 4 in the TBIAOTANT

James 4 in the TBT1E

James 4 in the TBT1E2

James 4 in the TFTIP

James 4 in the TFTU

James 4 in the TGNTATF3T

James 4 in the THAI

James 4 in the TNFD

James 4 in the TNT

James 4 in the TNTIK

James 4 in the TNTIL

James 4 in the TNTIN

James 4 in the TNTIP

James 4 in the TNTIZ

James 4 in the TOMA

James 4 in the TTENT

James 4 in the UBG

James 4 in the UGV

James 4 in the UGV2

James 4 in the UGV3

James 4 in the VBL

James 4 in the VDCC

James 4 in the YALU

James 4 in the YAPE

James 4 in the YBVTP

James 4 in the ZBP