James 5 (BOKCV)
1 Basi sikilizeni, ninyi matajiri, lieni na kuomboleza kwa ajili ya hali mbaya sana inayowajia. 2 Utajiri wenu umeoza na mavazi yenu yameliwa na nondo. 3 Dhahabu yenu na fedha yenu vimeliwa na kutu. Kutu yake itashuhudia dhidi yenu nayo itaila miili yenu kama vile moto. Mmejiwekea hazina kwa ajili ya siku za mwisho. 4 Angalieni! Ule ujira wa vibarua waliolima mashamba yenu mliouzuia kwa hila unapiga kelele dhidi yenu na vilio vya wavunaji vimefika masikioni mwa Bwana Mwenye Nguvu Zote. 5 Mmeishi duniani kwa anasa na kwa starehe, mmejinenepesha tayari kwa siku ya kuchinjwa. 6 Mmewahukumu na kuwaua watu wenye haki, waliokuwa hawapingani nanyi. 7 Kwa hiyo, ndugu zangu, vumilieni hadi kuja kwake Bwana. Angalieni jinsi mkulima angojavyo ardhi itoe mavuno yake yaliyo ya thamani na jinsi anavyovumilia kwa ajili ya kupata mvua za kwanza na za mwisho. 8 Ninyi nanyi vumilieni, tena simameni imara, kwa sababu kuja kwa Bwana kumekaribia. 9 Ndugu zangu, msinungʼunikiane msije mkahukumiwa. Hakimu amesimama mlangoni! 10 Ndugu zangu, waangalieni manabii walionena kwa Jina la Bwana, ili kuwa mfano wa uvumilivu katika kukabiliana na mateso. 11 Kama mnavyojua, tunawahesabu kuwa wabarikiwa wale waliovumilia. Mmesikia habari za uvumilivu wake Ayubu na mmeona kile ambacho hatimaye Bwana alimtendea. Bwana ni mwingi wa huruma, na amejaa rehema. 12 Zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, iwe kwa mbingu au kwa dunia, au kwa kitu kingine chochote. “Ndiyo” yenu na iwe ndiyo, na “Hapana” yenu iwe hapana, la sivyo mtahukumiwa. 13 Je, mtu yeyote miongoni mwenu amepatwa na taabu? Basi inampasa aombe. Je, kuna yeyote mwenye furaha? Basi na aimbe nyimbo za kusifu. 14 Je, kuna yeyote miongoni mwenu aliye mgonjwa? Basi inampasa awaite wazee wa kanisa wamwombee na kumpaka mafuta kwa Jina la Bwana. 15 Kule kuomba kwa imani kutamwokoa huyo mgonjwa, naye Bwana atamwinua na kama ametenda dhambi, atasamehewa. 16 Kwa hiyo ungamianeni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana ili mpate kuponywa. Maombi ya mwenye haki yana nguvu tena yanafaa sana. 17 Eliya alikuwa mwanadamu kama sisi. Akaomba kwa bidii kwamba mvua isinyeshe, nayo haikunyesha juu ya nchi kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita. 18 Kisha akaomba tena, nazo mbingu zikatoa mvua nayo ardhi ikatoa mazao yake. 19 Ndugu zangu, yeyote miongoni mwenu akipotoka na kuicha kweli, naye akarejezwa na mtu mwingine, 20 hamna budi kujua kwamba yeyote amrejezaye mwenye dhambi kutoka upotovu wake, ataiokoa roho ya huyo mwenye dhambi kutoka mauti na kusitiri wingi wa dhambi.
In Other Versions
James 5 in the ANGEFD
James 5 in the ANTPNG2D
James 5 in the AS21
James 5 in the BAGH
James 5 in the BBPNG
James 5 in the BBT1E
James 5 in the BDS
James 5 in the BEV
James 5 in the BHAD
James 5 in the BIB
James 5 in the BLPT
James 5 in the BNT
James 5 in the BNTABOOT
James 5 in the BNTLV
James 5 in the BOATCB
James 5 in the BOATCB2
James 5 in the BOBCV
James 5 in the BOCNT
James 5 in the BOECS
James 5 in the BOGWICC
James 5 in the BOHCB
James 5 in the BOHCV
James 5 in the BOHLNT
James 5 in the BOHNTLTAL
James 5 in the BOICB
James 5 in the BOILNTAP
James 5 in the BOITCV
James 5 in the BOKCV2
James 5 in the BOKHWOG
James 5 in the BOKSSV
James 5 in the BOLCB
James 5 in the BOLCB2
James 5 in the BOMCV
James 5 in the BONAV
James 5 in the BONCB
James 5 in the BONLT
James 5 in the BONUT2
James 5 in the BOPLNT
James 5 in the BOSCB
James 5 in the BOSNC
James 5 in the BOTLNT
James 5 in the BOVCB
James 5 in the BOYCB
James 5 in the BPBB
James 5 in the BPH
James 5 in the BSB
James 5 in the CCB
James 5 in the CUV
James 5 in the CUVS
James 5 in the DBT
James 5 in the DGDNT
James 5 in the DHNT
James 5 in the DNT
James 5 in the ELBE
James 5 in the EMTV
James 5 in the ESV
James 5 in the FBV
James 5 in the FEB
James 5 in the GGMNT
James 5 in the GNT
James 5 in the HARY
James 5 in the HNT
James 5 in the IRVA
James 5 in the IRVB
James 5 in the IRVG
James 5 in the IRVH
James 5 in the IRVK
James 5 in the IRVM
James 5 in the IRVM2
James 5 in the IRVO
James 5 in the IRVP
James 5 in the IRVT
James 5 in the IRVT2
James 5 in the IRVU
James 5 in the ISVN
James 5 in the JSNT
James 5 in the KAPI
James 5 in the KBT1ETNIK
James 5 in the KBV
James 5 in the KJV
James 5 in the KNFD
James 5 in the LBA
James 5 in the LBLA
James 5 in the LNT
James 5 in the LSV
James 5 in the MAAL
James 5 in the MBV
James 5 in the MBV2
James 5 in the MHNT
James 5 in the MKNFD
James 5 in the MNG
James 5 in the MNT
James 5 in the MNT2
James 5 in the MRS1T
James 5 in the NAA
James 5 in the NASB
James 5 in the NBLA
James 5 in the NBS
James 5 in the NBVTP
James 5 in the NET2
James 5 in the NIV11
James 5 in the NNT
James 5 in the NNT2
James 5 in the NNT3
James 5 in the PDDPT
James 5 in the PFNT
James 5 in the RMNT
James 5 in the SBIAS
James 5 in the SBIBS
James 5 in the SBIBS2
James 5 in the SBICS
James 5 in the SBIDS
James 5 in the SBIGS
James 5 in the SBIHS
James 5 in the SBIIS
James 5 in the SBIIS2
James 5 in the SBIIS3
James 5 in the SBIKS
James 5 in the SBIKS2
James 5 in the SBIMS
James 5 in the SBIOS
James 5 in the SBIPS
James 5 in the SBISS
James 5 in the SBITS
James 5 in the SBITS2
James 5 in the SBITS3
James 5 in the SBITS4
James 5 in the SBIUS
James 5 in the SBIVS
James 5 in the SBT
James 5 in the SBT1E
James 5 in the SCHL
James 5 in the SNT
James 5 in the SUSU
James 5 in the SUSU2
James 5 in the SYNO
James 5 in the TBIAOTANT
James 5 in the TBT1E
James 5 in the TBT1E2
James 5 in the TFTIP
James 5 in the TFTU
James 5 in the TGNTATF3T
James 5 in the THAI
James 5 in the TNFD
James 5 in the TNT
James 5 in the TNTIK
James 5 in the TNTIL
James 5 in the TNTIN
James 5 in the TNTIP
James 5 in the TNTIZ
James 5 in the TOMA
James 5 in the TTENT
James 5 in the UBG
James 5 in the UGV
James 5 in the UGV2
James 5 in the UGV3
James 5 in the VBL
James 5 in the VDCC
James 5 in the YALU
James 5 in the YAPE
James 5 in the YBVTP
James 5 in the ZBP