Judges 15 (BOKCV)
1 Baada ya kitambo kidogo, wakati wa mavuno ya ngano, Samsoni akachukua mwana-mbuzi, kwenda kumzuru mkewe. Akasema, “Nataka kuingia chumbani kwa mke wangu.” Lakini baba yake huyo mwanamke hakumruhusu kuingia. 2 Huyo baba mkwe wake akamwambia, “Nilikuwa na hakika kwamba ulimkataa, hivyo mimi nikampa rafiki yako. Je, mdogo wake wa kike si mzuri zaidi kuliko yeye? Mchukue huyo badala yake.” 3 Samsoni akawaambia, “Wakati huu, nitakapowadhuru Wafilisti, sitakuwa na lawama.” 4 Hivyo Samsoni akatoka akawakamata mbweha 300 na kuwafunga wawili wawili kwa mikia yao kila mmoja kwa mwingine. Kisha akafungia mwenge wa moto, kwenye mikia ya kila jozi moja ya mbweha aliyokuwa ameifunga, 5 akawasha ile mienge na kuwaachia wale mbweha katika mashamba ya Wafilisti ya nafaka zilizosimamishwa katika matita. Akateketeza matita ya nafaka zilizosimama, pamoja na mashamba ya mizabibu na viunga vya mizeituni. 6 Ndipo Wafilisti wakauliza, “Ni nani aliyetenda jambo hili?” Wakaambiwa, “Ni Samsoni, yule mkwewe Mtimna, kwa sababu alimchukua mkewe akampa mwenzake.”Hivyo Wafilisti wakapanda wakamteketeza kwa moto yeye huyo mwanamke pamoja na baba yake. 7 Samsoni akawaambia, “Kwa kuwa mmetenda hivyo, hakika sitatulia mpaka niwe nimelipiza kisasi juu yenu.” 8 Akawashambulia kwa ukali kwa mapigo makuu na kuwaua watu wengi sana. Kisha akateremka na kukaa katika ufa kwenye mwamba wa Etamu. 9 Wafilisti wakapanda na kupiga kambi huko Yuda na kuenea huko Lehi. 10 Watu wa Yuda wakawauliza, “Kwa nini mmekuja kupigana nasi?”Wakawajibu, “Tumekuja ili kumkamata Samsoni na kumtenda kama alivyotutendea.” 11 Ndipo watu 3,000 toka Yuda walipoteremka na kwenda kwenye ufa wa mwamba huko Etamu, na kumwambia Samsoni, “Je, hujatambua kuwa Wafilisti wanatutawala? Ni nini hiki ulichotutendea?”Akawajibu, “Mimi nimewatendea tu kile walichonitendea.” 12 Wakamwambia, “Tumekuja kukufunga na kukutia mikononi mwa Wafilisti.”Samsoni akawaambia, “Niapieni kuwa hamtaniua ninyi wenyewe.” 13 Wakamjibu, “Sisi hatutakuua, bali tutakufunga tu na kukutia mikononi mwao.” Basi wakamfunga kwa kamba mbili mpya. Wakamchukua toka huko kwenye ufa katika mwamba. 14 Alipokaribia Lehi, Wafilisti wakamjia wakipiga kelele. Roho wa BWANA akamjia juu yake kwa nguvu. Kamba zilizomfunga mikono yake zikawa kama kitani iliyochomwa kwa moto, na vifungo vyake vikaanguka chini toka mikononi mwake. 15 Ndipo akaona mfupa mpya wa taya la punda, akanyoosha mkono, akauchukua na kuua nao Wafilisti wapatao 1,000. 16 Ndipo Samsoni akasema,“Kwa taya la pundamalundo juu ya malundo.Kwa taya la pundanimeua watu 1,000.” 17 Alipomaliza kusema, akautupa ule mfupa wa taya; na mahali pale pakaitwa Ramath-Lehi. 18 Kwa kuwa alikuwa amesikia kiu sana, akamlilia BWANA akisema, “Umempa mtumishi wako ushindi huu mkuu. Je, sasa nife kwa kiu na kuangukia mikononi mwa hawa watu wasiotahiriwa?” 19 BWANA akafunua shimo huko Lehi, pakatoka maji. Samsoni alipoyanywa, nguvu zikamrudia na kuhuika. Hivyo chemchemi ile ikaitwa En-Hakore, nayo iko mpaka leo huko Lehi. 20 Samsoni akawa mwamuzi wa Waisraeli katika siku za Wafilisti kwa muda wa miaka ishirini.
In Other Versions
Judges 15 in the ANGEFD
Judges 15 in the ANTPNG2D
Judges 15 in the AS21
Judges 15 in the BAGH
Judges 15 in the BBPNG
Judges 15 in the BBT1E
Judges 15 in the BDS
Judges 15 in the BEV
Judges 15 in the BHAD
Judges 15 in the BIB
Judges 15 in the BLPT
Judges 15 in the BNT
Judges 15 in the BNTABOOT
Judges 15 in the BNTLV
Judges 15 in the BOATCB
Judges 15 in the BOATCB2
Judges 15 in the BOBCV
Judges 15 in the BOCNT
Judges 15 in the BOECS
Judges 15 in the BOGWICC
Judges 15 in the BOHCB
Judges 15 in the BOHCV
Judges 15 in the BOHLNT
Judges 15 in the BOHNTLTAL
Judges 15 in the BOICB
Judges 15 in the BOILNTAP
Judges 15 in the BOITCV
Judges 15 in the BOKCV2
Judges 15 in the BOKHWOG
Judges 15 in the BOKSSV
Judges 15 in the BOLCB
Judges 15 in the BOLCB2
Judges 15 in the BOMCV
Judges 15 in the BONAV
Judges 15 in the BONCB
Judges 15 in the BONLT
Judges 15 in the BONUT2
Judges 15 in the BOPLNT
Judges 15 in the BOSCB
Judges 15 in the BOSNC
Judges 15 in the BOTLNT
Judges 15 in the BOVCB
Judges 15 in the BOYCB
Judges 15 in the BPBB
Judges 15 in the BPH
Judges 15 in the BSB
Judges 15 in the CCB
Judges 15 in the CUV
Judges 15 in the CUVS
Judges 15 in the DBT
Judges 15 in the DGDNT
Judges 15 in the DHNT
Judges 15 in the DNT
Judges 15 in the ELBE
Judges 15 in the EMTV
Judges 15 in the ESV
Judges 15 in the FBV
Judges 15 in the FEB
Judges 15 in the GGMNT
Judges 15 in the GNT
Judges 15 in the HARY
Judges 15 in the HNT
Judges 15 in the IRVA
Judges 15 in the IRVB
Judges 15 in the IRVG
Judges 15 in the IRVH
Judges 15 in the IRVK
Judges 15 in the IRVM
Judges 15 in the IRVM2
Judges 15 in the IRVO
Judges 15 in the IRVP
Judges 15 in the IRVT
Judges 15 in the IRVT2
Judges 15 in the IRVU
Judges 15 in the ISVN
Judges 15 in the JSNT
Judges 15 in the KAPI
Judges 15 in the KBT1ETNIK
Judges 15 in the KBV
Judges 15 in the KJV
Judges 15 in the KNFD
Judges 15 in the LBA
Judges 15 in the LBLA
Judges 15 in the LNT
Judges 15 in the LSV
Judges 15 in the MAAL
Judges 15 in the MBV
Judges 15 in the MBV2
Judges 15 in the MHNT
Judges 15 in the MKNFD
Judges 15 in the MNG
Judges 15 in the MNT
Judges 15 in the MNT2
Judges 15 in the MRS1T
Judges 15 in the NAA
Judges 15 in the NASB
Judges 15 in the NBLA
Judges 15 in the NBS
Judges 15 in the NBVTP
Judges 15 in the NET2
Judges 15 in the NIV11
Judges 15 in the NNT
Judges 15 in the NNT2
Judges 15 in the NNT3
Judges 15 in the PDDPT
Judges 15 in the PFNT
Judges 15 in the RMNT
Judges 15 in the SBIAS
Judges 15 in the SBIBS
Judges 15 in the SBIBS2
Judges 15 in the SBICS
Judges 15 in the SBIDS
Judges 15 in the SBIGS
Judges 15 in the SBIHS
Judges 15 in the SBIIS
Judges 15 in the SBIIS2
Judges 15 in the SBIIS3
Judges 15 in the SBIKS
Judges 15 in the SBIKS2
Judges 15 in the SBIMS
Judges 15 in the SBIOS
Judges 15 in the SBIPS
Judges 15 in the SBISS
Judges 15 in the SBITS
Judges 15 in the SBITS2
Judges 15 in the SBITS3
Judges 15 in the SBITS4
Judges 15 in the SBIUS
Judges 15 in the SBIVS
Judges 15 in the SBT
Judges 15 in the SBT1E
Judges 15 in the SCHL
Judges 15 in the SNT
Judges 15 in the SUSU
Judges 15 in the SUSU2
Judges 15 in the SYNO
Judges 15 in the TBIAOTANT
Judges 15 in the TBT1E
Judges 15 in the TBT1E2
Judges 15 in the TFTIP
Judges 15 in the TFTU
Judges 15 in the TGNTATF3T
Judges 15 in the THAI
Judges 15 in the TNFD
Judges 15 in the TNT
Judges 15 in the TNTIK
Judges 15 in the TNTIL
Judges 15 in the TNTIN
Judges 15 in the TNTIP
Judges 15 in the TNTIZ
Judges 15 in the TOMA
Judges 15 in the TTENT
Judges 15 in the UBG
Judges 15 in the UGV
Judges 15 in the UGV2
Judges 15 in the UGV3
Judges 15 in the VBL
Judges 15 in the VDCC
Judges 15 in the YALU
Judges 15 in the YAPE
Judges 15 in the YBVTP
Judges 15 in the ZBP