Jeremiah 1 (BOKCV)

1 Maneno ya Yeremia mwana wa Hilkia, mmoja wa makuhani katika mji wa Anathothi, katika nchi ya Benyamini. 2 Neno la BWANA lilimjia katika mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda, 3 na pia wakati wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, mpaka mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, wakati watu wa Yerusalemu walipopelekwa uhamishoni. 4 Neno la BWANA lilinijia, kusema, 5 “Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako, nilikujua;kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalum;nilikuweka uwe nabii kwa mataifa.” 6 Nami nikasema, “Aa, BWANA Mwenyezi, sijui kusema, kwani mimi ni mtoto mdogo tu.” 7 Lakini BWANA akaniambia, “Usiseme, ‘Mimi ni mtoto mdogo tu.’ Utaenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza. 8 Usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe,” asema BWANA. 9 Kisha BWANA akaunyoosha mkono wake na kugusa kinywa changu, akaniambia, “Sasa nimeyaweka maneno yangu kinywani mwako. 10 Tazama, leo nimekuweka juu ya mataifa na falme ili kungʼoa na kubomoa, kuharibu na kuangamiza, kujenga na kupanda.” 11 Neno la BWANA likanijia kusema, “Je, Yeremia unaona nini?”Nami nikajibu, “Naona tawi la mti wa mlozi.” 12 BWANA akaniambia, “Umeona vyema kwa maana ninaliangalia neno langu ili kuona kwamba limetimizwa.” 13 Neno la BWANA likanijia tena, “Unaona nini?”Nikajibu, “Naona chungu kinachochemka, kikiwa kimeinama kutoka kaskazini.” 14 BWANA akaniambia, “Kutoka kaskazini maafa yatamwagwa kwa wote waishio katika nchi. 15 Nitawaita watu wote wa falme za kaskazini,” asema BWANA.“Wafalme wao watakuja na kuweka viti vyao vya enzikatika maingilio ya malango ya Yerusalemu,watakuja dhidi ya kuta zake zote zinazouzunguka,na dhidi ya miji yote ya Yuda. 16 Nitatoa hukumu zangu kwa watu wangukwa sababu ya uovu wao wa kuniacha mimi,kwa kufukiza uvumba kwa miungu minginena kuabudu kile ambacho mikono yao imekitengeneza. 17 “Jiandae! Simama useme chochote nitakachokuamuru. Usiwaogope, la sivyo nitakufanya uwaogope wao. 18 Leo nimekufanya mji wenye ngome, nguzo ya chuma, na ukuta wa shaba ili kusimama dhidi ya nchi yote: dhidi ya wafalme wa Yuda, maafisa wake, makuhani wake na watu wa nchi hiyo. 19 Watapigana nawe lakini hawatakushinda, kwa kuwa niko pamoja nawe, nami nitakuokoa,” asema BWANA.

In Other Versions

Jeremiah 1 in the ANGEFD

Jeremiah 1 in the ANTPNG2D

Jeremiah 1 in the AS21

Jeremiah 1 in the BAGH

Jeremiah 1 in the BBPNG

Jeremiah 1 in the BBT1E

Jeremiah 1 in the BDS

Jeremiah 1 in the BEV

Jeremiah 1 in the BHAD

Jeremiah 1 in the BIB

Jeremiah 1 in the BLPT

Jeremiah 1 in the BNT

Jeremiah 1 in the BNTABOOT

Jeremiah 1 in the BNTLV

Jeremiah 1 in the BOATCB

Jeremiah 1 in the BOATCB2

Jeremiah 1 in the BOBCV

Jeremiah 1 in the BOCNT

Jeremiah 1 in the BOECS

Jeremiah 1 in the BOGWICC

Jeremiah 1 in the BOHCB

Jeremiah 1 in the BOHCV

Jeremiah 1 in the BOHLNT

Jeremiah 1 in the BOHNTLTAL

Jeremiah 1 in the BOICB

Jeremiah 1 in the BOILNTAP

Jeremiah 1 in the BOITCV

Jeremiah 1 in the BOKCV2

Jeremiah 1 in the BOKHWOG

Jeremiah 1 in the BOKSSV

Jeremiah 1 in the BOLCB

Jeremiah 1 in the BOLCB2

Jeremiah 1 in the BOMCV

Jeremiah 1 in the BONAV

Jeremiah 1 in the BONCB

Jeremiah 1 in the BONLT

Jeremiah 1 in the BONUT2

Jeremiah 1 in the BOPLNT

Jeremiah 1 in the BOSCB

Jeremiah 1 in the BOSNC

Jeremiah 1 in the BOTLNT

Jeremiah 1 in the BOVCB

Jeremiah 1 in the BOYCB

Jeremiah 1 in the BPBB

Jeremiah 1 in the BPH

Jeremiah 1 in the BSB

Jeremiah 1 in the CCB

Jeremiah 1 in the CUV

Jeremiah 1 in the CUVS

Jeremiah 1 in the DBT

Jeremiah 1 in the DGDNT

Jeremiah 1 in the DHNT

Jeremiah 1 in the DNT

Jeremiah 1 in the ELBE

Jeremiah 1 in the EMTV

Jeremiah 1 in the ESV

Jeremiah 1 in the FBV

Jeremiah 1 in the FEB

Jeremiah 1 in the GGMNT

Jeremiah 1 in the GNT

Jeremiah 1 in the HARY

Jeremiah 1 in the HNT

Jeremiah 1 in the IRVA

Jeremiah 1 in the IRVB

Jeremiah 1 in the IRVG

Jeremiah 1 in the IRVH

Jeremiah 1 in the IRVK

Jeremiah 1 in the IRVM

Jeremiah 1 in the IRVM2

Jeremiah 1 in the IRVO

Jeremiah 1 in the IRVP

Jeremiah 1 in the IRVT

Jeremiah 1 in the IRVT2

Jeremiah 1 in the IRVU

Jeremiah 1 in the ISVN

Jeremiah 1 in the JSNT

Jeremiah 1 in the KAPI

Jeremiah 1 in the KBT1ETNIK

Jeremiah 1 in the KBV

Jeremiah 1 in the KJV

Jeremiah 1 in the KNFD

Jeremiah 1 in the LBA

Jeremiah 1 in the LBLA

Jeremiah 1 in the LNT

Jeremiah 1 in the LSV

Jeremiah 1 in the MAAL

Jeremiah 1 in the MBV

Jeremiah 1 in the MBV2

Jeremiah 1 in the MHNT

Jeremiah 1 in the MKNFD

Jeremiah 1 in the MNG

Jeremiah 1 in the MNT

Jeremiah 1 in the MNT2

Jeremiah 1 in the MRS1T

Jeremiah 1 in the NAA

Jeremiah 1 in the NASB

Jeremiah 1 in the NBLA

Jeremiah 1 in the NBS

Jeremiah 1 in the NBVTP

Jeremiah 1 in the NET2

Jeremiah 1 in the NIV11

Jeremiah 1 in the NNT

Jeremiah 1 in the NNT2

Jeremiah 1 in the NNT3

Jeremiah 1 in the PDDPT

Jeremiah 1 in the PFNT

Jeremiah 1 in the RMNT

Jeremiah 1 in the SBIAS

Jeremiah 1 in the SBIBS

Jeremiah 1 in the SBIBS2

Jeremiah 1 in the SBICS

Jeremiah 1 in the SBIDS

Jeremiah 1 in the SBIGS

Jeremiah 1 in the SBIHS

Jeremiah 1 in the SBIIS

Jeremiah 1 in the SBIIS2

Jeremiah 1 in the SBIIS3

Jeremiah 1 in the SBIKS

Jeremiah 1 in the SBIKS2

Jeremiah 1 in the SBIMS

Jeremiah 1 in the SBIOS

Jeremiah 1 in the SBIPS

Jeremiah 1 in the SBISS

Jeremiah 1 in the SBITS

Jeremiah 1 in the SBITS2

Jeremiah 1 in the SBITS3

Jeremiah 1 in the SBITS4

Jeremiah 1 in the SBIUS

Jeremiah 1 in the SBIVS

Jeremiah 1 in the SBT

Jeremiah 1 in the SBT1E

Jeremiah 1 in the SCHL

Jeremiah 1 in the SNT

Jeremiah 1 in the SUSU

Jeremiah 1 in the SUSU2

Jeremiah 1 in the SYNO

Jeremiah 1 in the TBIAOTANT

Jeremiah 1 in the TBT1E

Jeremiah 1 in the TBT1E2

Jeremiah 1 in the TFTIP

Jeremiah 1 in the TFTU

Jeremiah 1 in the TGNTATF3T

Jeremiah 1 in the THAI

Jeremiah 1 in the TNFD

Jeremiah 1 in the TNT

Jeremiah 1 in the TNTIK

Jeremiah 1 in the TNTIL

Jeremiah 1 in the TNTIN

Jeremiah 1 in the TNTIP

Jeremiah 1 in the TNTIZ

Jeremiah 1 in the TOMA

Jeremiah 1 in the TTENT

Jeremiah 1 in the UBG

Jeremiah 1 in the UGV

Jeremiah 1 in the UGV2

Jeremiah 1 in the UGV3

Jeremiah 1 in the VBL

Jeremiah 1 in the VDCC

Jeremiah 1 in the YALU

Jeremiah 1 in the YAPE

Jeremiah 1 in the YBVTP

Jeremiah 1 in the ZBP