Jeremiah 46 (BOKCV)

1 Hili ni neno la BWANA lililomjia nabii Yeremia kuhusu mataifa: 2 Kuhusu Misri: Huu ni ujumbe dhidi ya jeshi la Farao Neko mfalme wa Misri, lililoshindwa huko Karkemishi kwenye Mto Frati na Nebukadneza mfalme wa Babeli, katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda: 3 “Wekeni tayari ngao zenu, kubwa na ndogo,mtoke kwa ajili ya vita! 4 Fungieni farasi lijamu,pandeni farasi!Shikeni nafasi zenumkiwa mmevaa chapeo!Isugueni mikuki yenu,vaeni dirii vifuani! 5 Je, ninaona nini?Wametiwa hofu,wanarudi nyuma,askari wao wameshindwa.Wanakimbia kwa harakapasipo kutazama nyuma,tena kuna hofu kuu kila upande,”asema BWANA. 6 Walio wepesi na wenye mbio hawawezi kukimbia,wala wenye nguvu hawawezi kutoroka.Kaskazini, kando ya Mto Frati,wanajikwaa na kuanguka. 7 “Ni nani huyu ajiinuaye kama Mto Naili,kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi? 8 Misri hujiinua kama Mto Naili,kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi.Husema, ‘Nitainuka na kufunika dunia,nitaiangamiza miji na watu wake.’ 9 Songeni mbele, enyi farasi!Endesheni kwa ukali, enyi magari ya farasi,Endeleeni mbele, enyi mashujaa:watu wa Kushi na Putu wachukuao ngao,watu wa Ludi wavutao upinde. 10 Lakini ile siku ni ya Bwana, BWANA Mwenye Nguvu Zote,siku ya kulipiza kisasi,kisasi juu ya adui zake.Upanga utakula hata utakapotosheka,hadi utakapozima kiu yake kwa damu.Kwa maana Bwana, BWANA Mwenye Nguvu Zote, atatoa dhabihukwenye nchi ya kaskazini, kando ya Mto Frati. 11 “Panda hadi Gileadi ukapate zeri,ee Bikira Binti wa Misri.Lakini umetumia dawa nyingi bila mafanikio;huwezi kupona. 12 Mataifa yatasikia juu ya aibu yako,kilio chako kitaijaza dunia.Shujaa mmoja atajikwaa juu ya mwingine,nao wataanguka chini pamoja.” 13 Huu ndio ujumbe BWANA aliomwambia nabii Yeremia kuhusu kuja kwa Nebukadneza mfalme wa Babeli ili kuishambulia Misri: 14 “Tangaza hili katika Misri, nawe ulihubiri katika Migdoli,hubiri pia katika Memfisi na Tahpanhesi:‘Shikeni nafasi zenu na mwe tayari,kwa kuwa upanga unawala wale wanaokuzunguka.’ 15 Kwa nini mashujaa wako wamesombwana kupelekwa mbali?Hawawezi kusimama, kwa maana BWANAatawasukuma awaangushe chini. 16 Watajikwaa mara kwa mara,wataangukiana wao kwa wao.Watasema, ‘Amka, turudikwa watu wetu na nchi yetu,mbali na upanga wa mtesi.’ 17 Huko watatangaza,‘Farao mfalme wa Misri ni makelele tu,amekosa wasaa wake.’ 18 “Kwa hakika kama niishivyo,” asema Mfalme,ambaye jina lake ni BWANA Mwenye Nguvu Zote,“mmoja atakuja ambaye ni kama Tabori miongoni mwa milima,kama Karmeli kando ya bahari. 19 Funga mizigo yako kwenda uhamishoni,wewe ukaaye Misri,kwa kuwa Memfisi utaangamizwana kuwa magofu pasipo mkazi. 20 “Misri ni mtamba mzuri,lakini kipanga anakuja dhidi yake kutoka kaskazini. 21 Askari wake waliokodiwa katika safu zakewako kama ndama walionenepeshwa.Wao pia watageuka na kukimbia pamoja,hawataweza kuhimili vita,kwa maana siku ya msiba inakuja juu yao,wakati wao wa kuadhibiwa. 22 Misri atatoa sauti kama ya nyoka anayekimbiakadiri adui anavyowasogelea na majeshi,watakuja dhidi yake wakiwa na mashoka,kama watu wakatao miti. 23 Wataufyeka msitu wake,”asema BWANA,“hata kama umesongamana kiasi gani.Ni wengi kuliko nzige,hawawezi kuhesabika. 24 Binti wa Misri ataaibishwa,atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini.” 25 BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asema: “Nakaribia kuleta adhabu juu ya Amoni mungu wa Thebesi, na juu ya Farao, Misri na miungu yake, na wafalme wake, pamoja na wale wanaomtegemea Farao. 26 Nitawatia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na maafisa wake. Hatimaye, hata hivyo, Misri itakaliwa kama nyakati zilizopita,” asema BWANA. 27 “Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu,usifadhaike, ee Israeli.Hakika nitakuokoa kutoka nchi za mbali,uzao wako kutoka nchi ya uhamisho wao.Yakobo atakuwa tena na amani na salama,wala hakuna hata mmoja atakayewatia hofu. 28 Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu,kwa maana mimi niko pamoja nawe,”asema BWANA.“Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yoteambayo miongoni mwake nimekutawanya,sitakuangamiza wewe kabisa.Nitakurudi, lakini kwa haki tu,wala sitakuacha kabisa bila kukuadhibu.”

In Other Versions

Jeremiah 46 in the ANGEFD

Jeremiah 46 in the ANTPNG2D

Jeremiah 46 in the AS21

Jeremiah 46 in the BAGH

Jeremiah 46 in the BBPNG

Jeremiah 46 in the BBT1E

Jeremiah 46 in the BDS

Jeremiah 46 in the BEV

Jeremiah 46 in the BHAD

Jeremiah 46 in the BIB

Jeremiah 46 in the BLPT

Jeremiah 46 in the BNT

Jeremiah 46 in the BNTABOOT

Jeremiah 46 in the BNTLV

Jeremiah 46 in the BOATCB

Jeremiah 46 in the BOATCB2

Jeremiah 46 in the BOBCV

Jeremiah 46 in the BOCNT

Jeremiah 46 in the BOECS

Jeremiah 46 in the BOGWICC

Jeremiah 46 in the BOHCB

Jeremiah 46 in the BOHCV

Jeremiah 46 in the BOHLNT

Jeremiah 46 in the BOHNTLTAL

Jeremiah 46 in the BOICB

Jeremiah 46 in the BOILNTAP

Jeremiah 46 in the BOITCV

Jeremiah 46 in the BOKCV2

Jeremiah 46 in the BOKHWOG

Jeremiah 46 in the BOKSSV

Jeremiah 46 in the BOLCB

Jeremiah 46 in the BOLCB2

Jeremiah 46 in the BOMCV

Jeremiah 46 in the BONAV

Jeremiah 46 in the BONCB

Jeremiah 46 in the BONLT

Jeremiah 46 in the BONUT2

Jeremiah 46 in the BOPLNT

Jeremiah 46 in the BOSCB

Jeremiah 46 in the BOSNC

Jeremiah 46 in the BOTLNT

Jeremiah 46 in the BOVCB

Jeremiah 46 in the BOYCB

Jeremiah 46 in the BPBB

Jeremiah 46 in the BPH

Jeremiah 46 in the BSB

Jeremiah 46 in the CCB

Jeremiah 46 in the CUV

Jeremiah 46 in the CUVS

Jeremiah 46 in the DBT

Jeremiah 46 in the DGDNT

Jeremiah 46 in the DHNT

Jeremiah 46 in the DNT

Jeremiah 46 in the ELBE

Jeremiah 46 in the EMTV

Jeremiah 46 in the ESV

Jeremiah 46 in the FBV

Jeremiah 46 in the FEB

Jeremiah 46 in the GGMNT

Jeremiah 46 in the GNT

Jeremiah 46 in the HARY

Jeremiah 46 in the HNT

Jeremiah 46 in the IRVA

Jeremiah 46 in the IRVB

Jeremiah 46 in the IRVG

Jeremiah 46 in the IRVH

Jeremiah 46 in the IRVK

Jeremiah 46 in the IRVM

Jeremiah 46 in the IRVM2

Jeremiah 46 in the IRVO

Jeremiah 46 in the IRVP

Jeremiah 46 in the IRVT

Jeremiah 46 in the IRVT2

Jeremiah 46 in the IRVU

Jeremiah 46 in the ISVN

Jeremiah 46 in the JSNT

Jeremiah 46 in the KAPI

Jeremiah 46 in the KBT1ETNIK

Jeremiah 46 in the KBV

Jeremiah 46 in the KJV

Jeremiah 46 in the KNFD

Jeremiah 46 in the LBA

Jeremiah 46 in the LBLA

Jeremiah 46 in the LNT

Jeremiah 46 in the LSV

Jeremiah 46 in the MAAL

Jeremiah 46 in the MBV

Jeremiah 46 in the MBV2

Jeremiah 46 in the MHNT

Jeremiah 46 in the MKNFD

Jeremiah 46 in the MNG

Jeremiah 46 in the MNT

Jeremiah 46 in the MNT2

Jeremiah 46 in the MRS1T

Jeremiah 46 in the NAA

Jeremiah 46 in the NASB

Jeremiah 46 in the NBLA

Jeremiah 46 in the NBS

Jeremiah 46 in the NBVTP

Jeremiah 46 in the NET2

Jeremiah 46 in the NIV11

Jeremiah 46 in the NNT

Jeremiah 46 in the NNT2

Jeremiah 46 in the NNT3

Jeremiah 46 in the PDDPT

Jeremiah 46 in the PFNT

Jeremiah 46 in the RMNT

Jeremiah 46 in the SBIAS

Jeremiah 46 in the SBIBS

Jeremiah 46 in the SBIBS2

Jeremiah 46 in the SBICS

Jeremiah 46 in the SBIDS

Jeremiah 46 in the SBIGS

Jeremiah 46 in the SBIHS

Jeremiah 46 in the SBIIS

Jeremiah 46 in the SBIIS2

Jeremiah 46 in the SBIIS3

Jeremiah 46 in the SBIKS

Jeremiah 46 in the SBIKS2

Jeremiah 46 in the SBIMS

Jeremiah 46 in the SBIOS

Jeremiah 46 in the SBIPS

Jeremiah 46 in the SBISS

Jeremiah 46 in the SBITS

Jeremiah 46 in the SBITS2

Jeremiah 46 in the SBITS3

Jeremiah 46 in the SBITS4

Jeremiah 46 in the SBIUS

Jeremiah 46 in the SBIVS

Jeremiah 46 in the SBT

Jeremiah 46 in the SBT1E

Jeremiah 46 in the SCHL

Jeremiah 46 in the SNT

Jeremiah 46 in the SUSU

Jeremiah 46 in the SUSU2

Jeremiah 46 in the SYNO

Jeremiah 46 in the TBIAOTANT

Jeremiah 46 in the TBT1E

Jeremiah 46 in the TBT1E2

Jeremiah 46 in the TFTIP

Jeremiah 46 in the TFTU

Jeremiah 46 in the TGNTATF3T

Jeremiah 46 in the THAI

Jeremiah 46 in the TNFD

Jeremiah 46 in the TNT

Jeremiah 46 in the TNTIK

Jeremiah 46 in the TNTIL

Jeremiah 46 in the TNTIN

Jeremiah 46 in the TNTIP

Jeremiah 46 in the TNTIZ

Jeremiah 46 in the TOMA

Jeremiah 46 in the TTENT

Jeremiah 46 in the UBG

Jeremiah 46 in the UGV

Jeremiah 46 in the UGV2

Jeremiah 46 in the UGV3

Jeremiah 46 in the VBL

Jeremiah 46 in the VDCC

Jeremiah 46 in the YALU

Jeremiah 46 in the YAPE

Jeremiah 46 in the YBVTP

Jeremiah 46 in the ZBP