John 15 (BOKCV)
1 “Mimi ndimi mzabibu wa kweli na Baba yangu ndiye mkulima. 2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata, nalo kila tawi lizaalo, hulisafisha ili lipate kuzaa matunda zaidi. 3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililonena nanyi. 4 Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa matunda lisipokaa ndani ya mzabibu, vivyo hivyo ninyi msipokaa ndani yangu hamwezi kuzaa matunda. 5 “Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa sana, maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya jambo lolote. 6 Mtu yeyote asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka. Matawi kama hayo hukusanywa na kutupwa motoni, yakateketea. 7 Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtatendewa. 8 Kwa hiyo Baba yangu hutukuzwa, kwa vile mzaavyo matunda mengi, nanyi mtakuwa wanafunzi wangu. 9 “Kama vile Baba alivyonipenda mimi, hivyo ndivyo mimi nilivyowapenda ninyi. Basi kaeni katika pendo langu. 10 Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. 11 Nimewaambia mambo haya ili furaha yangu iwe ndani yenu na furaha yenu iwe kamili. 12 Amri yangu ndiyo hii: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi. 13 Hakuna mtu mwenye upendo mkuu kuliko huu, mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. 14 Ninyi ni rafiki zangu mkifanya ninayowaamuru. 15 Siwaiti ninyi watumishi tena, kwa sababu watumishi hawajui bwana wao analofanya, bali nimewaita ninyi rafiki, kwa maana nimewajulisha mambo yote niliyoyasikia kutoka kwa Baba yangu. 16 Si ninyi mlionichagua, bali mimi ndiye niliyewachagua ninyi na kuwaweka mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kudumu. Ili nalo lolote mtakalomwomba Baba katika Jina langu, awape ninyi. 17 Amri yangu ndiyo hii: Mpendane. 18 “Kama ulimwengu ukiwachukia ninyi, kumbukeni kwamba ulinichukia mimi kabla yenu. 19 Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungeliwapenda kama vile unavyowapenda walio wake. Kwa sababu ninyi si wa ulimwengu, lakini mimi nimewachagua kutoka ulimwengu, hii ndiyo sababu ulimwengu unawachukia. 20 Kumbukeni lile neno nililowaambia, ‘Hakuna mtumishi aliye mkuu kuliko bwana wake.’ Kama wamenitesa mimi, nanyi pia watawatesa. Kama wamelishika neno langu, watalishika na neno lenu pia. 21 Watawatendea ninyi haya yote kwa ajili ya Jina langu, kwa sababu hawamjui yeye aliyenituma. 22 Kama sikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia ya dhambi. Lakini sasa hawana udhuru kwa ajili ya dhambi zao. 23 Yeyote anayenichukia mimi, anamchukia pia na Baba yangu. 24 Kama sikuwa nimefanya miujiza ambayo haijapata kufanywa na mtu mwingine yeyote, wasingalikuwa na hatia ya dhambi. Lakini sasa wameiona miujiza hii na bado wakatuchukia mimi na Baba yangu. 25 Lakini hii ni kutimiza lile neno lililoandikwa kwenye Sheria kwamba, ‘Walinichukia pasipo sababu.’ 26 “Lakini atakapokuja huyo Msaidizi nitakayemtuma kwenu kutoka kwa Baba, yaani, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi. 27 Ninyi nanyi itawapasa kushuhudia kwa sababu mmekuwa pamoja nami tangu mwanzo.
In Other Versions
John 15 in the ANGEFD
John 15 in the ANTPNG2D
John 15 in the AS21
John 15 in the BAGH
John 15 in the BBPNG
John 15 in the BBT1E
John 15 in the BDS
John 15 in the BEV
John 15 in the BHAD
John 15 in the BIB
John 15 in the BLPT
John 15 in the BNT
John 15 in the BNTABOOT
John 15 in the BNTLV
John 15 in the BOATCB
John 15 in the BOATCB2
John 15 in the BOBCV
John 15 in the BOCNT
John 15 in the BOECS
John 15 in the BOGWICC
John 15 in the BOHCB
John 15 in the BOHCV
John 15 in the BOHLNT
John 15 in the BOHNTLTAL
John 15 in the BOICB
John 15 in the BOILNTAP
John 15 in the BOITCV
John 15 in the BOKCV2
John 15 in the BOKHWOG
John 15 in the BOKSSV
John 15 in the BOLCB
John 15 in the BOLCB2
John 15 in the BOMCV
John 15 in the BONAV
John 15 in the BONCB
John 15 in the BONLT
John 15 in the BONUT2
John 15 in the BOPLNT
John 15 in the BOSCB
John 15 in the BOSNC
John 15 in the BOTLNT
John 15 in the BOVCB
John 15 in the BOYCB
John 15 in the BPBB
John 15 in the BPH
John 15 in the BSB
John 15 in the CCB
John 15 in the CUV
John 15 in the CUVS
John 15 in the DBT
John 15 in the DGDNT
John 15 in the DHNT
John 15 in the DNT
John 15 in the ELBE
John 15 in the EMTV
John 15 in the ESV
John 15 in the FBV
John 15 in the FEB
John 15 in the GGMNT
John 15 in the GNT
John 15 in the HARY
John 15 in the HNT
John 15 in the IRVA
John 15 in the IRVB
John 15 in the IRVG
John 15 in the IRVH
John 15 in the IRVK
John 15 in the IRVM
John 15 in the IRVM2
John 15 in the IRVO
John 15 in the IRVP
John 15 in the IRVT
John 15 in the IRVT2
John 15 in the IRVU
John 15 in the ISVN
John 15 in the JSNT
John 15 in the KAPI
John 15 in the KBT1ETNIK
John 15 in the KBV
John 15 in the KJV
John 15 in the KNFD
John 15 in the LBA
John 15 in the LBLA
John 15 in the LNT
John 15 in the LSV
John 15 in the MAAL
John 15 in the MBV
John 15 in the MBV2
John 15 in the MHNT
John 15 in the MKNFD
John 15 in the MNG
John 15 in the MNT
John 15 in the MNT2
John 15 in the MRS1T
John 15 in the NAA
John 15 in the NASB
John 15 in the NBLA
John 15 in the NBS
John 15 in the NBVTP
John 15 in the NET2
John 15 in the NIV11
John 15 in the NNT
John 15 in the NNT2
John 15 in the NNT3
John 15 in the PDDPT
John 15 in the PFNT
John 15 in the RMNT
John 15 in the SBIAS
John 15 in the SBIBS
John 15 in the SBIBS2
John 15 in the SBICS
John 15 in the SBIDS
John 15 in the SBIGS
John 15 in the SBIHS
John 15 in the SBIIS
John 15 in the SBIIS2
John 15 in the SBIIS3
John 15 in the SBIKS
John 15 in the SBIKS2
John 15 in the SBIMS
John 15 in the SBIOS
John 15 in the SBIPS
John 15 in the SBISS
John 15 in the SBITS
John 15 in the SBITS2
John 15 in the SBITS3
John 15 in the SBITS4
John 15 in the SBIUS
John 15 in the SBIVS
John 15 in the SBT
John 15 in the SBT1E
John 15 in the SCHL
John 15 in the SNT
John 15 in the SUSU
John 15 in the SUSU2
John 15 in the SYNO
John 15 in the TBIAOTANT
John 15 in the TBT1E
John 15 in the TBT1E2
John 15 in the TFTIP
John 15 in the TFTU
John 15 in the TGNTATF3T
John 15 in the THAI
John 15 in the TNFD
John 15 in the TNT
John 15 in the TNTIK
John 15 in the TNTIL
John 15 in the TNTIN
John 15 in the TNTIP
John 15 in the TNTIZ
John 15 in the TOMA
John 15 in the TTENT
John 15 in the UBG
John 15 in the UGV
John 15 in the UGV2
John 15 in the UGV3
John 15 in the VBL
John 15 in the VDCC
John 15 in the YALU
John 15 in the YAPE
John 15 in the YBVTP
John 15 in the ZBP