Job 1 (BOKCV)

1 Katika nchi ya Usi paliishi mtu ambaye aliitwa Ayubu. Mtu huyu alikuwa hana hatia, naye alikuwa mkamilifu; alimcha Mungu na kuepukana na uovu. 2 Alikuwa na wana saba na binti watatu, 3 naye alikuwa na kondoo elfu saba, ngamia elfu tatu, jozi mia tano za maksai, na punda mia tano, tena alikuwa na idadi kubwa ya watumishi. Alikuwa mtu mkuu sana miongoni mwa watu wa Mashariki. 4 Wanawe walikuwa na desturi ya kufanya karamu katika nyumba zao kwa zamu, nao wangewaalika umbu zao watatu ili kula na kunywa pamoja nao. 5 Wakati kipindi cha karamu kilimalizika, Ayubu angetuma waitwe na kuwafanyia utakaso. Angetoa dhabihu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya kila mmoja wao asubuhi na mapema, akifikiri, “Pengine wanangu wametenda dhambi na kumlaani Mungu mioyoni mwao.” Hii ilikuwa ndiyo desturi ya kawaida ya Ayubu. 6 Siku moja wana wa Mungu walikwenda kujionyesha mbele za BWANA. Shetani naye akaja pamoja nao. 7 BWANA akamwambia Shetani, “Umetoka wapi?”Shetani akamjibu BWANA, “Natoka kuzunguka pote duniani, nikitembea huku na huko humo.” 8 Ndipo BWANA akamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Hakuna mtu mwingine duniani aliye kama yeye, asiye na hatia, ni mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuepukana na uovu.” 9 Shetani akamjibu BWANA, “Je, Ayubu anamcha Mungu bure? 10 Je, wewe hukumjengea boma pande zote yeye na wa nyumbani mwake pamoja na kila kitu alicho nacho? Kazi za mikono yake umezibariki na hivyo makundi yake ya kondoo na mbuzi pamoja na ya wanyama yameenea katika nchi nzima. 11 Lakini nyoosha mkono wako na kupiga kila kitu alicho nacho, naye kwa hakika atakulaani mbele za uso wako.” 12 BWANA akamwambia Shetani, “Vema sana, kwa hiyo, kila kitu alicho nacho kiko mikononi mwako, lakini juu ya huyo mtu mwenyewe usimguse hata kwa kidole.”Ndipo Shetani akatoka mbele za BWANA. 13 Siku moja watoto wa Ayubu walipokuwa wakifanya karamu wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa, 14 akaja mjumbe kwa Ayubu na kusema, “Maksai walikuwa wakilima na punda walikuwa wakilisha karibu nao, 15 Waseba wakawashambulia na kuchukua mifugo. Kisha wakawaua watumishi kwa upanga, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari!” 16 Alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Moto wa Mungu ulishuka kutoka mbinguni na kuteketeza kondoo na watumishi, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari!” 17 Alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Wakaldayo waliunda vikosi vitatu vya uvamizi na kuwaangukia ngamia wako na kuwachukua wakaondoka nao. Wakawaua watumishi kwa upanga, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari.” 18 Alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Wana wako na binti zako walipokuwa wakifanya karamu, wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa, 19 ghafula upepo wenye nguvu ukavuma kutoka jangwani, nao ukaipiga nyumba hiyo pembe zake nne. Ikawaangukia hao watoto nao wamekufa, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari!” 20 Ndipo Ayubu akasimama, akararua joho lake na kunyoa nywele zake. Kisha akaanguka chini katika kuabudu 21 na kusema:“Nilitoka tumboni mwa mama yangu uchi,nami nitaondoka uchi, BWANA alinipa, naye BWANA ameviondoa,jina la BWANA litukuzwe.” 22 Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi kwa kumlaumu Mungu kwa kufanya ubaya.

In Other Versions

Job 1 in the ANGEFD

Job 1 in the ANTPNG2D

Job 1 in the AS21

Job 1 in the BAGH

Job 1 in the BBPNG

Job 1 in the BBT1E

Job 1 in the BDS

Job 1 in the BEV

Job 1 in the BHAD

Job 1 in the BIB

Job 1 in the BLPT

Job 1 in the BNT

Job 1 in the BNTABOOT

Job 1 in the BNTLV

Job 1 in the BOATCB

Job 1 in the BOATCB2

Job 1 in the BOBCV

Job 1 in the BOCNT

Job 1 in the BOECS

Job 1 in the BOGWICC

Job 1 in the BOHCB

Job 1 in the BOHCV

Job 1 in the BOHLNT

Job 1 in the BOHNTLTAL

Job 1 in the BOICB

Job 1 in the BOILNTAP

Job 1 in the BOITCV

Job 1 in the BOKCV2

Job 1 in the BOKHWOG

Job 1 in the BOKSSV

Job 1 in the BOLCB

Job 1 in the BOLCB2

Job 1 in the BOMCV

Job 1 in the BONAV

Job 1 in the BONCB

Job 1 in the BONLT

Job 1 in the BONUT2

Job 1 in the BOPLNT

Job 1 in the BOSCB

Job 1 in the BOSNC

Job 1 in the BOTLNT

Job 1 in the BOVCB

Job 1 in the BOYCB

Job 1 in the BPBB

Job 1 in the BPH

Job 1 in the BSB

Job 1 in the CCB

Job 1 in the CUV

Job 1 in the CUVS

Job 1 in the DBT

Job 1 in the DGDNT

Job 1 in the DHNT

Job 1 in the DNT

Job 1 in the ELBE

Job 1 in the EMTV

Job 1 in the ESV

Job 1 in the FBV

Job 1 in the FEB

Job 1 in the GGMNT

Job 1 in the GNT

Job 1 in the HARY

Job 1 in the HNT

Job 1 in the IRVA

Job 1 in the IRVB

Job 1 in the IRVG

Job 1 in the IRVH

Job 1 in the IRVK

Job 1 in the IRVM

Job 1 in the IRVM2

Job 1 in the IRVO

Job 1 in the IRVP

Job 1 in the IRVT

Job 1 in the IRVT2

Job 1 in the IRVU

Job 1 in the ISVN

Job 1 in the JSNT

Job 1 in the KAPI

Job 1 in the KBT1ETNIK

Job 1 in the KBV

Job 1 in the KJV

Job 1 in the KNFD

Job 1 in the LBA

Job 1 in the LBLA

Job 1 in the LNT

Job 1 in the LSV

Job 1 in the MAAL

Job 1 in the MBV

Job 1 in the MBV2

Job 1 in the MHNT

Job 1 in the MKNFD

Job 1 in the MNG

Job 1 in the MNT

Job 1 in the MNT2

Job 1 in the MRS1T

Job 1 in the NAA

Job 1 in the NASB

Job 1 in the NBLA

Job 1 in the NBS

Job 1 in the NBVTP

Job 1 in the NET2

Job 1 in the NIV11

Job 1 in the NNT

Job 1 in the NNT2

Job 1 in the NNT3

Job 1 in the PDDPT

Job 1 in the PFNT

Job 1 in the RMNT

Job 1 in the SBIAS

Job 1 in the SBIBS

Job 1 in the SBIBS2

Job 1 in the SBICS

Job 1 in the SBIDS

Job 1 in the SBIGS

Job 1 in the SBIHS

Job 1 in the SBIIS

Job 1 in the SBIIS2

Job 1 in the SBIIS3

Job 1 in the SBIKS

Job 1 in the SBIKS2

Job 1 in the SBIMS

Job 1 in the SBIOS

Job 1 in the SBIPS

Job 1 in the SBISS

Job 1 in the SBITS

Job 1 in the SBITS2

Job 1 in the SBITS3

Job 1 in the SBITS4

Job 1 in the SBIUS

Job 1 in the SBIVS

Job 1 in the SBT

Job 1 in the SBT1E

Job 1 in the SCHL

Job 1 in the SNT

Job 1 in the SUSU

Job 1 in the SUSU2

Job 1 in the SYNO

Job 1 in the TBIAOTANT

Job 1 in the TBT1E

Job 1 in the TBT1E2

Job 1 in the TFTIP

Job 1 in the TFTU

Job 1 in the TGNTATF3T

Job 1 in the THAI

Job 1 in the TNFD

Job 1 in the TNT

Job 1 in the TNTIK

Job 1 in the TNTIL

Job 1 in the TNTIN

Job 1 in the TNTIP

Job 1 in the TNTIZ

Job 1 in the TOMA

Job 1 in the TTENT

Job 1 in the UBG

Job 1 in the UGV

Job 1 in the UGV2

Job 1 in the UGV3

Job 1 in the VBL

Job 1 in the VDCC

Job 1 in the YALU

Job 1 in the YAPE

Job 1 in the YBVTP

Job 1 in the ZBP