Joshua 11 (BOKCV)

1 Ikawa Yabini mfalme wa Hazori aliposikia habari za mambo haya, akatuma ujumbe kwa Yobabu mfalme wa Madoni, na kwa mfalme wa Shimroni, na kwa mfalme wa Akishafu, 2 na pia kwa wafalme wa upande wa kaskazini wale waliokuwa milimani, katika Araba upande wa kusini mwa Kinerethi, kwenye shefela, upande wa magharibi na katika miinuko ya Nafoth-Dori upande wa magharibi; 3 kwa Wakanaani upande wa mashariki na magharibi; kwa Waamori, Wahiti, Waperizi na Wayebusi katika nchi ya vilima; na kwa Wahivi chini ya Hermoni katika eneo ya Mispa. 4 Wakaja na vikosi vyao vyote na hesabu kubwa ya farasi na magari ya kuvutwa na farasi, jeshi kubwa, kama wingi wa mchanga ulio pwani ya bahari. 5 Wafalme hawa wote wakaunganisha majeshi yao na kupiga kambi pamoja kwenye Maji ya Meromu, ili kupigana dhidi ya Israeli. 6 BWANA akamwambia Yoshua, “Usiwaogope, kwa sababu kesho saa kama hii nitawatia wote mikononi mwa Israeli, wakiwa wameuawa. Utakata mishipa ya nyuma ya miguu ya farasi wao na kuyachoma moto magari yao ya vita.” 7 Hivyo Yoshua pamoja na jeshi lake lote wakaja dhidi yao ghafula kwenye Maji ya Meromu kuwashambulia, 8 naye BWANA akawatia mikononi mwa Israeli. Wakawashinda na kuwafukuza hadi Sidoni Kuu na kuwafikisha Misrefoth-Maimu, hadi Bonde la Mispa upande wa mashariki, hadi pakawa hakuna yeyote aliyebaki. 9 Yoshua akawatendea kama BWANA alivyoamuru. Akakata mishipa ya nyuma ya miguu ya farasi wao na kuchoma moto magari yao ya vita. 10 Wakati huo Yoshua akarudi na kuuteka mji wa Hazori na kumuua mfalme wake kwa upanga. (Hazori ulikuwa mji mkuu wa falme hizo zote.) 11 Kila aliyekuwa ndani yake wakamuua kwa upanga. Wakawaangamiza kabisa, wala hawakusaza chochote chenye pumzi na akauchoma Hazori kwenyewe kwa moto. 12 Yoshua akaiteka hii miji yote ya kifalme pamoja na wafalme wake na kuwapiga kwa upanga. Akawaangamiza kabisa wote, jinsi Mose mtumishi wa BWANA alivyowaagiza. 13 Lakini Israeli hawakuichoma moto hata mojawapo ya miji iliyojengwa katika vilima vyao vidogo isipokuwa mji wa Hazori ambao Yoshua aliuchoma moto. 14 Waisraeli wakajichukulia nyara zote na mifugo yote ya miji hii, bali waliwaua watu wote kwa upanga hadi walipowaangamiza kabisa, pasipo kumbakiza yeyote mwenye pumzi. 15 Kama vile BWANA alivyomwagiza Mose mtumishi wake, vivyo hivyo Mose alimwagiza Yoshua, naye Yoshua akafanya kama vivyo, hakukosa kufanya lolote katika yale yote BWANA aliyomwagiza Mose. 16 Yoshua akaiteka nchi hii yote: nchi ya vilima, Negebu yote, eneo yote ya Gosheni, shefela ya upande wa magharibi, Araba na milima ya Israeli pamoja na shefela zao, 17 kuanzia Mlima Halaki ambao umeinuka kuelekea Seiri hadi Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni chini ya Mlima Hermoni. Akawateka wafalme wake wote, akawapiga na kuwaua. 18 Yoshua akapigana vita dhidi ya wafalme hawa wote kwa muda mrefu. 19 Hakuna mji wowote katika eneo hili uliofanya mkataba wa amani na Israeli, isipokuwa hao Wahivi wa Gibeoni. Wengine wote walishindwa katika vita. 20 Kwa maana BWANA mwenyewe ndiye aliifanya mioyo yao iwe migumu, ili kupigana vita dhidi ya Israeli ili apate kuwafutilia mbali pasipo huruma, kama BWANA alivyomwagiza Mose. 21 Wakati huo Yoshua akaenda kuwaangamiza Waanaki kutoka nchi ya vilima: kuanzia Hebroni, Debiri na Anabu, na kutoka nchi yote ya vilima ya Yuda na kutoka nchi yote ya vilima ya Israeli. Yoshua akawaangamiza kabisa pamoja na miji yao. 22 Hawakubaki Waanaki wowote katika nchi ya Israeli, ila tu katika nchi ya Gaza, Gathi na Ashdodi. 23 Hivyo Yoshua akaiteka nchi hiyo yote kama vile BWANA alivyokuwa amemwagiza Mose, naye Yoshua akawapa Israeli kuwa urithi wao, kulingana na walivyogawanyika katika kabila zao.Ndipo nchi ikawa na amani bila vita.

In Other Versions

Joshua 11 in the ANGEFD

Joshua 11 in the ANTPNG2D

Joshua 11 in the AS21

Joshua 11 in the BAGH

Joshua 11 in the BBPNG

Joshua 11 in the BBT1E

Joshua 11 in the BDS

Joshua 11 in the BEV

Joshua 11 in the BHAD

Joshua 11 in the BIB

Joshua 11 in the BLPT

Joshua 11 in the BNT

Joshua 11 in the BNTABOOT

Joshua 11 in the BNTLV

Joshua 11 in the BOATCB

Joshua 11 in the BOATCB2

Joshua 11 in the BOBCV

Joshua 11 in the BOCNT

Joshua 11 in the BOECS

Joshua 11 in the BOGWICC

Joshua 11 in the BOHCB

Joshua 11 in the BOHCV

Joshua 11 in the BOHLNT

Joshua 11 in the BOHNTLTAL

Joshua 11 in the BOICB

Joshua 11 in the BOILNTAP

Joshua 11 in the BOITCV

Joshua 11 in the BOKCV2

Joshua 11 in the BOKHWOG

Joshua 11 in the BOKSSV

Joshua 11 in the BOLCB

Joshua 11 in the BOLCB2

Joshua 11 in the BOMCV

Joshua 11 in the BONAV

Joshua 11 in the BONCB

Joshua 11 in the BONLT

Joshua 11 in the BONUT2

Joshua 11 in the BOPLNT

Joshua 11 in the BOSCB

Joshua 11 in the BOSNC

Joshua 11 in the BOTLNT

Joshua 11 in the BOVCB

Joshua 11 in the BOYCB

Joshua 11 in the BPBB

Joshua 11 in the BPH

Joshua 11 in the BSB

Joshua 11 in the CCB

Joshua 11 in the CUV

Joshua 11 in the CUVS

Joshua 11 in the DBT

Joshua 11 in the DGDNT

Joshua 11 in the DHNT

Joshua 11 in the DNT

Joshua 11 in the ELBE

Joshua 11 in the EMTV

Joshua 11 in the ESV

Joshua 11 in the FBV

Joshua 11 in the FEB

Joshua 11 in the GGMNT

Joshua 11 in the GNT

Joshua 11 in the HARY

Joshua 11 in the HNT

Joshua 11 in the IRVA

Joshua 11 in the IRVB

Joshua 11 in the IRVG

Joshua 11 in the IRVH

Joshua 11 in the IRVK

Joshua 11 in the IRVM

Joshua 11 in the IRVM2

Joshua 11 in the IRVO

Joshua 11 in the IRVP

Joshua 11 in the IRVT

Joshua 11 in the IRVT2

Joshua 11 in the IRVU

Joshua 11 in the ISVN

Joshua 11 in the JSNT

Joshua 11 in the KAPI

Joshua 11 in the KBT1ETNIK

Joshua 11 in the KBV

Joshua 11 in the KJV

Joshua 11 in the KNFD

Joshua 11 in the LBA

Joshua 11 in the LBLA

Joshua 11 in the LNT

Joshua 11 in the LSV

Joshua 11 in the MAAL

Joshua 11 in the MBV

Joshua 11 in the MBV2

Joshua 11 in the MHNT

Joshua 11 in the MKNFD

Joshua 11 in the MNG

Joshua 11 in the MNT

Joshua 11 in the MNT2

Joshua 11 in the MRS1T

Joshua 11 in the NAA

Joshua 11 in the NASB

Joshua 11 in the NBLA

Joshua 11 in the NBS

Joshua 11 in the NBVTP

Joshua 11 in the NET2

Joshua 11 in the NIV11

Joshua 11 in the NNT

Joshua 11 in the NNT2

Joshua 11 in the NNT3

Joshua 11 in the PDDPT

Joshua 11 in the PFNT

Joshua 11 in the RMNT

Joshua 11 in the SBIAS

Joshua 11 in the SBIBS

Joshua 11 in the SBIBS2

Joshua 11 in the SBICS

Joshua 11 in the SBIDS

Joshua 11 in the SBIGS

Joshua 11 in the SBIHS

Joshua 11 in the SBIIS

Joshua 11 in the SBIIS2

Joshua 11 in the SBIIS3

Joshua 11 in the SBIKS

Joshua 11 in the SBIKS2

Joshua 11 in the SBIMS

Joshua 11 in the SBIOS

Joshua 11 in the SBIPS

Joshua 11 in the SBISS

Joshua 11 in the SBITS

Joshua 11 in the SBITS2

Joshua 11 in the SBITS3

Joshua 11 in the SBITS4

Joshua 11 in the SBIUS

Joshua 11 in the SBIVS

Joshua 11 in the SBT

Joshua 11 in the SBT1E

Joshua 11 in the SCHL

Joshua 11 in the SNT

Joshua 11 in the SUSU

Joshua 11 in the SUSU2

Joshua 11 in the SYNO

Joshua 11 in the TBIAOTANT

Joshua 11 in the TBT1E

Joshua 11 in the TBT1E2

Joshua 11 in the TFTIP

Joshua 11 in the TFTU

Joshua 11 in the TGNTATF3T

Joshua 11 in the THAI

Joshua 11 in the TNFD

Joshua 11 in the TNT

Joshua 11 in the TNTIK

Joshua 11 in the TNTIL

Joshua 11 in the TNTIN

Joshua 11 in the TNTIP

Joshua 11 in the TNTIZ

Joshua 11 in the TOMA

Joshua 11 in the TTENT

Joshua 11 in the UBG

Joshua 11 in the UGV

Joshua 11 in the UGV2

Joshua 11 in the UGV3

Joshua 11 in the VBL

Joshua 11 in the VDCC

Joshua 11 in the YALU

Joshua 11 in the YAPE

Joshua 11 in the YBVTP

Joshua 11 in the ZBP