Joshua 17 (BOKCV)
1 Huu ndio mgawo wa kabila la Manase kama mzaliwa wa kwanza wa Yosefu, yaani kwa ajili ya Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase. Makiri alikuwa baba wa Wagileadi, ambao walipokea Gileadi na Bashani kwa sababu Wamakiri walikuwa askari wakuu. 2 Kwa hiyo mgawo huu ulikuwa kwa ajili ya watu wa Manase waliokuwa wamebaki, ambao ni koo za Abiezeri, Heleki, Asirieli, Shekemu, Heferi na Shemida. Hawa ndio wanaume wale wengine wa uzao wa Manase mwana wa Yosefu kwa koo zao. 3 Basi Selofehadi mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase hakuwa na wana waume ila mabinti tu, ambao majina yao yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa. 4 Wakamwendea kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi, wakasema: “BWANA alimwagiza Mose atupatie urithi miongoni mwa ndugu zetu.” Kwa hiyo Yoshua akawapa urithi pamoja na ndugu wa baba yao, kufuatana na agizo la BWANA. 5 Fungu la Manase lilikuwa na sehemu kumi za nchi, licha ya Gileadi na Bashani mashariki mwa Yordani, 6 kwa sababu wale binti za kabila la Manase walipokea urithi miongoni mwa wana wa kiume. Nchi ya Gileadi ilikuwa mali ya wazao wa Manase waliobaki. 7 Eneo la Manase lilienea kuanzia Asheri hadi Mikmeta mashariki mwa Shekemu. Mpaka ule ulielekea upande wa kusini kutoka pale kujumuisha watu walioishi En-Tapua. 8 (Nchi ya Tapua ilikuwa mali ya Manase, lakini Tapua yenyewe iliyo mpakani mwa nchi ya Manase ilikuwa ya Waefraimu.) 9 Kisha mpaka ule uliendelea kuelekea kusini hadi Bonde la Kana. Kulikuwepo miji ya Efraimu iliyokuwa miongoni mwa miji ya Manase, lakini mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa lile bonde na kuishia kwenye bahari. 10 Nchi ya kusini ilikuwa ya Efraimu, na ile iliyokuwa upande wa kaskazini ilikuwa ya Manase. Eneo la Manase lilifika bahari na ikapakana na Asheri upande wa kaskazini, na Isakari upande wa mashariki. 11 Katika Isakari na Asheri Manase alikuwa na miji pia: Beth-Shani, Ibleamu na watu wa Dori, Endori, Taanaki na Megido, pamoja na vijiji vyote vinavyohusika na miji hiyo (ya tatu katika orodha ni Nafothi). 12 Lakini Wamanase hawakuweza kuimiliki miji hii, kwa kuwa Wakanaani walikazana kuishi katika maeneo hayo. 13 Hata hivyo, Waisraeli walivyoendelea kupata nguvu waliwatumikisha Wakanaani na kuwatia katika kazi za kulazimishwa, lakini hawakuwafukuza kabisa. 14 Watu wa Yosefu wakamwambia Yoshua, “Kwa nini umetupa sisi mgawo mmoja tu na sehemu moja tu kuwa urithi? Sisi tu watu wengi sana, na BWANA ametubariki kwa wingi.” 15 Yoshua akajibu, “Kama ninyi ni wengi sana, na kama nchi ya vilima ya Efraimu ni ndogo sana kwenu, pandeni msituni mkafyeke eneo kwa ajili yenu wenyewe huko kwenye nchi ya Waperizi na Warefai.” 16 Watu wa Yosefu wakajibu, “Hiyo nchi ya vilima haitutoshi, nao Wakanaani wote wanaoishi katika tambarare wanayo magari ya vita ya chuma, wote wa Beth-Shani na miji yake, na wale walio katika Bonde la Yezreeli.” 17 Lakini Yoshua akanena na nyumba ya Yosefu, yaani Efraimu na Manase: “Ninyi ni wengi sana na wenye nguvu sana. Hamtakuwa na mgawo mmoja tu, 18 bali pia nchi hii ya kilima yenye msitu. Ifyekeni, nayo mipaka yake itakuwa yenu umbali mtakaoweza kufika. Ingawa Wakanaani wana magari ya chuma, nao wana nguvu, mwaweza kuwafukuza humo.”
In Other Versions
Joshua 17 in the ANGEFD
Joshua 17 in the ANTPNG2D
Joshua 17 in the AS21
Joshua 17 in the BAGH
Joshua 17 in the BBPNG
Joshua 17 in the BBT1E
Joshua 17 in the BDS
Joshua 17 in the BEV
Joshua 17 in the BHAD
Joshua 17 in the BIB
Joshua 17 in the BLPT
Joshua 17 in the BNT
Joshua 17 in the BNTABOOT
Joshua 17 in the BNTLV
Joshua 17 in the BOATCB
Joshua 17 in the BOATCB2
Joshua 17 in the BOBCV
Joshua 17 in the BOCNT
Joshua 17 in the BOECS
Joshua 17 in the BOGWICC
Joshua 17 in the BOHCB
Joshua 17 in the BOHCV
Joshua 17 in the BOHLNT
Joshua 17 in the BOHNTLTAL
Joshua 17 in the BOICB
Joshua 17 in the BOILNTAP
Joshua 17 in the BOITCV
Joshua 17 in the BOKCV2
Joshua 17 in the BOKHWOG
Joshua 17 in the BOKSSV
Joshua 17 in the BOLCB
Joshua 17 in the BOLCB2
Joshua 17 in the BOMCV
Joshua 17 in the BONAV
Joshua 17 in the BONCB
Joshua 17 in the BONLT
Joshua 17 in the BONUT2
Joshua 17 in the BOPLNT
Joshua 17 in the BOSCB
Joshua 17 in the BOSNC
Joshua 17 in the BOTLNT
Joshua 17 in the BOVCB
Joshua 17 in the BOYCB
Joshua 17 in the BPBB
Joshua 17 in the BPH
Joshua 17 in the BSB
Joshua 17 in the CCB
Joshua 17 in the CUV
Joshua 17 in the CUVS
Joshua 17 in the DBT
Joshua 17 in the DGDNT
Joshua 17 in the DHNT
Joshua 17 in the DNT
Joshua 17 in the ELBE
Joshua 17 in the EMTV
Joshua 17 in the ESV
Joshua 17 in the FBV
Joshua 17 in the FEB
Joshua 17 in the GGMNT
Joshua 17 in the GNT
Joshua 17 in the HARY
Joshua 17 in the HNT
Joshua 17 in the IRVA
Joshua 17 in the IRVB
Joshua 17 in the IRVG
Joshua 17 in the IRVH
Joshua 17 in the IRVK
Joshua 17 in the IRVM
Joshua 17 in the IRVM2
Joshua 17 in the IRVO
Joshua 17 in the IRVP
Joshua 17 in the IRVT
Joshua 17 in the IRVT2
Joshua 17 in the IRVU
Joshua 17 in the ISVN
Joshua 17 in the JSNT
Joshua 17 in the KAPI
Joshua 17 in the KBT1ETNIK
Joshua 17 in the KBV
Joshua 17 in the KJV
Joshua 17 in the KNFD
Joshua 17 in the LBA
Joshua 17 in the LBLA
Joshua 17 in the LNT
Joshua 17 in the LSV
Joshua 17 in the MAAL
Joshua 17 in the MBV
Joshua 17 in the MBV2
Joshua 17 in the MHNT
Joshua 17 in the MKNFD
Joshua 17 in the MNG
Joshua 17 in the MNT
Joshua 17 in the MNT2
Joshua 17 in the MRS1T
Joshua 17 in the NAA
Joshua 17 in the NASB
Joshua 17 in the NBLA
Joshua 17 in the NBS
Joshua 17 in the NBVTP
Joshua 17 in the NET2
Joshua 17 in the NIV11
Joshua 17 in the NNT
Joshua 17 in the NNT2
Joshua 17 in the NNT3
Joshua 17 in the PDDPT
Joshua 17 in the PFNT
Joshua 17 in the RMNT
Joshua 17 in the SBIAS
Joshua 17 in the SBIBS
Joshua 17 in the SBIBS2
Joshua 17 in the SBICS
Joshua 17 in the SBIDS
Joshua 17 in the SBIGS
Joshua 17 in the SBIHS
Joshua 17 in the SBIIS
Joshua 17 in the SBIIS2
Joshua 17 in the SBIIS3
Joshua 17 in the SBIKS
Joshua 17 in the SBIKS2
Joshua 17 in the SBIMS
Joshua 17 in the SBIOS
Joshua 17 in the SBIPS
Joshua 17 in the SBISS
Joshua 17 in the SBITS
Joshua 17 in the SBITS2
Joshua 17 in the SBITS3
Joshua 17 in the SBITS4
Joshua 17 in the SBIUS
Joshua 17 in the SBIVS
Joshua 17 in the SBT
Joshua 17 in the SBT1E
Joshua 17 in the SCHL
Joshua 17 in the SNT
Joshua 17 in the SUSU
Joshua 17 in the SUSU2
Joshua 17 in the SYNO
Joshua 17 in the TBIAOTANT
Joshua 17 in the TBT1E
Joshua 17 in the TBT1E2
Joshua 17 in the TFTIP
Joshua 17 in the TFTU
Joshua 17 in the TGNTATF3T
Joshua 17 in the THAI
Joshua 17 in the TNFD
Joshua 17 in the TNT
Joshua 17 in the TNTIK
Joshua 17 in the TNTIL
Joshua 17 in the TNTIN
Joshua 17 in the TNTIP
Joshua 17 in the TNTIZ
Joshua 17 in the TOMA
Joshua 17 in the TTENT
Joshua 17 in the UBG
Joshua 17 in the UGV
Joshua 17 in the UGV2
Joshua 17 in the UGV3
Joshua 17 in the VBL
Joshua 17 in the VDCC
Joshua 17 in the YALU
Joshua 17 in the YAPE
Joshua 17 in the YBVTP
Joshua 17 in the ZBP