Joshua 2 (BOKCV)

1 Kisha Yoshua mwana wa Nuni kwa siri akawatuma wapelelezi wawili kutoka Shitimu, akawaambia, “Nendeni mkaikague hiyo nchi, hasa Yeriko.” Kwa hiyo wakaenda na kuingia kwenye nyumba ya kahaba mmoja jina lake Rahabu na kukaa humo. 2 Mfalme wa Yeriko akaambiwa, “Tazama! Baadhi ya Waisraeli wamekuja huku usiku huu kuipeleleza nchi.” 3 Hivyo mfalme wa Yeriko akatuma huu ujumbe kwa Rahabu: “Watoe wale watu waliokujia na kuingia nyumbani mwako, kwa sababu wamekuja kuipeleleza nchi yote.” 4 Lakini huyo mwanamke alikuwa amewachukua hao watu wawili na kuwaficha. Akasema, “Naam, watu hao walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka. 5 Kulipoingia giza, wakati wa kufunga lango la mji, watu hao waliondoka. Sijui njia waliyoiendea. Wafuatilieni haraka. Huenda mkawapata.” 6 (Lakini alikuwa amewapandisha darini akawafunika kwa mabua ya kitani aliyokuwa ameyatandika darini.) 7 Basi hao watu wakaondoka kuwafuatilia hao wapelelezi katika njia ile inayoelekea vivuko vya Yordani, mara tu wafuatiliaji walipotoka nje, lango likafungwa. 8 Kabla wale wapelelezi hawajalala, Rahabu akawaendea huko juu darini, 9 akawaambia, “Ninajua kuwa BWANA amewapa nchi hii na hofu kuu imetuangukia kwa sababu yenu, kiasi kwamba wote waishio katika nchi hii wanayeyuka kwa hofu kwa sababu yenu. 10 Tumesikia jinsi BWANA alivyokausha maji ya Bahari ya Shamu kwa ajili yenu mlipotoka Misri, pia lile mlilowatendea Sihoni na Ogu, wafalme wawili wa Waamori mashariki mwa Yordani, ambao mliwaangamiza kabisa. 11 Tuliposikia juu ya hili, mioyo yetu iliyeyuka na kila mmoja alikosa ujasiri kwa sababu yenu, kwa maana BWANA Mungu wenu ni Mungu juu mbinguni na duniani chini. 12 Sasa basi, tafadhali niapieni kwa BWANA, kwamba mtaitendea hisani jamaa ya baba yangu, kwa kuwa mimi nimewatendea hisani. Nipeni ishara ya uaminifu 13 kwamba mtayahifadhi maisha ya baba yangu na mama yangu, ndugu zangu wa kiume na wa kike, pamoja na wale wote walio wa kwao na kwamba mtatuokoa na kifo.” 14 Wale watu wakamhakikishia Rahabu, “Uhai wetu kwa uhai wenu! Ikiwa hutatoa habari ya nini tunachofanya, wakati BWANA atakapotupa nchi hii, tutawatendea kwa hisani na kwa uaminifu.” 15 Kisha akawateremsha dirishani kwa kamba, kwa kuwa nyumba yake aliyokuwa anaishi ilikuwa sehemu ya ukuta wa mji. 16 Alikuwa amewaambia, “Nendeni vilimani ili wale wafuatiliaji wasiwapate. Jificheni huko kwa siku tatu mpaka watakaporudi, hatimaye mwende zenu.” 17 Wale watu wakamwambia, “Hiki kiapo ulichotuapisha hakitatufunga, 18 isipokuwa, hapo tutakapoingia katika nchi hii, utakuwa umefunga hii kamba nyekundu dirishani pale ulipotuteremshia na kama utakuwa umewaleta baba yako na mama yako, ndugu zako na jamaa yako yote ndani ya nyumba yako. 19 Ikiwa mtu yeyote atatoka nje ya nyumba yako akaenda mtaani, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe, hatutawajibika. Lakini yule ambaye atakuwa ndani pamoja nawe, kama mkono wa mtu yeyote ukiwa juu yake damu yake itakuwa juu ya vichwa vyetu. 20 Lakini ikiwa utatoa habari ya shughuli yetu tunayofanya, tutakuwa tumefunguliwa kutoka kwenye kiapo hiki ulichotufanya tuape.” 21 Naye akajibu, “Nimekubali. Na iwe kama mnavyosema.” Kwa hiyo akaagana nao, nao wakaondoka. Yeye akaifunga ile kamba nyekundu dirishani. 22 Walipoondoka, wakaelekea vilimani na kukaa huko siku tatu, hadi wale waliokuwa wakiwafuatilia wakawa wamewatafuta njia nzima na kurudi pasipo kuwapata. 23 Ndipo wale watu wawili wakaanza kurudi. Wakashuka kutoka kule vilimani, wakavuka mto na kuja kwa Yoshua mwana wa Nuni, na kumweleza kila kitu kilichowapata. 24 Wakamwambia Yoshua, “Hakika BWANA ametupa nchi yote mikononi mwetu; watu wote wanayeyuka kwa hofu kwa sababu yetu.”

In Other Versions

Joshua 2 in the ANGEFD

Joshua 2 in the ANTPNG2D

Joshua 2 in the AS21

Joshua 2 in the BAGH

Joshua 2 in the BBPNG

Joshua 2 in the BBT1E

Joshua 2 in the BDS

Joshua 2 in the BEV

Joshua 2 in the BHAD

Joshua 2 in the BIB

Joshua 2 in the BLPT

Joshua 2 in the BNT

Joshua 2 in the BNTABOOT

Joshua 2 in the BNTLV

Joshua 2 in the BOATCB

Joshua 2 in the BOATCB2

Joshua 2 in the BOBCV

Joshua 2 in the BOCNT

Joshua 2 in the BOECS

Joshua 2 in the BOGWICC

Joshua 2 in the BOHCB

Joshua 2 in the BOHCV

Joshua 2 in the BOHLNT

Joshua 2 in the BOHNTLTAL

Joshua 2 in the BOICB

Joshua 2 in the BOILNTAP

Joshua 2 in the BOITCV

Joshua 2 in the BOKCV2

Joshua 2 in the BOKHWOG

Joshua 2 in the BOKSSV

Joshua 2 in the BOLCB

Joshua 2 in the BOLCB2

Joshua 2 in the BOMCV

Joshua 2 in the BONAV

Joshua 2 in the BONCB

Joshua 2 in the BONLT

Joshua 2 in the BONUT2

Joshua 2 in the BOPLNT

Joshua 2 in the BOSCB

Joshua 2 in the BOSNC

Joshua 2 in the BOTLNT

Joshua 2 in the BOVCB

Joshua 2 in the BOYCB

Joshua 2 in the BPBB

Joshua 2 in the BPH

Joshua 2 in the BSB

Joshua 2 in the CCB

Joshua 2 in the CUV

Joshua 2 in the CUVS

Joshua 2 in the DBT

Joshua 2 in the DGDNT

Joshua 2 in the DHNT

Joshua 2 in the DNT

Joshua 2 in the ELBE

Joshua 2 in the EMTV

Joshua 2 in the ESV

Joshua 2 in the FBV

Joshua 2 in the FEB

Joshua 2 in the GGMNT

Joshua 2 in the GNT

Joshua 2 in the HARY

Joshua 2 in the HNT

Joshua 2 in the IRVA

Joshua 2 in the IRVB

Joshua 2 in the IRVG

Joshua 2 in the IRVH

Joshua 2 in the IRVK

Joshua 2 in the IRVM

Joshua 2 in the IRVM2

Joshua 2 in the IRVO

Joshua 2 in the IRVP

Joshua 2 in the IRVT

Joshua 2 in the IRVT2

Joshua 2 in the IRVU

Joshua 2 in the ISVN

Joshua 2 in the JSNT

Joshua 2 in the KAPI

Joshua 2 in the KBT1ETNIK

Joshua 2 in the KBV

Joshua 2 in the KJV

Joshua 2 in the KNFD

Joshua 2 in the LBA

Joshua 2 in the LBLA

Joshua 2 in the LNT

Joshua 2 in the LSV

Joshua 2 in the MAAL

Joshua 2 in the MBV

Joshua 2 in the MBV2

Joshua 2 in the MHNT

Joshua 2 in the MKNFD

Joshua 2 in the MNG

Joshua 2 in the MNT

Joshua 2 in the MNT2

Joshua 2 in the MRS1T

Joshua 2 in the NAA

Joshua 2 in the NASB

Joshua 2 in the NBLA

Joshua 2 in the NBS

Joshua 2 in the NBVTP

Joshua 2 in the NET2

Joshua 2 in the NIV11

Joshua 2 in the NNT

Joshua 2 in the NNT2

Joshua 2 in the NNT3

Joshua 2 in the PDDPT

Joshua 2 in the PFNT

Joshua 2 in the RMNT

Joshua 2 in the SBIAS

Joshua 2 in the SBIBS

Joshua 2 in the SBIBS2

Joshua 2 in the SBICS

Joshua 2 in the SBIDS

Joshua 2 in the SBIGS

Joshua 2 in the SBIHS

Joshua 2 in the SBIIS

Joshua 2 in the SBIIS2

Joshua 2 in the SBIIS3

Joshua 2 in the SBIKS

Joshua 2 in the SBIKS2

Joshua 2 in the SBIMS

Joshua 2 in the SBIOS

Joshua 2 in the SBIPS

Joshua 2 in the SBISS

Joshua 2 in the SBITS

Joshua 2 in the SBITS2

Joshua 2 in the SBITS3

Joshua 2 in the SBITS4

Joshua 2 in the SBIUS

Joshua 2 in the SBIVS

Joshua 2 in the SBT

Joshua 2 in the SBT1E

Joshua 2 in the SCHL

Joshua 2 in the SNT

Joshua 2 in the SUSU

Joshua 2 in the SUSU2

Joshua 2 in the SYNO

Joshua 2 in the TBIAOTANT

Joshua 2 in the TBT1E

Joshua 2 in the TBT1E2

Joshua 2 in the TFTIP

Joshua 2 in the TFTU

Joshua 2 in the TGNTATF3T

Joshua 2 in the THAI

Joshua 2 in the TNFD

Joshua 2 in the TNT

Joshua 2 in the TNTIK

Joshua 2 in the TNTIL

Joshua 2 in the TNTIN

Joshua 2 in the TNTIP

Joshua 2 in the TNTIZ

Joshua 2 in the TOMA

Joshua 2 in the TTENT

Joshua 2 in the UBG

Joshua 2 in the UGV

Joshua 2 in the UGV2

Joshua 2 in the UGV3

Joshua 2 in the VBL

Joshua 2 in the VDCC

Joshua 2 in the YALU

Joshua 2 in the YAPE

Joshua 2 in the YBVTP

Joshua 2 in the ZBP