Malachi 2 (BOKCV)

1 “Sasa onyo hili ni kwa ajili yenu, enyi makuhani. 2 Kama hamtasikiliza, na kama hamtaki kuielekeza mioyo yenu kuheshimu Jina langu, nitatuma laana juu yenu, nami nitalaani baraka zenu. Naam, nimekwisha kuzilaani, kwa sababu hamkuielekeza mioyo yenu kuniheshimu mimi,” Asema BWANA Mwenye Nguvu Zote. 3 “Kwa sababu yenu nitawakatilia mbali wazao wenu. Nitazipaka nyuso zenu mavi, mavi ya dhabihu zenu. Nanyi mtafukuzwa pamoja nazo mtoke mbele zangu. 4 Nanyi mtajua kuwa nimewapelekea onyo hili ili kwamba Agano langu na Lawi lipate kuendelea,” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote. 5 “Agano langu lilikuwa pamoja naye, agano la uhai na amani, nami nilimpa yote, ili aniche na kuniheshimu, naye akaniheshimu na kusimama akilicha Jina langu. 6 Fundisho la kweli lilikuwa kinywani mwake, wala hakuna uongo wowote uliopatikana katika midomo yake. Alitembea nami katika amani na unyofu, naye akawageuza wengi kutoka dhambini. 7 “Kwa maana yapasa midomo ya kuhani kuhifadhi maarifa. Tena kutoka kinywani mwake watu wangepaswa kutafuta mafundisho, kwa sababu yeye ni mjumbe wa BWANA Mwenye Nguvu Zote. 8 Lakini mmegeuka mkaiacha njia, na kwa mafundisho yenu mmesababisha wengi kujikwaa. Mmevunja agano na Lawi,” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote. 9 “Kwa hiyo nimewasababisha ninyi kudharauliwa na kufedheheshwa mbele ya watu wote, kwa sababu hamkufuata njia zangu, bali mmeonyesha upendeleo katika mambo ya sheria.” 10 Je, sote hatuna Baba mmoja? Hatukuumbwa na Mungu mmoja? Kwa nini basi tunalinajisi Agano la baba zetu kwa kukosa uaminifu kila mmoja kwa mwenzake? 11 Yuda amevunja uaminifu. Jambo la kuchukiza limetendeka katika Israeli na katika Yerusalemu: Yuda amepanajisi mahali patakatifu apendapo BWANA, kwa kuoa binti wa mungu mgeni. 12 Kwa maana kwa mtu yeyote atendaye jambo hili, BWANA na amkatilie mbali kutoka hema za Yakobo, hata kama huwa anamletea BWANA Mwenye Nguvu Zote sadaka. 13 Kitu kingine mnachokifanya: Mnaifurikisha madhabahu ya BWANA kwa machozi. Mnalia na kuugua kwa sababu yeye haziangalii tena sadaka zenu wala hazikubali kwa furaha kutoka mikononi mwenu. 14 Mnauliza, “Kwa nini?” Ni kwa sababu BWANA ni shahidi kati yako na mke wa ujana wako, kwa sababu umevunja uaminifu naye, ingawa yeye ni mwenzako, mke wa agano lako la ndoa. 15 Je, BWANA hakuwafanya wao kuwa mmoja? Katika mwili na katika roho wao ni wa Mungu. Kwa nini wawe mmoja? Kwa sababu Mungu alikuwa akitafuta mzao mwenye kumcha Mungu. Kwa hiyo jihadharini wenyewe katika roho zenu, mtu asivunje uaminifu kwa mke wa ujana wake. 16 “Ninachukia kuachana,” asema BWANA, Mungu wa Israeli, “pia nachukia mtu anayejivika jeuri kama vazi,” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote.Kwa hiyo jihadharini wenyewe katika roho zenu, wala msije mkavunja uaminifu. 17 Mmemchosha BWANA kwa maneno yenu.Nanyi mnauliza, “Tumemchosha kwa namna gani?”Mmemchosha kwa kusema, “Wote watendao mabaya ni wema machoni pa BWANA, naye anapendezwa nao” au “Mungu wa haki yuko wapi?”

In Other Versions

Malachi 2 in the ANGEFD

Malachi 2 in the ANTPNG2D

Malachi 2 in the AS21

Malachi 2 in the BAGH

Malachi 2 in the BBPNG

Malachi 2 in the BBT1E

Malachi 2 in the BDS

Malachi 2 in the BEV

Malachi 2 in the BHAD

Malachi 2 in the BIB

Malachi 2 in the BLPT

Malachi 2 in the BNT

Malachi 2 in the BNTABOOT

Malachi 2 in the BNTLV

Malachi 2 in the BOATCB

Malachi 2 in the BOATCB2

Malachi 2 in the BOBCV

Malachi 2 in the BOCNT

Malachi 2 in the BOECS

Malachi 2 in the BOGWICC

Malachi 2 in the BOHCB

Malachi 2 in the BOHCV

Malachi 2 in the BOHLNT

Malachi 2 in the BOHNTLTAL

Malachi 2 in the BOICB

Malachi 2 in the BOILNTAP

Malachi 2 in the BOITCV

Malachi 2 in the BOKCV2

Malachi 2 in the BOKHWOG

Malachi 2 in the BOKSSV

Malachi 2 in the BOLCB

Malachi 2 in the BOLCB2

Malachi 2 in the BOMCV

Malachi 2 in the BONAV

Malachi 2 in the BONCB

Malachi 2 in the BONLT

Malachi 2 in the BONUT2

Malachi 2 in the BOPLNT

Malachi 2 in the BOSCB

Malachi 2 in the BOSNC

Malachi 2 in the BOTLNT

Malachi 2 in the BOVCB

Malachi 2 in the BOYCB

Malachi 2 in the BPBB

Malachi 2 in the BPH

Malachi 2 in the BSB

Malachi 2 in the CCB

Malachi 2 in the CUV

Malachi 2 in the CUVS

Malachi 2 in the DBT

Malachi 2 in the DGDNT

Malachi 2 in the DHNT

Malachi 2 in the DNT

Malachi 2 in the ELBE

Malachi 2 in the EMTV

Malachi 2 in the ESV

Malachi 2 in the FBV

Malachi 2 in the FEB

Malachi 2 in the GGMNT

Malachi 2 in the GNT

Malachi 2 in the HARY

Malachi 2 in the HNT

Malachi 2 in the IRVA

Malachi 2 in the IRVB

Malachi 2 in the IRVG

Malachi 2 in the IRVH

Malachi 2 in the IRVK

Malachi 2 in the IRVM

Malachi 2 in the IRVM2

Malachi 2 in the IRVO

Malachi 2 in the IRVP

Malachi 2 in the IRVT

Malachi 2 in the IRVT2

Malachi 2 in the IRVU

Malachi 2 in the ISVN

Malachi 2 in the JSNT

Malachi 2 in the KAPI

Malachi 2 in the KBT1ETNIK

Malachi 2 in the KBV

Malachi 2 in the KJV

Malachi 2 in the KNFD

Malachi 2 in the LBA

Malachi 2 in the LBLA

Malachi 2 in the LNT

Malachi 2 in the LSV

Malachi 2 in the MAAL

Malachi 2 in the MBV

Malachi 2 in the MBV2

Malachi 2 in the MHNT

Malachi 2 in the MKNFD

Malachi 2 in the MNG

Malachi 2 in the MNT

Malachi 2 in the MNT2

Malachi 2 in the MRS1T

Malachi 2 in the NAA

Malachi 2 in the NASB

Malachi 2 in the NBLA

Malachi 2 in the NBS

Malachi 2 in the NBVTP

Malachi 2 in the NET2

Malachi 2 in the NIV11

Malachi 2 in the NNT

Malachi 2 in the NNT2

Malachi 2 in the NNT3

Malachi 2 in the PDDPT

Malachi 2 in the PFNT

Malachi 2 in the RMNT

Malachi 2 in the SBIAS

Malachi 2 in the SBIBS

Malachi 2 in the SBIBS2

Malachi 2 in the SBICS

Malachi 2 in the SBIDS

Malachi 2 in the SBIGS

Malachi 2 in the SBIHS

Malachi 2 in the SBIIS

Malachi 2 in the SBIIS2

Malachi 2 in the SBIIS3

Malachi 2 in the SBIKS

Malachi 2 in the SBIKS2

Malachi 2 in the SBIMS

Malachi 2 in the SBIOS

Malachi 2 in the SBIPS

Malachi 2 in the SBISS

Malachi 2 in the SBITS

Malachi 2 in the SBITS2

Malachi 2 in the SBITS3

Malachi 2 in the SBITS4

Malachi 2 in the SBIUS

Malachi 2 in the SBIVS

Malachi 2 in the SBT

Malachi 2 in the SBT1E

Malachi 2 in the SCHL

Malachi 2 in the SNT

Malachi 2 in the SUSU

Malachi 2 in the SUSU2

Malachi 2 in the SYNO

Malachi 2 in the TBIAOTANT

Malachi 2 in the TBT1E

Malachi 2 in the TBT1E2

Malachi 2 in the TFTIP

Malachi 2 in the TFTU

Malachi 2 in the TGNTATF3T

Malachi 2 in the THAI

Malachi 2 in the TNFD

Malachi 2 in the TNT

Malachi 2 in the TNTIK

Malachi 2 in the TNTIL

Malachi 2 in the TNTIN

Malachi 2 in the TNTIP

Malachi 2 in the TNTIZ

Malachi 2 in the TOMA

Malachi 2 in the TTENT

Malachi 2 in the UBG

Malachi 2 in the UGV

Malachi 2 in the UGV2

Malachi 2 in the UGV3

Malachi 2 in the VBL

Malachi 2 in the VDCC

Malachi 2 in the YALU

Malachi 2 in the YAPE

Malachi 2 in the YBVTP

Malachi 2 in the ZBP