Nehemiah 2 (BOKCV)
1 Katika mwezi wa Nisani mwaka wa ishirini wa utawala wa Mfalme Artashasta, wakati divai ilipoletwa kwake, niliichukua na kumpa mfalme. Sikuwahi kuonekana mwenye huzuni mbele yake kabla ya hapo. 2 Basi mfalme akaniuliza, “Kwa nini uso wako unaonekana una huzuni wakati wewe si mgonjwa? Jambo hili si kitu kingine bali ni huzuni ya moyo.”Niliogopa sana, 3 lakini nikamwambia mfalme, “Mfalme na aishi milele! Kwa nini uso wangu usiwe na huzuni wakati mji walipozikwa baba zangu umebaki magofu, na malango yake yameteketezwa kwa moto?” 4 Mfalme akaniambia, “Je, haja yako ni gani?”Ndipo nikaomba kwa Mungu wa mbinguni, 5 na nikamjibu mfalme, “Kama ikimpendeza mfalme, na kama mtumishi wako amepata kibali machoni pake, anitume kule mji wa Yuda, mahali baba zangu walipozikwa, ili niweze kuujenga upya.” 6 Kisha mfalme, na malkia akiwa ameketi karibu naye, akaniuliza, “Safari yako itachukua muda gani, nawe utarudi lini?” Ilimpendeza mfalme kunituma, kwa hiyo nikapanga muda. 7 Pia nikamwambia, “Kama ikimpendeza mfalme, naomba nipewe barua kwa watawala wa Ngʼambo ya Frati, ili wanipe ulinzi mpaka nifike Yuda. 8 Naomba nipewe barua nipeleke kwa Asafu, mtunzaji wa msitu wa mfalme, ili anipe miti ya kutengeneza boriti kwa ajili ya malango ya ngome ya Hekalu, na ukuta wa mji, na makao yangu nitakapoishi.” Kwa kuwa mkono wenye neema wa Mungu wangu ulikuwa juu yangu, mfalme akanijalia ombi langu. 9 Basi nilienda kwa watawala wa Ngʼambo ya Frati na kuwapa barua za mfalme. Pia mfalme alikuwa ametuma maafisa wa jeshi na askari wapanda farasi pamoja nami. 10 Sanbalati Mhoroni na Tobia afisa Mwamoni waliposikia juu ya jambo hili, waliudhika sana kwamba amekuja mtu kuinua ustawi wa Waisraeli. 11 Nilienda Yerusalemu, na baada ya kukaa huko siku tatu, 12 nikaondoka wakati wa usiku pamoja na watu wachache. Sikuwa nimemwambia mtu yeyote kile ambacho Mungu wangu alikuwa ameweka moyoni mwangu kufanya kwa ajili ya Yerusalemu. Hapakuwepo na mnyama yeyote pamoja nami isipokuwa yule niliyekuwa nimempanda. 13 Nikatoka nje usiku kupitia Lango la Bondeni, kuelekea Kisima cha Joka na Lango la Samadi, nikikagua kuta za Yerusalemu zilizokuwa zimebomolewa, na malango yake yaliyokuwa yameteketezwa kwa moto. 14 Kisha nikaelekea mpaka Lango la Chemchemi na Bwawa la Mfalme, lakini hapakuwepo nafasi ya kutosha kwa ajili ya mnyama wangu kupita, 15 kwa hiyo nikapandia bondeni usiku nikikagua ukuta. Mwishoni nikarudi na kuingia tena kupitia Lango la Bondeni. 16 Maafisa hawakujua nilikokwenda wala nilichokuwa nikifanya, kwa sababu mpaka sasa nilikuwa bado sijasema lolote kwa Wayahudi, wala makuhani, wala wakuu, wala maafisa, wala mtu yeyote ambaye angefanya kazi. 17 Ndipo nilipowaambia, “Mnaona taabu tuliyo nayo: Yerusalemu imebaki magofu na malango yake yameteketezwa kwa moto. Njooni tujenge upya ukuta wa Yerusalemu, nasi hatutakuwa tena katika aibu hii.” 18 Pia niliwaambia kuhusu mkono wenye neema wa Mungu wangu uliokuwa juu yangu, na kile mfalme alichokuwa ameniambia.Wakajibu, “Haya! Tuanze kujenga tena.” Kwa hiyo wakaanza kazi hii njema. 19 Lakini Sanbalati Mhoroni, Tobia afisa Mwamoni, na Geshemu Mwarabu waliposikia kuhusu jambo hili, walitudhihaki na kutucheka. Wakauliza, “Ni nini hiki mnachokifanya? Je, mnaasi dhidi ya mfalme?” 20 Nikawajibu kwa kusema, “Mungu wa mbinguni atatufanikisha. Sisi watumishi wake tutaanza kujenga upya, lakini kwenu ninyi, hamna sehemu wala dai lolote wala kumbukumbu la haki katika Yerusalemu.”
In Other Versions
Nehemiah 2 in the ANGEFD
Nehemiah 2 in the ANTPNG2D
Nehemiah 2 in the AS21
Nehemiah 2 in the BAGH
Nehemiah 2 in the BBPNG
Nehemiah 2 in the BBT1E
Nehemiah 2 in the BDS
Nehemiah 2 in the BEV
Nehemiah 2 in the BHAD
Nehemiah 2 in the BIB
Nehemiah 2 in the BLPT
Nehemiah 2 in the BNT
Nehemiah 2 in the BNTABOOT
Nehemiah 2 in the BNTLV
Nehemiah 2 in the BOATCB
Nehemiah 2 in the BOATCB2
Nehemiah 2 in the BOBCV
Nehemiah 2 in the BOCNT
Nehemiah 2 in the BOECS
Nehemiah 2 in the BOGWICC
Nehemiah 2 in the BOHCB
Nehemiah 2 in the BOHCV
Nehemiah 2 in the BOHLNT
Nehemiah 2 in the BOHNTLTAL
Nehemiah 2 in the BOICB
Nehemiah 2 in the BOILNTAP
Nehemiah 2 in the BOITCV
Nehemiah 2 in the BOKCV2
Nehemiah 2 in the BOKHWOG
Nehemiah 2 in the BOKSSV
Nehemiah 2 in the BOLCB
Nehemiah 2 in the BOLCB2
Nehemiah 2 in the BOMCV
Nehemiah 2 in the BONAV
Nehemiah 2 in the BONCB
Nehemiah 2 in the BONLT
Nehemiah 2 in the BONUT2
Nehemiah 2 in the BOPLNT
Nehemiah 2 in the BOSCB
Nehemiah 2 in the BOSNC
Nehemiah 2 in the BOTLNT
Nehemiah 2 in the BOVCB
Nehemiah 2 in the BOYCB
Nehemiah 2 in the BPBB
Nehemiah 2 in the BPH
Nehemiah 2 in the BSB
Nehemiah 2 in the CCB
Nehemiah 2 in the CUV
Nehemiah 2 in the CUVS
Nehemiah 2 in the DBT
Nehemiah 2 in the DGDNT
Nehemiah 2 in the DHNT
Nehemiah 2 in the DNT
Nehemiah 2 in the ELBE
Nehemiah 2 in the EMTV
Nehemiah 2 in the ESV
Nehemiah 2 in the FBV
Nehemiah 2 in the FEB
Nehemiah 2 in the GGMNT
Nehemiah 2 in the GNT
Nehemiah 2 in the HARY
Nehemiah 2 in the HNT
Nehemiah 2 in the IRVA
Nehemiah 2 in the IRVB
Nehemiah 2 in the IRVG
Nehemiah 2 in the IRVH
Nehemiah 2 in the IRVK
Nehemiah 2 in the IRVM
Nehemiah 2 in the IRVM2
Nehemiah 2 in the IRVO
Nehemiah 2 in the IRVP
Nehemiah 2 in the IRVT
Nehemiah 2 in the IRVT2
Nehemiah 2 in the IRVU
Nehemiah 2 in the ISVN
Nehemiah 2 in the JSNT
Nehemiah 2 in the KAPI
Nehemiah 2 in the KBT1ETNIK
Nehemiah 2 in the KBV
Nehemiah 2 in the KJV
Nehemiah 2 in the KNFD
Nehemiah 2 in the LBA
Nehemiah 2 in the LBLA
Nehemiah 2 in the LNT
Nehemiah 2 in the LSV
Nehemiah 2 in the MAAL
Nehemiah 2 in the MBV
Nehemiah 2 in the MBV2
Nehemiah 2 in the MHNT
Nehemiah 2 in the MKNFD
Nehemiah 2 in the MNG
Nehemiah 2 in the MNT
Nehemiah 2 in the MNT2
Nehemiah 2 in the MRS1T
Nehemiah 2 in the NAA
Nehemiah 2 in the NASB
Nehemiah 2 in the NBLA
Nehemiah 2 in the NBS
Nehemiah 2 in the NBVTP
Nehemiah 2 in the NET2
Nehemiah 2 in the NIV11
Nehemiah 2 in the NNT
Nehemiah 2 in the NNT2
Nehemiah 2 in the NNT3
Nehemiah 2 in the PDDPT
Nehemiah 2 in the PFNT
Nehemiah 2 in the RMNT
Nehemiah 2 in the SBIAS
Nehemiah 2 in the SBIBS
Nehemiah 2 in the SBIBS2
Nehemiah 2 in the SBICS
Nehemiah 2 in the SBIDS
Nehemiah 2 in the SBIGS
Nehemiah 2 in the SBIHS
Nehemiah 2 in the SBIIS
Nehemiah 2 in the SBIIS2
Nehemiah 2 in the SBIIS3
Nehemiah 2 in the SBIKS
Nehemiah 2 in the SBIKS2
Nehemiah 2 in the SBIMS
Nehemiah 2 in the SBIOS
Nehemiah 2 in the SBIPS
Nehemiah 2 in the SBISS
Nehemiah 2 in the SBITS
Nehemiah 2 in the SBITS2
Nehemiah 2 in the SBITS3
Nehemiah 2 in the SBITS4
Nehemiah 2 in the SBIUS
Nehemiah 2 in the SBIVS
Nehemiah 2 in the SBT
Nehemiah 2 in the SBT1E
Nehemiah 2 in the SCHL
Nehemiah 2 in the SNT
Nehemiah 2 in the SUSU
Nehemiah 2 in the SUSU2
Nehemiah 2 in the SYNO
Nehemiah 2 in the TBIAOTANT
Nehemiah 2 in the TBT1E
Nehemiah 2 in the TBT1E2
Nehemiah 2 in the TFTIP
Nehemiah 2 in the TFTU
Nehemiah 2 in the TGNTATF3T
Nehemiah 2 in the THAI
Nehemiah 2 in the TNFD
Nehemiah 2 in the TNT
Nehemiah 2 in the TNTIK
Nehemiah 2 in the TNTIL
Nehemiah 2 in the TNTIN
Nehemiah 2 in the TNTIP
Nehemiah 2 in the TNTIZ
Nehemiah 2 in the TOMA
Nehemiah 2 in the TTENT
Nehemiah 2 in the UBG
Nehemiah 2 in the UGV
Nehemiah 2 in the UGV2
Nehemiah 2 in the UGV3
Nehemiah 2 in the VBL
Nehemiah 2 in the VDCC
Nehemiah 2 in the YALU
Nehemiah 2 in the YAPE
Nehemiah 2 in the YBVTP
Nehemiah 2 in the ZBP