Numbers 2 (BOKCV)
1 BWANA aliwaambia Mose na Aroni: 2 “Waisraeli watapiga kambi zao kuzunguka Hema la Kukutania kwa umbali fulani kutoka kwenye hema, kila mwanaume chini ya alama yake pamoja na bendera ya jamaa yake.” 3 Kwa upande wa mashariki kuelekea mawio ya jua, kambi ya makundi ya Yuda watapiga kambi chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Yuda ni Nashoni mwana wa Aminadabu. 4 Kundi lake lina watu 74,600. 5 Kabila la Isakari watapiga kambi karibu na Yuda. Kiongozi wa watu wa Isakari ni Nethaneli mwana wa Suari. 6 Kundi lake lina watu 54,400. 7 Kabila la Zabuloni litafuata. Kiongozi wa watu wa Zabuloni ni Eliabu mwana wa Heloni. 8 Kundi lake lina watu 57,400. 9 Wanaume wote walio katika kambi ya Yuda, kufuatana na makundi yao, ni 186,400. Wao watatangulia kuondoka. 10 Kwa upande wa kusini kutakuwa kambi ya makundi ya Reubeni chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Reubeni ni Elisuri mwana wa Shedeuri. 11 Kundi lake lina watu 46,500. 12 Kabila la Simeoni watapiga kambi karibu na Reubeni. Kiongozi wa watu wa Simeoni ni Shelumieli mwana wa Surishadai. 13 Kundi lake lina watu 59,300. 14 Kabila la Gadi litafuata. Kiongozi wa watu wa Gadi ni Eliasafu mwana wa Deueli. 15 Kundi lake lina watu 45,650. 16 Wanaume wote walio katika kambi ya Reubeni, kufuatana na makundi yao, ni 151,450. Nao watakuwa nafasi ya pili kuondoka. 17 Kisha Hema la Kukutania na kambi ya Walawi vitakuwa katikati ya kambi zote. Wao watasafiri kwa utaratibu ule ule kama walivyopiga kambi, kila mmoja mahali pake mwenyewe chini ya alama yake. 18 Upande wa magharibi kutakuwepo na kambi ya makundi ya Efraimu chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Efraimu ni Elishama mwana wa Amihudi. 19 Kundi lake lina watu 40,500. 20 Kabila la Manase litafuata baada ya Efraimu. Kiongozi wa watu wa Manase ni Gamalieli mwana wa Pedasuri. 21 Kundi lake lina watu 32,200. 22 Kabila la Benyamini litafuata baada ya Manase. Kiongozi wa watu wa Benyamini ni Abidani mwana wa Gideoni. 23 Kundi lake lina watu 35,400. 24 Wanaume wote walio katika kambi ya Efraimu kufuatana na makundi yao ni 108,100. Nao watakuwa nafasi ya tatu kuondoka. 25 Upande wa kaskazini kutakuwa na makundi ya kambi ya Dani, chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Dani ni Ahiezeri mwana wa Amishadai. 26 Kundi lake lina watu 62,700. 27 Kabila la Asheri watapiga kambi karibu na Dani. Kiongozi wa watu wa Asheri ni Pagieli mwana wa Okrani. 28 Kundi lake lina watu 41,500. 29 Kabila la Naftali litafuata. Kiongozi wa watu wa Naftali ni Ahira mwana wa Enani. 30 Kundi lake lina watu 53,400. 31 Wanaume wote walio katika kambi ya Dani ni 157,600. Wao watakuwa wa mwisho kuondoka chini ya alama yao. 32 Hawa ndio Waisraeli, wakiwa wamehesabiwa kufuatana na jamaa zao. Wote walio kambini kwa makundi yao ni watu 603,550. 33 Hata hivyo, Walawi hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine, kama BWANA alivyomwagiza Mose. 34 Kwa hiyo Waisraeli wakafanya kila kitu BWANA alichomwamuru Mose. Hivyo ndivyo walivyopiga kambi chini ya alama zao, pia hivyo ndivyo walivyoondoka, kila mmoja akiwa na ukoo wake na jamaa yake.
In Other Versions
Numbers 2 in the ANGEFD
Numbers 2 in the ANTPNG2D
Numbers 2 in the AS21
Numbers 2 in the BAGH
Numbers 2 in the BBPNG
Numbers 2 in the BBT1E
Numbers 2 in the BDS
Numbers 2 in the BEV
Numbers 2 in the BHAD
Numbers 2 in the BIB
Numbers 2 in the BLPT
Numbers 2 in the BNT
Numbers 2 in the BNTABOOT
Numbers 2 in the BNTLV
Numbers 2 in the BOATCB
Numbers 2 in the BOATCB2
Numbers 2 in the BOBCV
Numbers 2 in the BOCNT
Numbers 2 in the BOECS
Numbers 2 in the BOGWICC
Numbers 2 in the BOHCB
Numbers 2 in the BOHCV
Numbers 2 in the BOHLNT
Numbers 2 in the BOHNTLTAL
Numbers 2 in the BOICB
Numbers 2 in the BOILNTAP
Numbers 2 in the BOITCV
Numbers 2 in the BOKCV2
Numbers 2 in the BOKHWOG
Numbers 2 in the BOKSSV
Numbers 2 in the BOLCB
Numbers 2 in the BOLCB2
Numbers 2 in the BOMCV
Numbers 2 in the BONAV
Numbers 2 in the BONCB
Numbers 2 in the BONLT
Numbers 2 in the BONUT2
Numbers 2 in the BOPLNT
Numbers 2 in the BOSCB
Numbers 2 in the BOSNC
Numbers 2 in the BOTLNT
Numbers 2 in the BOVCB
Numbers 2 in the BOYCB
Numbers 2 in the BPBB
Numbers 2 in the BPH
Numbers 2 in the BSB
Numbers 2 in the CCB
Numbers 2 in the CUV
Numbers 2 in the CUVS
Numbers 2 in the DBT
Numbers 2 in the DGDNT
Numbers 2 in the DHNT
Numbers 2 in the DNT
Numbers 2 in the ELBE
Numbers 2 in the EMTV
Numbers 2 in the ESV
Numbers 2 in the FBV
Numbers 2 in the FEB
Numbers 2 in the GGMNT
Numbers 2 in the GNT
Numbers 2 in the HARY
Numbers 2 in the HNT
Numbers 2 in the IRVA
Numbers 2 in the IRVB
Numbers 2 in the IRVG
Numbers 2 in the IRVH
Numbers 2 in the IRVK
Numbers 2 in the IRVM
Numbers 2 in the IRVM2
Numbers 2 in the IRVO
Numbers 2 in the IRVP
Numbers 2 in the IRVT
Numbers 2 in the IRVT2
Numbers 2 in the IRVU
Numbers 2 in the ISVN
Numbers 2 in the JSNT
Numbers 2 in the KAPI
Numbers 2 in the KBT1ETNIK
Numbers 2 in the KBV
Numbers 2 in the KJV
Numbers 2 in the KNFD
Numbers 2 in the LBA
Numbers 2 in the LBLA
Numbers 2 in the LNT
Numbers 2 in the LSV
Numbers 2 in the MAAL
Numbers 2 in the MBV
Numbers 2 in the MBV2
Numbers 2 in the MHNT
Numbers 2 in the MKNFD
Numbers 2 in the MNG
Numbers 2 in the MNT
Numbers 2 in the MNT2
Numbers 2 in the MRS1T
Numbers 2 in the NAA
Numbers 2 in the NASB
Numbers 2 in the NBLA
Numbers 2 in the NBS
Numbers 2 in the NBVTP
Numbers 2 in the NET2
Numbers 2 in the NIV11
Numbers 2 in the NNT
Numbers 2 in the NNT2
Numbers 2 in the NNT3
Numbers 2 in the PDDPT
Numbers 2 in the PFNT
Numbers 2 in the RMNT
Numbers 2 in the SBIAS
Numbers 2 in the SBIBS
Numbers 2 in the SBIBS2
Numbers 2 in the SBICS
Numbers 2 in the SBIDS
Numbers 2 in the SBIGS
Numbers 2 in the SBIHS
Numbers 2 in the SBIIS
Numbers 2 in the SBIIS2
Numbers 2 in the SBIIS3
Numbers 2 in the SBIKS
Numbers 2 in the SBIKS2
Numbers 2 in the SBIMS
Numbers 2 in the SBIOS
Numbers 2 in the SBIPS
Numbers 2 in the SBISS
Numbers 2 in the SBITS
Numbers 2 in the SBITS2
Numbers 2 in the SBITS3
Numbers 2 in the SBITS4
Numbers 2 in the SBIUS
Numbers 2 in the SBIVS
Numbers 2 in the SBT
Numbers 2 in the SBT1E
Numbers 2 in the SCHL
Numbers 2 in the SNT
Numbers 2 in the SUSU
Numbers 2 in the SUSU2
Numbers 2 in the SYNO
Numbers 2 in the TBIAOTANT
Numbers 2 in the TBT1E
Numbers 2 in the TBT1E2
Numbers 2 in the TFTIP
Numbers 2 in the TFTU
Numbers 2 in the TGNTATF3T
Numbers 2 in the THAI
Numbers 2 in the TNFD
Numbers 2 in the TNT
Numbers 2 in the TNTIK
Numbers 2 in the TNTIL
Numbers 2 in the TNTIN
Numbers 2 in the TNTIP
Numbers 2 in the TNTIZ
Numbers 2 in the TOMA
Numbers 2 in the TTENT
Numbers 2 in the UBG
Numbers 2 in the UGV
Numbers 2 in the UGV2
Numbers 2 in the UGV3
Numbers 2 in the VBL
Numbers 2 in the VDCC
Numbers 2 in the YALU
Numbers 2 in the YAPE
Numbers 2 in the YBVTP
Numbers 2 in the ZBP