Psalms 100 (BOKCV)
undefined Zaburi ya shukrani. 1 Mpigieni BWANA kelele za shangwe, dunia yote. 2 Mwabuduni BWANA kwa furaha;njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe. 3 Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu.Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake;sisi tu watu wake,kondoo wa malisho yake. 4 Ingieni malangoni mwake kwa shukranina katika nyua zake kwa kusifu,mshukuruni yeye na kulisifu jina lake. 5 Kwa maana BWANA ni mwemana upendo wake wadumu milele;uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.