Psalms 87 (BOKCV)
undefined Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo. 1 Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu; 2 BWANA anayapenda malango ya Sayunikuliko makao yote ya Yakobo. 3 Mambo matukufu yanasemwa juu yako,ee mji wa Mungu: 4 “Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babelimiongoni mwa wale wanaonikubali mimi:Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi,nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ” 5 Kuhusu Sayuni itasemwa hivi,“Huyu na yule walizaliwa humo,naye Aliye Juu Sana mwenyeweatamwimarisha.” 6 BWANA ataandika katika orodha ya mataifa:“Huyu alizaliwa Sayuni.” 7 Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba,“Chemchemi zangu zote ziko kwako.”