Ruth 1 (BOKCV)
1 Wakati Waamuzi walipotawala Israeli, kulikuwa na njaa katika nchi. Mtu mmoja kutoka nchi ya Bethlehemu ya Yuda, pamoja na mke wake na wanawe wawili, akaenda kuishi katika nchi ya Moabu. 2 Mtu huyu aliitwa Elimeleki, mkewe aliitwa Naomi, na hao wanawe wawili waliitwa Maloni na Kilioni. Walikuwa Waefrathi kutoka Bethlehemu ya Yuda. Wakaenda katika nchi ya Moabu, wakaishi huko. 3 Elimeleki mumewe Naomi akafa, hivyo Naomi akabaki na wanawe wawili. 4 Nao wakaoa wanawake Wamoabu, jina la mmoja aliitwa Orpa, na wa pili aliitwa Ruthu. Baada ya kama miaka kumi, 5 Maloni na Kilioni pia wakafa. Basi Naomi akabaki hana mume wala wanawe wawili. 6 Aliposikia akiwa huko Moabu kwamba BWANA amewasaidia watu wake kwa kuwapa chakula, Naomi na wakweze wakajiandaa kurudi nyumbani. 7 Yeye na wakweze wawili wakaondoka pale walipokuwa wakiishi na kushika njia kurudi nchi ya Yuda. 8 Ndipo Naomi akawaambia wale wakwe zake wawili, “Rudini, kila mmoja wenu nyumbani kwa mama yake. BWANA na awatendee fadhili kama mlivyowatendea hao waliofariki, na pia mimi. 9 BWANA na amjalie kila mmoja wenu maisha mema nyumbani kwa mume mwingine.”Kisha akawabusu, nao wakalia kwa sauti kubwa, 10 wakamwambia, “Tutarudi pamoja na wewe nyumbani kwa watu wako.” 11 Lakini Naomi akasema, “Rudini nyumbani, binti zangu. Kwa nini mnifuate? Je, mimi nitaweza tena kuwa na wana wengine ambao wataweza kuwaoa ninyi? 12 Rudini nyumbani, binti zangu; mimi ni mzee kiasi kwamba siwezi kumpata mume mwingine. Hata kama ningefikiria kuwa bado kuna tumaini kwangu, hata kama ningekuwa na mume usiku huu na kuwazaa wana, 13 je, mngesubiri mpaka wakue? Mngebakia bila kuolewa mkiwasubiri? La, hasha, binti zangu. Nimepata uchungu kuliko ninyi, kwa sababu mkono wa BWANA umekuwa kinyume nami!” 14 Kisha wakalia tena kwa sauti. Orpa akambusu mama mkwe wake, akaenda zake, lakini Ruthu akaambatana naye. 15 Naomi akamwambia, “Tazama, mwenzako anarejea kwa watu wake na kwa miungu yake. Rudi pamoja naye.” 16 Lakini Ruthu akajibu, “Usinisihi nikuache au niache kukufuata. Utakakokwenda nami nitakwenda, na wewe utakapoishi nitaishi. Watu wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako atakuwa Mungu wangu. 17 Pale utakapofia nami nitafia hapo, na papo hapo nitazikwa. BWANA na aniadhibu vikali, kama kitu kingine chochote kitanitenga nawe isipokuwa kifo.” 18 Naomi alipotambua kwamba Ruthu amenuia kufuatana naye, hakuendelea kumsihi tena. 19 Kwa hiyo hao wanawake wawili wakaondoka, wakafika Bethlehemu. Walipofika Bethlehemu, mji mzima ulitaharuki, wanawake wakashangaa, wakasema, “Huyu aweza kuwa ni Naomi?” 20 Akawaambia, “Msiniite tena Naomi, niiteni Mara, kwa sababu Mwenyezi amenitendea mambo machungu sana. 21 Mimi niliondoka hali nimejaa, lakini BWANA amenirudisha mtupu. Kwa nini kuniita Naomi? BWANA amenitendea mambo machungu; Mwenyezi ameniletea msiba.” 22 Kwa hiyo Naomi alirudi pamoja na Ruthu Mmoabu mkwe wake, nao wakafika Bethlehemu mwanzoni mwa kuvuna shayiri.
In Other Versions
Ruth 1 in the ANGEFD
Ruth 1 in the ANTPNG2D
Ruth 1 in the AS21
Ruth 1 in the BAGH
Ruth 1 in the BBPNG
Ruth 1 in the BBT1E
Ruth 1 in the BDS
Ruth 1 in the BEV
Ruth 1 in the BHAD
Ruth 1 in the BIB
Ruth 1 in the BLPT
Ruth 1 in the BNT
Ruth 1 in the BNTABOOT
Ruth 1 in the BNTLV
Ruth 1 in the BOATCB
Ruth 1 in the BOATCB2
Ruth 1 in the BOBCV
Ruth 1 in the BOCNT
Ruth 1 in the BOECS
Ruth 1 in the BOGWICC
Ruth 1 in the BOHCB
Ruth 1 in the BOHCV
Ruth 1 in the BOHLNT
Ruth 1 in the BOHNTLTAL
Ruth 1 in the BOICB
Ruth 1 in the BOILNTAP
Ruth 1 in the BOITCV
Ruth 1 in the BOKCV2
Ruth 1 in the BOKHWOG
Ruth 1 in the BOKSSV
Ruth 1 in the BOLCB
Ruth 1 in the BOLCB2
Ruth 1 in the BOMCV
Ruth 1 in the BONAV
Ruth 1 in the BONCB
Ruth 1 in the BONLT
Ruth 1 in the BONUT2
Ruth 1 in the BOPLNT
Ruth 1 in the BOSCB
Ruth 1 in the BOSNC
Ruth 1 in the BOTLNT
Ruth 1 in the BOVCB
Ruth 1 in the BOYCB
Ruth 1 in the BPBB
Ruth 1 in the BPH
Ruth 1 in the BSB
Ruth 1 in the CCB
Ruth 1 in the CUV
Ruth 1 in the CUVS
Ruth 1 in the DBT
Ruth 1 in the DGDNT
Ruth 1 in the DHNT
Ruth 1 in the DNT
Ruth 1 in the ELBE
Ruth 1 in the EMTV
Ruth 1 in the ESV
Ruth 1 in the FBV
Ruth 1 in the FEB
Ruth 1 in the GGMNT
Ruth 1 in the GNT
Ruth 1 in the HARY
Ruth 1 in the HNT
Ruth 1 in the IRVA
Ruth 1 in the IRVB
Ruth 1 in the IRVG
Ruth 1 in the IRVH
Ruth 1 in the IRVK
Ruth 1 in the IRVM
Ruth 1 in the IRVM2
Ruth 1 in the IRVO
Ruth 1 in the IRVP
Ruth 1 in the IRVT
Ruth 1 in the IRVT2
Ruth 1 in the IRVU
Ruth 1 in the ISVN
Ruth 1 in the JSNT
Ruth 1 in the KAPI
Ruth 1 in the KBT1ETNIK
Ruth 1 in the KBV
Ruth 1 in the KJV
Ruth 1 in the KNFD
Ruth 1 in the LBA
Ruth 1 in the LBLA
Ruth 1 in the LNT
Ruth 1 in the LSV
Ruth 1 in the MAAL
Ruth 1 in the MBV
Ruth 1 in the MBV2
Ruth 1 in the MHNT
Ruth 1 in the MKNFD
Ruth 1 in the MNG
Ruth 1 in the MNT
Ruth 1 in the MNT2
Ruth 1 in the MRS1T
Ruth 1 in the NAA
Ruth 1 in the NASB
Ruth 1 in the NBLA
Ruth 1 in the NBS
Ruth 1 in the NBVTP
Ruth 1 in the NET2
Ruth 1 in the NIV11
Ruth 1 in the NNT
Ruth 1 in the NNT2
Ruth 1 in the NNT3
Ruth 1 in the PDDPT
Ruth 1 in the PFNT
Ruth 1 in the RMNT
Ruth 1 in the SBIAS
Ruth 1 in the SBIBS
Ruth 1 in the SBIBS2
Ruth 1 in the SBICS
Ruth 1 in the SBIDS
Ruth 1 in the SBIGS
Ruth 1 in the SBIHS
Ruth 1 in the SBIIS
Ruth 1 in the SBIIS2
Ruth 1 in the SBIIS3
Ruth 1 in the SBIKS
Ruth 1 in the SBIKS2
Ruth 1 in the SBIMS
Ruth 1 in the SBIOS
Ruth 1 in the SBIPS
Ruth 1 in the SBISS
Ruth 1 in the SBITS
Ruth 1 in the SBITS2
Ruth 1 in the SBITS3
Ruth 1 in the SBITS4
Ruth 1 in the SBIUS
Ruth 1 in the SBIVS
Ruth 1 in the SBT
Ruth 1 in the SBT1E
Ruth 1 in the SCHL
Ruth 1 in the SNT
Ruth 1 in the SUSU
Ruth 1 in the SUSU2
Ruth 1 in the SYNO
Ruth 1 in the TBIAOTANT
Ruth 1 in the TBT1E
Ruth 1 in the TBT1E2
Ruth 1 in the TFTIP
Ruth 1 in the TFTU
Ruth 1 in the TGNTATF3T
Ruth 1 in the THAI
Ruth 1 in the TNFD
Ruth 1 in the TNT
Ruth 1 in the TNTIK
Ruth 1 in the TNTIL
Ruth 1 in the TNTIN
Ruth 1 in the TNTIP
Ruth 1 in the TNTIZ
Ruth 1 in the TOMA
Ruth 1 in the TTENT
Ruth 1 in the UBG
Ruth 1 in the UGV
Ruth 1 in the UGV2
Ruth 1 in the UGV3
Ruth 1 in the VBL
Ruth 1 in the VDCC
Ruth 1 in the YALU
Ruth 1 in the YAPE
Ruth 1 in the YBVTP
Ruth 1 in the ZBP