Zechariah 8 (BOKCV)
1 Neno la BWANA Mwenye Nguvu Zote likanijia tena. 2 Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: “Nina wivu sana kwa ajili ya Sayuni, ninawaka wivu kwa ajili yake.” 3 Hili ndilo asemalo BWANA: “Nitarudi Sayuni na kufanya makao Yerusalemu. Kisha Yerusalemu utaitwa mji wa kweli, mlima wa BWANA Mwenye Nguvu Zote utaitwa Mlima Mtakatifu.” 4 Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: “Kwa mara nyingine tena wazee wanaume kwa wanawake walioshiba umri wataketi katika barabara za Yerusalemu, kila mmoja akiwa na mkongojo wake mkononi kwa sababu ya umri wake. 5 Barabara za mji zitajaa wavulana na wasichana wanaocheza humo.” 6 Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: “Mambo haya yanaweza kuonekana ya ajabu kwa mabaki ya watu wakati huo, lakini yaweza kuwa ya ajabu kwangu?” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote. 7 Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: “Nitawaokoa watu wangu kutoka nchi za mashariki na magharibi. 8 Nitawarudisha waje kuishi Yerusalemu, watakuwa watu wangu nami nitakuwa mwaminifu na wa haki kwao kama Mungu wao.” 9 Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: “Ninyi ambao sasa mnasikia maneno haya yanayozungumzwa na manabii ambao walikuwepo wakati wa kuwekwa kwa msingi wa nyumba ya BWANA Mwenye Nguvu Zote, mikono yenu na iwe na nguvu ili Hekalu liweze kujengwa. 10 Kabla ya wakati huo, hapakuwepo na ujira kwa mtu wala mnyama. Hakuna mtu aliyeweza kufanya shughuli yake kwa usalama kwa sababu ya adui yake, kwa kuwa nilikuwa nimemfanya kila mtu adui wa jirani yake. 11 Lakini sasa sitawatendea mabaki ya watu hawa kama nilivyowatenda zamani,” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote. 12 “Mbegu itakua vizuri, mzabibu utazaa matunda yake, ardhi itatoa mazao yake, na mbingu zitadondosha umande wake. Vitu hivi vyote nitawapa mabaki ya watu kama urithi wao. 13 Jinsi mlivyokuwa kitu cha laana katikati ya mataifa, ee Yuda na Israeli, ndivyo nitakavyowaokoa, nanyi mtakuwa baraka. Msiogope, bali iacheni mikono yenu iwe na nguvu.” 14 Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: “Kama nilivyokuwa nimekusudia kuleta maangamizi juu yenu, wakati baba zenu waliponikasirisha na sikuonyesha huruma,” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote, 15 “hivyo sasa nimeazimia kufanya mema tena kwa Yerusalemu na Yuda. Msiogope. 16 Haya ndiyo mtakayoyafanya: Semeni kweli kila mtu kwa mwenzake, na mtoe hukumu ya kweli na haki kwenye mahakama zenu, 17 usipange mabaya dhidi ya jirani yako, wala msipende kuapa kwa uongo. Nayachukia yote haya,” asema BWANA. 18 Neno la BWANA Mwenye Nguvu Zote likanijia tena. 19 Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: “Saumu za miezi ya nne, tano, saba na kumi itakuwa sikukuu za furaha na za shangwe kwa Yuda. Kwa hiyo uipende kweli na amani.” 20 Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: “Mataifa mengi na wakazi wa miji mingi watakuja, 21 na wenyeji wa mji mmoja watakwenda kwenye mji mwingine na kusema, ‘Twende mara moja na tukamsihi BWANA, na kumtafuta BWANA Mwenye Nguvu Zote. Mimi mwenyewe ninakwenda.’ 22 Pia watu wa kabila nyingi na mataifa yenye nguvu yatakuja Yerusalemu kumtafuta BWANA Mwenye Nguvu Zote na kumsihi.” 23 Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: “Katika siku hizo watu kumi kutoka lugha zote na mataifa, watangʼangʼania upindo wa joho la Myahudi mmoja na kusema, ‘Twende pamoja nawe kwa sababu tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nawe.’ ”
In Other Versions
Zechariah 8 in the ANGEFD
Zechariah 8 in the ANTPNG2D
Zechariah 8 in the AS21
Zechariah 8 in the BAGH
Zechariah 8 in the BBPNG
Zechariah 8 in the BBT1E
Zechariah 8 in the BDS
Zechariah 8 in the BEV
Zechariah 8 in the BHAD
Zechariah 8 in the BIB
Zechariah 8 in the BLPT
Zechariah 8 in the BNT
Zechariah 8 in the BNTABOOT
Zechariah 8 in the BNTLV
Zechariah 8 in the BOATCB
Zechariah 8 in the BOATCB2
Zechariah 8 in the BOBCV
Zechariah 8 in the BOCNT
Zechariah 8 in the BOECS
Zechariah 8 in the BOGWICC
Zechariah 8 in the BOHCB
Zechariah 8 in the BOHCV
Zechariah 8 in the BOHLNT
Zechariah 8 in the BOHNTLTAL
Zechariah 8 in the BOICB
Zechariah 8 in the BOILNTAP
Zechariah 8 in the BOITCV
Zechariah 8 in the BOKCV2
Zechariah 8 in the BOKHWOG
Zechariah 8 in the BOKSSV
Zechariah 8 in the BOLCB
Zechariah 8 in the BOLCB2
Zechariah 8 in the BOMCV
Zechariah 8 in the BONAV
Zechariah 8 in the BONCB
Zechariah 8 in the BONLT
Zechariah 8 in the BONUT2
Zechariah 8 in the BOPLNT
Zechariah 8 in the BOSCB
Zechariah 8 in the BOSNC
Zechariah 8 in the BOTLNT
Zechariah 8 in the BOVCB
Zechariah 8 in the BOYCB
Zechariah 8 in the BPBB
Zechariah 8 in the BPH
Zechariah 8 in the BSB
Zechariah 8 in the CCB
Zechariah 8 in the CUV
Zechariah 8 in the CUVS
Zechariah 8 in the DBT
Zechariah 8 in the DGDNT
Zechariah 8 in the DHNT
Zechariah 8 in the DNT
Zechariah 8 in the ELBE
Zechariah 8 in the EMTV
Zechariah 8 in the ESV
Zechariah 8 in the FBV
Zechariah 8 in the FEB
Zechariah 8 in the GGMNT
Zechariah 8 in the GNT
Zechariah 8 in the HARY
Zechariah 8 in the HNT
Zechariah 8 in the IRVA
Zechariah 8 in the IRVB
Zechariah 8 in the IRVG
Zechariah 8 in the IRVH
Zechariah 8 in the IRVK
Zechariah 8 in the IRVM
Zechariah 8 in the IRVM2
Zechariah 8 in the IRVO
Zechariah 8 in the IRVP
Zechariah 8 in the IRVT
Zechariah 8 in the IRVT2
Zechariah 8 in the IRVU
Zechariah 8 in the ISVN
Zechariah 8 in the JSNT
Zechariah 8 in the KAPI
Zechariah 8 in the KBT1ETNIK
Zechariah 8 in the KBV
Zechariah 8 in the KJV
Zechariah 8 in the KNFD
Zechariah 8 in the LBA
Zechariah 8 in the LBLA
Zechariah 8 in the LNT
Zechariah 8 in the LSV
Zechariah 8 in the MAAL
Zechariah 8 in the MBV
Zechariah 8 in the MBV2
Zechariah 8 in the MHNT
Zechariah 8 in the MKNFD
Zechariah 8 in the MNG
Zechariah 8 in the MNT
Zechariah 8 in the MNT2
Zechariah 8 in the MRS1T
Zechariah 8 in the NAA
Zechariah 8 in the NASB
Zechariah 8 in the NBLA
Zechariah 8 in the NBS
Zechariah 8 in the NBVTP
Zechariah 8 in the NET2
Zechariah 8 in the NIV11
Zechariah 8 in the NNT
Zechariah 8 in the NNT2
Zechariah 8 in the NNT3
Zechariah 8 in the PDDPT
Zechariah 8 in the PFNT
Zechariah 8 in the RMNT
Zechariah 8 in the SBIAS
Zechariah 8 in the SBIBS
Zechariah 8 in the SBIBS2
Zechariah 8 in the SBICS
Zechariah 8 in the SBIDS
Zechariah 8 in the SBIGS
Zechariah 8 in the SBIHS
Zechariah 8 in the SBIIS
Zechariah 8 in the SBIIS2
Zechariah 8 in the SBIIS3
Zechariah 8 in the SBIKS
Zechariah 8 in the SBIKS2
Zechariah 8 in the SBIMS
Zechariah 8 in the SBIOS
Zechariah 8 in the SBIPS
Zechariah 8 in the SBISS
Zechariah 8 in the SBITS
Zechariah 8 in the SBITS2
Zechariah 8 in the SBITS3
Zechariah 8 in the SBITS4
Zechariah 8 in the SBIUS
Zechariah 8 in the SBIVS
Zechariah 8 in the SBT
Zechariah 8 in the SBT1E
Zechariah 8 in the SCHL
Zechariah 8 in the SNT
Zechariah 8 in the SUSU
Zechariah 8 in the SUSU2
Zechariah 8 in the SYNO
Zechariah 8 in the TBIAOTANT
Zechariah 8 in the TBT1E
Zechariah 8 in the TBT1E2
Zechariah 8 in the TFTIP
Zechariah 8 in the TFTU
Zechariah 8 in the TGNTATF3T
Zechariah 8 in the THAI
Zechariah 8 in the TNFD
Zechariah 8 in the TNT
Zechariah 8 in the TNTIK
Zechariah 8 in the TNTIL
Zechariah 8 in the TNTIN
Zechariah 8 in the TNTIP
Zechariah 8 in the TNTIZ
Zechariah 8 in the TOMA
Zechariah 8 in the TTENT
Zechariah 8 in the UBG
Zechariah 8 in the UGV
Zechariah 8 in the UGV2
Zechariah 8 in the UGV3
Zechariah 8 in the VBL
Zechariah 8 in the VDCC
Zechariah 8 in the YALU
Zechariah 8 in the YAPE
Zechariah 8 in the YBVTP
Zechariah 8 in the ZBP