1 Chronicles 19 (BOKCV)

1 Baada ya muda, Nahashi mfalme wa Waamoni akafa, mwanawe akaingia mahali pake. 2 Daudi akawaza, “Nitamtendea wema Hanuni mwana wa Nahashi, kwa sababu baba yake alinitendea wema.”Hivyo Daudi akatuma wajumbe ili kumfariji Hanuni kwa ajili ya kifo cha baba yake. Watu wa Daudi walipofika kwa Hanuni katika nchi ya Waamoni ili kumfariji, 3 wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni, “Hivi unadhani Daudi anamheshimu baba yako kwa kuwatuma wajumbe kukufariji? Je, hawa watu hawakuja kuipeleleza na kuidadisi nchi ili waishinde?” 4 Kwa hiyo Hanuni akawakamata watu wa Daudi, akawanyoa ndevu akakata nguo zao katikati kwenye matako, akawaacha waende zao. 5 Mtu mmoja alipofika na kumpasha Daudi habari za watu hawa, akawatuma wajumbe wengine kuwalaki, kwa maana walikuwa wamevunjiwa heshima sana. Mfalme akasema, “Kaeni huko Yeriko mpaka ndevu zenu ziote, ndipo mje.” 6 Waamoni walipotambua kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, Hanuni na Waamoni wakatuma talanta 1,000 za fedha ili kukodisha magari ya vita pamoja na waendeshaji wa hayo magari ya kukokotwa na farasi, kutoka Aramu-Naharaimu, Aramu-Maaka na Soba. 7 Wakakodisha magari ya vita 32,000 yakiwa na waendeshaji wake, pamoja na mfalme wa Maaka na vikosi vyake, wakaja na kupiga kambi karibu na Medeba. Waamoni nao wakakusanyika toka miji yao, wakatoka ili kupigana vita. 8 Daudi aliposikia jambo hili, akamtuma Yoabu na jeshi lote la wapiganaji. 9 Waamoni wakatoka wakajipanga wakiwa tayari kwa vita langoni la mji wao, wakati wale wafalme wengine waliokuja nao walijipanga kwa vita uwanjani. 10 Yoabu akaona kuwa mbele yake na nyuma yake kumepangwa vita; kwa hiyo akachagua baadhi ya vikosi vilivyo bora sana katika Israeli akavipanga dhidi ya Waaramu. 11 Akawaweka wale wanajeshi wengine waliobaki chini ya amri ya Abishai ndugu yake, nao wakapangwa ili wakabiliane na Waamoni. 12 Yoabu akasema, “Kama Waaramu watanizidi nguvu, basi itakupasa wewe unisaidie; lakini kama Waamoni watakuzidi nguvu, basi mimi nitakusaidia. 13 Uwe hodari na tupigane kwa ujasiri kwa ajili ya watu wetu na miji ya Mungu wetu. BWANA atafanya lile lililo jema machoni pake.” 14 Basi Yoabu na vikosi vyake wakasonga mbele kupigana na Waaramu, nao Waaramu wakakimbia mbele yake. 15 Waamoni walipoona Waaramu wanakimbia, nao pia wakakimbia mbele ya nduguye Abishai na kuingia ndani ya mji. Basi Yoabu akarudi Yerusalemu. 16 Baada ya Waaramu kuona kwamba wameshindwa na Israeli, wakapeleka wajumbe na kuwataka Waaramu wengine kutoka ngʼambo ya Mto Frati, wakiongozwa na Shofaki, jemadari wa jeshi la Hadadezeri. 17 Daudi alipoambiwa haya, akawakusanya Israeli wote na kuvuka Yordani. Akasonga mbele dhidi yao na akajipanga kuwakabili. Daudi akapanga vita ili kupigana na Waaramu, nao wakapigana dhidi yake. 18 Lakini Waaramu wakakimbia mbele ya Israeli, naye Daudi akawaua waendesha magari 7,000 na askari wao wa miguu 40,000. Pia akamuua Shofaki, jemadari wa jeshi lao. 19 Raiya wa Hadadezeri walipoona kuwa wameshindwa na Israeli, wakafanya mapatano ya amani na Daudi, wakawa watumishi wake.Hivyo Waaramu hawakukubali kuwasaidia Waamoni tena.

In Other Versions

1 Chronicles 19 in the ANGEFD

1 Chronicles 19 in the ANTPNG2D

1 Chronicles 19 in the AS21

1 Chronicles 19 in the BAGH

1 Chronicles 19 in the BBPNG

1 Chronicles 19 in the BBT1E

1 Chronicles 19 in the BDS

1 Chronicles 19 in the BEV

1 Chronicles 19 in the BHAD

1 Chronicles 19 in the BIB

1 Chronicles 19 in the BLPT

1 Chronicles 19 in the BNT

1 Chronicles 19 in the BNTABOOT

1 Chronicles 19 in the BNTLV

1 Chronicles 19 in the BOATCB

1 Chronicles 19 in the BOATCB2

1 Chronicles 19 in the BOBCV

1 Chronicles 19 in the BOCNT

1 Chronicles 19 in the BOECS

1 Chronicles 19 in the BOGWICC

1 Chronicles 19 in the BOHCB

1 Chronicles 19 in the BOHCV

1 Chronicles 19 in the BOHLNT

1 Chronicles 19 in the BOHNTLTAL

1 Chronicles 19 in the BOICB

1 Chronicles 19 in the BOILNTAP

1 Chronicles 19 in the BOITCV

1 Chronicles 19 in the BOKCV2

1 Chronicles 19 in the BOKHWOG

1 Chronicles 19 in the BOKSSV

1 Chronicles 19 in the BOLCB

1 Chronicles 19 in the BOLCB2

1 Chronicles 19 in the BOMCV

1 Chronicles 19 in the BONAV

1 Chronicles 19 in the BONCB

1 Chronicles 19 in the BONLT

1 Chronicles 19 in the BONUT2

1 Chronicles 19 in the BOPLNT

1 Chronicles 19 in the BOSCB

1 Chronicles 19 in the BOSNC

1 Chronicles 19 in the BOTLNT

1 Chronicles 19 in the BOVCB

1 Chronicles 19 in the BOYCB

1 Chronicles 19 in the BPBB

1 Chronicles 19 in the BPH

1 Chronicles 19 in the BSB

1 Chronicles 19 in the CCB

1 Chronicles 19 in the CUV

1 Chronicles 19 in the CUVS

1 Chronicles 19 in the DBT

1 Chronicles 19 in the DGDNT

1 Chronicles 19 in the DHNT

1 Chronicles 19 in the DNT

1 Chronicles 19 in the ELBE

1 Chronicles 19 in the EMTV

1 Chronicles 19 in the ESV

1 Chronicles 19 in the FBV

1 Chronicles 19 in the FEB

1 Chronicles 19 in the GGMNT

1 Chronicles 19 in the GNT

1 Chronicles 19 in the HARY

1 Chronicles 19 in the HNT

1 Chronicles 19 in the IRVA

1 Chronicles 19 in the IRVB

1 Chronicles 19 in the IRVG

1 Chronicles 19 in the IRVH

1 Chronicles 19 in the IRVK

1 Chronicles 19 in the IRVM

1 Chronicles 19 in the IRVM2

1 Chronicles 19 in the IRVO

1 Chronicles 19 in the IRVP

1 Chronicles 19 in the IRVT

1 Chronicles 19 in the IRVT2

1 Chronicles 19 in the IRVU

1 Chronicles 19 in the ISVN

1 Chronicles 19 in the JSNT

1 Chronicles 19 in the KAPI

1 Chronicles 19 in the KBT1ETNIK

1 Chronicles 19 in the KBV

1 Chronicles 19 in the KJV

1 Chronicles 19 in the KNFD

1 Chronicles 19 in the LBA

1 Chronicles 19 in the LBLA

1 Chronicles 19 in the LNT

1 Chronicles 19 in the LSV

1 Chronicles 19 in the MAAL

1 Chronicles 19 in the MBV

1 Chronicles 19 in the MBV2

1 Chronicles 19 in the MHNT

1 Chronicles 19 in the MKNFD

1 Chronicles 19 in the MNG

1 Chronicles 19 in the MNT

1 Chronicles 19 in the MNT2

1 Chronicles 19 in the MRS1T

1 Chronicles 19 in the NAA

1 Chronicles 19 in the NASB

1 Chronicles 19 in the NBLA

1 Chronicles 19 in the NBS

1 Chronicles 19 in the NBVTP

1 Chronicles 19 in the NET2

1 Chronicles 19 in the NIV11

1 Chronicles 19 in the NNT

1 Chronicles 19 in the NNT2

1 Chronicles 19 in the NNT3

1 Chronicles 19 in the PDDPT

1 Chronicles 19 in the PFNT

1 Chronicles 19 in the RMNT

1 Chronicles 19 in the SBIAS

1 Chronicles 19 in the SBIBS

1 Chronicles 19 in the SBIBS2

1 Chronicles 19 in the SBICS

1 Chronicles 19 in the SBIDS

1 Chronicles 19 in the SBIGS

1 Chronicles 19 in the SBIHS

1 Chronicles 19 in the SBIIS

1 Chronicles 19 in the SBIIS2

1 Chronicles 19 in the SBIIS3

1 Chronicles 19 in the SBIKS

1 Chronicles 19 in the SBIKS2

1 Chronicles 19 in the SBIMS

1 Chronicles 19 in the SBIOS

1 Chronicles 19 in the SBIPS

1 Chronicles 19 in the SBISS

1 Chronicles 19 in the SBITS

1 Chronicles 19 in the SBITS2

1 Chronicles 19 in the SBITS3

1 Chronicles 19 in the SBITS4

1 Chronicles 19 in the SBIUS

1 Chronicles 19 in the SBIVS

1 Chronicles 19 in the SBT

1 Chronicles 19 in the SBT1E

1 Chronicles 19 in the SCHL

1 Chronicles 19 in the SNT

1 Chronicles 19 in the SUSU

1 Chronicles 19 in the SUSU2

1 Chronicles 19 in the SYNO

1 Chronicles 19 in the TBIAOTANT

1 Chronicles 19 in the TBT1E

1 Chronicles 19 in the TBT1E2

1 Chronicles 19 in the TFTIP

1 Chronicles 19 in the TFTU

1 Chronicles 19 in the TGNTATF3T

1 Chronicles 19 in the THAI

1 Chronicles 19 in the TNFD

1 Chronicles 19 in the TNT

1 Chronicles 19 in the TNTIK

1 Chronicles 19 in the TNTIL

1 Chronicles 19 in the TNTIN

1 Chronicles 19 in the TNTIP

1 Chronicles 19 in the TNTIZ

1 Chronicles 19 in the TOMA

1 Chronicles 19 in the TTENT

1 Chronicles 19 in the UBG

1 Chronicles 19 in the UGV

1 Chronicles 19 in the UGV2

1 Chronicles 19 in the UGV3

1 Chronicles 19 in the VBL

1 Chronicles 19 in the VDCC

1 Chronicles 19 in the YALU

1 Chronicles 19 in the YAPE

1 Chronicles 19 in the YBVTP

1 Chronicles 19 in the ZBP