1 Corinthians 12 (BOKCV)

1 Basi ndugu zangu, kuhusu karama za rohoni, sitaki mkose kufahamu. 2 Mnajua kwamba mlipokuwa watu wasiomjua Mungu, kwa njia moja au ingine mlishawishika na kupotoshwa mkielekezwa kwa sanamu zisizonena. 3 Kwa hiyo nawaambieni ya kuwa hakuna mtu anayeongozwa na Roho wa Mungu anayeweza kusema, “Yesu na alaaniwe.” Pia hakuna mtu awezaye kusema, “Yesu ni Bwana,” isipokuwa ameongozwa na Roho Mtakatifu. 4 Kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni yule yule. 5 Kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni yule yule. 6 Kisha kuna tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule atendaye kazi zote kwa watu wote. 7 Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote. 8 Maana mtu mmoja kwa Roho hupewa neno la hekima na mwingine neno la maarifa kwa Roho huyo huyo. 9 Mtu mwingine imani kwa huyo Roho na mwingine karama za kuponya kwa huyo Roho mmoja. 10 Kwa mwingine matendo ya miujiza, kwa mwingine unabii kwa mwingine kupambanua roho, kwa mwingine aina mbalimbali za lugha, na kwa mwingine bado, tafsiri za lugha. 11 Haya yote hufanywa na huyo huyo Roho mmoja, Roho naye humgawia kila mtu, kama apendavyo. 12 Kama vile mwili ulivyo mmoja nao una viungo vingi, navyo viungo vyote vya mwili ingawa ni vingi, ni mwili mmoja, vivyo hivyo na Kristo. 13 Kwa maana katika Roho mmoja wote tulibatizwa katika mwili mmoja, kama ni Wayahudi au Wayunani, kama ni watumwa au watu huru, nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja. 14 Basi mwili si kiungo kimoja, bali ni viungo vingi. 15 Kama mguu ungesema, “Kwa kuwa mimi si mkono basi mimi si wa mwili,” hiyo isingefanya huo mguu usiwe sehemu ya mwili. 16 Na kama sikio lingesema, “Kwa kuwa mimi si jicho, basi mimi si wa mwili,” hiyo isingefanya hilo sikio lisiwe sehemu ya mwili. 17 Kama mwili wote ungelikuwa jicho, kusikia kungekuwa wapi? Au kama mwili wote ungelikuwa sikio, kunusa kungekuwa wapi? 18 Lakini kama ilivyo, Mungu ameweka viungo katika mwili, kila kimoja kama alivyopenda. 19 Kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi? 20 Kama ulivyo, una viungo vingi, lakini mwili ni mmoja. 21 Jicho haliwezi kuuambia mkono, “Sina haja nawe!” Wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu, “Sina haja na ninyi!” 22 Lakini badala yake, vile viungo vya mwili vinavyoonekana kuwa dhaifu, ndivyo ambavyo ni vya muhimu sana. 23 Navyo vile viungo tunavyoviona havina heshima, ndivyo tunavipa heshima maalum. Vile viungo vya mwili ambavyo havina uzuri, tunavipa heshima ya pekee; 24 wakati vile viungo vyenye uzuri havihitaji utunzaji wa pekee. Lakini Mungu ameviweka pamoja viungo vya mwili na akavipa heshima zaidi vile vilivyopungukiwa, 25 ili pasiwe na mafarakano katika mwili, bali viungo vyote vihudumiane kwa usawa kila kimoja na mwenzake. 26 Kama kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia pamoja nacho, kama kiungo kimoja kikipewa heshima, viungo vyote hufurahi pamoja nacho. 27 Sasa ninyi ni mwili wa Kristo na kila mmoja wenu ni sehemu ya huo mwili. 28 Mungu ameweka katika kanisa, kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu, kisha watenda miujiza, pia karama za kuponya, karama za kusaidiana, karama za uongozi, aina mbalimbali za lugha. 29 Je, wote ni mitume? Je, wote ni manabii? Je, wote ni walimu? Je, wote wanatenda miujiza? 30 Je, wote wana karama ya kuponya? Je, wote hunena kwa lugha mpya? Je, wote wanatafsiri? 31 Basi tamanini sana karama zilizo kuu.Nami nitawaonyesha njia iliyo bora zaidi.

In Other Versions

1 Corinthians 12 in the ANGEFD

1 Corinthians 12 in the ANTPNG2D

1 Corinthians 12 in the AS21

1 Corinthians 12 in the BAGH

1 Corinthians 12 in the BBPNG

1 Corinthians 12 in the BBT1E

1 Corinthians 12 in the BDS

1 Corinthians 12 in the BEV

1 Corinthians 12 in the BHAD

1 Corinthians 12 in the BIB

1 Corinthians 12 in the BLPT

1 Corinthians 12 in the BNT

1 Corinthians 12 in the BNTABOOT

1 Corinthians 12 in the BNTLV

1 Corinthians 12 in the BOATCB

1 Corinthians 12 in the BOATCB2

1 Corinthians 12 in the BOBCV

1 Corinthians 12 in the BOCNT

1 Corinthians 12 in the BOECS

1 Corinthians 12 in the BOGWICC

1 Corinthians 12 in the BOHCB

1 Corinthians 12 in the BOHCV

1 Corinthians 12 in the BOHLNT

1 Corinthians 12 in the BOHNTLTAL

1 Corinthians 12 in the BOICB

1 Corinthians 12 in the BOILNTAP

1 Corinthians 12 in the BOITCV

1 Corinthians 12 in the BOKCV2

1 Corinthians 12 in the BOKHWOG

1 Corinthians 12 in the BOKSSV

1 Corinthians 12 in the BOLCB

1 Corinthians 12 in the BOLCB2

1 Corinthians 12 in the BOMCV

1 Corinthians 12 in the BONAV

1 Corinthians 12 in the BONCB

1 Corinthians 12 in the BONLT

1 Corinthians 12 in the BONUT2

1 Corinthians 12 in the BOPLNT

1 Corinthians 12 in the BOSCB

1 Corinthians 12 in the BOSNC

1 Corinthians 12 in the BOTLNT

1 Corinthians 12 in the BOVCB

1 Corinthians 12 in the BOYCB

1 Corinthians 12 in the BPBB

1 Corinthians 12 in the BPH

1 Corinthians 12 in the BSB

1 Corinthians 12 in the CCB

1 Corinthians 12 in the CUV

1 Corinthians 12 in the CUVS

1 Corinthians 12 in the DBT

1 Corinthians 12 in the DGDNT

1 Corinthians 12 in the DHNT

1 Corinthians 12 in the DNT

1 Corinthians 12 in the ELBE

1 Corinthians 12 in the EMTV

1 Corinthians 12 in the ESV

1 Corinthians 12 in the FBV

1 Corinthians 12 in the FEB

1 Corinthians 12 in the GGMNT

1 Corinthians 12 in the GNT

1 Corinthians 12 in the HARY

1 Corinthians 12 in the HNT

1 Corinthians 12 in the IRVA

1 Corinthians 12 in the IRVB

1 Corinthians 12 in the IRVG

1 Corinthians 12 in the IRVH

1 Corinthians 12 in the IRVK

1 Corinthians 12 in the IRVM

1 Corinthians 12 in the IRVM2

1 Corinthians 12 in the IRVO

1 Corinthians 12 in the IRVP

1 Corinthians 12 in the IRVT

1 Corinthians 12 in the IRVT2

1 Corinthians 12 in the IRVU

1 Corinthians 12 in the ISVN

1 Corinthians 12 in the JSNT

1 Corinthians 12 in the KAPI

1 Corinthians 12 in the KBT1ETNIK

1 Corinthians 12 in the KBV

1 Corinthians 12 in the KJV

1 Corinthians 12 in the KNFD

1 Corinthians 12 in the LBA

1 Corinthians 12 in the LBLA

1 Corinthians 12 in the LNT

1 Corinthians 12 in the LSV

1 Corinthians 12 in the MAAL

1 Corinthians 12 in the MBV

1 Corinthians 12 in the MBV2

1 Corinthians 12 in the MHNT

1 Corinthians 12 in the MKNFD

1 Corinthians 12 in the MNG

1 Corinthians 12 in the MNT

1 Corinthians 12 in the MNT2

1 Corinthians 12 in the MRS1T

1 Corinthians 12 in the NAA

1 Corinthians 12 in the NASB

1 Corinthians 12 in the NBLA

1 Corinthians 12 in the NBS

1 Corinthians 12 in the NBVTP

1 Corinthians 12 in the NET2

1 Corinthians 12 in the NIV11

1 Corinthians 12 in the NNT

1 Corinthians 12 in the NNT2

1 Corinthians 12 in the NNT3

1 Corinthians 12 in the PDDPT

1 Corinthians 12 in the PFNT

1 Corinthians 12 in the RMNT

1 Corinthians 12 in the SBIAS

1 Corinthians 12 in the SBIBS

1 Corinthians 12 in the SBIBS2

1 Corinthians 12 in the SBICS

1 Corinthians 12 in the SBIDS

1 Corinthians 12 in the SBIGS

1 Corinthians 12 in the SBIHS

1 Corinthians 12 in the SBIIS

1 Corinthians 12 in the SBIIS2

1 Corinthians 12 in the SBIIS3

1 Corinthians 12 in the SBIKS

1 Corinthians 12 in the SBIKS2

1 Corinthians 12 in the SBIMS

1 Corinthians 12 in the SBIOS

1 Corinthians 12 in the SBIPS

1 Corinthians 12 in the SBISS

1 Corinthians 12 in the SBITS

1 Corinthians 12 in the SBITS2

1 Corinthians 12 in the SBITS3

1 Corinthians 12 in the SBITS4

1 Corinthians 12 in the SBIUS

1 Corinthians 12 in the SBIVS

1 Corinthians 12 in the SBT

1 Corinthians 12 in the SBT1E

1 Corinthians 12 in the SCHL

1 Corinthians 12 in the SNT

1 Corinthians 12 in the SUSU

1 Corinthians 12 in the SUSU2

1 Corinthians 12 in the SYNO

1 Corinthians 12 in the TBIAOTANT

1 Corinthians 12 in the TBT1E

1 Corinthians 12 in the TBT1E2

1 Corinthians 12 in the TFTIP

1 Corinthians 12 in the TFTU

1 Corinthians 12 in the TGNTATF3T

1 Corinthians 12 in the THAI

1 Corinthians 12 in the TNFD

1 Corinthians 12 in the TNT

1 Corinthians 12 in the TNTIK

1 Corinthians 12 in the TNTIL

1 Corinthians 12 in the TNTIN

1 Corinthians 12 in the TNTIP

1 Corinthians 12 in the TNTIZ

1 Corinthians 12 in the TOMA

1 Corinthians 12 in the TTENT

1 Corinthians 12 in the UBG

1 Corinthians 12 in the UGV

1 Corinthians 12 in the UGV2

1 Corinthians 12 in the UGV3

1 Corinthians 12 in the VBL

1 Corinthians 12 in the VDCC

1 Corinthians 12 in the YALU

1 Corinthians 12 in the YAPE

1 Corinthians 12 in the YBVTP

1 Corinthians 12 in the ZBP