1 Samuel 3 (BOKCV)

1 Kijana Samweli alihudumu mbele za BWANA chini ya Eli. Katika siku zile neno la Mungu lilikuwa adimu, hapakuwepo na maono mengi. 2 Usiku mmoja Eli, ambaye macho yake yalikuwa yamefifia sana kiasi kwamba aliona kwa shida sana, alikuwa amelala mahali pake pa kawaida. 3 Taa ya Mungu bado ilikuwa haijazimika, na Samweli alikuwa amelala Hekaluni mwa BWANA, ambapo Sanduku la Mungu lilikuwako. 4 Kisha BWANA akamwita Samweli.Samweli akajibu, “Mimi hapa.” 5 Naye akakimbia kwa Eli na kumwambia, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.”Lakini Eli akasema, “Sikukuita; rudi ukalale.” Hivyo akaenda kulala. 6 BWANA akaita tena, “Samweli!” Naye Samweli akaamka, kwenda kwa Eli na kusema, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.”Eli akasema, “Mwanangu, sikukuita, rudi ukalale.” 7 Wakati huu Samweli alikuwa bado hajamjua BWANA. Neno la BWANA lilikuwa bado halijafunuliwa kwake. 8 BWANA akamwita Samweli mara ya tatu, naye Samweli akaamka kwenda kwa Eli na kusema, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.”Ndipo Eli akatambua kuwa BWANA alikuwa akimwita kijana. 9 Hivyo Eli akamwambia Samweli, “Nenda ukalale, na kama akikuita, sema, ‘Nena BWANA, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza.’ ” Hivyo Samweli akaenda na kulala mahali pake. 10 BWANA akaja akasimama hapo, akiita kama mara zile nyingine, “Samweli! Samweli!”Kisha Samweli akasema, “Nena BWANA, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza.” 11 Naye BWANA akamwambia Samweli: “Tazama, nipo karibu kufanya kitu katika Israeli ambacho kitafanya masikio ya kila mmoja atakayesikia yawashe. 12 Wakati huo nitatimiza dhidi ya Eli kila kitu nilichonena dhidi ya jamaa yake, kuanzia mwanzo mpaka mwisho. 13 Kwa kuwa nilimwambia kwamba ningehukumu jamaa yake milele kwa sababu ya dhambi aliyoijua, wanawe kumkufuru Mungu, naye akashindwa kuwazuia. 14 Kwa hiyo, nikaapa kuhusu nyumba ya Eli, ‘Hatia ya nyumba ya Eli kamwe haitaweza kufidiwa kwa dhabihu au sadaka.’ ” 15 Samweli akalala mpaka asubuhi, kisha akafungua milango ya nyumba ya BWANA. Aliogopa kumwambia Eli yale maono, 16 lakini Eli akamwita na kumwambia, “Samweli mwanangu.”Samweli akamjibu, “Mimi hapa.” 17 Eli akamuuliza, “Ni nini alichokuambia? Usinifiche. BWANA na ashughulike nawe, tena kwa ukali, kama utanificha chochote alichokuambia.” 18 Kwa hiyo Samweli akamwambia kila kitu, bila kumficha chochote. Ndipo Eli akasema, “Yeye ni BWANA; na afanye lile lililo jema machoni pake!” 19 BWANA alikuwa pamoja na Samweli alipokuwa akikua, na hakuacha hata moja ya maneno yake lianguke chini. 20 Nao Israeli wote kuanzia Dani hadi Beer-Sheba wakatambua kuwa Samweli amethibitishwa kuwa nabii wa BWANA. 21 BWANA akaendelea kutokea huko Shilo, na huko kujidhihirisha kwa Samweli kwa njia ya neno lake.

In Other Versions

1 Samuel 3 in the ANGEFD

1 Samuel 3 in the ANTPNG2D

1 Samuel 3 in the AS21

1 Samuel 3 in the BAGH

1 Samuel 3 in the BBPNG

1 Samuel 3 in the BBT1E

1 Samuel 3 in the BDS

1 Samuel 3 in the BEV

1 Samuel 3 in the BHAD

1 Samuel 3 in the BIB

1 Samuel 3 in the BLPT

1 Samuel 3 in the BNT

1 Samuel 3 in the BNTABOOT

1 Samuel 3 in the BNTLV

1 Samuel 3 in the BOATCB

1 Samuel 3 in the BOATCB2

1 Samuel 3 in the BOBCV

1 Samuel 3 in the BOCNT

1 Samuel 3 in the BOECS

1 Samuel 3 in the BOGWICC

1 Samuel 3 in the BOHCB

1 Samuel 3 in the BOHCV

1 Samuel 3 in the BOHLNT

1 Samuel 3 in the BOHNTLTAL

1 Samuel 3 in the BOICB

1 Samuel 3 in the BOILNTAP

1 Samuel 3 in the BOITCV

1 Samuel 3 in the BOKCV2

1 Samuel 3 in the BOKHWOG

1 Samuel 3 in the BOKSSV

1 Samuel 3 in the BOLCB

1 Samuel 3 in the BOLCB2

1 Samuel 3 in the BOMCV

1 Samuel 3 in the BONAV

1 Samuel 3 in the BONCB

1 Samuel 3 in the BONLT

1 Samuel 3 in the BONUT2

1 Samuel 3 in the BOPLNT

1 Samuel 3 in the BOSCB

1 Samuel 3 in the BOSNC

1 Samuel 3 in the BOTLNT

1 Samuel 3 in the BOVCB

1 Samuel 3 in the BOYCB

1 Samuel 3 in the BPBB

1 Samuel 3 in the BPH

1 Samuel 3 in the BSB

1 Samuel 3 in the CCB

1 Samuel 3 in the CUV

1 Samuel 3 in the CUVS

1 Samuel 3 in the DBT

1 Samuel 3 in the DGDNT

1 Samuel 3 in the DHNT

1 Samuel 3 in the DNT

1 Samuel 3 in the ELBE

1 Samuel 3 in the EMTV

1 Samuel 3 in the ESV

1 Samuel 3 in the FBV

1 Samuel 3 in the FEB

1 Samuel 3 in the GGMNT

1 Samuel 3 in the GNT

1 Samuel 3 in the HARY

1 Samuel 3 in the HNT

1 Samuel 3 in the IRVA

1 Samuel 3 in the IRVB

1 Samuel 3 in the IRVG

1 Samuel 3 in the IRVH

1 Samuel 3 in the IRVK

1 Samuel 3 in the IRVM

1 Samuel 3 in the IRVM2

1 Samuel 3 in the IRVO

1 Samuel 3 in the IRVP

1 Samuel 3 in the IRVT

1 Samuel 3 in the IRVT2

1 Samuel 3 in the IRVU

1 Samuel 3 in the ISVN

1 Samuel 3 in the JSNT

1 Samuel 3 in the KAPI

1 Samuel 3 in the KBT1ETNIK

1 Samuel 3 in the KBV

1 Samuel 3 in the KJV

1 Samuel 3 in the KNFD

1 Samuel 3 in the LBA

1 Samuel 3 in the LBLA

1 Samuel 3 in the LNT

1 Samuel 3 in the LSV

1 Samuel 3 in the MAAL

1 Samuel 3 in the MBV

1 Samuel 3 in the MBV2

1 Samuel 3 in the MHNT

1 Samuel 3 in the MKNFD

1 Samuel 3 in the MNG

1 Samuel 3 in the MNT

1 Samuel 3 in the MNT2

1 Samuel 3 in the MRS1T

1 Samuel 3 in the NAA

1 Samuel 3 in the NASB

1 Samuel 3 in the NBLA

1 Samuel 3 in the NBS

1 Samuel 3 in the NBVTP

1 Samuel 3 in the NET2

1 Samuel 3 in the NIV11

1 Samuel 3 in the NNT

1 Samuel 3 in the NNT2

1 Samuel 3 in the NNT3

1 Samuel 3 in the PDDPT

1 Samuel 3 in the PFNT

1 Samuel 3 in the RMNT

1 Samuel 3 in the SBIAS

1 Samuel 3 in the SBIBS

1 Samuel 3 in the SBIBS2

1 Samuel 3 in the SBICS

1 Samuel 3 in the SBIDS

1 Samuel 3 in the SBIGS

1 Samuel 3 in the SBIHS

1 Samuel 3 in the SBIIS

1 Samuel 3 in the SBIIS2

1 Samuel 3 in the SBIIS3

1 Samuel 3 in the SBIKS

1 Samuel 3 in the SBIKS2

1 Samuel 3 in the SBIMS

1 Samuel 3 in the SBIOS

1 Samuel 3 in the SBIPS

1 Samuel 3 in the SBISS

1 Samuel 3 in the SBITS

1 Samuel 3 in the SBITS2

1 Samuel 3 in the SBITS3

1 Samuel 3 in the SBITS4

1 Samuel 3 in the SBIUS

1 Samuel 3 in the SBIVS

1 Samuel 3 in the SBT

1 Samuel 3 in the SBT1E

1 Samuel 3 in the SCHL

1 Samuel 3 in the SNT

1 Samuel 3 in the SUSU

1 Samuel 3 in the SUSU2

1 Samuel 3 in the SYNO

1 Samuel 3 in the TBIAOTANT

1 Samuel 3 in the TBT1E

1 Samuel 3 in the TBT1E2

1 Samuel 3 in the TFTIP

1 Samuel 3 in the TFTU

1 Samuel 3 in the TGNTATF3T

1 Samuel 3 in the THAI

1 Samuel 3 in the TNFD

1 Samuel 3 in the TNT

1 Samuel 3 in the TNTIK

1 Samuel 3 in the TNTIL

1 Samuel 3 in the TNTIN

1 Samuel 3 in the TNTIP

1 Samuel 3 in the TNTIZ

1 Samuel 3 in the TOMA

1 Samuel 3 in the TTENT

1 Samuel 3 in the UBG

1 Samuel 3 in the UGV

1 Samuel 3 in the UGV2

1 Samuel 3 in the UGV3

1 Samuel 3 in the VBL

1 Samuel 3 in the VDCC

1 Samuel 3 in the YALU

1 Samuel 3 in the YAPE

1 Samuel 3 in the YBVTP

1 Samuel 3 in the ZBP