2 Chronicles 21 (BOKCV)

1 Yehoshafati akalala na baba zake, akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi. Mwanawe Yehoramu akawa mfalme baada yake. 2 Ndugu zake Yehoramu, wana wa Yehoshafati walikuwa: Azaria, Yehieli, Zekaria, Azaria, Mikaeli na Shefatia. Hawa wote walikuwa wana wa Yehoshafati mfalme wa Israeli 3 Baba yao alikuwa amewapa zawadi nyingi za fedha na dhahabu na vitu vya thamani, pamoja na miji yenye ngome huko Yuda, bali ufalme akampa Yehoramu kwa sababu alikuwa mwanawe mzaliwa wa kwanza. 4 Baada ya Yehoramu kujiimarisha katika ufalme wa baba yake, akawaua kwa upanga ndugu zake wote pamoja na baadhi ya wakuu wa Israeli. 5 Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka minane. 6 Akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa imefanya, kwa kuwa alimwoa binti wa Ahabu. Akatenda maovu machoni pa BWANA. 7 Hata hivyo, kwa sababu ya Agano ambalo BWANA alikuwa amefanya na Daudi, BWANA hakuwa radhi kuangamiza nyumba ya Daudi. Mungu alikuwa ameahidi kuidumisha taa kwa ajili yake na wazao wake milele. 8 Wakati wa Yehoramu, Edomu waliasi dhidi ya Yuda na kujiwekea mfalme wao wenyewe. 9 Basi Yehoramu akaenda huko pamoja na maafisa wake na magari yake ya vita. Waedomu wakamzunguka yeye na majemadari wake wa magari yake ya vita, lakini akaondoka, akapenya usiku na kuwashambulia Waedomu. 10 Hadi leo Edomu wameasi dhidi ya Yuda.Libna pia wakaasi wakati huo huo kwa sababu Yehoramu alikuwa amemwacha BWANA, Mungu wa baba zake. 11 Alikuwa pia ametengeneza mahali pa juu pa kuabudia miungu katika vilima vya Yuda na akawa amewasababisha watu wa Yerusalemu kufanya uzinzi na akawa amewapotosha watu wa Yuda. 12 Yehoramu akapokea barua kutoka kwa nabii Eliya iliyosema:“Hili ndilo BWANA, Mungu wa Daudi baba yako, asemalo: ‘Hukuenenda katika njia za Yehoshafati baba yako au za Asa mfalme wa Yuda. 13 Lakini umeenenda katika njia za wafalme wa Israeli, nawe umewaongoza Yuda na watu wa Yerusalemu kuzini, kama vile nyumba ya Ahabu ilivyofanya. Pia umewaua ndugu zako mwenyewe, watu wa nyumbani mwa baba yako, watu waliokuwa bora kuliko wewe. 14 Hivyo basi BWANA yu karibu kuwapiga watu wako, wanao, wake zako na kila kitu kilicho chako, kwa pigo zito. 15 Wewe mwenyewe utaugua sana kwa ugonjwa wa tumbo kwa muda mrefu, hadi ugonjwa utakaposababisha matumbo yako kutoka nje.’ ” 16 BWANA akaamsha chuki ya Wafilisti na ya Waarabu walioishi karibu na Wakushi dhidi ya Yehoramu. 17 Wakaishambulia Yuda, wakaivamia na kuchukua mali zote zilizopatikana katika jumba la mfalme pamoja na wanawe na wake zake. Hakubakiziwa mwana yeyote isipokuwa Ahazia aliyekuwa mdogo wa wote. 18 Baada ya mambo haya yote, BWANA akampiga Yehoramu kwa ugonjwa usioponyeka wa matumbo. 19 Ikawa baada ya muda, mwisho wa mwaka wa pili, matumbo yake yakatoka nje kwa sababu ya ugonjwa, naye akafa katika maumivu makali sana. Watu wake hawakuwasha moto kwa heshima yake, kama walivyokuwa wamewafanyia baba zake. 20 Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipokuwa mfalme, naye akatawala huko Yerusalemu miaka minane. Akafa, bila kusikitikiwa na mtu yeyote, naye akazikwa katika Mji wa Daudi, lakini si katika makaburi ya wafalme.

In Other Versions

2 Chronicles 21 in the ANGEFD

2 Chronicles 21 in the ANTPNG2D

2 Chronicles 21 in the AS21

2 Chronicles 21 in the BAGH

2 Chronicles 21 in the BBPNG

2 Chronicles 21 in the BBT1E

2 Chronicles 21 in the BDS

2 Chronicles 21 in the BEV

2 Chronicles 21 in the BHAD

2 Chronicles 21 in the BIB

2 Chronicles 21 in the BLPT

2 Chronicles 21 in the BNT

2 Chronicles 21 in the BNTABOOT

2 Chronicles 21 in the BNTLV

2 Chronicles 21 in the BOATCB

2 Chronicles 21 in the BOATCB2

2 Chronicles 21 in the BOBCV

2 Chronicles 21 in the BOCNT

2 Chronicles 21 in the BOECS

2 Chronicles 21 in the BOGWICC

2 Chronicles 21 in the BOHCB

2 Chronicles 21 in the BOHCV

2 Chronicles 21 in the BOHLNT

2 Chronicles 21 in the BOHNTLTAL

2 Chronicles 21 in the BOICB

2 Chronicles 21 in the BOILNTAP

2 Chronicles 21 in the BOITCV

2 Chronicles 21 in the BOKCV2

2 Chronicles 21 in the BOKHWOG

2 Chronicles 21 in the BOKSSV

2 Chronicles 21 in the BOLCB

2 Chronicles 21 in the BOLCB2

2 Chronicles 21 in the BOMCV

2 Chronicles 21 in the BONAV

2 Chronicles 21 in the BONCB

2 Chronicles 21 in the BONLT

2 Chronicles 21 in the BONUT2

2 Chronicles 21 in the BOPLNT

2 Chronicles 21 in the BOSCB

2 Chronicles 21 in the BOSNC

2 Chronicles 21 in the BOTLNT

2 Chronicles 21 in the BOVCB

2 Chronicles 21 in the BOYCB

2 Chronicles 21 in the BPBB

2 Chronicles 21 in the BPH

2 Chronicles 21 in the BSB

2 Chronicles 21 in the CCB

2 Chronicles 21 in the CUV

2 Chronicles 21 in the CUVS

2 Chronicles 21 in the DBT

2 Chronicles 21 in the DGDNT

2 Chronicles 21 in the DHNT

2 Chronicles 21 in the DNT

2 Chronicles 21 in the ELBE

2 Chronicles 21 in the EMTV

2 Chronicles 21 in the ESV

2 Chronicles 21 in the FBV

2 Chronicles 21 in the FEB

2 Chronicles 21 in the GGMNT

2 Chronicles 21 in the GNT

2 Chronicles 21 in the HARY

2 Chronicles 21 in the HNT

2 Chronicles 21 in the IRVA

2 Chronicles 21 in the IRVB

2 Chronicles 21 in the IRVG

2 Chronicles 21 in the IRVH

2 Chronicles 21 in the IRVK

2 Chronicles 21 in the IRVM

2 Chronicles 21 in the IRVM2

2 Chronicles 21 in the IRVO

2 Chronicles 21 in the IRVP

2 Chronicles 21 in the IRVT

2 Chronicles 21 in the IRVT2

2 Chronicles 21 in the IRVU

2 Chronicles 21 in the ISVN

2 Chronicles 21 in the JSNT

2 Chronicles 21 in the KAPI

2 Chronicles 21 in the KBT1ETNIK

2 Chronicles 21 in the KBV

2 Chronicles 21 in the KJV

2 Chronicles 21 in the KNFD

2 Chronicles 21 in the LBA

2 Chronicles 21 in the LBLA

2 Chronicles 21 in the LNT

2 Chronicles 21 in the LSV

2 Chronicles 21 in the MAAL

2 Chronicles 21 in the MBV

2 Chronicles 21 in the MBV2

2 Chronicles 21 in the MHNT

2 Chronicles 21 in the MKNFD

2 Chronicles 21 in the MNG

2 Chronicles 21 in the MNT

2 Chronicles 21 in the MNT2

2 Chronicles 21 in the MRS1T

2 Chronicles 21 in the NAA

2 Chronicles 21 in the NASB

2 Chronicles 21 in the NBLA

2 Chronicles 21 in the NBS

2 Chronicles 21 in the NBVTP

2 Chronicles 21 in the NET2

2 Chronicles 21 in the NIV11

2 Chronicles 21 in the NNT

2 Chronicles 21 in the NNT2

2 Chronicles 21 in the NNT3

2 Chronicles 21 in the PDDPT

2 Chronicles 21 in the PFNT

2 Chronicles 21 in the RMNT

2 Chronicles 21 in the SBIAS

2 Chronicles 21 in the SBIBS

2 Chronicles 21 in the SBIBS2

2 Chronicles 21 in the SBICS

2 Chronicles 21 in the SBIDS

2 Chronicles 21 in the SBIGS

2 Chronicles 21 in the SBIHS

2 Chronicles 21 in the SBIIS

2 Chronicles 21 in the SBIIS2

2 Chronicles 21 in the SBIIS3

2 Chronicles 21 in the SBIKS

2 Chronicles 21 in the SBIKS2

2 Chronicles 21 in the SBIMS

2 Chronicles 21 in the SBIOS

2 Chronicles 21 in the SBIPS

2 Chronicles 21 in the SBISS

2 Chronicles 21 in the SBITS

2 Chronicles 21 in the SBITS2

2 Chronicles 21 in the SBITS3

2 Chronicles 21 in the SBITS4

2 Chronicles 21 in the SBIUS

2 Chronicles 21 in the SBIVS

2 Chronicles 21 in the SBT

2 Chronicles 21 in the SBT1E

2 Chronicles 21 in the SCHL

2 Chronicles 21 in the SNT

2 Chronicles 21 in the SUSU

2 Chronicles 21 in the SUSU2

2 Chronicles 21 in the SYNO

2 Chronicles 21 in the TBIAOTANT

2 Chronicles 21 in the TBT1E

2 Chronicles 21 in the TBT1E2

2 Chronicles 21 in the TFTIP

2 Chronicles 21 in the TFTU

2 Chronicles 21 in the TGNTATF3T

2 Chronicles 21 in the THAI

2 Chronicles 21 in the TNFD

2 Chronicles 21 in the TNT

2 Chronicles 21 in the TNTIK

2 Chronicles 21 in the TNTIL

2 Chronicles 21 in the TNTIN

2 Chronicles 21 in the TNTIP

2 Chronicles 21 in the TNTIZ

2 Chronicles 21 in the TOMA

2 Chronicles 21 in the TTENT

2 Chronicles 21 in the UBG

2 Chronicles 21 in the UGV

2 Chronicles 21 in the UGV2

2 Chronicles 21 in the UGV3

2 Chronicles 21 in the VBL

2 Chronicles 21 in the VDCC

2 Chronicles 21 in the YALU

2 Chronicles 21 in the YAPE

2 Chronicles 21 in the YBVTP

2 Chronicles 21 in the ZBP