2 Chronicles 3 (BOKCV)
1 Ndipo Solomoni akaanza kujenga Hekalu la BWANA katika Yerusalemu juu ya Mlima Moria, pale ambapo BWANA alikuwa amemtokea Daudi baba yake. Ilikuwa katika kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi, mahali palipotolewa na Daudi. 2 Alianza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili katika mwaka wa nne wa utawala wake. 3 Msingi aliouweka Solomoni kwa ajili ya kulijenga Hekalu la Mungu ulikuwa urefu wa dhiraa sitini na upana dhiraa ishirini. 4 Ukumbi wa mbele wa Hekalu ulikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, yaani, kuanzia upande mmoja hadi upande mwingine wa upana wa nyumba hiyo na kimo chake dhiraa thelathini.Akaufunika ndani kwa dhahabu safi. 5 Akaufunika ukumbi mkuu kwa mbao za miberoshi na kufunikwa kwa dhahabu safi na kuupamba kwa miti ya mitende na kuifanyizia kwa minyororo. 6 Alilipamba Hekalu kwa vito vya thamani. Hiyo dhahabu aliyotumia ilikuwa dhahabu ya Parvaimu. 7 Akazifunika boriti za dari, miimo na vizingiti vya milango, kuta na milango ya Hekalu kwa dhahabu, naye akatia nakshi ya makerubi kwenye kuta. 8 Akajenga Patakatifu pa Patakatifu, urefu na upana wake ulikuwa dhiraa ishirini, sawasawa na upana wa Hekalu. Alifunika ndani kwa talanta 120 za dhahabu safi. 9 Misumari ya dhahabu ilikuwa na uzito wa shekeli hamsini. Alivifunika pia vyumba vya juu kwa dhahabu. 10 Katika sehemu ya Patakatifu pa Patakatifu akafanyiza jozi moja ya makerubi ya kuchongwa na kuyafunika kwa dhahabu. 11 Urefu wa mabawa ya hao makerubi ulikuwa jumla ya dhiraa ishirini. Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa dhiraa tano, nalo liligusa ukuta wa Hekalu, bawa lake lingine, lilikuwa pia na urefu wa dhiraa tano, ambalo liligusa bawa la kerubi lingine. 12 Vivyo hivyo bawa moja la kerubi wa pili lilikuwa na urefu wa dhiraa tano na liligusa ukuta mwingine wa pili wa Hekalu na bawa lake lingine, lilikuwa pia na urefu wa dhiraa tano nalo liligusa bawa la kerubi wa kwanza. 13 Mabawa ya makerubi hawa yalitanda dhiraa ishirini. Walisimama kwa miguu yao, nyuso zao zikielekea ukumbi mkubwa. 14 Akatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na za kitani safi, na kutarizi makerubi juu yake. 15 Mbele ya Hekalu Solomoni akatengeneza nguzo mbili, ambazo kwa pamoja zilikuwa na dhiraa thelathini na tano kwenda juu kwake, na urefu wa kila moja ilikuwa na taji juu yake yenye dhiraa tano. 16 Akatengeneza minyororo iliyosokotwa, na kuiweka juu ya zile nguzo. Pia akatengeneza makomamanga 100, na kuyashikamanisha kwenye minyororo. 17 Akazisimamisha hizo nguzo mbele ya Hekalu, moja upande wa kusini na nyingine upande wa kaskazini. Ile moja ya upande wa kusini akaiita Yakini, na ya upande wa kaskazini akaiita Boazi.
In Other Versions
2 Chronicles 3 in the ANGEFD
2 Chronicles 3 in the ANTPNG2D
2 Chronicles 3 in the AS21
2 Chronicles 3 in the BAGH
2 Chronicles 3 in the BBPNG
2 Chronicles 3 in the BBT1E
2 Chronicles 3 in the BDS
2 Chronicles 3 in the BEV
2 Chronicles 3 in the BHAD
2 Chronicles 3 in the BIB
2 Chronicles 3 in the BLPT
2 Chronicles 3 in the BNT
2 Chronicles 3 in the BNTABOOT
2 Chronicles 3 in the BNTLV
2 Chronicles 3 in the BOATCB
2 Chronicles 3 in the BOATCB2
2 Chronicles 3 in the BOBCV
2 Chronicles 3 in the BOCNT
2 Chronicles 3 in the BOECS
2 Chronicles 3 in the BOGWICC
2 Chronicles 3 in the BOHCB
2 Chronicles 3 in the BOHCV
2 Chronicles 3 in the BOHLNT
2 Chronicles 3 in the BOHNTLTAL
2 Chronicles 3 in the BOICB
2 Chronicles 3 in the BOILNTAP
2 Chronicles 3 in the BOITCV
2 Chronicles 3 in the BOKCV2
2 Chronicles 3 in the BOKHWOG
2 Chronicles 3 in the BOKSSV
2 Chronicles 3 in the BOLCB
2 Chronicles 3 in the BOLCB2
2 Chronicles 3 in the BOMCV
2 Chronicles 3 in the BONAV
2 Chronicles 3 in the BONCB
2 Chronicles 3 in the BONLT
2 Chronicles 3 in the BONUT2
2 Chronicles 3 in the BOPLNT
2 Chronicles 3 in the BOSCB
2 Chronicles 3 in the BOSNC
2 Chronicles 3 in the BOTLNT
2 Chronicles 3 in the BOVCB
2 Chronicles 3 in the BOYCB
2 Chronicles 3 in the BPBB
2 Chronicles 3 in the BPH
2 Chronicles 3 in the BSB
2 Chronicles 3 in the CCB
2 Chronicles 3 in the CUV
2 Chronicles 3 in the CUVS
2 Chronicles 3 in the DBT
2 Chronicles 3 in the DGDNT
2 Chronicles 3 in the DHNT
2 Chronicles 3 in the DNT
2 Chronicles 3 in the ELBE
2 Chronicles 3 in the EMTV
2 Chronicles 3 in the ESV
2 Chronicles 3 in the FBV
2 Chronicles 3 in the FEB
2 Chronicles 3 in the GGMNT
2 Chronicles 3 in the GNT
2 Chronicles 3 in the HARY
2 Chronicles 3 in the HNT
2 Chronicles 3 in the IRVA
2 Chronicles 3 in the IRVB
2 Chronicles 3 in the IRVG
2 Chronicles 3 in the IRVH
2 Chronicles 3 in the IRVK
2 Chronicles 3 in the IRVM
2 Chronicles 3 in the IRVM2
2 Chronicles 3 in the IRVO
2 Chronicles 3 in the IRVP
2 Chronicles 3 in the IRVT
2 Chronicles 3 in the IRVT2
2 Chronicles 3 in the IRVU
2 Chronicles 3 in the ISVN
2 Chronicles 3 in the JSNT
2 Chronicles 3 in the KAPI
2 Chronicles 3 in the KBT1ETNIK
2 Chronicles 3 in the KBV
2 Chronicles 3 in the KJV
2 Chronicles 3 in the KNFD
2 Chronicles 3 in the LBA
2 Chronicles 3 in the LBLA
2 Chronicles 3 in the LNT
2 Chronicles 3 in the LSV
2 Chronicles 3 in the MAAL
2 Chronicles 3 in the MBV
2 Chronicles 3 in the MBV2
2 Chronicles 3 in the MHNT
2 Chronicles 3 in the MKNFD
2 Chronicles 3 in the MNG
2 Chronicles 3 in the MNT
2 Chronicles 3 in the MNT2
2 Chronicles 3 in the MRS1T
2 Chronicles 3 in the NAA
2 Chronicles 3 in the NASB
2 Chronicles 3 in the NBLA
2 Chronicles 3 in the NBS
2 Chronicles 3 in the NBVTP
2 Chronicles 3 in the NET2
2 Chronicles 3 in the NIV11
2 Chronicles 3 in the NNT
2 Chronicles 3 in the NNT2
2 Chronicles 3 in the NNT3
2 Chronicles 3 in the PDDPT
2 Chronicles 3 in the PFNT
2 Chronicles 3 in the RMNT
2 Chronicles 3 in the SBIAS
2 Chronicles 3 in the SBIBS
2 Chronicles 3 in the SBIBS2
2 Chronicles 3 in the SBICS
2 Chronicles 3 in the SBIDS
2 Chronicles 3 in the SBIGS
2 Chronicles 3 in the SBIHS
2 Chronicles 3 in the SBIIS
2 Chronicles 3 in the SBIIS2
2 Chronicles 3 in the SBIIS3
2 Chronicles 3 in the SBIKS
2 Chronicles 3 in the SBIKS2
2 Chronicles 3 in the SBIMS
2 Chronicles 3 in the SBIOS
2 Chronicles 3 in the SBIPS
2 Chronicles 3 in the SBISS
2 Chronicles 3 in the SBITS
2 Chronicles 3 in the SBITS2
2 Chronicles 3 in the SBITS3
2 Chronicles 3 in the SBITS4
2 Chronicles 3 in the SBIUS
2 Chronicles 3 in the SBIVS
2 Chronicles 3 in the SBT
2 Chronicles 3 in the SBT1E
2 Chronicles 3 in the SCHL
2 Chronicles 3 in the SNT
2 Chronicles 3 in the SUSU
2 Chronicles 3 in the SUSU2
2 Chronicles 3 in the SYNO
2 Chronicles 3 in the TBIAOTANT
2 Chronicles 3 in the TBT1E
2 Chronicles 3 in the TBT1E2
2 Chronicles 3 in the TFTIP
2 Chronicles 3 in the TFTU
2 Chronicles 3 in the TGNTATF3T
2 Chronicles 3 in the THAI
2 Chronicles 3 in the TNFD
2 Chronicles 3 in the TNT
2 Chronicles 3 in the TNTIK
2 Chronicles 3 in the TNTIL
2 Chronicles 3 in the TNTIN
2 Chronicles 3 in the TNTIP
2 Chronicles 3 in the TNTIZ
2 Chronicles 3 in the TOMA
2 Chronicles 3 in the TTENT
2 Chronicles 3 in the UBG
2 Chronicles 3 in the UGV
2 Chronicles 3 in the UGV2
2 Chronicles 3 in the UGV3
2 Chronicles 3 in the VBL
2 Chronicles 3 in the VDCC
2 Chronicles 3 in the YALU
2 Chronicles 3 in the YAPE
2 Chronicles 3 in the YBVTP
2 Chronicles 3 in the ZBP