2 Corinthians 1 (BOKCV)

1 Barua hii ni kutoka kwangu mimi Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu,Kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, pamoja na watakatifu wote walioko Akaya yote: 2 Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo iwe nanyi. 3 Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa huruma na Mungu wa faraja yote. 4 Yeye hutufariji katika taabu zetu, ili tuweze kuwafariji walio katika taabu yoyote kwa faraja ambayo sisi wenyewe tumepokea kutoka kwa Mungu. 5 Kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi ndani ya maisha yetu, hivyo ndivyo faraja yetu inavyofurika kwa njia ya Kristo. 6 Kama tunataabika, ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu; kama tukifarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu, iwaleteayo saburi ya mateso yale yale yanayotupata. 7 Nalo tumaini letu kwenu ni thabiti, kwa sababu tunajua kwamba kama vile mnavyoshiriki mateso yetu, ndivyo pia mnavyoshiriki katika faraja yetu. 8 Ndugu wapendwa, hatutaki mkose kujua kuhusu zile taabu tulizopata huko Asia. Kwa maana tulilemewa na mizigo sana, kiasi cha kushindwa kuvumilia, hata tulikata tamaa ya kuishi. 9 Kwa kweli, mioyoni mwetu tulihisi tumekabiliwa na hukumu ya kifo, ili tusijitegemee sisi wenyewe bali tumtegemee Mungu afufuaye wafu. 10 Yeye aliyetuokoa kwenye hatari kubwa ya kifo na atatuokoa tena. Kwake yeye tumeweka tumaini letu kwamba ataendelea kutuokoa. 11 Kama vile mlivyoungana kusaidiana nasi katika maombi, hivyo wengi watatoa shukrani kwa niaba yetu kwa ajili ya baraka za neema tulizopata kwa majibu ya maombi ya wengi. 12 Basi haya ndiyo majivuno yetu: Dhamiri yetu inatushuhudia kwamba tumeenenda katika ulimwengu na hasa katika uhusiano wetu na ninyi, katika utakatifu na uaminifu utokao kwa Mungu. Hatukufanya hivyo kwa hekima ya kidunia bali kwa neema ya Mungu. 13 Kwa maana hatuwaandikii mambo ambayo hamwezi kusoma au kuyaelewa. Natumaini kwamba, 14 kama vile mlivyotuelewa kwa sehemu, mtakuja kuelewa kwa ukamilifu ili mweze kujivuna kwa ajili yetu, kama na sisi tutakavyojivuna kwa ajili yenu katika siku ya Bwana Yesu. 15 Kwa kuwa nilikuwa na uhakika wa mambo haya, nilitaka nije kwenu kwanza, ili mpate faida mara mbili. 16 Nilipanga kuwatembelea nikiwa safarini kwenda Makedonia na kurudi tena kwenu nikitoka Makedonia, ili mnisafirishe katika safari yangu ya kwenda Uyahudi. 17 Nilipopanga jambo hili, je, nilikuwa kigeugeu? Au ninafanya mipango yangu kwa hali ya mwili, ili niseme, “Ndiyo, ndiyo” na “Siyo, siyo” wakati huo huo? 18 Hakika kama Mungu alivyo mwaminifu, maneno yetu kwenu hayajawa “Ndiyo na Siyo.” 19 Kwa kuwa Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, ambaye tulimhubiri kwenu: Mimi, Silvano na Timotheo, hakuwa “Ndiyo” na “Siyo,” bali kwake yeye siku zote ni “Ndiyo.” 20 Kwa maana ahadi zote za Mungu zilizo katika Kristo ni “Ndiyo.” Kwa sababu hii ni kwake yeye tunasema “Amen” kwa utukufu wa Mungu. 21 Basi ni Mungu atufanyaye sisi pamoja nanyi kusimama imara katika Kristo. Ametutia mafuta 22 kwa kututia muhuri wake na kutupa Roho wake mioyoni mwetu kuwa rehani kwa ajili ya kututhibitishia kile kijacho. 23 Mungu ni shahidi wangu kwamba ilikuwa ni kwa ajili ya kuwahurumia ninyi sikurudi Korintho. 24 Si kwamba tunatawala imani yenu, bali twatenda kazi pamoja nanyi kwa ajili ya furaha yenu, kwa sababu ni kwa imani mwasimama imara.

In Other Versions

2 Corinthians 1 in the ANGEFD

2 Corinthians 1 in the ANTPNG2D

2 Corinthians 1 in the AS21

2 Corinthians 1 in the BAGH

2 Corinthians 1 in the BBPNG

2 Corinthians 1 in the BBT1E

2 Corinthians 1 in the BDS

2 Corinthians 1 in the BEV

2 Corinthians 1 in the BHAD

2 Corinthians 1 in the BIB

2 Corinthians 1 in the BLPT

2 Corinthians 1 in the BNT

2 Corinthians 1 in the BNTABOOT

2 Corinthians 1 in the BNTLV

2 Corinthians 1 in the BOATCB

2 Corinthians 1 in the BOATCB2

2 Corinthians 1 in the BOBCV

2 Corinthians 1 in the BOCNT

2 Corinthians 1 in the BOECS

2 Corinthians 1 in the BOGWICC

2 Corinthians 1 in the BOHCB

2 Corinthians 1 in the BOHCV

2 Corinthians 1 in the BOHLNT

2 Corinthians 1 in the BOHNTLTAL

2 Corinthians 1 in the BOICB

2 Corinthians 1 in the BOILNTAP

2 Corinthians 1 in the BOITCV

2 Corinthians 1 in the BOKCV2

2 Corinthians 1 in the BOKHWOG

2 Corinthians 1 in the BOKSSV

2 Corinthians 1 in the BOLCB

2 Corinthians 1 in the BOLCB2

2 Corinthians 1 in the BOMCV

2 Corinthians 1 in the BONAV

2 Corinthians 1 in the BONCB

2 Corinthians 1 in the BONLT

2 Corinthians 1 in the BONUT2

2 Corinthians 1 in the BOPLNT

2 Corinthians 1 in the BOSCB

2 Corinthians 1 in the BOSNC

2 Corinthians 1 in the BOTLNT

2 Corinthians 1 in the BOVCB

2 Corinthians 1 in the BOYCB

2 Corinthians 1 in the BPBB

2 Corinthians 1 in the BPH

2 Corinthians 1 in the BSB

2 Corinthians 1 in the CCB

2 Corinthians 1 in the CUV

2 Corinthians 1 in the CUVS

2 Corinthians 1 in the DBT

2 Corinthians 1 in the DGDNT

2 Corinthians 1 in the DHNT

2 Corinthians 1 in the DNT

2 Corinthians 1 in the ELBE

2 Corinthians 1 in the EMTV

2 Corinthians 1 in the ESV

2 Corinthians 1 in the FBV

2 Corinthians 1 in the FEB

2 Corinthians 1 in the GGMNT

2 Corinthians 1 in the GNT

2 Corinthians 1 in the HARY

2 Corinthians 1 in the HNT

2 Corinthians 1 in the IRVA

2 Corinthians 1 in the IRVB

2 Corinthians 1 in the IRVG

2 Corinthians 1 in the IRVH

2 Corinthians 1 in the IRVK

2 Corinthians 1 in the IRVM

2 Corinthians 1 in the IRVM2

2 Corinthians 1 in the IRVO

2 Corinthians 1 in the IRVP

2 Corinthians 1 in the IRVT

2 Corinthians 1 in the IRVT2

2 Corinthians 1 in the IRVU

2 Corinthians 1 in the ISVN

2 Corinthians 1 in the JSNT

2 Corinthians 1 in the KAPI

2 Corinthians 1 in the KBT1ETNIK

2 Corinthians 1 in the KBV

2 Corinthians 1 in the KJV

2 Corinthians 1 in the KNFD

2 Corinthians 1 in the LBA

2 Corinthians 1 in the LBLA

2 Corinthians 1 in the LNT

2 Corinthians 1 in the LSV

2 Corinthians 1 in the MAAL

2 Corinthians 1 in the MBV

2 Corinthians 1 in the MBV2

2 Corinthians 1 in the MHNT

2 Corinthians 1 in the MKNFD

2 Corinthians 1 in the MNG

2 Corinthians 1 in the MNT

2 Corinthians 1 in the MNT2

2 Corinthians 1 in the MRS1T

2 Corinthians 1 in the NAA

2 Corinthians 1 in the NASB

2 Corinthians 1 in the NBLA

2 Corinthians 1 in the NBS

2 Corinthians 1 in the NBVTP

2 Corinthians 1 in the NET2

2 Corinthians 1 in the NIV11

2 Corinthians 1 in the NNT

2 Corinthians 1 in the NNT2

2 Corinthians 1 in the NNT3

2 Corinthians 1 in the PDDPT

2 Corinthians 1 in the PFNT

2 Corinthians 1 in the RMNT

2 Corinthians 1 in the SBIAS

2 Corinthians 1 in the SBIBS

2 Corinthians 1 in the SBIBS2

2 Corinthians 1 in the SBICS

2 Corinthians 1 in the SBIDS

2 Corinthians 1 in the SBIGS

2 Corinthians 1 in the SBIHS

2 Corinthians 1 in the SBIIS

2 Corinthians 1 in the SBIIS2

2 Corinthians 1 in the SBIIS3

2 Corinthians 1 in the SBIKS

2 Corinthians 1 in the SBIKS2

2 Corinthians 1 in the SBIMS

2 Corinthians 1 in the SBIOS

2 Corinthians 1 in the SBIPS

2 Corinthians 1 in the SBISS

2 Corinthians 1 in the SBITS

2 Corinthians 1 in the SBITS2

2 Corinthians 1 in the SBITS3

2 Corinthians 1 in the SBITS4

2 Corinthians 1 in the SBIUS

2 Corinthians 1 in the SBIVS

2 Corinthians 1 in the SBT

2 Corinthians 1 in the SBT1E

2 Corinthians 1 in the SCHL

2 Corinthians 1 in the SNT

2 Corinthians 1 in the SUSU

2 Corinthians 1 in the SUSU2

2 Corinthians 1 in the SYNO

2 Corinthians 1 in the TBIAOTANT

2 Corinthians 1 in the TBT1E

2 Corinthians 1 in the TBT1E2

2 Corinthians 1 in the TFTIP

2 Corinthians 1 in the TFTU

2 Corinthians 1 in the TGNTATF3T

2 Corinthians 1 in the THAI

2 Corinthians 1 in the TNFD

2 Corinthians 1 in the TNT

2 Corinthians 1 in the TNTIK

2 Corinthians 1 in the TNTIL

2 Corinthians 1 in the TNTIN

2 Corinthians 1 in the TNTIP

2 Corinthians 1 in the TNTIZ

2 Corinthians 1 in the TOMA

2 Corinthians 1 in the TTENT

2 Corinthians 1 in the UBG

2 Corinthians 1 in the UGV

2 Corinthians 1 in the UGV2

2 Corinthians 1 in the UGV3

2 Corinthians 1 in the VBL

2 Corinthians 1 in the VDCC

2 Corinthians 1 in the YALU

2 Corinthians 1 in the YAPE

2 Corinthians 1 in the YBVTP

2 Corinthians 1 in the ZBP