2 Corinthians 5 (BOKCV)
1 Kwa maana twajua kama hema yetu ya dunia tunayoishi ikiharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu, nyumba iliyo ya milele kule mbinguni, isiyojengwa kwa mikono ya wanadamu. 2 Katika hema hii twalia kwa uchungu, tukitamani kuvikwa makao yetu ya mbinguni, 3 kwa kuwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tena kuwa uchi. 4 Kwa kuwa tukiwa bado katika hema hii twalia kwa uchungu na kulemewa, kwa sababu hatutaki kuvuliwa bali kuvikwa makao yetu ya mbinguni ili kwamba kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima. 5 Basi Mungu ndiye alitufanya kwa ajili ya jambo lilo hilo naye ametupa Roho Mtakatifu kuwa amana, akituhakikishia ahadi ya kile kijacho. 6 Kwa hiyo siku zote tunalo tumaini, hata ingawa tunajua kwamba wakati tukiwa katika mwili huu, tuko mbali na Bwana, 7 kwa maana twaenenda kwa imani wala si kwa kuona. 8 Naam, tunalo tumaini na ingekuwa bora zaidi kuuacha mwili huu na kwenda kukaa na Bwana. 9 Kwa hiyo, kama tuko katika mwili huu au tuko mbali nao, lengo letu ni kumpendeza Bwana. 10 Kwa kuwa sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mmoja apate kulipwa kwa ajili ya yale ambayo yametendwa katika mwili wake, yakiwa mema au mabaya. 11 Basi, kwa kuwa tunajua kumcha Bwana, tunajitahidi kuwavuta wengine. Lakini Mungu anatufahamu dhahiri, nami natumaini kwamba tu dhahiri katika dhamiri zenu pia. 12 Sio kwamba tunajaribu kujistahilisha kwenu tena, lakini tunataka kuwapa nafasi ili mwone fahari juu yetu mweze kuwajibu hao wanaoona fahari juu ya mambo yanayoonekana badala ya mambo yaliyo moyoni. 13 Kama tumerukwa na akili, ni kwa ajili ya Mungu; kama tuna akili timamu, ni kwa ajili yenu. 14 Kwa kuwa upendo wa Kristo unatutia nguvu, kwa sababu tunasadiki kuwa mmoja alikufa kwa ajili ya wote, kwa hiyo wote walikufa. 15 Naye alikufa kwa ajili ya watu wote, ili kwamba wote wanaoishi wasiishi tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa na kufufuliwa tena kwa ajili yao. 16 Hivyo tangu sasa hatumwangalii mtu yeyote kwa mtazamo wa kibinadamu. Ingawa wakati fulani tulimwangalia Kristo kwa namna ya kibinadamu, hatumwangalii tena hivyo. 17 Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya. 18 Haya yote yanatokana na Mungu, ambaye ametupatanisha sisi na nafsi yake kwa njia ya Yesu Kristo na kutupata sisi huduma ya upatanisho: 19 Kwamba Mungu alikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake mwenyewe, akiwa hawahesabii watu dhambi zao. Naye ametukabidhi sisi ujumbe huu wa upatanisho. 20 Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Kristo, kana kwamba Mungu anawasihi kupitia kwa vinywa vyetu. Nasi twawaomba sana ninyi kwa niaba ya Kristo, mpatanishwe na Mungu. 21 Kwa maana Mungu alimfanya yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu kwake yeye.
In Other Versions
2 Corinthians 5 in the ANGEFD
2 Corinthians 5 in the ANTPNG2D
2 Corinthians 5 in the AS21
2 Corinthians 5 in the BAGH
2 Corinthians 5 in the BBPNG
2 Corinthians 5 in the BBT1E
2 Corinthians 5 in the BDS
2 Corinthians 5 in the BEV
2 Corinthians 5 in the BHAD
2 Corinthians 5 in the BIB
2 Corinthians 5 in the BLPT
2 Corinthians 5 in the BNT
2 Corinthians 5 in the BNTABOOT
2 Corinthians 5 in the BNTLV
2 Corinthians 5 in the BOATCB
2 Corinthians 5 in the BOATCB2
2 Corinthians 5 in the BOBCV
2 Corinthians 5 in the BOCNT
2 Corinthians 5 in the BOECS
2 Corinthians 5 in the BOGWICC
2 Corinthians 5 in the BOHCB
2 Corinthians 5 in the BOHCV
2 Corinthians 5 in the BOHLNT
2 Corinthians 5 in the BOHNTLTAL
2 Corinthians 5 in the BOICB
2 Corinthians 5 in the BOILNTAP
2 Corinthians 5 in the BOITCV
2 Corinthians 5 in the BOKCV2
2 Corinthians 5 in the BOKHWOG
2 Corinthians 5 in the BOKSSV
2 Corinthians 5 in the BOLCB
2 Corinthians 5 in the BOLCB2
2 Corinthians 5 in the BOMCV
2 Corinthians 5 in the BONAV
2 Corinthians 5 in the BONCB
2 Corinthians 5 in the BONLT
2 Corinthians 5 in the BONUT2
2 Corinthians 5 in the BOPLNT
2 Corinthians 5 in the BOSCB
2 Corinthians 5 in the BOSNC
2 Corinthians 5 in the BOTLNT
2 Corinthians 5 in the BOVCB
2 Corinthians 5 in the BOYCB
2 Corinthians 5 in the BPBB
2 Corinthians 5 in the BPH
2 Corinthians 5 in the BSB
2 Corinthians 5 in the CCB
2 Corinthians 5 in the CUV
2 Corinthians 5 in the CUVS
2 Corinthians 5 in the DBT
2 Corinthians 5 in the DGDNT
2 Corinthians 5 in the DHNT
2 Corinthians 5 in the DNT
2 Corinthians 5 in the ELBE
2 Corinthians 5 in the EMTV
2 Corinthians 5 in the ESV
2 Corinthians 5 in the FBV
2 Corinthians 5 in the FEB
2 Corinthians 5 in the GGMNT
2 Corinthians 5 in the GNT
2 Corinthians 5 in the HARY
2 Corinthians 5 in the HNT
2 Corinthians 5 in the IRVA
2 Corinthians 5 in the IRVB
2 Corinthians 5 in the IRVG
2 Corinthians 5 in the IRVH
2 Corinthians 5 in the IRVK
2 Corinthians 5 in the IRVM
2 Corinthians 5 in the IRVM2
2 Corinthians 5 in the IRVO
2 Corinthians 5 in the IRVP
2 Corinthians 5 in the IRVT
2 Corinthians 5 in the IRVT2
2 Corinthians 5 in the IRVU
2 Corinthians 5 in the ISVN
2 Corinthians 5 in the JSNT
2 Corinthians 5 in the KAPI
2 Corinthians 5 in the KBT1ETNIK
2 Corinthians 5 in the KBV
2 Corinthians 5 in the KJV
2 Corinthians 5 in the KNFD
2 Corinthians 5 in the LBA
2 Corinthians 5 in the LBLA
2 Corinthians 5 in the LNT
2 Corinthians 5 in the LSV
2 Corinthians 5 in the MAAL
2 Corinthians 5 in the MBV
2 Corinthians 5 in the MBV2
2 Corinthians 5 in the MHNT
2 Corinthians 5 in the MKNFD
2 Corinthians 5 in the MNG
2 Corinthians 5 in the MNT
2 Corinthians 5 in the MNT2
2 Corinthians 5 in the MRS1T
2 Corinthians 5 in the NAA
2 Corinthians 5 in the NASB
2 Corinthians 5 in the NBLA
2 Corinthians 5 in the NBS
2 Corinthians 5 in the NBVTP
2 Corinthians 5 in the NET2
2 Corinthians 5 in the NIV11
2 Corinthians 5 in the NNT
2 Corinthians 5 in the NNT2
2 Corinthians 5 in the NNT3
2 Corinthians 5 in the PDDPT
2 Corinthians 5 in the PFNT
2 Corinthians 5 in the RMNT
2 Corinthians 5 in the SBIAS
2 Corinthians 5 in the SBIBS
2 Corinthians 5 in the SBIBS2
2 Corinthians 5 in the SBICS
2 Corinthians 5 in the SBIDS
2 Corinthians 5 in the SBIGS
2 Corinthians 5 in the SBIHS
2 Corinthians 5 in the SBIIS
2 Corinthians 5 in the SBIIS2
2 Corinthians 5 in the SBIIS3
2 Corinthians 5 in the SBIKS
2 Corinthians 5 in the SBIKS2
2 Corinthians 5 in the SBIMS
2 Corinthians 5 in the SBIOS
2 Corinthians 5 in the SBIPS
2 Corinthians 5 in the SBISS
2 Corinthians 5 in the SBITS
2 Corinthians 5 in the SBITS2
2 Corinthians 5 in the SBITS3
2 Corinthians 5 in the SBITS4
2 Corinthians 5 in the SBIUS
2 Corinthians 5 in the SBIVS
2 Corinthians 5 in the SBT
2 Corinthians 5 in the SBT1E
2 Corinthians 5 in the SCHL
2 Corinthians 5 in the SNT
2 Corinthians 5 in the SUSU
2 Corinthians 5 in the SUSU2
2 Corinthians 5 in the SYNO
2 Corinthians 5 in the TBIAOTANT
2 Corinthians 5 in the TBT1E
2 Corinthians 5 in the TBT1E2
2 Corinthians 5 in the TFTIP
2 Corinthians 5 in the TFTU
2 Corinthians 5 in the TGNTATF3T
2 Corinthians 5 in the THAI
2 Corinthians 5 in the TNFD
2 Corinthians 5 in the TNT
2 Corinthians 5 in the TNTIK
2 Corinthians 5 in the TNTIL
2 Corinthians 5 in the TNTIN
2 Corinthians 5 in the TNTIP
2 Corinthians 5 in the TNTIZ
2 Corinthians 5 in the TOMA
2 Corinthians 5 in the TTENT
2 Corinthians 5 in the UBG
2 Corinthians 5 in the UGV
2 Corinthians 5 in the UGV2
2 Corinthians 5 in the UGV3
2 Corinthians 5 in the VBL
2 Corinthians 5 in the VDCC
2 Corinthians 5 in the YALU
2 Corinthians 5 in the YAPE
2 Corinthians 5 in the YBVTP
2 Corinthians 5 in the ZBP