2 Kings 1 (BOKCV)

1 Baada ya kifo cha Mfalme Ahabu, nchi ya Moabu iliasi dhidi ya Israeli. 2 Basi Ahazia alikuwa ameanguka huko Samaria kutoka baraza ya chumba chake cha juu, akaumia. Hivyo akatuma wajumbe, akiwaambia, “Nendeni mkaulize kwa Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni, mkaone kama nitapona kutokana na kuumia huku.” 3 Lakini malaika wa BWANA akamwambia Eliya, Mtishbi, “Panda ukakutane na wajumbe wa mfalme wa Samaria, uwaulize, ‘Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli ndiyo maana mnakwenda kumuuliza Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni?’ 4 Kwa hiyo hili ndilo asemalo BWANA, ‘Hutaondoka kwenye kitanda unachokilalia. Hakika utakufa!’ ” Hivyo Eliya akaenda. 5 Wajumbe waliporudi kwa mfalme, akawauliza, “Kwa nini mmerudi?” 6 Wakamjibu, “Mtu fulani alikuja kukutana nasi, naye akatuambia, ‘Rudini kwa mfalme aliyewatuma na mkamwambie, “Hili ndilo asemalo BWANA: Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli ndiyo maana unawatuma watu kwenda kuuliza kwa Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni? Kwa hiyo hutaondoka kwenye kitanda unachokilalia. Hakika utakufa!” ’ ” 7 Mfalme akawauliza, “Alikuwa mtu wa namna gani ambaye mlikutana naye, akawaambia hili?” 8 Wakamjibu, “Alikuwa mtu aliyekuwa na vazi la manyoya na mkanda wa ngozi kiunoni mwake.”Mfalme akasema, “Huyo alikuwa ni Eliya, Mtishbi.” 9 Ndipo mfalme akamtuma mkuu mmoja wa kikosi pamoja na kikosi chake cha askari hamsini kwa nabii Eliya. Yule mkuu wa kikosi akamwendea Eliya, aliyekuwa ameketi juu ya kilima, na kumwambia, “Mtu wa Mungu, mfalme anasema, ‘Shuka chini!’ ” 10 Eliya akamjibu yule mkuu wa kikosi, “Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, moto na ushuke kutoka mbinguni ukuteketeze wewe na watu wako hamsini!” Ndipo moto ukashuka kutoka mbinguni na kuwateketeza yule mkuu wa kikosi pamoja na watu wake. 11 Aliposikia hili, mfalme akatuma kwa Eliya mkuu wa kikosi mwingine na askari wake hamsini. Yule mkuu wa kikosi akamwambia Eliya, “Mtu wa Mungu, hili ndilo asemalo mfalme, ‘Shuka chini mara moja!’ ” 12 Eliya akajibu, “Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, moto na ushuke kutoka mbinguni ukuteketeze wewe na watu wako hamsini!” Ndipo moto wa Mungu ukashuka kutoka mbinguni, ukamteketeza yeye na watu wake hamsini. 13 Hivyo mfalme akatuma mkuu wa kikosi wa tatu na watu wake hamsini. Huyu mkuu wa kikosi wa tatu akapanda na kupiga magoti mbele ya Eliya, akiomba, “Mtu wa Mungu, tafadhali niachie uhai wangu na uhai wa hawa watu hamsini, watumishi wako! 14 Tazama, moto umeshuka kutoka mbinguni na kuwateketeza wale wakuu wa vikosi viwili vya kwanza pamoja na watu wao. Lakini sasa niachie uhai wangu!” 15 Malaika wa BWANA akamwambia Eliya, “Shuka pamoja naye, usimwogope.” Hivyo Eliya akainuka na kushuka pamoja naye kwa mfalme. 16 Akamwambia mfalme, “Hili ndilo asemalo BWANA: Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli wa kumuuliza habari, ndiyo maana ukatuma wajumbe kuuliza Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni? Kwa sababu umefanya hili, kamwe hutaondoka kwenye kitanda unachokilalia. Hakika utakufa!” 17 Hivyo akafa, sawasawa na lile neno la BWANA ambalo Eliya alikuwa amesema.Kwa kuwa Ahazia hakuwa na mwana, Yoramu akawa mfalme baada yake katika mwaka wa pili wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda. 18 Kwa matukio mengine ya utawala wa Ahazia na yale aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?

In Other Versions

2 Kings 1 in the ANGEFD

2 Kings 1 in the ANTPNG2D

2 Kings 1 in the AS21

2 Kings 1 in the BAGH

2 Kings 1 in the BBPNG

2 Kings 1 in the BBT1E

2 Kings 1 in the BDS

2 Kings 1 in the BEV

2 Kings 1 in the BHAD

2 Kings 1 in the BIB

2 Kings 1 in the BLPT

2 Kings 1 in the BNT

2 Kings 1 in the BNTABOOT

2 Kings 1 in the BNTLV

2 Kings 1 in the BOATCB

2 Kings 1 in the BOATCB2

2 Kings 1 in the BOBCV

2 Kings 1 in the BOCNT

2 Kings 1 in the BOECS

2 Kings 1 in the BOGWICC

2 Kings 1 in the BOHCB

2 Kings 1 in the BOHCV

2 Kings 1 in the BOHLNT

2 Kings 1 in the BOHNTLTAL

2 Kings 1 in the BOICB

2 Kings 1 in the BOILNTAP

2 Kings 1 in the BOITCV

2 Kings 1 in the BOKCV2

2 Kings 1 in the BOKHWOG

2 Kings 1 in the BOKSSV

2 Kings 1 in the BOLCB

2 Kings 1 in the BOLCB2

2 Kings 1 in the BOMCV

2 Kings 1 in the BONAV

2 Kings 1 in the BONCB

2 Kings 1 in the BONLT

2 Kings 1 in the BONUT2

2 Kings 1 in the BOPLNT

2 Kings 1 in the BOSCB

2 Kings 1 in the BOSNC

2 Kings 1 in the BOTLNT

2 Kings 1 in the BOVCB

2 Kings 1 in the BOYCB

2 Kings 1 in the BPBB

2 Kings 1 in the BPH

2 Kings 1 in the BSB

2 Kings 1 in the CCB

2 Kings 1 in the CUV

2 Kings 1 in the CUVS

2 Kings 1 in the DBT

2 Kings 1 in the DGDNT

2 Kings 1 in the DHNT

2 Kings 1 in the DNT

2 Kings 1 in the ELBE

2 Kings 1 in the EMTV

2 Kings 1 in the ESV

2 Kings 1 in the FBV

2 Kings 1 in the FEB

2 Kings 1 in the GGMNT

2 Kings 1 in the GNT

2 Kings 1 in the HARY

2 Kings 1 in the HNT

2 Kings 1 in the IRVA

2 Kings 1 in the IRVB

2 Kings 1 in the IRVG

2 Kings 1 in the IRVH

2 Kings 1 in the IRVK

2 Kings 1 in the IRVM

2 Kings 1 in the IRVM2

2 Kings 1 in the IRVO

2 Kings 1 in the IRVP

2 Kings 1 in the IRVT

2 Kings 1 in the IRVT2

2 Kings 1 in the IRVU

2 Kings 1 in the ISVN

2 Kings 1 in the JSNT

2 Kings 1 in the KAPI

2 Kings 1 in the KBT1ETNIK

2 Kings 1 in the KBV

2 Kings 1 in the KJV

2 Kings 1 in the KNFD

2 Kings 1 in the LBA

2 Kings 1 in the LBLA

2 Kings 1 in the LNT

2 Kings 1 in the LSV

2 Kings 1 in the MAAL

2 Kings 1 in the MBV

2 Kings 1 in the MBV2

2 Kings 1 in the MHNT

2 Kings 1 in the MKNFD

2 Kings 1 in the MNG

2 Kings 1 in the MNT

2 Kings 1 in the MNT2

2 Kings 1 in the MRS1T

2 Kings 1 in the NAA

2 Kings 1 in the NASB

2 Kings 1 in the NBLA

2 Kings 1 in the NBS

2 Kings 1 in the NBVTP

2 Kings 1 in the NET2

2 Kings 1 in the NIV11

2 Kings 1 in the NNT

2 Kings 1 in the NNT2

2 Kings 1 in the NNT3

2 Kings 1 in the PDDPT

2 Kings 1 in the PFNT

2 Kings 1 in the RMNT

2 Kings 1 in the SBIAS

2 Kings 1 in the SBIBS

2 Kings 1 in the SBIBS2

2 Kings 1 in the SBICS

2 Kings 1 in the SBIDS

2 Kings 1 in the SBIGS

2 Kings 1 in the SBIHS

2 Kings 1 in the SBIIS

2 Kings 1 in the SBIIS2

2 Kings 1 in the SBIIS3

2 Kings 1 in the SBIKS

2 Kings 1 in the SBIKS2

2 Kings 1 in the SBIMS

2 Kings 1 in the SBIOS

2 Kings 1 in the SBIPS

2 Kings 1 in the SBISS

2 Kings 1 in the SBITS

2 Kings 1 in the SBITS2

2 Kings 1 in the SBITS3

2 Kings 1 in the SBITS4

2 Kings 1 in the SBIUS

2 Kings 1 in the SBIVS

2 Kings 1 in the SBT

2 Kings 1 in the SBT1E

2 Kings 1 in the SCHL

2 Kings 1 in the SNT

2 Kings 1 in the SUSU

2 Kings 1 in the SUSU2

2 Kings 1 in the SYNO

2 Kings 1 in the TBIAOTANT

2 Kings 1 in the TBT1E

2 Kings 1 in the TBT1E2

2 Kings 1 in the TFTIP

2 Kings 1 in the TFTU

2 Kings 1 in the TGNTATF3T

2 Kings 1 in the THAI

2 Kings 1 in the TNFD

2 Kings 1 in the TNT

2 Kings 1 in the TNTIK

2 Kings 1 in the TNTIL

2 Kings 1 in the TNTIN

2 Kings 1 in the TNTIP

2 Kings 1 in the TNTIZ

2 Kings 1 in the TOMA

2 Kings 1 in the TTENT

2 Kings 1 in the UBG

2 Kings 1 in the UGV

2 Kings 1 in the UGV2

2 Kings 1 in the UGV3

2 Kings 1 in the VBL

2 Kings 1 in the VDCC

2 Kings 1 in the YALU

2 Kings 1 in the YAPE

2 Kings 1 in the YBVTP

2 Kings 1 in the ZBP