2 Samuel 21 (BOKCV)
1 Wakati wa utawala wa Daudi kulikuwa na njaa kwa miaka mitatu mfululizo, kwa hiyo Daudi akautafuta uso wa BWANA. BWANA akasema, “Ni kwa sababu ya Sauli na nyumba yake iliyotiwa madoa ya damu, kwa sababu aliwaua Wagibeoni.” 2 Mfalme akawaita Wagibeoni na kuzumgumza nao. (Wagibeoni hawakuwa wa wana wa Israeli, ila walikuwa mabaki ya Waamori. Waisraeli walikuwa wameapa kuwaacha hai, lakini Sauli katika wivu wake kwa ajili ya Israeli na Yuda, alikuwa amejaribu kuwaangamiza.) 3 Daudi akawauliza Wagibeoni, “Niwatendee nini? Nitawaridhishaje ili mbariki urithi wa BWANA?” 4 Wagibeoni wakamjibu, “Hatuna haki ya kudai fedha wala dhahabu kutoka kwa Sauli au jamaa yake, wala hatuna haki ya kumuua mtu yeyote katika Israeli.”Daudi akawauliza, “Mnataka niwafanyie nini?” 5 Wakamjibu mfalme, “Kwa habari ya mtu aliyetuangamiza na kufanya hila mbaya dhidi yetu ili kwamba tuangamizwe na tusiwe na yeyote katika Israeli, 6 tupatieni wazao wake saba wa kiume tuwaue hadharani mbele za BWANA huko Gibea ya Sauli, aliyekuwa amechaguliwa na BWANA.”Basi mfalme akasema, “Nitawakabidhi kwenu.” 7 Mfalme akamhifadhi Mefiboshethi mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli, kwa sababu ya kile kiapo mbele za BWANA kati ya Daudi na Yonathani. 8 Lakini mfalme akamchukua Armoni na Mefiboshethi, wana wawili wa Rispa binti Aiya, ambao alikuwa amemzalia Sauli, pamoja na wana watano wa Merabu binti Sauli, aliokuwa amemzalia Adrieli mwana wa Barzilai, Mmeholathi. 9 Akawakabidhi kwa Wagibeoni, ambao waliwaua na kuwaweka wazi juu ya kilima mbele za BWANA. Wote saba walianguka kwa pamoja; waliuawa katika siku za kwanza za mavuno, mara tu uvunaji wa shayiri ulipokuwa unaanza. 10 Rispa binti Aiya akachukua nguo ya gunia, akajitandikia juu ya mwamba. Kuanzia mwanzo wa mavuno mpaka mvua ziliponyesha juu ya miili ya hao waliouawa, Rispa hakuruhusu ndege wa angani kuwagusa wakati wa mchana, wala wanyama wa mwitu wakati wa usiku. 11 Daudi alipoambiwa kile Rispa binti Aiya, suria wa Sauli, alichokuwa amekifanya, 12 alikwenda akachukua mifupa ya Sauli na mwanawe Yonathani kutoka kwa watu wa Yabeshi-Gileadi. (Walikuwa wameichukua kwa siri kutoka uwanja wa watu wote huko Beth-Shani, mahali ambapo Wafilisti walikuwa wamewatundika baada ya kumuua Sauli huko Gilboa.) 13 Daudi akaileta mifupa ya Sauli na ya mwanawe Yonathani kutoka huko, pia mifupa ya wale waliokuwa wameuawa na kutupwa ilikusanywa. 14 Wakazika mifupa ya Sauli na ya mwanawe Yonathani katika kaburi la Kishi, babaye Sauli, huko Sela katika nchi ya Benyamini, nao wakafanya kila kitu mfalme alichoagiza. Baada ya hayo, Mungu akajibu maombi kwa ajili ya nchi. 15 Kwa mara nyingine tena kulikuwa na vita kati ya Wafilisti na Israeli. Daudi akashuka pamoja na watu wake ili kupigana dhidi ya Wafilisti, naye akawa amechoka sana. 16 Naye Ishbi-Benobu, mmoja wa wazao wa Warefai, ambaye mkuki wake ulikuwa na uzito wa shekeli 300 za shaba, alikuwa amejifunga upanga mpya, naye alisema angemuua Daudi. 17 Lakini Abishai mwana wa Seruya akaja kumwokoa Daudi; akampiga huyo Mfilisti, akamwangusha chini na kumuua. Ndipo watu wakamwapia Daudi, wakisema, “Kamwe hutakwenda tena nasi vitani, ili kwamba taa ya Israeli isije ikazimwa.” 18 Baada ya muda, kukawa na vita nyingine na Wafilisti, huko Gobu. Wakati huo Sibekai, Mhushathi, akamuua Safu, mmoja wa wazao wa Warefai. 19 Katika vita vingine na Wafilisti huko Gobu, Elhanani mwana wa Yaare-Oregimu, Mbethlehemu, alimuua nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa na mpini kama mti wa mfumaji. 20 Katika vita vingine tena, vilivyopiganwa huko Gathi, kulikuwako na mtu mmoja mkubwa mwenye vidole sita katika kila mkono na vidole sita kila mguu, jumla vidole ishirini na vinne. Yeye alikuwa pia mzao wa Mrefai. 21 Alipowadhihaki Israeli, Yonathani mwana wa Shimea, nduguye Daudi, akamuua. 22 Hawa wanne walikuwa wazao wa Warefai huko Gathi, nao walianguka kwa mikono ya Daudi na watu wake.
In Other Versions
2 Samuel 21 in the ANGEFD
2 Samuel 21 in the ANTPNG2D
2 Samuel 21 in the AS21
2 Samuel 21 in the BAGH
2 Samuel 21 in the BBPNG
2 Samuel 21 in the BBT1E
2 Samuel 21 in the BDS
2 Samuel 21 in the BEV
2 Samuel 21 in the BHAD
2 Samuel 21 in the BIB
2 Samuel 21 in the BLPT
2 Samuel 21 in the BNT
2 Samuel 21 in the BNTABOOT
2 Samuel 21 in the BNTLV
2 Samuel 21 in the BOATCB
2 Samuel 21 in the BOATCB2
2 Samuel 21 in the BOBCV
2 Samuel 21 in the BOCNT
2 Samuel 21 in the BOECS
2 Samuel 21 in the BOGWICC
2 Samuel 21 in the BOHCB
2 Samuel 21 in the BOHCV
2 Samuel 21 in the BOHLNT
2 Samuel 21 in the BOHNTLTAL
2 Samuel 21 in the BOICB
2 Samuel 21 in the BOILNTAP
2 Samuel 21 in the BOITCV
2 Samuel 21 in the BOKCV2
2 Samuel 21 in the BOKHWOG
2 Samuel 21 in the BOKSSV
2 Samuel 21 in the BOLCB
2 Samuel 21 in the BOLCB2
2 Samuel 21 in the BOMCV
2 Samuel 21 in the BONAV
2 Samuel 21 in the BONCB
2 Samuel 21 in the BONLT
2 Samuel 21 in the BONUT2
2 Samuel 21 in the BOPLNT
2 Samuel 21 in the BOSCB
2 Samuel 21 in the BOSNC
2 Samuel 21 in the BOTLNT
2 Samuel 21 in the BOVCB
2 Samuel 21 in the BOYCB
2 Samuel 21 in the BPBB
2 Samuel 21 in the BPH
2 Samuel 21 in the BSB
2 Samuel 21 in the CCB
2 Samuel 21 in the CUV
2 Samuel 21 in the CUVS
2 Samuel 21 in the DBT
2 Samuel 21 in the DGDNT
2 Samuel 21 in the DHNT
2 Samuel 21 in the DNT
2 Samuel 21 in the ELBE
2 Samuel 21 in the EMTV
2 Samuel 21 in the ESV
2 Samuel 21 in the FBV
2 Samuel 21 in the FEB
2 Samuel 21 in the GGMNT
2 Samuel 21 in the GNT
2 Samuel 21 in the HARY
2 Samuel 21 in the HNT
2 Samuel 21 in the IRVA
2 Samuel 21 in the IRVB
2 Samuel 21 in the IRVG
2 Samuel 21 in the IRVH
2 Samuel 21 in the IRVK
2 Samuel 21 in the IRVM
2 Samuel 21 in the IRVM2
2 Samuel 21 in the IRVO
2 Samuel 21 in the IRVP
2 Samuel 21 in the IRVT
2 Samuel 21 in the IRVT2
2 Samuel 21 in the IRVU
2 Samuel 21 in the ISVN
2 Samuel 21 in the JSNT
2 Samuel 21 in the KAPI
2 Samuel 21 in the KBT1ETNIK
2 Samuel 21 in the KBV
2 Samuel 21 in the KJV
2 Samuel 21 in the KNFD
2 Samuel 21 in the LBA
2 Samuel 21 in the LBLA
2 Samuel 21 in the LNT
2 Samuel 21 in the LSV
2 Samuel 21 in the MAAL
2 Samuel 21 in the MBV
2 Samuel 21 in the MBV2
2 Samuel 21 in the MHNT
2 Samuel 21 in the MKNFD
2 Samuel 21 in the MNG
2 Samuel 21 in the MNT
2 Samuel 21 in the MNT2
2 Samuel 21 in the MRS1T
2 Samuel 21 in the NAA
2 Samuel 21 in the NASB
2 Samuel 21 in the NBLA
2 Samuel 21 in the NBS
2 Samuel 21 in the NBVTP
2 Samuel 21 in the NET2
2 Samuel 21 in the NIV11
2 Samuel 21 in the NNT
2 Samuel 21 in the NNT2
2 Samuel 21 in the NNT3
2 Samuel 21 in the PDDPT
2 Samuel 21 in the PFNT
2 Samuel 21 in the RMNT
2 Samuel 21 in the SBIAS
2 Samuel 21 in the SBIBS
2 Samuel 21 in the SBIBS2
2 Samuel 21 in the SBICS
2 Samuel 21 in the SBIDS
2 Samuel 21 in the SBIGS
2 Samuel 21 in the SBIHS
2 Samuel 21 in the SBIIS
2 Samuel 21 in the SBIIS2
2 Samuel 21 in the SBIIS3
2 Samuel 21 in the SBIKS
2 Samuel 21 in the SBIKS2
2 Samuel 21 in the SBIMS
2 Samuel 21 in the SBIOS
2 Samuel 21 in the SBIPS
2 Samuel 21 in the SBISS
2 Samuel 21 in the SBITS
2 Samuel 21 in the SBITS2
2 Samuel 21 in the SBITS3
2 Samuel 21 in the SBITS4
2 Samuel 21 in the SBIUS
2 Samuel 21 in the SBIVS
2 Samuel 21 in the SBT
2 Samuel 21 in the SBT1E
2 Samuel 21 in the SCHL
2 Samuel 21 in the SNT
2 Samuel 21 in the SUSU
2 Samuel 21 in the SUSU2
2 Samuel 21 in the SYNO
2 Samuel 21 in the TBIAOTANT
2 Samuel 21 in the TBT1E
2 Samuel 21 in the TBT1E2
2 Samuel 21 in the TFTIP
2 Samuel 21 in the TFTU
2 Samuel 21 in the TGNTATF3T
2 Samuel 21 in the THAI
2 Samuel 21 in the TNFD
2 Samuel 21 in the TNT
2 Samuel 21 in the TNTIK
2 Samuel 21 in the TNTIL
2 Samuel 21 in the TNTIN
2 Samuel 21 in the TNTIP
2 Samuel 21 in the TNTIZ
2 Samuel 21 in the TOMA
2 Samuel 21 in the TTENT
2 Samuel 21 in the UBG
2 Samuel 21 in the UGV
2 Samuel 21 in the UGV2
2 Samuel 21 in the UGV3
2 Samuel 21 in the VBL
2 Samuel 21 in the VDCC
2 Samuel 21 in the YALU
2 Samuel 21 in the YAPE
2 Samuel 21 in the YBVTP
2 Samuel 21 in the ZBP