2 Timothy 4 (BOKCV)

1 Nakuagiza mbele za Mungu na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu watu walio hai na waliokufa wakati wa kuja kwake na ufalme wake, kwamba: 2 Hubiri Neno; kuwa tayari wakati ufaao na wakati usiofaa; karipia, kemea na utie moyo kwa uvumilivu wote na kwa mafundisho mazuri. 3 Maana wakati utakuja watu watakapokataa kuyakubali mafundisho yenye uzima. Badala yake, ili kutimiza tamaa zao wenyewe, watajikusanyia idadi kubwa ya walimu wapate kuwaambia yale ambayo masikio yao yanayowasha yanatamani kuyasikia. 4 Watakataa kusikiliza kweli na kuzigeukia hadithi za uongo. 5 Kwa habari yako wewe, vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza wajibu wote wa huduma yako. 6 Kwa maana mimi sasa ni tayari kumiminwa kama sadaka ya kinywaji, nayo saa yangu ya kuondoka imetimia. 7 Nimevipiga vita vizuri, mashindano nimeyamaliza, imani nimeilinda. 8 Sasa nimewekewa taji ya haki ambayo Bwana, mwamuzi wa haki, atanitunukia siku ile: wala si mimi tu, bali pia wote ambao wamengoja kwa shauku kudhihirishwa kwake. 9 Jitahidi kuja kwangu upesi 10 kwa sababu Dema, kwa kuupenda ulimwengu, ameniacha na amekwenda Thesalonike. Kreske amekwenda Galatia na Tito amekwenda Dalmatia. 11 Ni Luka peke yake aliye hapa pamoja nami. Mtafute Marko uje naye kwa sababu ananifaa sana katika huduma yangu. 12 Nimemtuma Tikiko huko Efeso. 13 Utakapokuja, niletee lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa na vile vitabu vyangu, hasa vile vya ngozi. 14 Aleksanda yule mfua chuma alinitendea ubaya mkubwa. Bwana atamlipa kwa ajili ya yale aliyotenda. 15 Wewe pia ujihadhari naye kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu. 16 Katika utetezi wangu wa mara ya kwanza, hakuna hata mmoja aliyeniunga mkono, bali kila mmoja aliniacha. Namwomba Mungu wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. 17 Lakini Bwana alisimama upande wangu akanitia nguvu, ili kupitia kwangu lile Neno lihubiriwe kwa ukamilifu, watu wote Mataifa wapate kulisikia. Mimi niliokolewa kutoka kinywa cha simba. 18 Bwana ataniokoa katika kila shambulio baya na kunileta salama katika Ufalme wake wa mbinguni. Atukuzwe yeye milele na milele. Amen. 19 Wasalimu Prisila na Akila, na wote wa nyumbani kwa Onesiforo. 20 Erasto alibaki Korintho. Nami nikamwacha Trofimo huko Mileto akiwa mgonjwa. 21 Jitahidi ufike huku kabla ya majira ya baridi. Eubulo anakusalimu, vivyo hivyo Pude, Lino, Klaudia na ndugu wote. 22 Bwana awe pamoja na roho yako. Neema iwe pamoja nanyi. Amen.

In Other Versions

2 Timothy 4 in the ANGEFD

2 Timothy 4 in the ANTPNG2D

2 Timothy 4 in the AS21

2 Timothy 4 in the BAGH

2 Timothy 4 in the BBPNG

2 Timothy 4 in the BBT1E

2 Timothy 4 in the BDS

2 Timothy 4 in the BEV

2 Timothy 4 in the BHAD

2 Timothy 4 in the BIB

2 Timothy 4 in the BLPT

2 Timothy 4 in the BNT

2 Timothy 4 in the BNTABOOT

2 Timothy 4 in the BNTLV

2 Timothy 4 in the BOATCB

2 Timothy 4 in the BOATCB2

2 Timothy 4 in the BOBCV

2 Timothy 4 in the BOCNT

2 Timothy 4 in the BOECS

2 Timothy 4 in the BOGWICC

2 Timothy 4 in the BOHCB

2 Timothy 4 in the BOHCV

2 Timothy 4 in the BOHLNT

2 Timothy 4 in the BOHNTLTAL

2 Timothy 4 in the BOICB

2 Timothy 4 in the BOILNTAP

2 Timothy 4 in the BOITCV

2 Timothy 4 in the BOKCV2

2 Timothy 4 in the BOKHWOG

2 Timothy 4 in the BOKSSV

2 Timothy 4 in the BOLCB

2 Timothy 4 in the BOLCB2

2 Timothy 4 in the BOMCV

2 Timothy 4 in the BONAV

2 Timothy 4 in the BONCB

2 Timothy 4 in the BONLT

2 Timothy 4 in the BONUT2

2 Timothy 4 in the BOPLNT

2 Timothy 4 in the BOSCB

2 Timothy 4 in the BOSNC

2 Timothy 4 in the BOTLNT

2 Timothy 4 in the BOVCB

2 Timothy 4 in the BOYCB

2 Timothy 4 in the BPBB

2 Timothy 4 in the BPH

2 Timothy 4 in the BSB

2 Timothy 4 in the CCB

2 Timothy 4 in the CUV

2 Timothy 4 in the CUVS

2 Timothy 4 in the DBT

2 Timothy 4 in the DGDNT

2 Timothy 4 in the DHNT

2 Timothy 4 in the DNT

2 Timothy 4 in the ELBE

2 Timothy 4 in the EMTV

2 Timothy 4 in the ESV

2 Timothy 4 in the FBV

2 Timothy 4 in the FEB

2 Timothy 4 in the GGMNT

2 Timothy 4 in the GNT

2 Timothy 4 in the HARY

2 Timothy 4 in the HNT

2 Timothy 4 in the IRVA

2 Timothy 4 in the IRVB

2 Timothy 4 in the IRVG

2 Timothy 4 in the IRVH

2 Timothy 4 in the IRVK

2 Timothy 4 in the IRVM

2 Timothy 4 in the IRVM2

2 Timothy 4 in the IRVO

2 Timothy 4 in the IRVP

2 Timothy 4 in the IRVT

2 Timothy 4 in the IRVT2

2 Timothy 4 in the IRVU

2 Timothy 4 in the ISVN

2 Timothy 4 in the JSNT

2 Timothy 4 in the KAPI

2 Timothy 4 in the KBT1ETNIK

2 Timothy 4 in the KBV

2 Timothy 4 in the KJV

2 Timothy 4 in the KNFD

2 Timothy 4 in the LBA

2 Timothy 4 in the LBLA

2 Timothy 4 in the LNT

2 Timothy 4 in the LSV

2 Timothy 4 in the MAAL

2 Timothy 4 in the MBV

2 Timothy 4 in the MBV2

2 Timothy 4 in the MHNT

2 Timothy 4 in the MKNFD

2 Timothy 4 in the MNG

2 Timothy 4 in the MNT

2 Timothy 4 in the MNT2

2 Timothy 4 in the MRS1T

2 Timothy 4 in the NAA

2 Timothy 4 in the NASB

2 Timothy 4 in the NBLA

2 Timothy 4 in the NBS

2 Timothy 4 in the NBVTP

2 Timothy 4 in the NET2

2 Timothy 4 in the NIV11

2 Timothy 4 in the NNT

2 Timothy 4 in the NNT2

2 Timothy 4 in the NNT3

2 Timothy 4 in the PDDPT

2 Timothy 4 in the PFNT

2 Timothy 4 in the RMNT

2 Timothy 4 in the SBIAS

2 Timothy 4 in the SBIBS

2 Timothy 4 in the SBIBS2

2 Timothy 4 in the SBICS

2 Timothy 4 in the SBIDS

2 Timothy 4 in the SBIGS

2 Timothy 4 in the SBIHS

2 Timothy 4 in the SBIIS

2 Timothy 4 in the SBIIS2

2 Timothy 4 in the SBIIS3

2 Timothy 4 in the SBIKS

2 Timothy 4 in the SBIKS2

2 Timothy 4 in the SBIMS

2 Timothy 4 in the SBIOS

2 Timothy 4 in the SBIPS

2 Timothy 4 in the SBISS

2 Timothy 4 in the SBITS

2 Timothy 4 in the SBITS2

2 Timothy 4 in the SBITS3

2 Timothy 4 in the SBITS4

2 Timothy 4 in the SBIUS

2 Timothy 4 in the SBIVS

2 Timothy 4 in the SBT

2 Timothy 4 in the SBT1E

2 Timothy 4 in the SCHL

2 Timothy 4 in the SNT

2 Timothy 4 in the SUSU

2 Timothy 4 in the SUSU2

2 Timothy 4 in the SYNO

2 Timothy 4 in the TBIAOTANT

2 Timothy 4 in the TBT1E

2 Timothy 4 in the TBT1E2

2 Timothy 4 in the TFTIP

2 Timothy 4 in the TFTU

2 Timothy 4 in the TGNTATF3T

2 Timothy 4 in the THAI

2 Timothy 4 in the TNFD

2 Timothy 4 in the TNT

2 Timothy 4 in the TNTIK

2 Timothy 4 in the TNTIL

2 Timothy 4 in the TNTIN

2 Timothy 4 in the TNTIP

2 Timothy 4 in the TNTIZ

2 Timothy 4 in the TOMA

2 Timothy 4 in the TTENT

2 Timothy 4 in the UBG

2 Timothy 4 in the UGV

2 Timothy 4 in the UGV2

2 Timothy 4 in the UGV3

2 Timothy 4 in the VBL

2 Timothy 4 in the VDCC

2 Timothy 4 in the YALU

2 Timothy 4 in the YAPE

2 Timothy 4 in the YBVTP

2 Timothy 4 in the ZBP