Exodus 22 (BOKCV)

1 “Kama mtu akiiba maksai au kondoo na kumchinja au kumuuza, ni lazima alipe ngʼombe watano badala ya maksai mmoja na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja. 2 “Kama mwizi akishikwa anavunja nyumba akapigwa hata akafa, aliyemuua hana hatia ya kumwaga damu; 3 lakini jambo hilo likitokea wakati jua limechomoza, huyo mtu atakuwa na hatia ya kumwaga damu.“Mwizi huyo sharti alipe, lakini kama hana kitu, lazima auzwe ili alipe kwa ajili ya wizi wake. 4 “Kama mnyama aliyeibwa akikutwa hai mikononi mwake, ikiwa ni maksai au punda au kondoo, lazima alipe mara mbili. 5 “Kama mtu akichunga mifugo yake katika shamba au shamba la mizabibu, na akawaachia wajilishe katika shamba la mtu mwingine, ni lazima alipe vitu bora kutoka kwenye shamba lake mwenyewe au kutoka shamba lake la mizabibu. 6 “Kama moto ukiwaka na kuenea kwenye vichaka vya miiba na kuteketeza miganda ya nafaka au nafaka ambayo haijavunwa, au kuteketeza shamba lote, mtu yule aliyewasha moto lazima alipe. 7 “Kama mtu akimpa jirani yake fedha au mali nyingine amtunzie, na kama vikiibwa kutoka nyumba ya huyo jirani, kama mwizi atashikwa, lazima alipe mara mbili. 8 Lakini mwizi asipopatikana, mwenye nyumba atafika mbele ya waamuzi ili kuthibitisha kuwa hakuchukua mali ya mwenzake. 9 Pakiwepo jambo lolote la mali isiyo halali, ikiwa ni maksai, punda, kondoo, mavazi, ama mali yoyote iliyopotea ambayo fulani atasema, ‘Hii ni mali yangu,’ pande zote mbili wataleta mashauri yao mbele ya waamuzi. Yule ambaye waamuzi watamwona kuwa na hatia atamlipa jirani yake mara mbili. 10 “Kama mtu akimpa jirani yake punda, ngʼombe, kondoo au mnyama mwingine yeyote amtunzie, akifa au akijeruhiwa au akichukuliwa wakati haonekani na mtu yeyote, 11 jambo hili kati yao wawili litaamuliwa kwa kuapa kiapo mbele za BWANA, kwamba huyo jirani hakuhusika na wizi wa mali ya jirani yake. Mwenye mali itampasa akubali jambo hili, na hakuna malipo yatakayohitajika. 12 Lakini kama mnyama aliibwa kwa jirani, itampasa amlipe mwenye mnyama. 13 Kama ameraruliwa na mnyama pori, ataleta mabaki ya mnyama kama ushahidi, naye hatadaiwa kulipa mnyama aliyeraruliwa. 14 “Kama mtu akimwazima mnyama kutoka kwa jirani yake, na kama akiumia au akafa na mwenye mnyama hayupo, lazima amlipe huyo mnyama. 15 Lakini mwenye mnyama akiwa angalipo na mnyama wake, mwazimaji hatalazimika kumlipa. Kama mnyama alikuwa amekodishwa, fedha iliyolipwa kwa kukodisha inatosha kwa kufidia hasara. 16 “Kama mtu akimshawishi bikira ambaye hajaposwa na akilala naye, lazima alipe mahari, kisha atamwoa msichana huyo. 17 Baba wa msichana akikataa katakata kumpa huyo mtu huyo msichana wake, bado ni lazima huyo mtu atalipa mahari kama inavyostahili malipo ya ubikira. 18 “Usiruhusu mwanamke mchawi aishi. 19 “Mtu yeyote aziniye na mnyama lazima auawe. 20 “Mtu awaye yote anayemtolea mungu mwingine dhabihu isipokuwa BWANA, lazima aangamizwe. 21 “Usimtendee mgeni vibaya au kumwonea, kwa kuwa nanyi mlikuwa wageni huko Misri. 22 “Usimdhulumu mjane wala yatima. 23 Kama ukifanya hivyo nao wakinililia, hakika nitasikia kilio chao. 24 Hasira yangu itawaka, nami nitawaua kwa upanga, wake zenu watakuwa wajane na watoto wenu watakuwa yatima. 25 “Kama ukimkopesha mmojawapo wa watu wangu fedha ambaye ni mhitaji, usiwe kama mtu mkopesha fedha; usimtoze riba. 26 Kama ukichukua vazi la jirani kama rehani, ulirudishe kwake kabla jua kuzama, 27 kwa kuwa vazi lake ndilo pekee alilo nalo la kumfunika mwili wake. Ni nini kingine atajifunika nacho? Atakaponililia, nitasikia, kwa kuwa nina huruma. 28 “Usimkufuru Mungu au kumlaani mtawala wa watu wako. 29 “Usiache kutoa sadaka kutoka ghala lako au mapipa yako.“Lazima unipe mzaliwa wa kwanza wa wana wako. 30 Ufanye vivyo hivyo kwa ngʼombe wako na kwa kondoo wako. Waache wakae na mama zao kwa siku saba, lakini siku ya nane unipe. 31 “Ninyi mtakuwa watu wangu watakatifu. Kwa hiyo msile nyama ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama pori; mtupieni mbwa.

In Other Versions

Exodus 22 in the ANGEFD

Exodus 22 in the ANTPNG2D

Exodus 22 in the AS21

Exodus 22 in the BAGH

Exodus 22 in the BBPNG

Exodus 22 in the BBT1E

Exodus 22 in the BDS

Exodus 22 in the BEV

Exodus 22 in the BHAD

Exodus 22 in the BIB

Exodus 22 in the BLPT

Exodus 22 in the BNT

Exodus 22 in the BNTABOOT

Exodus 22 in the BNTLV

Exodus 22 in the BOATCB

Exodus 22 in the BOATCB2

Exodus 22 in the BOBCV

Exodus 22 in the BOCNT

Exodus 22 in the BOECS

Exodus 22 in the BOGWICC

Exodus 22 in the BOHCB

Exodus 22 in the BOHCV

Exodus 22 in the BOHLNT

Exodus 22 in the BOHNTLTAL

Exodus 22 in the BOICB

Exodus 22 in the BOILNTAP

Exodus 22 in the BOITCV

Exodus 22 in the BOKCV2

Exodus 22 in the BOKHWOG

Exodus 22 in the BOKSSV

Exodus 22 in the BOLCB

Exodus 22 in the BOLCB2

Exodus 22 in the BOMCV

Exodus 22 in the BONAV

Exodus 22 in the BONCB

Exodus 22 in the BONLT

Exodus 22 in the BONUT2

Exodus 22 in the BOPLNT

Exodus 22 in the BOSCB

Exodus 22 in the BOSNC

Exodus 22 in the BOTLNT

Exodus 22 in the BOVCB

Exodus 22 in the BOYCB

Exodus 22 in the BPBB

Exodus 22 in the BPH

Exodus 22 in the BSB

Exodus 22 in the CCB

Exodus 22 in the CUV

Exodus 22 in the CUVS

Exodus 22 in the DBT

Exodus 22 in the DGDNT

Exodus 22 in the DHNT

Exodus 22 in the DNT

Exodus 22 in the ELBE

Exodus 22 in the EMTV

Exodus 22 in the ESV

Exodus 22 in the FBV

Exodus 22 in the FEB

Exodus 22 in the GGMNT

Exodus 22 in the GNT

Exodus 22 in the HARY

Exodus 22 in the HNT

Exodus 22 in the IRVA

Exodus 22 in the IRVB

Exodus 22 in the IRVG

Exodus 22 in the IRVH

Exodus 22 in the IRVK

Exodus 22 in the IRVM

Exodus 22 in the IRVM2

Exodus 22 in the IRVO

Exodus 22 in the IRVP

Exodus 22 in the IRVT

Exodus 22 in the IRVT2

Exodus 22 in the IRVU

Exodus 22 in the ISVN

Exodus 22 in the JSNT

Exodus 22 in the KAPI

Exodus 22 in the KBT1ETNIK

Exodus 22 in the KBV

Exodus 22 in the KJV

Exodus 22 in the KNFD

Exodus 22 in the LBA

Exodus 22 in the LBLA

Exodus 22 in the LNT

Exodus 22 in the LSV

Exodus 22 in the MAAL

Exodus 22 in the MBV

Exodus 22 in the MBV2

Exodus 22 in the MHNT

Exodus 22 in the MKNFD

Exodus 22 in the MNG

Exodus 22 in the MNT

Exodus 22 in the MNT2

Exodus 22 in the MRS1T

Exodus 22 in the NAA

Exodus 22 in the NASB

Exodus 22 in the NBLA

Exodus 22 in the NBS

Exodus 22 in the NBVTP

Exodus 22 in the NET2

Exodus 22 in the NIV11

Exodus 22 in the NNT

Exodus 22 in the NNT2

Exodus 22 in the NNT3

Exodus 22 in the PDDPT

Exodus 22 in the PFNT

Exodus 22 in the RMNT

Exodus 22 in the SBIAS

Exodus 22 in the SBIBS

Exodus 22 in the SBIBS2

Exodus 22 in the SBICS

Exodus 22 in the SBIDS

Exodus 22 in the SBIGS

Exodus 22 in the SBIHS

Exodus 22 in the SBIIS

Exodus 22 in the SBIIS2

Exodus 22 in the SBIIS3

Exodus 22 in the SBIKS

Exodus 22 in the SBIKS2

Exodus 22 in the SBIMS

Exodus 22 in the SBIOS

Exodus 22 in the SBIPS

Exodus 22 in the SBISS

Exodus 22 in the SBITS

Exodus 22 in the SBITS2

Exodus 22 in the SBITS3

Exodus 22 in the SBITS4

Exodus 22 in the SBIUS

Exodus 22 in the SBIVS

Exodus 22 in the SBT

Exodus 22 in the SBT1E

Exodus 22 in the SCHL

Exodus 22 in the SNT

Exodus 22 in the SUSU

Exodus 22 in the SUSU2

Exodus 22 in the SYNO

Exodus 22 in the TBIAOTANT

Exodus 22 in the TBT1E

Exodus 22 in the TBT1E2

Exodus 22 in the TFTIP

Exodus 22 in the TFTU

Exodus 22 in the TGNTATF3T

Exodus 22 in the THAI

Exodus 22 in the TNFD

Exodus 22 in the TNT

Exodus 22 in the TNTIK

Exodus 22 in the TNTIL

Exodus 22 in the TNTIN

Exodus 22 in the TNTIP

Exodus 22 in the TNTIZ

Exodus 22 in the TOMA

Exodus 22 in the TTENT

Exodus 22 in the UBG

Exodus 22 in the UGV

Exodus 22 in the UGV2

Exodus 22 in the UGV3

Exodus 22 in the VBL

Exodus 22 in the VDCC

Exodus 22 in the YALU

Exodus 22 in the YAPE

Exodus 22 in the YBVTP

Exodus 22 in the ZBP