Ezekiel 42 (BOKCV)
1 Ndipo yule mtu akaniongoza kuelekea kaskazini mpaka kwenye ua wa nje na kunileta mpaka kwenye vyumba vinavyoelekeana na ua wa Hekalu na kuelekeana na ukuta wa nje upande wa kaskazini. 2 Jengo ambalo mlango wake ulielekea kaskazini lilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja na upana wa dhiraa hamsini. 3 Mbele ya zile dhiraa ishirini za ule ua wa ndani unaoelekeana na ile njia ya ua wa nje, kuliinuka vyumba virefu kimoja baada ya kingine vya ghorofa tatu. 4 Mbele ya hivi vyumba kulikuwa na njia ya ndani yenye upana wa dhiraa kumi na urefu wa dhiraa mia moja. Milango yake ilikuwa upande wa kaskazini. 5 Basi vyumba vya juu vilikuwa vyembamba zaidi, kwa kuwa ujia ulichukua nafasi zaidi ndani yake kuliko katika vyumba vya sakafu ya chini na vya katikati ya jengo. 6 Vyumba katika ghorofa ya tatu havikuwa na nguzo, kama kumbi zilivyokuwa nazo, kwa hiyo eneo la sakafu ya vyumba vya juu lilikuwa ni dogo kuliko la sakafu ya chini na ya kati. 7 Kulikuwa na ukuta wa nje uliokuwa sambamba na vile vyumba na ukumbi wa nje, ulitokeza urefu wa dhiraa hamsini. 8 Wakati safu ya vyumba katika ua wa nje vilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini, vile vyumba vilivyokuwa karibu zaidi na Hekalu vilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja. 9 Vyumba vya chini vilikuwa na ingilio upande wa mashariki unapoingia kutoka ukumbi wa nje. 10 Upande wa kusini kufuata urefu wa ukuta wa ukumbi wa nje, unaopakana na ukumbi wa Hekalu na kuelekeana na ukuta wa nje, kulikuwa na vyumba 11 vyenye ujia unayopita mbele yake. Hivi vilifanana na vile vyumba vya upande wa kaskazini, vilikuwa na urefu na upana ulio sawa, mahali pa kutokea na vipimo vyake vilikuwa sawa. Kama ilivyokuwa milango ya upande wa kaskazini, 12 ndivyo ilivyokuwa milango ya vyumba vya upande wa kusini. Kulikuwa na ingilio kuanzia mwanzo wa njia ambao ulikuwa sambamba na ukuta wa pili uliokuwa upande wa mashariki, ambako ndiko kwa kuingia vyumbani. 13 Kisha akaniambia, “Vyumba vya upande wa kaskazini na vya upande wa kusini ambavyo vinaelekeana na ukumbi wa Hekalu ni vyumba vya makuhani, mahali ambapo wale makuhani ambao humkaribia BWANA watakula zile sadaka takatifu sana. Huko ndiko watakakoweka zile sadaka takatifu sana, yaani, sadaka za nafaka, sadaka za dhambi na sadaka za hatia, kwa kuwa mahali ni patakatifu. 14 Mara makuhani waingiapo mahali patakatifu, hawaruhusiwi kwenda kwenye ukumbi wa nje mpaka wayaache mavazi ambayo walivaa wakiwa wanahudumu, kwa kuwa hayo mavazi ni matakatifu. Inawapasa kuvaa mavazi mengine kabla hawajakaribia eneo lililo wazi kwa ajili ya watu.” 15 Alipomaliza kupima vile vilivyokuwa katika eneo la ndani la Hekalu, akanitoa nje kupitia lango la upande wa mashariki na kupima eneo lote linalozunguka: 16 Akapima upande wa mashariki kwa ule ufito wa kupimia, nao ulikuwa dhiraa 500 17 Akapima upande wa kaskazini, nao ulikuwa dhiraa 500 kwa ufito ule wa kupimia. 18 Tena akapima upande wa kusini, nao ulikuwa dhiraa 500 kwa ufito ule wa kupimia. 19 Kisha akageukia upande wa magharibi na kuupima, ulikuwa dhiraa 500 kwa ufito ule wa kupimia. 20 Hivyo akapima eneo katika pande zote nne. Lilikuwa na ukuta kulizunguka wenye urefu wa dhiraa 500 na upana wa dhiraa 500, uliotenganisha mahali Patakatifu na eneo la watu wote.
In Other Versions
Ezekiel 42 in the ANGEFD
Ezekiel 42 in the ANTPNG2D
Ezekiel 42 in the AS21
Ezekiel 42 in the BAGH
Ezekiel 42 in the BBPNG
Ezekiel 42 in the BBT1E
Ezekiel 42 in the BDS
Ezekiel 42 in the BEV
Ezekiel 42 in the BHAD
Ezekiel 42 in the BIB
Ezekiel 42 in the BLPT
Ezekiel 42 in the BNT
Ezekiel 42 in the BNTABOOT
Ezekiel 42 in the BNTLV
Ezekiel 42 in the BOATCB
Ezekiel 42 in the BOATCB2
Ezekiel 42 in the BOBCV
Ezekiel 42 in the BOCNT
Ezekiel 42 in the BOECS
Ezekiel 42 in the BOGWICC
Ezekiel 42 in the BOHCB
Ezekiel 42 in the BOHCV
Ezekiel 42 in the BOHLNT
Ezekiel 42 in the BOHNTLTAL
Ezekiel 42 in the BOICB
Ezekiel 42 in the BOILNTAP
Ezekiel 42 in the BOITCV
Ezekiel 42 in the BOKCV2
Ezekiel 42 in the BOKHWOG
Ezekiel 42 in the BOKSSV
Ezekiel 42 in the BOLCB
Ezekiel 42 in the BOLCB2
Ezekiel 42 in the BOMCV
Ezekiel 42 in the BONAV
Ezekiel 42 in the BONCB
Ezekiel 42 in the BONLT
Ezekiel 42 in the BONUT2
Ezekiel 42 in the BOPLNT
Ezekiel 42 in the BOSCB
Ezekiel 42 in the BOSNC
Ezekiel 42 in the BOTLNT
Ezekiel 42 in the BOVCB
Ezekiel 42 in the BOYCB
Ezekiel 42 in the BPBB
Ezekiel 42 in the BPH
Ezekiel 42 in the BSB
Ezekiel 42 in the CCB
Ezekiel 42 in the CUV
Ezekiel 42 in the CUVS
Ezekiel 42 in the DBT
Ezekiel 42 in the DGDNT
Ezekiel 42 in the DHNT
Ezekiel 42 in the DNT
Ezekiel 42 in the ELBE
Ezekiel 42 in the EMTV
Ezekiel 42 in the ESV
Ezekiel 42 in the FBV
Ezekiel 42 in the FEB
Ezekiel 42 in the GGMNT
Ezekiel 42 in the GNT
Ezekiel 42 in the HARY
Ezekiel 42 in the HNT
Ezekiel 42 in the IRVA
Ezekiel 42 in the IRVB
Ezekiel 42 in the IRVG
Ezekiel 42 in the IRVH
Ezekiel 42 in the IRVK
Ezekiel 42 in the IRVM
Ezekiel 42 in the IRVM2
Ezekiel 42 in the IRVO
Ezekiel 42 in the IRVP
Ezekiel 42 in the IRVT
Ezekiel 42 in the IRVT2
Ezekiel 42 in the IRVU
Ezekiel 42 in the ISVN
Ezekiel 42 in the JSNT
Ezekiel 42 in the KAPI
Ezekiel 42 in the KBT1ETNIK
Ezekiel 42 in the KBV
Ezekiel 42 in the KJV
Ezekiel 42 in the KNFD
Ezekiel 42 in the LBA
Ezekiel 42 in the LBLA
Ezekiel 42 in the LNT
Ezekiel 42 in the LSV
Ezekiel 42 in the MAAL
Ezekiel 42 in the MBV
Ezekiel 42 in the MBV2
Ezekiel 42 in the MHNT
Ezekiel 42 in the MKNFD
Ezekiel 42 in the MNG
Ezekiel 42 in the MNT
Ezekiel 42 in the MNT2
Ezekiel 42 in the MRS1T
Ezekiel 42 in the NAA
Ezekiel 42 in the NASB
Ezekiel 42 in the NBLA
Ezekiel 42 in the NBS
Ezekiel 42 in the NBVTP
Ezekiel 42 in the NET2
Ezekiel 42 in the NIV11
Ezekiel 42 in the NNT
Ezekiel 42 in the NNT2
Ezekiel 42 in the NNT3
Ezekiel 42 in the PDDPT
Ezekiel 42 in the PFNT
Ezekiel 42 in the RMNT
Ezekiel 42 in the SBIAS
Ezekiel 42 in the SBIBS
Ezekiel 42 in the SBIBS2
Ezekiel 42 in the SBICS
Ezekiel 42 in the SBIDS
Ezekiel 42 in the SBIGS
Ezekiel 42 in the SBIHS
Ezekiel 42 in the SBIIS
Ezekiel 42 in the SBIIS2
Ezekiel 42 in the SBIIS3
Ezekiel 42 in the SBIKS
Ezekiel 42 in the SBIKS2
Ezekiel 42 in the SBIMS
Ezekiel 42 in the SBIOS
Ezekiel 42 in the SBIPS
Ezekiel 42 in the SBISS
Ezekiel 42 in the SBITS
Ezekiel 42 in the SBITS2
Ezekiel 42 in the SBITS3
Ezekiel 42 in the SBITS4
Ezekiel 42 in the SBIUS
Ezekiel 42 in the SBIVS
Ezekiel 42 in the SBT
Ezekiel 42 in the SBT1E
Ezekiel 42 in the SCHL
Ezekiel 42 in the SNT
Ezekiel 42 in the SUSU
Ezekiel 42 in the SUSU2
Ezekiel 42 in the SYNO
Ezekiel 42 in the TBIAOTANT
Ezekiel 42 in the TBT1E
Ezekiel 42 in the TBT1E2
Ezekiel 42 in the TFTIP
Ezekiel 42 in the TFTU
Ezekiel 42 in the TGNTATF3T
Ezekiel 42 in the THAI
Ezekiel 42 in the TNFD
Ezekiel 42 in the TNT
Ezekiel 42 in the TNTIK
Ezekiel 42 in the TNTIL
Ezekiel 42 in the TNTIN
Ezekiel 42 in the TNTIP
Ezekiel 42 in the TNTIZ
Ezekiel 42 in the TOMA
Ezekiel 42 in the TTENT
Ezekiel 42 in the UBG
Ezekiel 42 in the UGV
Ezekiel 42 in the UGV2
Ezekiel 42 in the UGV3
Ezekiel 42 in the VBL
Ezekiel 42 in the VDCC
Ezekiel 42 in the YALU
Ezekiel 42 in the YAPE
Ezekiel 42 in the YBVTP
Ezekiel 42 in the ZBP