Ezekiel 5 (BOKCV)

1 “Mwanadamu, sasa chukua upanga mkali na uutumie kama wembe wa kinyozi ili kunyolea nywele za kichwa chako na ndevu zako. Kisha uchukue mizani ya kupimia ukazigawanye nywele hizo. 2 Wakati siku zako za kuzingirwa zitakapokwisha, choma theluthi moja ya hizo nywele zako kwa moto ndani ya mji. Chukua theluthi nyingine ya hizo nywele uzipige kwa upanga kuuzunguka mji wote na theluthi nyingine ya mwisho utaitawanya kwa upepo. Kwa kuwa nitawafuatia kwa upanga uliofutwa. 3 Lakini chukua nywele chache uzifungie ndani ya pindo la vazi lako. 4 Tena chukua nywele nyingine chache uzitupe motoni uziteketeze. Moto utaenea kutoka humo na kufika katika nyumba yote ya Israeli. 5 “Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Huu ndio Yerusalemu ambao nimeuweka katikati ya mataifa ukiwa umezungukwa na nchi pande zote. 6 Lakini katika uovu wake umeasi sheria na amri zangu kuliko mataifa na nchi zinazouzunguka. Umeasi sheria zangu wala haukufuata amri zangu. 7 “Kwa hiyo hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Ninyi mmekuwa wakaidi kuliko mataifa yanayowazunguka na hamkufuata amri zangu wala kuzishika sheria zangu. Wala hamkuweza hata kuzifuata kawaida za mataifa yanayowazunguka. 8 “Kwa hiyo, hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo, Mimi mwenyewe, niko kinyume nanyi Yerusalemu, nitawapiga kwa adhabu yangu mbele ya mataifa. 9 Kwa ajili ya sanamu zenu zote za machukizo, nitawafanyia kile ambacho kamwe sijawafanyia kabla wala kamwe sitawafanyia tena. 10 Kwa hiyo katikati yenu baba watakula watoto wao na watoto watakula baba zao. Nitawapiga kwa adhabu, nami nitawatawanya watu wenu walionusurika pande zote za dunia. 11 Kwa hiyo hakika kama niishivyo, asema BWANA Mwenyezi, kwa kuwa mmenajisi mahali pangu patakatifu kwa sanamu zenu mbaya sana na desturi zenu za machukizo, mimi mwenyewe nitaondoa fadhili zangu kwenu. 12 Theluthi ya watu wako watakufa kwa tauni au kwa njaa humu ndani yako, theluthi nyingine itaanguka kwa upanga nje ya kuta zako, nayo theluthi nyingine nitaitawanya kwenye pande nne kuwafuatia kwa upanga uliofutwa. 13 “Ndipo hasira yangu itakapokoma na ghadhabu yangu dhidi yao itatulia, nami nitakuwa nimelipiza kisasi. Baada ya kuimaliza ghadhabu yangu juu yao, watajua kuwa mimi BWANA nimenena katika wivu wangu. 14 “Nitakuangamiza na kukufanya kitu cha kudharauliwa miongoni mwa mataifa yanayokuzunguka, machoni pa watu wote wapitao karibu nawe. 15 Utakuwa kitu cha kudharauliwa na cha aibu, cha dhihaka, ovyo na kitu cha kutisha kwa mataifa yanayokuzunguka, nitakapokupiga kwa adhabu yangu katika hasira na ghadhabu yangu kwa kukukemea kwa ukali. Mimi BWANA nimesema. 16 Nitakapokupiga kwa mishale yangu ya kufisha na yenye kuharibu ya njaa, nitaipiga ili kukuangamiza. Nitaleta njaa zaidi na zaidi juu yako na kukomesha upatikanaji wa chakula kwako. 17 Nitapeleka njaa na wanyama wa mwituni dhidi yenu, navyo vitawaacha bila watoto. Tauni na umwagaji wa damu utapita katikati yenu, nami nitaleta upanga juu yenu. Mimi BWANA nimenena haya.”

In Other Versions

Ezekiel 5 in the ANGEFD

Ezekiel 5 in the ANTPNG2D

Ezekiel 5 in the AS21

Ezekiel 5 in the BAGH

Ezekiel 5 in the BBPNG

Ezekiel 5 in the BBT1E

Ezekiel 5 in the BDS

Ezekiel 5 in the BEV

Ezekiel 5 in the BHAD

Ezekiel 5 in the BIB

Ezekiel 5 in the BLPT

Ezekiel 5 in the BNT

Ezekiel 5 in the BNTABOOT

Ezekiel 5 in the BNTLV

Ezekiel 5 in the BOATCB

Ezekiel 5 in the BOATCB2

Ezekiel 5 in the BOBCV

Ezekiel 5 in the BOCNT

Ezekiel 5 in the BOECS

Ezekiel 5 in the BOGWICC

Ezekiel 5 in the BOHCB

Ezekiel 5 in the BOHCV

Ezekiel 5 in the BOHLNT

Ezekiel 5 in the BOHNTLTAL

Ezekiel 5 in the BOICB

Ezekiel 5 in the BOILNTAP

Ezekiel 5 in the BOITCV

Ezekiel 5 in the BOKCV2

Ezekiel 5 in the BOKHWOG

Ezekiel 5 in the BOKSSV

Ezekiel 5 in the BOLCB

Ezekiel 5 in the BOLCB2

Ezekiel 5 in the BOMCV

Ezekiel 5 in the BONAV

Ezekiel 5 in the BONCB

Ezekiel 5 in the BONLT

Ezekiel 5 in the BONUT2

Ezekiel 5 in the BOPLNT

Ezekiel 5 in the BOSCB

Ezekiel 5 in the BOSNC

Ezekiel 5 in the BOTLNT

Ezekiel 5 in the BOVCB

Ezekiel 5 in the BOYCB

Ezekiel 5 in the BPBB

Ezekiel 5 in the BPH

Ezekiel 5 in the BSB

Ezekiel 5 in the CCB

Ezekiel 5 in the CUV

Ezekiel 5 in the CUVS

Ezekiel 5 in the DBT

Ezekiel 5 in the DGDNT

Ezekiel 5 in the DHNT

Ezekiel 5 in the DNT

Ezekiel 5 in the ELBE

Ezekiel 5 in the EMTV

Ezekiel 5 in the ESV

Ezekiel 5 in the FBV

Ezekiel 5 in the FEB

Ezekiel 5 in the GGMNT

Ezekiel 5 in the GNT

Ezekiel 5 in the HARY

Ezekiel 5 in the HNT

Ezekiel 5 in the IRVA

Ezekiel 5 in the IRVB

Ezekiel 5 in the IRVG

Ezekiel 5 in the IRVH

Ezekiel 5 in the IRVK

Ezekiel 5 in the IRVM

Ezekiel 5 in the IRVM2

Ezekiel 5 in the IRVO

Ezekiel 5 in the IRVP

Ezekiel 5 in the IRVT

Ezekiel 5 in the IRVT2

Ezekiel 5 in the IRVU

Ezekiel 5 in the ISVN

Ezekiel 5 in the JSNT

Ezekiel 5 in the KAPI

Ezekiel 5 in the KBT1ETNIK

Ezekiel 5 in the KBV

Ezekiel 5 in the KJV

Ezekiel 5 in the KNFD

Ezekiel 5 in the LBA

Ezekiel 5 in the LBLA

Ezekiel 5 in the LNT

Ezekiel 5 in the LSV

Ezekiel 5 in the MAAL

Ezekiel 5 in the MBV

Ezekiel 5 in the MBV2

Ezekiel 5 in the MHNT

Ezekiel 5 in the MKNFD

Ezekiel 5 in the MNG

Ezekiel 5 in the MNT

Ezekiel 5 in the MNT2

Ezekiel 5 in the MRS1T

Ezekiel 5 in the NAA

Ezekiel 5 in the NASB

Ezekiel 5 in the NBLA

Ezekiel 5 in the NBS

Ezekiel 5 in the NBVTP

Ezekiel 5 in the NET2

Ezekiel 5 in the NIV11

Ezekiel 5 in the NNT

Ezekiel 5 in the NNT2

Ezekiel 5 in the NNT3

Ezekiel 5 in the PDDPT

Ezekiel 5 in the PFNT

Ezekiel 5 in the RMNT

Ezekiel 5 in the SBIAS

Ezekiel 5 in the SBIBS

Ezekiel 5 in the SBIBS2

Ezekiel 5 in the SBICS

Ezekiel 5 in the SBIDS

Ezekiel 5 in the SBIGS

Ezekiel 5 in the SBIHS

Ezekiel 5 in the SBIIS

Ezekiel 5 in the SBIIS2

Ezekiel 5 in the SBIIS3

Ezekiel 5 in the SBIKS

Ezekiel 5 in the SBIKS2

Ezekiel 5 in the SBIMS

Ezekiel 5 in the SBIOS

Ezekiel 5 in the SBIPS

Ezekiel 5 in the SBISS

Ezekiel 5 in the SBITS

Ezekiel 5 in the SBITS2

Ezekiel 5 in the SBITS3

Ezekiel 5 in the SBITS4

Ezekiel 5 in the SBIUS

Ezekiel 5 in the SBIVS

Ezekiel 5 in the SBT

Ezekiel 5 in the SBT1E

Ezekiel 5 in the SCHL

Ezekiel 5 in the SNT

Ezekiel 5 in the SUSU

Ezekiel 5 in the SUSU2

Ezekiel 5 in the SYNO

Ezekiel 5 in the TBIAOTANT

Ezekiel 5 in the TBT1E

Ezekiel 5 in the TBT1E2

Ezekiel 5 in the TFTIP

Ezekiel 5 in the TFTU

Ezekiel 5 in the TGNTATF3T

Ezekiel 5 in the THAI

Ezekiel 5 in the TNFD

Ezekiel 5 in the TNT

Ezekiel 5 in the TNTIK

Ezekiel 5 in the TNTIL

Ezekiel 5 in the TNTIN

Ezekiel 5 in the TNTIP

Ezekiel 5 in the TNTIZ

Ezekiel 5 in the TOMA

Ezekiel 5 in the TTENT

Ezekiel 5 in the UBG

Ezekiel 5 in the UGV

Ezekiel 5 in the UGV2

Ezekiel 5 in the UGV3

Ezekiel 5 in the VBL

Ezekiel 5 in the VDCC

Ezekiel 5 in the YALU

Ezekiel 5 in the YAPE

Ezekiel 5 in the YBVTP

Ezekiel 5 in the ZBP