Ezra 5 (BOKCV)
1 Ndipo nabii Hagai na nabii Zekaria mzao wa Ido, wakawatolea unabii Wayahudi waliokuwa Yuda na Yerusalemu kwa jina la Mungu wa Israeli, aliyekuwa pamoja nao. 2 Ndipo Zerubabeli mwana wa Shealtieli na Yeshua mwana wa Yosadaki wakaanza kujenga tena nyumba ya Mungu huko Yerusalemu. Nao manabii wa Mungu walikuwa pamoja nao, wakiwasaidia. 3 Wakati ule Tatenai mtawala wa ngʼambo ya mto Frati na Shethar-Bozenai na wenzao waliwaendea, wakawauliza, “Ni nani aliyewapa ruhusa ya kujenga tena Hekalu hili na kurudishia upya kama lilivyokuwa?” 4 Pia waliwauliza, “Je, majina ya watu wanaofanya ujenzi huu ni nani?” 5 Lakini jicho la Mungu wao lilikuwa likiwaangalia wazee wa Wayahudi, nao hawakuzuiliwa kujenga mpaka taarifa ikaandikwa kwa Dario na majibu yake kupokelewa. 6 Hii ni nakala ya barua ile Tatenai, mtawala wa ngʼambo ya mto Frati na Shethar-Bozenai na wenzao maafisa wa ngʼambo ya mto Frati waliyompelekea Mfalme Dario. 7 Taarifa waliyompelekea ilisomeka kama ifuatavyo:Kwa Mfalme Dario:Salamu kwa moyo mkunjufu. 8 Inampasa Mfalme ajue kwamba tulikwenda katika eneo la Yuda, kwenye Hekalu la Mungu mkuu. Watu wanalijenga kwa mawe makubwa na kuweka mbao kwenye kuta. Kazi inafanyika kwa bidii na inaendelea kwa haraka chini ya uongozi wao. 9 Tuliwauliza viongozi, “Ni nani aliyewapa ruhusa kujenga upya Hekalu hili na kurejeza hali ya jengo kama lilivyokuwa?” 10 Pia tuliwauliza majina yao, ili tukuandikie kukujulisha majina ya viongozi wao. 11 Hili ndilo jibu walilotupa: “Sisi ni watumishi wa Mungu wa mbingu na nchi, nasi tunalijenga upya Hekalu ambalo lilijengwa miaka mingi iliyopita, lile ambalo mfalme mkuu wa Israeli alilijenga na kulikamilisha. 12 Lakini kwa sababu baba zetu walimkasirisha Mungu wa mbinguni, basi aliwatia mkononi mwa Nebukadneza, Mkaldayo, mfalme wa Babeli, ambaye aliliharibu Hekalu hili na kuwaondoa watu na kuwapeleka uhamishoni huko Babeli. 13 “Pamoja na hayo, katika mwaka wa kwanza wa kutawala Koreshi mfalme wa Babeli, Mfalme Koreshi alitoa amri ya kujengwa upya nyumba hii ya Mungu. 14 Yeye hata aliviondoa vyombo vya dhahabu na fedha vya nyumba ya Mungu, kutoka Hekalu la Babeli ambavyo Nebukadneza alikuwa amevichukua kutoka ndani ya Hekalu huko Yerusalemu na kuvileta katika Hekalu la Babeli.“Vyombo hivyo Mfalme Koreshi alimkabidhi mtu aliyeitwa Sheshbaza, ambaye Koreshi alikuwa amemteua awe mtawala, 15 naye akamwambia, ‘Chukua vyombo hivi uende ukaviweke ndani ya Hekalu huko Yerusalemu. Nawe uijenge upya nyumba ya Mungu mahali pake.’ 16 Hivyo huyu Sheshbaza alikuja na kuweka misingi ya nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu. Tangu siku hiyo hadi sasa imekuwa ikiendelea kujengwa lakini bado haijamalizika.” 17 Sasa kama ikimpendeza mfalme, uchunguzi na ufanyike katika kumbukumbu za maandishi ya ufalme mjini Babeli, kuona kama kweli Mfalme Koreshi alitoa amri ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika Yerusalemu. Kisha tunaomba mfalme na atutumie uamuzi wake kuhusu jambo hili.
In Other Versions
Ezra 5 in the ANGEFD
Ezra 5 in the ANTPNG2D
Ezra 5 in the AS21
Ezra 5 in the BAGH
Ezra 5 in the BBPNG
Ezra 5 in the BBT1E
Ezra 5 in the BDS
Ezra 5 in the BEV
Ezra 5 in the BHAD
Ezra 5 in the BIB
Ezra 5 in the BLPT
Ezra 5 in the BNT
Ezra 5 in the BNTABOOT
Ezra 5 in the BNTLV
Ezra 5 in the BOATCB
Ezra 5 in the BOATCB2
Ezra 5 in the BOBCV
Ezra 5 in the BOCNT
Ezra 5 in the BOECS
Ezra 5 in the BOGWICC
Ezra 5 in the BOHCB
Ezra 5 in the BOHCV
Ezra 5 in the BOHLNT
Ezra 5 in the BOHNTLTAL
Ezra 5 in the BOICB
Ezra 5 in the BOILNTAP
Ezra 5 in the BOITCV
Ezra 5 in the BOKCV2
Ezra 5 in the BOKHWOG
Ezra 5 in the BOKSSV
Ezra 5 in the BOLCB
Ezra 5 in the BOLCB2
Ezra 5 in the BOMCV
Ezra 5 in the BONAV
Ezra 5 in the BONCB
Ezra 5 in the BONLT
Ezra 5 in the BONUT2
Ezra 5 in the BOPLNT
Ezra 5 in the BOSCB
Ezra 5 in the BOSNC
Ezra 5 in the BOTLNT
Ezra 5 in the BOVCB
Ezra 5 in the BOYCB
Ezra 5 in the BPBB
Ezra 5 in the BPH
Ezra 5 in the BSB
Ezra 5 in the CCB
Ezra 5 in the CUV
Ezra 5 in the CUVS
Ezra 5 in the DBT
Ezra 5 in the DGDNT
Ezra 5 in the DHNT
Ezra 5 in the DNT
Ezra 5 in the ELBE
Ezra 5 in the EMTV
Ezra 5 in the ESV
Ezra 5 in the FBV
Ezra 5 in the FEB
Ezra 5 in the GGMNT
Ezra 5 in the GNT
Ezra 5 in the HARY
Ezra 5 in the HNT
Ezra 5 in the IRVA
Ezra 5 in the IRVB
Ezra 5 in the IRVG
Ezra 5 in the IRVH
Ezra 5 in the IRVK
Ezra 5 in the IRVM
Ezra 5 in the IRVM2
Ezra 5 in the IRVO
Ezra 5 in the IRVP
Ezra 5 in the IRVT
Ezra 5 in the IRVT2
Ezra 5 in the IRVU
Ezra 5 in the ISVN
Ezra 5 in the JSNT
Ezra 5 in the KAPI
Ezra 5 in the KBT1ETNIK
Ezra 5 in the KBV
Ezra 5 in the KJV
Ezra 5 in the KNFD
Ezra 5 in the LBA
Ezra 5 in the LBLA
Ezra 5 in the LNT
Ezra 5 in the LSV
Ezra 5 in the MAAL
Ezra 5 in the MBV
Ezra 5 in the MBV2
Ezra 5 in the MHNT
Ezra 5 in the MKNFD
Ezra 5 in the MNG
Ezra 5 in the MNT
Ezra 5 in the MNT2
Ezra 5 in the MRS1T
Ezra 5 in the NAA
Ezra 5 in the NASB
Ezra 5 in the NBLA
Ezra 5 in the NBS
Ezra 5 in the NBVTP
Ezra 5 in the NET2
Ezra 5 in the NIV11
Ezra 5 in the NNT
Ezra 5 in the NNT2
Ezra 5 in the NNT3
Ezra 5 in the PDDPT
Ezra 5 in the PFNT
Ezra 5 in the RMNT
Ezra 5 in the SBIAS
Ezra 5 in the SBIBS
Ezra 5 in the SBIBS2
Ezra 5 in the SBICS
Ezra 5 in the SBIDS
Ezra 5 in the SBIGS
Ezra 5 in the SBIHS
Ezra 5 in the SBIIS
Ezra 5 in the SBIIS2
Ezra 5 in the SBIIS3
Ezra 5 in the SBIKS
Ezra 5 in the SBIKS2
Ezra 5 in the SBIMS
Ezra 5 in the SBIOS
Ezra 5 in the SBIPS
Ezra 5 in the SBISS
Ezra 5 in the SBITS
Ezra 5 in the SBITS2
Ezra 5 in the SBITS3
Ezra 5 in the SBITS4
Ezra 5 in the SBIUS
Ezra 5 in the SBIVS
Ezra 5 in the SBT
Ezra 5 in the SBT1E
Ezra 5 in the SCHL
Ezra 5 in the SNT
Ezra 5 in the SUSU
Ezra 5 in the SUSU2
Ezra 5 in the SYNO
Ezra 5 in the TBIAOTANT
Ezra 5 in the TBT1E
Ezra 5 in the TBT1E2
Ezra 5 in the TFTIP
Ezra 5 in the TFTU
Ezra 5 in the TGNTATF3T
Ezra 5 in the THAI
Ezra 5 in the TNFD
Ezra 5 in the TNT
Ezra 5 in the TNTIK
Ezra 5 in the TNTIL
Ezra 5 in the TNTIN
Ezra 5 in the TNTIP
Ezra 5 in the TNTIZ
Ezra 5 in the TOMA
Ezra 5 in the TTENT
Ezra 5 in the UBG
Ezra 5 in the UGV
Ezra 5 in the UGV2
Ezra 5 in the UGV3
Ezra 5 in the VBL
Ezra 5 in the VDCC
Ezra 5 in the YALU
Ezra 5 in the YAPE
Ezra 5 in the YBVTP
Ezra 5 in the ZBP