Genesis 17 (BOKCV)
1 Abramu alipokuwa na miaka tisini na tisa, BWANA akamtokea akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi; enenda mbele zangu na uishi kwa unyofu. 2 Nami nitafanya Agano langu kati yangu na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.” 3 Abramu akaanguka kifudifudi, naye Mungu akamwambia, 4 “Kwa upande wangu, hili ndilo Agano langu na wewe: Wewe utakuwa baba wa mataifa mengi. 5 Jina lako hutaitwa tena Abramu, bali jina lako litakuwa Abrahamu, kwa maana nimekufanya wewe baba wa mataifa mengi. 6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, kwako yatatoka mataifa nao wafalme watatoka kwako. 7 Nitalithibitisha Agano langu kama Agano la milele kati yangu na wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo niwe Mungu wako na Mungu wa wazao wako. 8 Nchi yote ya Kanaani, unakoishi sasa kama mgeni, nitakupa kuwa milki yako milele, na uzao wako, nami nitakuwa Mungu wao.” 9 Ndipo Mungu akamwambia Abrahamu, “Kwa upande wako, lazima ushike Agano langu, wewe na wazao wako kwa ajili ya vizazi vijavyo. 10 Hili ni Agano langu na wewe pamoja na wazao wako baada yako, Agano mtakalolishika: Kila mwanaume miongoni mwenu atatahiriwa. 11 Mtafanyiwa tohara na hii itakuwa ni alama ya Agano kati yangu na ninyi. 12 Kwa vizazi vijavyo, kila mwanaume miongoni mwenu mwenye siku nane ni lazima atahiriwe, pamoja na watakaozaliwa nyumbani mwako au walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni, wale ambao sio watoto wako. 13 Awe amezaliwa nyumbani mwako au amenunuliwa kwa fedha yako, ni lazima watahiriwe. Agano langu katika mwili wako litakuwa ni Agano la milele. 14 Kila mwanaume asiyetahiriwa, ambaye hajapata tohara ya mwilini, atatengwa na watu wake, amelivunja Agano langu.” 15 Pia BWANA akamwambia Abrahamu, “Kwa upande wa Sarai mkeo, hutamwita tena Sarai bali jina lake litakuwa Sara. 16 Nitambariki na hakika nitakupatia mwana kwake. Nitambariki na kwamba atakuwa mama wa mataifa, wafalme wa mataifa watatoka kwake.” 17 Abrahamu akaanguka kifudifudi, akacheka na kusema moyoni mwake, “Je, mtu wa miaka mia moja aweza kuzaa mwana? Je, Sara atazaa mtoto katika umri wa miaka tisini?” 18 Abrahamu akamwambia Mungu, “Laiti Ishmaeli naye angeshiriki baraka yako!” 19 Ndipo Mungu akasema, “Ndiyo, lakini mkeo Sara atakuzalia wewe mwana, nawe utamwita jina lake Isaki. Nitalithibitisha Agano langu naye kama Agano la milele kwa ajili yake na wazao wake baada yake. 20 Kwa upande wa Ishmaeli, nimekusikia: hakika nitambariki, nitamfanya awe na uzao mwingi na nitaongeza sana idadi yake. Atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kubwa. 21 Lakini Agano langu nitalithibitisha kwa Isaki, ambaye Sara atakuzalia mwaka ujao majira kama haya.” 22 Wakati alipomaliza kuzungumza na Abrahamu, Mungu akapanda juu akaondoka kwa Abrahamu. 23 Siku ile ile, Abrahamu akamchukua Ishmaeli mwanawe na wote waliozaliwa nyumbani mwake pamoja na walionunuliwa kwa fedha zake, kila mwanaume wa nyumbani mwake, akawatahiri, kama Mungu alivyomwagiza. 24 Abrahamu alikuwa na umri wa miaka tisini na tisa alipotahiriwa, 25 naye Ishmaeli mwanawe alitahiriwa akiwa na umri wa miaka kumi na mitatu. 26 Abrahamu na Ishmaeli mwanawe walitahiriwa siku ile ile, 27 Kila mwanaume nyumbani mwa Abrahamu, pamoja na wote waliozaliwa nyumbani mwake au aliyenunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni, alitahiriwa pamoja naye.
In Other Versions
Genesis 17 in the ANGEFD
Genesis 17 in the ANTPNG2D
Genesis 17 in the AS21
Genesis 17 in the BAGH
Genesis 17 in the BBPNG
Genesis 17 in the BBT1E
Genesis 17 in the BDS
Genesis 17 in the BEV
Genesis 17 in the BHAD
Genesis 17 in the BIB
Genesis 17 in the BLPT
Genesis 17 in the BNT
Genesis 17 in the BNTABOOT
Genesis 17 in the BNTLV
Genesis 17 in the BOATCB
Genesis 17 in the BOATCB2
Genesis 17 in the BOBCV
Genesis 17 in the BOCNT
Genesis 17 in the BOECS
Genesis 17 in the BOGWICC
Genesis 17 in the BOHCB
Genesis 17 in the BOHCV
Genesis 17 in the BOHLNT
Genesis 17 in the BOHNTLTAL
Genesis 17 in the BOICB
Genesis 17 in the BOILNTAP
Genesis 17 in the BOITCV
Genesis 17 in the BOKCV2
Genesis 17 in the BOKHWOG
Genesis 17 in the BOKSSV
Genesis 17 in the BOLCB
Genesis 17 in the BOLCB2
Genesis 17 in the BOMCV
Genesis 17 in the BONAV
Genesis 17 in the BONCB
Genesis 17 in the BONLT
Genesis 17 in the BONUT2
Genesis 17 in the BOPLNT
Genesis 17 in the BOSCB
Genesis 17 in the BOSNC
Genesis 17 in the BOTLNT
Genesis 17 in the BOVCB
Genesis 17 in the BOYCB
Genesis 17 in the BPBB
Genesis 17 in the BPH
Genesis 17 in the BSB
Genesis 17 in the CCB
Genesis 17 in the CUV
Genesis 17 in the CUVS
Genesis 17 in the DBT
Genesis 17 in the DGDNT
Genesis 17 in the DHNT
Genesis 17 in the DNT
Genesis 17 in the ELBE
Genesis 17 in the EMTV
Genesis 17 in the ESV
Genesis 17 in the FBV
Genesis 17 in the FEB
Genesis 17 in the GGMNT
Genesis 17 in the GNT
Genesis 17 in the HARY
Genesis 17 in the HNT
Genesis 17 in the IRVA
Genesis 17 in the IRVB
Genesis 17 in the IRVG
Genesis 17 in the IRVH
Genesis 17 in the IRVK
Genesis 17 in the IRVM
Genesis 17 in the IRVM2
Genesis 17 in the IRVO
Genesis 17 in the IRVP
Genesis 17 in the IRVT
Genesis 17 in the IRVT2
Genesis 17 in the IRVU
Genesis 17 in the ISVN
Genesis 17 in the JSNT
Genesis 17 in the KAPI
Genesis 17 in the KBT1ETNIK
Genesis 17 in the KBV
Genesis 17 in the KJV
Genesis 17 in the KNFD
Genesis 17 in the LBA
Genesis 17 in the LBLA
Genesis 17 in the LNT
Genesis 17 in the LSV
Genesis 17 in the MAAL
Genesis 17 in the MBV
Genesis 17 in the MBV2
Genesis 17 in the MHNT
Genesis 17 in the MKNFD
Genesis 17 in the MNG
Genesis 17 in the MNT
Genesis 17 in the MNT2
Genesis 17 in the MRS1T
Genesis 17 in the NAA
Genesis 17 in the NASB
Genesis 17 in the NBLA
Genesis 17 in the NBS
Genesis 17 in the NBVTP
Genesis 17 in the NET2
Genesis 17 in the NIV11
Genesis 17 in the NNT
Genesis 17 in the NNT2
Genesis 17 in the NNT3
Genesis 17 in the PDDPT
Genesis 17 in the PFNT
Genesis 17 in the RMNT
Genesis 17 in the SBIAS
Genesis 17 in the SBIBS
Genesis 17 in the SBIBS2
Genesis 17 in the SBICS
Genesis 17 in the SBIDS
Genesis 17 in the SBIGS
Genesis 17 in the SBIHS
Genesis 17 in the SBIIS
Genesis 17 in the SBIIS2
Genesis 17 in the SBIIS3
Genesis 17 in the SBIKS
Genesis 17 in the SBIKS2
Genesis 17 in the SBIMS
Genesis 17 in the SBIOS
Genesis 17 in the SBIPS
Genesis 17 in the SBISS
Genesis 17 in the SBITS
Genesis 17 in the SBITS2
Genesis 17 in the SBITS3
Genesis 17 in the SBITS4
Genesis 17 in the SBIUS
Genesis 17 in the SBIVS
Genesis 17 in the SBT
Genesis 17 in the SBT1E
Genesis 17 in the SCHL
Genesis 17 in the SNT
Genesis 17 in the SUSU
Genesis 17 in the SUSU2
Genesis 17 in the SYNO
Genesis 17 in the TBIAOTANT
Genesis 17 in the TBT1E
Genesis 17 in the TBT1E2
Genesis 17 in the TFTIP
Genesis 17 in the TFTU
Genesis 17 in the TGNTATF3T
Genesis 17 in the THAI
Genesis 17 in the TNFD
Genesis 17 in the TNT
Genesis 17 in the TNTIK
Genesis 17 in the TNTIL
Genesis 17 in the TNTIN
Genesis 17 in the TNTIP
Genesis 17 in the TNTIZ
Genesis 17 in the TOMA
Genesis 17 in the TTENT
Genesis 17 in the UBG
Genesis 17 in the UGV
Genesis 17 in the UGV2
Genesis 17 in the UGV3
Genesis 17 in the VBL
Genesis 17 in the VDCC
Genesis 17 in the YALU
Genesis 17 in the YAPE
Genesis 17 in the YBVTP
Genesis 17 in the ZBP