Genesis 3 (BOKCV)
1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambao BWANA Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?” 2 Mwanamke akamjibu nyoka, “Tunaweza kula matunda ya miti iliyoko bustanini, 3 lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani, wala kuugusa, la sivyo mtakufa.’ ” 4 Lakini nyoka akamwambia mwanamke, “Hakika hamtakufa. 5 Kwa maana Mungu anajua ya kuwa wakati mtakapoyala, macho yenu yatafumbuliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” 6 Mwanamke alipoona ya kuwa tunda la mti huo lilikuwa zuri kwa chakula na la kupendeza macho, tena linatamanika kwa kujipatia hekima, basi akachuma katika matunda yake, akala, pia akampa mumewe, aliyekuwa pamoja naye, naye akala. 7 Ndipo macho yao wote wawili yakafumbuliwa, wakajiona kwamba walikuwa uchi; hivyo wakashona majani ya mtini, wakajifunika. 8 Ndipo yule mwanaume na mkewe, waliposikia sauti ya BWANA Mungu alipokuwa akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka mbele za BWANA Mungu katikati ya miti ya bustani. 9 Lakini BWANA Mungu akamwita Adamu, “Uko wapi?” 10 Naye akajibu, “Nilikusikia katika bustani nikaogopa kwa sababu nilikuwa uchi, hivyo nikajificha.” 11 Mungu akamuuliza, “Ni nani aliyekuambia ya kuwa ulikuwa uchi? Je, umekula matunda ya mti niliokuamuru usile?” 12 Adamu akasema, “Huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja nami alinipa sehemu ya tunda kutoka kwenye huo mti, nami nikala.” 13 Ndipo BWANA Mungu akamuuliza mwanamke, “Ni nini hili ambalo umelifanya?” Mwanamke akajibu, “Nyoka alinidanganya, nami nikala.” 14 Hivyo BWANA Mungu akamwambia nyoka, “Kwa kuwa umefanya hili,“Umelaaniwa kuliko wanyama wotewa kufugwa na wa porini!Utatambaa kwa tumbo lakona kula mavumbisiku zote za maisha yako. 15 Nami nitaweka uaduikati yako na huyo mwanamke,na kati ya uzao wako na wake,yeye atakuponda kichwa,nawe utamuuma kisigino.” 16 Kwa mwanamke akasema,“Nitakuzidishia sana utungu wakati wa kuzaa kwako;kwa utungu utazaa watoto.Tamaa yako itakuwa kwa mumeonaye atakutawala.” 17 Kwa Adamu akasema, “Kwa sababu umemsikiliza mke wako na ukala kutoka kwenye mti niliokuamuru, ‘Msile tunda lake,’“Ardhi imelaaniwa kwa sababu yako,kwa kazi ngumu utakula chakula kitokacho humosiku zote za maisha yako. 18 Itazaa miiba na mibaruti kwa ajili yako,nawe utakula mimea ya shambani. 19 Kwa jasho la uso wakoutakula chakula chakohadi utakaporudi ardhini,kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo,kwa kuwa wewe u mavumbina mavumbini wewe utarudi.” 20 Adamu akamwita mkewe Eva, kwa kuwa atakuwa mama wa wote walio hai. 21 BWANA Mungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika. 22 Kisha BWANA Mungu akasema, “Sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya. Sharti asiruhusiwe kunyoosha mkono wake na kuchuma pia kutoka mti wa uzima akala, naye akaishi milele.” 23 Hivyo BWANA Mungu akamfukuzia mbali kutoka Bustani ya Edeni, akalime ardhi ambamo alitolewa. 24 Baada ya kumfukuzia mbali Adamu, Mungu akaweka makerubi mashariki ya Bustani ya Edeni, pamoja na upanga wa moto ukimulika huku na huko kulinda njia ya kuuendea mti wa uzima.
In Other Versions
Genesis 3 in the ANGEFD
Genesis 3 in the ANTPNG2D
Genesis 3 in the AS21
Genesis 3 in the BAGH
Genesis 3 in the BBPNG
Genesis 3 in the BBT1E
Genesis 3 in the BDS
Genesis 3 in the BEV
Genesis 3 in the BHAD
Genesis 3 in the BIB
Genesis 3 in the BLPT
Genesis 3 in the BNT
Genesis 3 in the BNTABOOT
Genesis 3 in the BNTLV
Genesis 3 in the BOATCB
Genesis 3 in the BOATCB2
Genesis 3 in the BOBCV
Genesis 3 in the BOCNT
Genesis 3 in the BOECS
Genesis 3 in the BOGWICC
Genesis 3 in the BOHCB
Genesis 3 in the BOHCV
Genesis 3 in the BOHLNT
Genesis 3 in the BOHNTLTAL
Genesis 3 in the BOICB
Genesis 3 in the BOILNTAP
Genesis 3 in the BOITCV
Genesis 3 in the BOKCV2
Genesis 3 in the BOKHWOG
Genesis 3 in the BOKSSV
Genesis 3 in the BOLCB
Genesis 3 in the BOLCB2
Genesis 3 in the BOMCV
Genesis 3 in the BONAV
Genesis 3 in the BONCB
Genesis 3 in the BONLT
Genesis 3 in the BONUT2
Genesis 3 in the BOPLNT
Genesis 3 in the BOSCB
Genesis 3 in the BOSNC
Genesis 3 in the BOTLNT
Genesis 3 in the BOVCB
Genesis 3 in the BOYCB
Genesis 3 in the BPBB
Genesis 3 in the BPH
Genesis 3 in the BSB
Genesis 3 in the CCB
Genesis 3 in the CUV
Genesis 3 in the CUVS
Genesis 3 in the DBT
Genesis 3 in the DGDNT
Genesis 3 in the DHNT
Genesis 3 in the DNT
Genesis 3 in the ELBE
Genesis 3 in the EMTV
Genesis 3 in the ESV
Genesis 3 in the FBV
Genesis 3 in the FEB
Genesis 3 in the GGMNT
Genesis 3 in the GNT
Genesis 3 in the HARY
Genesis 3 in the HNT
Genesis 3 in the IRVA
Genesis 3 in the IRVB
Genesis 3 in the IRVG
Genesis 3 in the IRVH
Genesis 3 in the IRVK
Genesis 3 in the IRVM
Genesis 3 in the IRVM2
Genesis 3 in the IRVO
Genesis 3 in the IRVP
Genesis 3 in the IRVT
Genesis 3 in the IRVT2
Genesis 3 in the IRVU
Genesis 3 in the ISVN
Genesis 3 in the JSNT
Genesis 3 in the KAPI
Genesis 3 in the KBT1ETNIK
Genesis 3 in the KBV
Genesis 3 in the KJV
Genesis 3 in the KNFD
Genesis 3 in the LBA
Genesis 3 in the LBLA
Genesis 3 in the LNT
Genesis 3 in the LSV
Genesis 3 in the MAAL
Genesis 3 in the MBV
Genesis 3 in the MBV2
Genesis 3 in the MHNT
Genesis 3 in the MKNFD
Genesis 3 in the MNG
Genesis 3 in the MNT
Genesis 3 in the MNT2
Genesis 3 in the MRS1T
Genesis 3 in the NAA
Genesis 3 in the NASB
Genesis 3 in the NBLA
Genesis 3 in the NBS
Genesis 3 in the NBVTP
Genesis 3 in the NET2
Genesis 3 in the NIV11
Genesis 3 in the NNT
Genesis 3 in the NNT2
Genesis 3 in the NNT3
Genesis 3 in the PDDPT
Genesis 3 in the PFNT
Genesis 3 in the RMNT
Genesis 3 in the SBIAS
Genesis 3 in the SBIBS
Genesis 3 in the SBIBS2
Genesis 3 in the SBICS
Genesis 3 in the SBIDS
Genesis 3 in the SBIGS
Genesis 3 in the SBIHS
Genesis 3 in the SBIIS
Genesis 3 in the SBIIS2
Genesis 3 in the SBIIS3
Genesis 3 in the SBIKS
Genesis 3 in the SBIKS2
Genesis 3 in the SBIMS
Genesis 3 in the SBIOS
Genesis 3 in the SBIPS
Genesis 3 in the SBISS
Genesis 3 in the SBITS
Genesis 3 in the SBITS2
Genesis 3 in the SBITS3
Genesis 3 in the SBITS4
Genesis 3 in the SBIUS
Genesis 3 in the SBIVS
Genesis 3 in the SBT
Genesis 3 in the SBT1E
Genesis 3 in the SCHL
Genesis 3 in the SNT
Genesis 3 in the SUSU
Genesis 3 in the SUSU2
Genesis 3 in the SYNO
Genesis 3 in the TBIAOTANT
Genesis 3 in the TBT1E
Genesis 3 in the TBT1E2
Genesis 3 in the TFTIP
Genesis 3 in the TFTU
Genesis 3 in the TGNTATF3T
Genesis 3 in the THAI
Genesis 3 in the TNFD
Genesis 3 in the TNT
Genesis 3 in the TNTIK
Genesis 3 in the TNTIL
Genesis 3 in the TNTIN
Genesis 3 in the TNTIP
Genesis 3 in the TNTIZ
Genesis 3 in the TOMA
Genesis 3 in the TTENT
Genesis 3 in the UBG
Genesis 3 in the UGV
Genesis 3 in the UGV2
Genesis 3 in the UGV3
Genesis 3 in the VBL
Genesis 3 in the VDCC
Genesis 3 in the YALU
Genesis 3 in the YAPE
Genesis 3 in the YBVTP
Genesis 3 in the ZBP