Haggai 1 (BOKCV)

1 Katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario wa Uajemi, katika siku ya kwanza ya mwezi wa sita, neno la BWANA lilikuja kupitia kwa nabii Hagai kwenda kwa Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda na kwa Yoshua mwana wa kuhani mkuu Yehosadaki: 2 Hivi ndivyo asemavyo BWANA Mwenye Nguvu Zote: “Hawa watu husema, ‘Wakati haujawadia wa kujenga nyumba ya BWANA.’ ” 3 Kisha neno la BWANA likaja kupitia kwa nabii Hagai: 4 “Je, ni wakati wenu ninyi wa kuishi katika nyumba zenu zilizojengwa vizuri, wakati hii nyumba ikibaki, gofu?” 5 Sasa hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: “Zitafakarini vyema njia zenu. 6 Mmepanda vingi, lakini mmevuna haba. Mnakula lakini hamshibi, mnakunywa, lakini hamtosheki. Mnavaa nguo, lakini hamsikii joto. Mnapata mishahara, lakini inatoweka kama imewekwa kwenye mfuko uliotobokatoboka.” 7 Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: “Zitafakarini vyema njia zenu. 8 Pandeni milimani mkalete miti na kujenga nyumba, ili nipate kuifurahia, na nitukuzwe,” asema BWANA. 9 “Mlitarajia mengi, kumbe, yametokea kidogo. Ulichokileta nyumbani nilikipeperusha. Kwa nini?” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote. “Ni kwa sababu ya nyumba yangu, inayobaki katika hali ya magofu, wakati kila mmoja wenu anajishughulisha na nyumba yake mwenyewe. 10 Kwa hiyo, kwa sababu yenu mbingu zimezuia umande wake na ardhi mavuno yake. 11 Niliita ukame mashambani na milimani, kwenye nafaka, mvinyo mpya, mafuta pamoja na chochote kinachozalishwa na ardhi, juu ya watu na ngʼombe, pamoja na kazi za mikono yenu.” 12 Kisha Zerubabeli mwana wa Shealtieli, Yoshua kuhani mkuu mwana wa Yehosadaki, pamoja na mabaki yote ya watu wakaitii sauti ya BWANA Mungu wao pamoja na ujumbe wa nabii Hagai, kwa sababu alikuwa ametumwa na BWANA Mungu wao. Watu walimwogopa BWANA. 13 Kisha Hagai, mjumbe wa BWANA, akawapa watu ujumbe huu wa BWANA: “Mimi niko pamoja nanyi,” asema BWANA. 14 Kwa hiyo BWANA akachochea roho ya Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na roho ya kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki, pamoja na roho za mabaki yote ya watu. Walikuja wakaanza kufanya kazi katika nyumba ya BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wao, 15 katika siku ya ishirini na nne mwezi wa sita, katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario.

In Other Versions

Haggai 1 in the ANGEFD

Haggai 1 in the ANTPNG2D

Haggai 1 in the AS21

Haggai 1 in the BAGH

Haggai 1 in the BBPNG

Haggai 1 in the BBT1E

Haggai 1 in the BDS

Haggai 1 in the BEV

Haggai 1 in the BHAD

Haggai 1 in the BIB

Haggai 1 in the BLPT

Haggai 1 in the BNT

Haggai 1 in the BNTABOOT

Haggai 1 in the BNTLV

Haggai 1 in the BOATCB

Haggai 1 in the BOATCB2

Haggai 1 in the BOBCV

Haggai 1 in the BOCNT

Haggai 1 in the BOECS

Haggai 1 in the BOGWICC

Haggai 1 in the BOHCB

Haggai 1 in the BOHCV

Haggai 1 in the BOHLNT

Haggai 1 in the BOHNTLTAL

Haggai 1 in the BOICB

Haggai 1 in the BOILNTAP

Haggai 1 in the BOITCV

Haggai 1 in the BOKCV2

Haggai 1 in the BOKHWOG

Haggai 1 in the BOKSSV

Haggai 1 in the BOLCB

Haggai 1 in the BOLCB2

Haggai 1 in the BOMCV

Haggai 1 in the BONAV

Haggai 1 in the BONCB

Haggai 1 in the BONLT

Haggai 1 in the BONUT2

Haggai 1 in the BOPLNT

Haggai 1 in the BOSCB

Haggai 1 in the BOSNC

Haggai 1 in the BOTLNT

Haggai 1 in the BOVCB

Haggai 1 in the BOYCB

Haggai 1 in the BPBB

Haggai 1 in the BPH

Haggai 1 in the BSB

Haggai 1 in the CCB

Haggai 1 in the CUV

Haggai 1 in the CUVS

Haggai 1 in the DBT

Haggai 1 in the DGDNT

Haggai 1 in the DHNT

Haggai 1 in the DNT

Haggai 1 in the ELBE

Haggai 1 in the EMTV

Haggai 1 in the ESV

Haggai 1 in the FBV

Haggai 1 in the FEB

Haggai 1 in the GGMNT

Haggai 1 in the GNT

Haggai 1 in the HARY

Haggai 1 in the HNT

Haggai 1 in the IRVA

Haggai 1 in the IRVB

Haggai 1 in the IRVG

Haggai 1 in the IRVH

Haggai 1 in the IRVK

Haggai 1 in the IRVM

Haggai 1 in the IRVM2

Haggai 1 in the IRVO

Haggai 1 in the IRVP

Haggai 1 in the IRVT

Haggai 1 in the IRVT2

Haggai 1 in the IRVU

Haggai 1 in the ISVN

Haggai 1 in the JSNT

Haggai 1 in the KAPI

Haggai 1 in the KBT1ETNIK

Haggai 1 in the KBV

Haggai 1 in the KJV

Haggai 1 in the KNFD

Haggai 1 in the LBA

Haggai 1 in the LBLA

Haggai 1 in the LNT

Haggai 1 in the LSV

Haggai 1 in the MAAL

Haggai 1 in the MBV

Haggai 1 in the MBV2

Haggai 1 in the MHNT

Haggai 1 in the MKNFD

Haggai 1 in the MNG

Haggai 1 in the MNT

Haggai 1 in the MNT2

Haggai 1 in the MRS1T

Haggai 1 in the NAA

Haggai 1 in the NASB

Haggai 1 in the NBLA

Haggai 1 in the NBS

Haggai 1 in the NBVTP

Haggai 1 in the NET2

Haggai 1 in the NIV11

Haggai 1 in the NNT

Haggai 1 in the NNT2

Haggai 1 in the NNT3

Haggai 1 in the PDDPT

Haggai 1 in the PFNT

Haggai 1 in the RMNT

Haggai 1 in the SBIAS

Haggai 1 in the SBIBS

Haggai 1 in the SBIBS2

Haggai 1 in the SBICS

Haggai 1 in the SBIDS

Haggai 1 in the SBIGS

Haggai 1 in the SBIHS

Haggai 1 in the SBIIS

Haggai 1 in the SBIIS2

Haggai 1 in the SBIIS3

Haggai 1 in the SBIKS

Haggai 1 in the SBIKS2

Haggai 1 in the SBIMS

Haggai 1 in the SBIOS

Haggai 1 in the SBIPS

Haggai 1 in the SBISS

Haggai 1 in the SBITS

Haggai 1 in the SBITS2

Haggai 1 in the SBITS3

Haggai 1 in the SBITS4

Haggai 1 in the SBIUS

Haggai 1 in the SBIVS

Haggai 1 in the SBT

Haggai 1 in the SBT1E

Haggai 1 in the SCHL

Haggai 1 in the SNT

Haggai 1 in the SUSU

Haggai 1 in the SUSU2

Haggai 1 in the SYNO

Haggai 1 in the TBIAOTANT

Haggai 1 in the TBT1E

Haggai 1 in the TBT1E2

Haggai 1 in the TFTIP

Haggai 1 in the TFTU

Haggai 1 in the TGNTATF3T

Haggai 1 in the THAI

Haggai 1 in the TNFD

Haggai 1 in the TNT

Haggai 1 in the TNTIK

Haggai 1 in the TNTIL

Haggai 1 in the TNTIN

Haggai 1 in the TNTIP

Haggai 1 in the TNTIZ

Haggai 1 in the TOMA

Haggai 1 in the TTENT

Haggai 1 in the UBG

Haggai 1 in the UGV

Haggai 1 in the UGV2

Haggai 1 in the UGV3

Haggai 1 in the VBL

Haggai 1 in the VDCC

Haggai 1 in the YALU

Haggai 1 in the YAPE

Haggai 1 in the YBVTP

Haggai 1 in the ZBP