Isaiah 36 (BOKCV)
1 Katika mwaka wa kumi na nne wa utawala wa Mfalme Hezekia, Senakeribu mfalme wa Ashuru akaishambulia miji yote ya Yuda yenye ngome na kuiteka. 2 Kisha mfalme wa Ashuru akamtuma jemadari wa jeshi pamoja na jeshi kubwa kutoka Lakishi hadi kwa Mfalme Hezekia huko Yerusalemu. Jemadari wa jeshi akasimama kwenye mfereji wa Bwawa la Juu, lililojengwa katika barabara iendayo kwenye Uwanja wa Dobi. 3 Eliakimu mwana wa Hilkia aliyekuwa msimamizi wa jumba la kifalme, Shebna aliyekuwa katibu, na Yoa mwana wa Asafu mwandishi wakamwendea. 4 Jemadari wa jeshi akawaambia, “Mwambieni Hezekia,“ ‘Hili ndilo asemalo mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru: Ni wapi unapoweka hili tumaini lako? 5 Unasema mnayo mikakati na nguvu za kijeshi, lakini unasema maneno matupu tu. Je, wewe unamtegemea nani, hata ukaniasi mimi? 6 Tazama sasa, unaitegemea Misri, fimbo ile ya mwanzi uliopasuka, ambayo huuchoma na kuujeruhi mkono wa mtu akiiegemea! Hivyo ndivyo alivyo Farao mfalme wa Misri, kwa wote wanaomtegemea. 7 Nawe kama ukiniambia, “Tunamtumainia BWANA Mungu wetu”: je, siyo yeye ambaye Hezekia aliondoa mahali pake pa juu pa kuabudia miungu na madhabahu zake, akiwaambia Yuda na Yerusalemu, “Ni lazima mwabudu mbele ya madhabahu haya”? 8 “ ‘Njooni sasa, fanyeni mapatano na bwana wangu, mfalme wa Ashuru: Nitakupa farasi elfu mbili, kama unaweza kuwapandisha waendesha farasi juu yao! 9 Utawezaje kumzuia hata afisa mmoja aliye mdogo kati ya maafisa wa bwana wangu, ijapo unategemea Misri kwa magari ya vita na wapanda farasi? 10 Zaidi ya hayo, je, nimekuja kushambulia na kuangamiza nchi hii bila BWANA? BWANA mwenyewe ndiye aliniambia niishambulie nchi hii na kuiangamiza.’ ” 11 Ndipo Eliakimu, Shebna na Yoa wakamwambia yule jemadari wa jeshi, “Tafadhali zungumza na watumishi wako kwa lugha ya Kiaramu, kwa kuwa tunaifahamu. Usiseme nasi kwa Kiebrania watu walioko juu ya ukuta wakiwa wanasikia.” 12 Lakini yule jemadari wa jeshi akajibu, “Je, bwana wangu amenituma kutoa ujumbe huu kwa bwana wenu na kwenu tu? Je, hakunituma pia kwa watu walioketi ukutani, ambao, kama ninyi, itawabidi kula mavi yao na kunywa mikojo yao wenyewe?” 13 Kisha yule jemadari wa jeshi akasimama na kuita kwa lugha ya Kiebrania, akasema: “Sikieni maneno ya mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru! 14 Hili ndilo asemalo mfalme: Msikubali Hezekia awadanganye. Hawezi kuwaokoa! 15 Msikubali Hezekia awashawishi kumtumaini BWANA kwa kuwaambia, ‘Hakika BWANA atatuokoa. Mji huu hautaangukia mikononi mwa mfalme wa Ashuru.’ 16 “Msimsikilize Hezekia. Hili ndilo mfalme wa Ashuru asemalo: Fanyeni amani nami na mje kwangu. Kisha kila mmoja wenu atakula kutoka kwa mzabibu wake na mtini wake mwenyewe, na kunywa maji kutoka kisima chake mwenyewe, 17 mpaka nije nikawapeleke katika nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai mpya, nchi ya mkate na ya mashamba ya mizabibu. 18 “Msikubali Hezekia awapotoshe asemapo, ‘BWANA atatuokoa.’ Je, yuko mungu wa taifa lolote aliyewahi kuokoa nchi yake kutoka mkononi mwa mfalme wa Ashuru? 19 Iko wapi miungu ya Hamathi na ya Arpadi? Iko wapi miungu ya Sefarvaimu? Je, imeokoa Samaria kutoka mkononi mwangu? 20 Ni yupi miongoni mwa miungu yote ya nchi hizi ameweza kuokoa nchi yake mkononi mwangu? Inawezekanaje basi BWANA aiokoe Yerusalemu mkononi mwangu?” 21 Lakini wale watu wakakaa kimya, wala hawakujibu lolote, kwa kuwa mfalme alikuwa amewaamuru, “Msimjibu lolote.” 22 Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia msimamizi wa jumba la kifalme, Shebna katibu, na Yoa mwana wa Asafu, mwandishi wakamwendea Hezekia, nguo zao zikiwa zimeraruliwa, na kumwambia yale jemadari wa jeshi aliyoyasema.
In Other Versions
Isaiah 36 in the ANGEFD
Isaiah 36 in the ANTPNG2D
Isaiah 36 in the AS21
Isaiah 36 in the BAGH
Isaiah 36 in the BBPNG
Isaiah 36 in the BBT1E
Isaiah 36 in the BDS
Isaiah 36 in the BEV
Isaiah 36 in the BHAD
Isaiah 36 in the BIB
Isaiah 36 in the BLPT
Isaiah 36 in the BNT
Isaiah 36 in the BNTABOOT
Isaiah 36 in the BNTLV
Isaiah 36 in the BOATCB
Isaiah 36 in the BOATCB2
Isaiah 36 in the BOBCV
Isaiah 36 in the BOCNT
Isaiah 36 in the BOECS
Isaiah 36 in the BOGWICC
Isaiah 36 in the BOHCB
Isaiah 36 in the BOHCV
Isaiah 36 in the BOHLNT
Isaiah 36 in the BOHNTLTAL
Isaiah 36 in the BOICB
Isaiah 36 in the BOILNTAP
Isaiah 36 in the BOITCV
Isaiah 36 in the BOKCV2
Isaiah 36 in the BOKHWOG
Isaiah 36 in the BOKSSV
Isaiah 36 in the BOLCB
Isaiah 36 in the BOLCB2
Isaiah 36 in the BOMCV
Isaiah 36 in the BONAV
Isaiah 36 in the BONCB
Isaiah 36 in the BONLT
Isaiah 36 in the BONUT2
Isaiah 36 in the BOPLNT
Isaiah 36 in the BOSCB
Isaiah 36 in the BOSNC
Isaiah 36 in the BOTLNT
Isaiah 36 in the BOVCB
Isaiah 36 in the BOYCB
Isaiah 36 in the BPBB
Isaiah 36 in the BPH
Isaiah 36 in the BSB
Isaiah 36 in the CCB
Isaiah 36 in the CUV
Isaiah 36 in the CUVS
Isaiah 36 in the DBT
Isaiah 36 in the DGDNT
Isaiah 36 in the DHNT
Isaiah 36 in the DNT
Isaiah 36 in the ELBE
Isaiah 36 in the EMTV
Isaiah 36 in the ESV
Isaiah 36 in the FBV
Isaiah 36 in the FEB
Isaiah 36 in the GGMNT
Isaiah 36 in the GNT
Isaiah 36 in the HARY
Isaiah 36 in the HNT
Isaiah 36 in the IRVA
Isaiah 36 in the IRVB
Isaiah 36 in the IRVG
Isaiah 36 in the IRVH
Isaiah 36 in the IRVK
Isaiah 36 in the IRVM
Isaiah 36 in the IRVM2
Isaiah 36 in the IRVO
Isaiah 36 in the IRVP
Isaiah 36 in the IRVT
Isaiah 36 in the IRVT2
Isaiah 36 in the IRVU
Isaiah 36 in the ISVN
Isaiah 36 in the JSNT
Isaiah 36 in the KAPI
Isaiah 36 in the KBT1ETNIK
Isaiah 36 in the KBV
Isaiah 36 in the KJV
Isaiah 36 in the KNFD
Isaiah 36 in the LBA
Isaiah 36 in the LBLA
Isaiah 36 in the LNT
Isaiah 36 in the LSV
Isaiah 36 in the MAAL
Isaiah 36 in the MBV
Isaiah 36 in the MBV2
Isaiah 36 in the MHNT
Isaiah 36 in the MKNFD
Isaiah 36 in the MNG
Isaiah 36 in the MNT
Isaiah 36 in the MNT2
Isaiah 36 in the MRS1T
Isaiah 36 in the NAA
Isaiah 36 in the NASB
Isaiah 36 in the NBLA
Isaiah 36 in the NBS
Isaiah 36 in the NBVTP
Isaiah 36 in the NET2
Isaiah 36 in the NIV11
Isaiah 36 in the NNT
Isaiah 36 in the NNT2
Isaiah 36 in the NNT3
Isaiah 36 in the PDDPT
Isaiah 36 in the PFNT
Isaiah 36 in the RMNT
Isaiah 36 in the SBIAS
Isaiah 36 in the SBIBS
Isaiah 36 in the SBIBS2
Isaiah 36 in the SBICS
Isaiah 36 in the SBIDS
Isaiah 36 in the SBIGS
Isaiah 36 in the SBIHS
Isaiah 36 in the SBIIS
Isaiah 36 in the SBIIS2
Isaiah 36 in the SBIIS3
Isaiah 36 in the SBIKS
Isaiah 36 in the SBIKS2
Isaiah 36 in the SBIMS
Isaiah 36 in the SBIOS
Isaiah 36 in the SBIPS
Isaiah 36 in the SBISS
Isaiah 36 in the SBITS
Isaiah 36 in the SBITS2
Isaiah 36 in the SBITS3
Isaiah 36 in the SBITS4
Isaiah 36 in the SBIUS
Isaiah 36 in the SBIVS
Isaiah 36 in the SBT
Isaiah 36 in the SBT1E
Isaiah 36 in the SCHL
Isaiah 36 in the SNT
Isaiah 36 in the SUSU
Isaiah 36 in the SUSU2
Isaiah 36 in the SYNO
Isaiah 36 in the TBIAOTANT
Isaiah 36 in the TBT1E
Isaiah 36 in the TBT1E2
Isaiah 36 in the TFTIP
Isaiah 36 in the TFTU
Isaiah 36 in the TGNTATF3T
Isaiah 36 in the THAI
Isaiah 36 in the TNFD
Isaiah 36 in the TNT
Isaiah 36 in the TNTIK
Isaiah 36 in the TNTIL
Isaiah 36 in the TNTIN
Isaiah 36 in the TNTIP
Isaiah 36 in the TNTIZ
Isaiah 36 in the TOMA
Isaiah 36 in the TTENT
Isaiah 36 in the UBG
Isaiah 36 in the UGV
Isaiah 36 in the UGV2
Isaiah 36 in the UGV3
Isaiah 36 in the VBL
Isaiah 36 in the VDCC
Isaiah 36 in the YALU
Isaiah 36 in the YAPE
Isaiah 36 in the YBVTP
Isaiah 36 in the ZBP