Judges 2 (BOKCV)
1 Malaika wa BWANA akakwea kutoka Gilgali hadi Bokimu, naye akasema, “Niliwapandisha kutoka Misri na kuwaingiza katika nchi niliyoapa kuwapa baba zenu. Nikasema, ‘Kamwe sitalivunja Agano langu nanyi. 2 Nanyi msifanye agano na watu wa nchi hii, bali mtazibomoa madhabahu yao.’ Lakini ninyi hamkunitii mimi. Kwa nini mmefanya jambo hili? 3 Sasa basi ninawaambia kuwa sitawafukuza watoke katikati yenu ila watakuwa miiba kwenu, nao miungu yao itakuwa tanzi kwenu.” 4 Malaika wa BWANA alipomaliza kusema mambo haya kwa Waisraeli wote, watu wakalia kwa sauti kuu. 5 Wakapaita mahali pale Bokimu. Nao wakamtolea BWANA sadaka. 6 Baada ya Yoshua kuwapa watu ruhusa waende zao, Waisraeli wakaenda kwenye urithi wao wenyewe ili kumiliki nchi yao. 7 Watu wakamtumikia BWANA siku zote za maisha ya Yoshua, na za hao wazee walioishi baada ya Yoshua kufa, waliokuwa wameona mambo makuu ambayo BWANA alikuwa ametenda kwa ajili ya Israeli. 8 Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa BWANA, akafa akiwa na umri wa miaka 110. 9 Wakamzika katika nchi ya urithi wake, huko Timnath-Heresi katika nchi ya vilima ya Efraimu, kaskazini ya Mlima Gaashi. 10 Baada ya kizazi kile chote kukusanywa pamoja na baba zao, kikainuka kizazi kingine baada yao ambacho hakikumjua BWANA, wala matendo yale aliyokuwa ametenda kwa ajili ya Waisraeli. 11 Kwa hiyo Waisraeli wakatenda maovu machoni pa BWANA na kuwatumikia Mabaali. 12 Wakamwacha BWANA, Mungu wa baba zao, aliyekuwa amewatoa katika nchi ya Misri. Wakaifuata na kuiabudu miungu mbalimbali ya mataifa yanayowazunguka. Wakamkasirisha BWANA, 13 kwa sababu walimwacha na kutumikia Baali na Maashtorethi. 14 Hivyo hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa wavamizi waliowateka nyara. Akawauza katika mikono ya adui zao pande zote, hivyo hawakuweza tena kuwazuia adui zao. 15 Popote Israeli walipotoka kwenda kupigana, mkono wa BWANA ulikuwa kinyume nao ili kuwashinda, kama vile alivyokuwa amewaapia. Nao wakawa katika taabu kubwa. 16 Ndipo BWANA akawainua waamuzi, ambao waliwaokoa katika mikono ya hao watu waliowashambulia. 17 Lakini hawakuwasikiliza hata waamuzi wao, bali walifanya uasherati kwa kuifuata miungu mingine na kuiabudu. Waligeuka mara na kuiacha njia ambayo baba zao waliiendea, yaani, njia ya kutii amri za BWANA. 18 Kila mara BWANA alipowainulia mwamuzi, BWANA alikuwa pamoja na huyo mwamuzi, naye aliwaokoa kutoka mikononi mwa adui zao kwa kipindi chote alichoishi yule mwamuzi. Kwa kuwa BWANA aliwahurumia kwa sababu ya kilio chao cha huzuni kwa ajili ya wale waliokuwa wakiwatesa na kuwataabisha. 19 Lakini kila mara mwamuzi alipofariki, watu walirudia katika hali mbaya ya uovu zaidi kuliko baba zao, wakiifuata miungu mingine kuitumikia na kuiabudu. Walikataa kuacha matendo yao maovu na njia zao za ukaidi. 20 Kwa hiyo BWANA akawakasirikia sana Israeli na kusema, “Kwa kuwa taifa hili limevunja Agano lile nililofanya na baba zao na hawakunisikiliza, 21 mimi nami sitafukuza taifa lolote ambalo Yoshua aliliacha alipofariki. 22 Nitayatumia ili nipate kuwapima Israeli na kuona kama wataishika njia ya BWANA na kuenenda katika hiyo kama njia baba zao walivyofanya.” 23 BWANA alikuwa ameyaacha hayo mataifa yabaki; hakuyaondoa mara moja kwa kuyatia mikononi mwa Yoshua.
In Other Versions
Judges 2 in the ANGEFD
Judges 2 in the ANTPNG2D
Judges 2 in the AS21
Judges 2 in the BAGH
Judges 2 in the BBPNG
Judges 2 in the BBT1E
Judges 2 in the BDS
Judges 2 in the BEV
Judges 2 in the BHAD
Judges 2 in the BIB
Judges 2 in the BLPT
Judges 2 in the BNT
Judges 2 in the BNTABOOT
Judges 2 in the BNTLV
Judges 2 in the BOATCB
Judges 2 in the BOATCB2
Judges 2 in the BOBCV
Judges 2 in the BOCNT
Judges 2 in the BOECS
Judges 2 in the BOGWICC
Judges 2 in the BOHCB
Judges 2 in the BOHCV
Judges 2 in the BOHLNT
Judges 2 in the BOHNTLTAL
Judges 2 in the BOICB
Judges 2 in the BOILNTAP
Judges 2 in the BOITCV
Judges 2 in the BOKCV2
Judges 2 in the BOKHWOG
Judges 2 in the BOKSSV
Judges 2 in the BOLCB
Judges 2 in the BOLCB2
Judges 2 in the BOMCV
Judges 2 in the BONAV
Judges 2 in the BONCB
Judges 2 in the BONLT
Judges 2 in the BONUT2
Judges 2 in the BOPLNT
Judges 2 in the BOSCB
Judges 2 in the BOSNC
Judges 2 in the BOTLNT
Judges 2 in the BOVCB
Judges 2 in the BOYCB
Judges 2 in the BPBB
Judges 2 in the BPH
Judges 2 in the BSB
Judges 2 in the CCB
Judges 2 in the CUV
Judges 2 in the CUVS
Judges 2 in the DBT
Judges 2 in the DGDNT
Judges 2 in the DHNT
Judges 2 in the DNT
Judges 2 in the ELBE
Judges 2 in the EMTV
Judges 2 in the ESV
Judges 2 in the FBV
Judges 2 in the FEB
Judges 2 in the GGMNT
Judges 2 in the GNT
Judges 2 in the HARY
Judges 2 in the HNT
Judges 2 in the IRVA
Judges 2 in the IRVB
Judges 2 in the IRVG
Judges 2 in the IRVH
Judges 2 in the IRVK
Judges 2 in the IRVM
Judges 2 in the IRVM2
Judges 2 in the IRVO
Judges 2 in the IRVP
Judges 2 in the IRVT
Judges 2 in the IRVT2
Judges 2 in the IRVU
Judges 2 in the ISVN
Judges 2 in the JSNT
Judges 2 in the KAPI
Judges 2 in the KBT1ETNIK
Judges 2 in the KBV
Judges 2 in the KJV
Judges 2 in the KNFD
Judges 2 in the LBA
Judges 2 in the LBLA
Judges 2 in the LNT
Judges 2 in the LSV
Judges 2 in the MAAL
Judges 2 in the MBV
Judges 2 in the MBV2
Judges 2 in the MHNT
Judges 2 in the MKNFD
Judges 2 in the MNG
Judges 2 in the MNT
Judges 2 in the MNT2
Judges 2 in the MRS1T
Judges 2 in the NAA
Judges 2 in the NASB
Judges 2 in the NBLA
Judges 2 in the NBS
Judges 2 in the NBVTP
Judges 2 in the NET2
Judges 2 in the NIV11
Judges 2 in the NNT
Judges 2 in the NNT2
Judges 2 in the NNT3
Judges 2 in the PDDPT
Judges 2 in the PFNT
Judges 2 in the RMNT
Judges 2 in the SBIAS
Judges 2 in the SBIBS
Judges 2 in the SBIBS2
Judges 2 in the SBICS
Judges 2 in the SBIDS
Judges 2 in the SBIGS
Judges 2 in the SBIHS
Judges 2 in the SBIIS
Judges 2 in the SBIIS2
Judges 2 in the SBIIS3
Judges 2 in the SBIKS
Judges 2 in the SBIKS2
Judges 2 in the SBIMS
Judges 2 in the SBIOS
Judges 2 in the SBIPS
Judges 2 in the SBISS
Judges 2 in the SBITS
Judges 2 in the SBITS2
Judges 2 in the SBITS3
Judges 2 in the SBITS4
Judges 2 in the SBIUS
Judges 2 in the SBIVS
Judges 2 in the SBT
Judges 2 in the SBT1E
Judges 2 in the SCHL
Judges 2 in the SNT
Judges 2 in the SUSU
Judges 2 in the SUSU2
Judges 2 in the SYNO
Judges 2 in the TBIAOTANT
Judges 2 in the TBT1E
Judges 2 in the TBT1E2
Judges 2 in the TFTIP
Judges 2 in the TFTU
Judges 2 in the TGNTATF3T
Judges 2 in the THAI
Judges 2 in the TNFD
Judges 2 in the TNT
Judges 2 in the TNTIK
Judges 2 in the TNTIL
Judges 2 in the TNTIN
Judges 2 in the TNTIP
Judges 2 in the TNTIZ
Judges 2 in the TOMA
Judges 2 in the TTENT
Judges 2 in the UBG
Judges 2 in the UGV
Judges 2 in the UGV2
Judges 2 in the UGV3
Judges 2 in the VBL
Judges 2 in the VDCC
Judges 2 in the YALU
Judges 2 in the YAPE
Judges 2 in the YBVTP
Judges 2 in the ZBP