Jeremiah 14 (BOKCV)
1 Hili ndilo neno la BWANA kwa Yeremia kuhusu ukame: 2 “Yuda anaomboleza,miji yake inayodhoofika;wanaomboleza kwa ajili ya nchi,nacho kilio kinapanda kutoka Yerusalemu. 3 Wakuu wanawatuma watumishi wao maji;wanakwenda visimanilakini humo hakuna maji.Wanarudi na vyombo bila maji;wakiwa na hofu na kukata tamaa,wanafunika vichwa vyao. 4 Ardhi imepasuka nyufakwa sababu hakuna mvua katika nchi;wakulima wana hofuna wanafunika vichwa vyao. 5 Hata kulungu mashambanianamwacha mtoto wake aliyezaliwa wakati huo huokwa sababu hakuna majani. 6 Punda-mwitu wanasimama juu ya miinuko iliyo kamena kutweta kama mbweha;macho yao yanakosa nguvu za kuonakwa ajili ya kukosa malisho.” 7 Ingawa dhambi zetu zinashuhudia juu yetu,Ee BWANA, tenda jambo kwa ajili ya jina lako.Kwa kuwa kukengeuka kwetu ni kukubwa,nasi tumetenda dhambi dhidi yako. 8 Ee Tumaini la Israeli,Mwokozi wake wakati wa taabu,kwa nini unakuwa kama mgeni katika nchi,kama msafiri anayekaa kwa usiku mmoja tu? 9 Mbona unakuwa kama mtu aliyeshtukizwa,kama shujaa asiye na uwezo wa kuokoa?Wewe uko katikati yetu, Ee BWANA,nasi tunaitwa kwa jina lako;usituache! 10 Hili ndilo BWANA asemalo kuhusu watu hawa:“Wanapenda sana kutangatanga,hawaizuii miguu yao.Hivyo BWANA hawakubali;sasa ataukumbuka uovu waona kuwaadhibu kwa ajili ya dhambi zao.” 11 Kisha BWANA akaniambia, “Usiombe kwa ajili ya mafanikio ya watu hawa. 12 Ingawa wanafunga, sitasikiliza kilio chao; hata wakitoa dhabihu za kuteketezwa na dhabihu za nafaka, sitazikubali. Badala yake, nitawaangamiza kwa upanga, njaa na tauni.” 13 Lakini nikasema, “Aa, BWANA Mwenyezi, manabii wanaendelea kuwaambia, ‘Hamtaona upanga wala kukabiliwa na njaa. Naam, nitawapa amani ya kudumu mahali hapa.’ ” 14 Ndipo BWANA akaniambia, “Manabii wanatabiri uongo kwa jina langu. Sikuwatuma, wala sikuwaweka, wala sikusema nao. Wanawatabiria maono ya uongo, maaguzi, maono ya sanamu zisizofaa kitu, na madanganyo ya mawazo yao wenyewe. 15 Kwa hiyo, hili ndilo BWANA asemalo kuhusu manabii wanaotabiri kwa jina langu: Mimi sikuwatuma, lakini wanasema, ‘Hakuna upanga wala njaa itakayoigusa nchi hii.’ Manabii hao hao watakufa kwa upanga na njaa. 16 Nao watu hao wanaowatabiria watatupwa nje katika barabara za Yerusalemu kwa sababu ya njaa na upanga. Hapatakuwepo yeyote wa kuwazika wao au wake zao, wana wao au binti zao. Nitawamwagia maafa wanayostahili. 17 “Nena nao neno hili:“ ‘Macho yangu na yatiririkwe na machoziusiku na mchana bila kukoma;kwa kuwa binti yangu aliye bikira, yaani watu wangu,amepata jeraha baya,pigo la kuangamiza. 18 Kama nikienda mashambani,ninaona wale waliouawa kwa upanga;kama nikienda mjini,ninaona maangamizi ya njaa.Nabii na kuhani kwa pamojawamekwenda katika nchi wasiyoijua.’ ” 19 Je, umemkataa Yuda kabisa?Umemchukia Sayuni kabisa?Kwa nini umetuumizahata hatuwezi kuponyeka?Tulitarajia amani,lakini hakuna jema lililotujia;tulitarajia wakati wa kuponalakini kuna hofu kuu tu. 20 Ee BWANA, tunatambua uovu wetuna kosa la baba zetu;kweli tumetenda dhambi dhidi yako. 21 Kwa ajili ya jina lako usituchukie kabisa;usikidharau kiti chako cha enzi kilichotukuka.Kumbuka agano lako nasina usilivunje. 22 Je, kuna sanamu yoyote isiyofaa kitu ya mataifaiwezayo kuleta mvua?Je, anga peke yake zaweza kutoa mvua?La hasha, ni wewe peke yako,Ee BWANA, Mungu wetu.Kwa hiyo tumaini letu liko kwako,kwa kuwa wewe ndiwe ufanyaye haya yote.
In Other Versions
Jeremiah 14 in the ANGEFD
Jeremiah 14 in the ANTPNG2D
Jeremiah 14 in the AS21
Jeremiah 14 in the BAGH
Jeremiah 14 in the BBPNG
Jeremiah 14 in the BBT1E
Jeremiah 14 in the BDS
Jeremiah 14 in the BEV
Jeremiah 14 in the BHAD
Jeremiah 14 in the BIB
Jeremiah 14 in the BLPT
Jeremiah 14 in the BNT
Jeremiah 14 in the BNTABOOT
Jeremiah 14 in the BNTLV
Jeremiah 14 in the BOATCB
Jeremiah 14 in the BOATCB2
Jeremiah 14 in the BOBCV
Jeremiah 14 in the BOCNT
Jeremiah 14 in the BOECS
Jeremiah 14 in the BOGWICC
Jeremiah 14 in the BOHCB
Jeremiah 14 in the BOHCV
Jeremiah 14 in the BOHLNT
Jeremiah 14 in the BOHNTLTAL
Jeremiah 14 in the BOICB
Jeremiah 14 in the BOILNTAP
Jeremiah 14 in the BOITCV
Jeremiah 14 in the BOKCV2
Jeremiah 14 in the BOKHWOG
Jeremiah 14 in the BOKSSV
Jeremiah 14 in the BOLCB
Jeremiah 14 in the BOLCB2
Jeremiah 14 in the BOMCV
Jeremiah 14 in the BONAV
Jeremiah 14 in the BONCB
Jeremiah 14 in the BONLT
Jeremiah 14 in the BONUT2
Jeremiah 14 in the BOPLNT
Jeremiah 14 in the BOSCB
Jeremiah 14 in the BOSNC
Jeremiah 14 in the BOTLNT
Jeremiah 14 in the BOVCB
Jeremiah 14 in the BOYCB
Jeremiah 14 in the BPBB
Jeremiah 14 in the BPH
Jeremiah 14 in the BSB
Jeremiah 14 in the CCB
Jeremiah 14 in the CUV
Jeremiah 14 in the CUVS
Jeremiah 14 in the DBT
Jeremiah 14 in the DGDNT
Jeremiah 14 in the DHNT
Jeremiah 14 in the DNT
Jeremiah 14 in the ELBE
Jeremiah 14 in the EMTV
Jeremiah 14 in the ESV
Jeremiah 14 in the FBV
Jeremiah 14 in the FEB
Jeremiah 14 in the GGMNT
Jeremiah 14 in the GNT
Jeremiah 14 in the HARY
Jeremiah 14 in the HNT
Jeremiah 14 in the IRVA
Jeremiah 14 in the IRVB
Jeremiah 14 in the IRVG
Jeremiah 14 in the IRVH
Jeremiah 14 in the IRVK
Jeremiah 14 in the IRVM
Jeremiah 14 in the IRVM2
Jeremiah 14 in the IRVO
Jeremiah 14 in the IRVP
Jeremiah 14 in the IRVT
Jeremiah 14 in the IRVT2
Jeremiah 14 in the IRVU
Jeremiah 14 in the ISVN
Jeremiah 14 in the JSNT
Jeremiah 14 in the KAPI
Jeremiah 14 in the KBT1ETNIK
Jeremiah 14 in the KBV
Jeremiah 14 in the KJV
Jeremiah 14 in the KNFD
Jeremiah 14 in the LBA
Jeremiah 14 in the LBLA
Jeremiah 14 in the LNT
Jeremiah 14 in the LSV
Jeremiah 14 in the MAAL
Jeremiah 14 in the MBV
Jeremiah 14 in the MBV2
Jeremiah 14 in the MHNT
Jeremiah 14 in the MKNFD
Jeremiah 14 in the MNG
Jeremiah 14 in the MNT
Jeremiah 14 in the MNT2
Jeremiah 14 in the MRS1T
Jeremiah 14 in the NAA
Jeremiah 14 in the NASB
Jeremiah 14 in the NBLA
Jeremiah 14 in the NBS
Jeremiah 14 in the NBVTP
Jeremiah 14 in the NET2
Jeremiah 14 in the NIV11
Jeremiah 14 in the NNT
Jeremiah 14 in the NNT2
Jeremiah 14 in the NNT3
Jeremiah 14 in the PDDPT
Jeremiah 14 in the PFNT
Jeremiah 14 in the RMNT
Jeremiah 14 in the SBIAS
Jeremiah 14 in the SBIBS
Jeremiah 14 in the SBIBS2
Jeremiah 14 in the SBICS
Jeremiah 14 in the SBIDS
Jeremiah 14 in the SBIGS
Jeremiah 14 in the SBIHS
Jeremiah 14 in the SBIIS
Jeremiah 14 in the SBIIS2
Jeremiah 14 in the SBIIS3
Jeremiah 14 in the SBIKS
Jeremiah 14 in the SBIKS2
Jeremiah 14 in the SBIMS
Jeremiah 14 in the SBIOS
Jeremiah 14 in the SBIPS
Jeremiah 14 in the SBISS
Jeremiah 14 in the SBITS
Jeremiah 14 in the SBITS2
Jeremiah 14 in the SBITS3
Jeremiah 14 in the SBITS4
Jeremiah 14 in the SBIUS
Jeremiah 14 in the SBIVS
Jeremiah 14 in the SBT
Jeremiah 14 in the SBT1E
Jeremiah 14 in the SCHL
Jeremiah 14 in the SNT
Jeremiah 14 in the SUSU
Jeremiah 14 in the SUSU2
Jeremiah 14 in the SYNO
Jeremiah 14 in the TBIAOTANT
Jeremiah 14 in the TBT1E
Jeremiah 14 in the TBT1E2
Jeremiah 14 in the TFTIP
Jeremiah 14 in the TFTU
Jeremiah 14 in the TGNTATF3T
Jeremiah 14 in the THAI
Jeremiah 14 in the TNFD
Jeremiah 14 in the TNT
Jeremiah 14 in the TNTIK
Jeremiah 14 in the TNTIL
Jeremiah 14 in the TNTIN
Jeremiah 14 in the TNTIP
Jeremiah 14 in the TNTIZ
Jeremiah 14 in the TOMA
Jeremiah 14 in the TTENT
Jeremiah 14 in the UBG
Jeremiah 14 in the UGV
Jeremiah 14 in the UGV2
Jeremiah 14 in the UGV3
Jeremiah 14 in the VBL
Jeremiah 14 in the VDCC
Jeremiah 14 in the YALU
Jeremiah 14 in the YAPE
Jeremiah 14 in the YBVTP
Jeremiah 14 in the ZBP