Jeremiah 16 (BOKCV)
1 Kisha neno la BWANA likanijia: 2 “Kamwe usioe na kuwa na wana wala binti mahali hapa.” 3 Kwa maana hili ndilo asemalo BWANA kuhusu wana na binti wazaliwao katika nchi hii, na kuhusu wale wanawake ambao ni mama zao, na wale wanaume ambao ni baba zao: 4 “Watakufa kwa magonjwa ya kufisha. Hawataombolezewa wala kuzikwa, lakini watakuwa kama mavi yaliyosambaa juu ya ardhi. Watakufa kwa upanga na kwa njaa, nazo maiti zao zitakuwa chakula cha ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi.” 5 Kwa kuwa hili ndilo asemalo BWANA: “Usiingie katika nyumba ambayo kuna chakula cha matanga, usiende kuwaombolezea wala kuwahurumia, kwa sababu nimeziondoa baraka zangu, upendo wangu na huruma zangu kutoka kwa watu hawa,” asema BWANA. 6 “Wakubwa na wadogo watakufa katika nchi hii. Hawatazikwa wala kuombolezewa, na hakuna atakayejikatakata au kunyoa nywele za kichwa chake kwa ajili yao. 7 Hakuna yeyote atakayewapa chakula ili kuwafariji wale waombolezao kwa ajili ya wale waliokufa, hata akiwa amefiwa na baba au mama, wala hakuna yeyote atakayewapa kinywaji ili kuwafariji. 8 “Usiingie katika nyumba ambayo kuna karamu, na kuketi humo ili kula na kunywa. 9 Kwa kuwa hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote, aliye Mungu wa Israeli: ‘Mbele ya macho yako na katika siku zako, nitakomesha sauti zote za shangwe na za furaha, na pia sauti za bibi arusi na bwana arusi mahali hapa.’ 10 “Utakapowaambia watu hawa mambo haya yote na wakakuuliza, ‘Kwa nini BWANA ameamuru maafa makubwa kama haya dhidi yetu? Tumefanya kosa gani? Tumetenda dhambi gani dhidi ya BWANA, Mungu wetu?’ 11 Basi waambie, ‘Ni kwa sababu baba zenu waliniacha mimi, wakafuata miungu mingine ili kuitumikia na kuiabudu. Waliniacha mimi na hawakuishika sheria yangu,’ asema BWANA. 12 ‘Lakini ninyi mmetenda uovu zaidi kuliko baba zenu. Tazama jinsi ambavyo kila mmoja wenu anafuata ukaidi wa moyo wake mbaya, badala ya kunitii mimi. 13 Kwa hiyo nitawaondoa katika nchi hii na kuwatupa katika nchi ambayo ninyi wala baba zenu hamkuijua, nako huko mtaitumikia miungu mingine usiku na mchana, kwa maana sitawapa fadhili zangu huko.’ 14 “Hata hivyo, siku zinakuja,” asema BWANA, “wakati ambapo watu hawatasema tena, ‘Hakika kama BWANA aishivyo, aliyewapandisha Waisraeli kutoka Misri,’ 15 bali watasema, ‘Hakika kama BWANA aishivyo, aliyewatoa wana wa Israeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote alizokuwa amewafukuzia.’ Maana nitawarudisha katika nchi niliyowapa baba zao. 16 “Lakini sasa nitawaagiza wavuvi wengi,” asema BWANA, “nao watawavua. Baada ya hilo, nitawaagizia wawindaji wengi, nao watawawinda kwenye kila mlima na kilima, na katika nyufa za miamba. 17 Macho yangu yanaziona njia zao zote, hazikufichika kwangu, wala dhambi yao haikusitirika. 18 Nitawalipiza maradufu kwa ajili ya uovu wao na dhambi yao, kwa sababu wameinajisi nchi yangu kwa maumbo yasiyo na uhai ya vinyago vyao vibaya, na kuujaza urithi wangu na sanamu za kuchukiza.” 19 Ee BWANA, nguvu zangu na ngome yangu,kimbilio langu wakati wa taabu,kwako mataifa yatakujiakutoka miisho ya dunia na kusema,“Baba zetu hawakuwa na chochote zaidi ya miungu ya uongo,sanamu zisizofaa kituambazo hazikuwafaidia lolote. 20 Je, watu hujitengenezea miungu yao wenyewe?Naam, lakini hao si miungu!” 21 “Kwa hiyo nitawafundisha:wakati huu nitawafundishanguvu zangu na uwezo wangu.Ndipo watakapojuakuwa Jina langu ndimi BWANA.
In Other Versions
Jeremiah 16 in the ANGEFD
Jeremiah 16 in the ANTPNG2D
Jeremiah 16 in the AS21
Jeremiah 16 in the BAGH
Jeremiah 16 in the BBPNG
Jeremiah 16 in the BBT1E
Jeremiah 16 in the BDS
Jeremiah 16 in the BEV
Jeremiah 16 in the BHAD
Jeremiah 16 in the BIB
Jeremiah 16 in the BLPT
Jeremiah 16 in the BNT
Jeremiah 16 in the BNTABOOT
Jeremiah 16 in the BNTLV
Jeremiah 16 in the BOATCB
Jeremiah 16 in the BOATCB2
Jeremiah 16 in the BOBCV
Jeremiah 16 in the BOCNT
Jeremiah 16 in the BOECS
Jeremiah 16 in the BOGWICC
Jeremiah 16 in the BOHCB
Jeremiah 16 in the BOHCV
Jeremiah 16 in the BOHLNT
Jeremiah 16 in the BOHNTLTAL
Jeremiah 16 in the BOICB
Jeremiah 16 in the BOILNTAP
Jeremiah 16 in the BOITCV
Jeremiah 16 in the BOKCV2
Jeremiah 16 in the BOKHWOG
Jeremiah 16 in the BOKSSV
Jeremiah 16 in the BOLCB
Jeremiah 16 in the BOLCB2
Jeremiah 16 in the BOMCV
Jeremiah 16 in the BONAV
Jeremiah 16 in the BONCB
Jeremiah 16 in the BONLT
Jeremiah 16 in the BONUT2
Jeremiah 16 in the BOPLNT
Jeremiah 16 in the BOSCB
Jeremiah 16 in the BOSNC
Jeremiah 16 in the BOTLNT
Jeremiah 16 in the BOVCB
Jeremiah 16 in the BOYCB
Jeremiah 16 in the BPBB
Jeremiah 16 in the BPH
Jeremiah 16 in the BSB
Jeremiah 16 in the CCB
Jeremiah 16 in the CUV
Jeremiah 16 in the CUVS
Jeremiah 16 in the DBT
Jeremiah 16 in the DGDNT
Jeremiah 16 in the DHNT
Jeremiah 16 in the DNT
Jeremiah 16 in the ELBE
Jeremiah 16 in the EMTV
Jeremiah 16 in the ESV
Jeremiah 16 in the FBV
Jeremiah 16 in the FEB
Jeremiah 16 in the GGMNT
Jeremiah 16 in the GNT
Jeremiah 16 in the HARY
Jeremiah 16 in the HNT
Jeremiah 16 in the IRVA
Jeremiah 16 in the IRVB
Jeremiah 16 in the IRVG
Jeremiah 16 in the IRVH
Jeremiah 16 in the IRVK
Jeremiah 16 in the IRVM
Jeremiah 16 in the IRVM2
Jeremiah 16 in the IRVO
Jeremiah 16 in the IRVP
Jeremiah 16 in the IRVT
Jeremiah 16 in the IRVT2
Jeremiah 16 in the IRVU
Jeremiah 16 in the ISVN
Jeremiah 16 in the JSNT
Jeremiah 16 in the KAPI
Jeremiah 16 in the KBT1ETNIK
Jeremiah 16 in the KBV
Jeremiah 16 in the KJV
Jeremiah 16 in the KNFD
Jeremiah 16 in the LBA
Jeremiah 16 in the LBLA
Jeremiah 16 in the LNT
Jeremiah 16 in the LSV
Jeremiah 16 in the MAAL
Jeremiah 16 in the MBV
Jeremiah 16 in the MBV2
Jeremiah 16 in the MHNT
Jeremiah 16 in the MKNFD
Jeremiah 16 in the MNG
Jeremiah 16 in the MNT
Jeremiah 16 in the MNT2
Jeremiah 16 in the MRS1T
Jeremiah 16 in the NAA
Jeremiah 16 in the NASB
Jeremiah 16 in the NBLA
Jeremiah 16 in the NBS
Jeremiah 16 in the NBVTP
Jeremiah 16 in the NET2
Jeremiah 16 in the NIV11
Jeremiah 16 in the NNT
Jeremiah 16 in the NNT2
Jeremiah 16 in the NNT3
Jeremiah 16 in the PDDPT
Jeremiah 16 in the PFNT
Jeremiah 16 in the RMNT
Jeremiah 16 in the SBIAS
Jeremiah 16 in the SBIBS
Jeremiah 16 in the SBIBS2
Jeremiah 16 in the SBICS
Jeremiah 16 in the SBIDS
Jeremiah 16 in the SBIGS
Jeremiah 16 in the SBIHS
Jeremiah 16 in the SBIIS
Jeremiah 16 in the SBIIS2
Jeremiah 16 in the SBIIS3
Jeremiah 16 in the SBIKS
Jeremiah 16 in the SBIKS2
Jeremiah 16 in the SBIMS
Jeremiah 16 in the SBIOS
Jeremiah 16 in the SBIPS
Jeremiah 16 in the SBISS
Jeremiah 16 in the SBITS
Jeremiah 16 in the SBITS2
Jeremiah 16 in the SBITS3
Jeremiah 16 in the SBITS4
Jeremiah 16 in the SBIUS
Jeremiah 16 in the SBIVS
Jeremiah 16 in the SBT
Jeremiah 16 in the SBT1E
Jeremiah 16 in the SCHL
Jeremiah 16 in the SNT
Jeremiah 16 in the SUSU
Jeremiah 16 in the SUSU2
Jeremiah 16 in the SYNO
Jeremiah 16 in the TBIAOTANT
Jeremiah 16 in the TBT1E
Jeremiah 16 in the TBT1E2
Jeremiah 16 in the TFTIP
Jeremiah 16 in the TFTU
Jeremiah 16 in the TGNTATF3T
Jeremiah 16 in the THAI
Jeremiah 16 in the TNFD
Jeremiah 16 in the TNT
Jeremiah 16 in the TNTIK
Jeremiah 16 in the TNTIL
Jeremiah 16 in the TNTIN
Jeremiah 16 in the TNTIP
Jeremiah 16 in the TNTIZ
Jeremiah 16 in the TOMA
Jeremiah 16 in the TTENT
Jeremiah 16 in the UBG
Jeremiah 16 in the UGV
Jeremiah 16 in the UGV2
Jeremiah 16 in the UGV3
Jeremiah 16 in the VBL
Jeremiah 16 in the VDCC
Jeremiah 16 in the YALU
Jeremiah 16 in the YAPE
Jeremiah 16 in the YBVTP
Jeremiah 16 in the ZBP