Jeremiah 33 (BOKCV)

1 Wakati Yeremia alipokuwa angali amefungwa kwenye ua wa walinzi, neno la BWANA lilimjia mara ya pili kusema: 2 “Hili ndilo BWANA asemalo, yeye aliyeumba dunia, BWANA aliyeifanya na kuithibitisha, BWANA ndilo jina lake: 3 ‘Niite nami nitakuitika na kukuambia mambo makuu na yasiyochunguzika, usiyoyajua.’ 4 Kwa maana hili ndilo BWANA, Mungu wa Israeli, asemalo kuhusu nyumba katika mji huu na majumba ya kifalme ya Yuda yaliyobomolewa ili yatumiwe dhidi ya kule kuzungukwa na jeshi na upanga 5 katika kupigana na Wakaldayo: ‘Zitajazwa na maiti za watu nitakaowachinja katika hasira na ghadhabu yangu. Nitauficha uso wangu kwa sababu ya maovu yake yote. 6 “ ‘Hata hivyo, nitauletea afya na uponyaji, nitawaponya watu wangu na kuwafanya wafurahie amani tele na salama. 7 Nitawarudisha Yuda na Israeli kutoka nchi ya kutekwa kwao, na kuwajenga tena kama walivyokuwa hapo awali. 8 Nitawatakasa dhambi zote walizofanya dhidi yangu, na nitawasamehe dhambi zote za uasi dhidi yangu. 9 Kisha mji huu utaniletea utukufu, furaha, sifa na heshima mbele ya mataifa yote ya dunia yatakayosikia mambo yote mazuri ninayoufanyia. Nao watashangaa na kutetemeka kwa ajili ya wingi wa mafanikio na amani nitakayoupatia.’ 10 “Hili ndilo asemalo BWANA: ‘Mnasema kuhusu mahali hapa kwamba, “Ni mahali palipoachwa ukiwa, pasipo na wanadamu wala wanyama.” Lakini katika miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu ambazo zimeachwa, ambazo hazikaliwi na wanadamu wala wanyama, huko kutasikika kwa mara nyingine 11 sauti za shangwe na furaha, sauti za bibi na bwana arusi, na sauti za wale waletao sadaka za shukrani katika nyumba ya BWANA, wakisema,“ ‘ “Mshukuruni BWANA Mwenye Nguvu Zote,kwa maana BWANA ni mwema;upendo wake wadumu milele.”Kwa kuwa nitairudishia nchi baraka kama zilivyokuwa hapo awali,’ asema BWANA. 12 “Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: ‘Mahali hapa, ambapo ni ukiwa, pasipo na wanadamu wala wanyama: katika miji yake, patakuwepo tena malisho kwa ajili ya wachungaji kupumzisha makundi yao ya kondoo. 13 Katika miji ya nchi ya vilima, ya vilima vya magharibi na ya Negebu, katika nchi ya Benyamini, katika vijiji vinavyoizunguka Yerusalemu na katika miji ya Yuda, makundi ya kondoo yatapita tena chini ya mkono wa yeye ayahesabuye,’ asema BWANA. 14 “ ‘Siku zinakuja,’ asema BWANA, ‘wakati nitakapotimiza ahadi yangu ya rehema niliyoifanya kwa nyumba ya Israeli na kwa nyumba ya Yuda. 15 “ ‘Katika siku hizo na wakati huonitalifanya Tawi la haki lichipuke kutoka ukoo wa Daudi,naye atafanya lile lililo haki na sawakatika nchi. 16 Katika siku hizo, Yuda ataokolewana Yerusalemu ataishi salama.Hili ndilo jina atakaloitwa: BWANA Haki Yetu.’ 17 Kwa maana hili ndilo asemalo BWANA: ‘Daudi kamwe hatakosa mtu wa kukalia kiti cha enzi cha nyumba ya Israeli, 18 wala hata makuhani, ambao ni Walawi, kamwe hawatakosa mtu wa kusimama mbele zangu daima ili kutoa sadaka za kuteketezwa, ili kuteketeza sadaka ya nafaka na kutoa dhabihu.’ ” 19 Neno la BWANA likamjia Yeremia kusema: 20 “Hili ndilo asemalo BWANA: ‘Ikiwa mtaweza kuvunja agano langu kuhusu usiku na mchana, ili usiku na mchana visiwepo kwa nyakati zake, 21 basi agano langu na Daudi mtumishi wangu, na agano langu na Walawi ambao ni makuhani wanaohudumu mbele zangu, linaweza kuvunjwa, na Daudi hatakuwa tena na mzao wa kutawala katika kiti chake cha enzi. 22 Nitawafanya wazao wa Daudi mtumishi wangu na Walawi wanaohudumu mbele zangu wengi, wasioweza kuhesabika kama nyota za angani, tena wasiopimika kama mchanga wa ufuoni mwa bahari.’ ” 23 Neno la BWANA likamjia Yeremia kusema: 24 “Je, hujasikia kwamba watu hawa wanasema, ‘BWANA amezikataa zile falme mbili alizozichagua?’ Kwa hiyo wamewadharau watu wangu, na hawawaoni tena kama taifa. 25 Hili ndilo asemalo BWANA: ‘Kama sijathibitisha agano langu na usiku na mchana, na kuziweka wakfu sheria za mbingu na nchi, 26 basi nitawakataa wazao wa Yakobo na Daudi mtumishi wangu, na sitachagua mmoja wa wanawe kutawala juu ya wazao wa Abrahamu, Isaki na Yakobo. Kwa maana nitawarudisha kutoka nchi ya kutekwa kwao na kuwaonea huruma.’ ”

In Other Versions

Jeremiah 33 in the ANGEFD

Jeremiah 33 in the ANTPNG2D

Jeremiah 33 in the AS21

Jeremiah 33 in the BAGH

Jeremiah 33 in the BBPNG

Jeremiah 33 in the BBT1E

Jeremiah 33 in the BDS

Jeremiah 33 in the BEV

Jeremiah 33 in the BHAD

Jeremiah 33 in the BIB

Jeremiah 33 in the BLPT

Jeremiah 33 in the BNT

Jeremiah 33 in the BNTABOOT

Jeremiah 33 in the BNTLV

Jeremiah 33 in the BOATCB

Jeremiah 33 in the BOATCB2

Jeremiah 33 in the BOBCV

Jeremiah 33 in the BOCNT

Jeremiah 33 in the BOECS

Jeremiah 33 in the BOGWICC

Jeremiah 33 in the BOHCB

Jeremiah 33 in the BOHCV

Jeremiah 33 in the BOHLNT

Jeremiah 33 in the BOHNTLTAL

Jeremiah 33 in the BOICB

Jeremiah 33 in the BOILNTAP

Jeremiah 33 in the BOITCV

Jeremiah 33 in the BOKCV2

Jeremiah 33 in the BOKHWOG

Jeremiah 33 in the BOKSSV

Jeremiah 33 in the BOLCB

Jeremiah 33 in the BOLCB2

Jeremiah 33 in the BOMCV

Jeremiah 33 in the BONAV

Jeremiah 33 in the BONCB

Jeremiah 33 in the BONLT

Jeremiah 33 in the BONUT2

Jeremiah 33 in the BOPLNT

Jeremiah 33 in the BOSCB

Jeremiah 33 in the BOSNC

Jeremiah 33 in the BOTLNT

Jeremiah 33 in the BOVCB

Jeremiah 33 in the BOYCB

Jeremiah 33 in the BPBB

Jeremiah 33 in the BPH

Jeremiah 33 in the BSB

Jeremiah 33 in the CCB

Jeremiah 33 in the CUV

Jeremiah 33 in the CUVS

Jeremiah 33 in the DBT

Jeremiah 33 in the DGDNT

Jeremiah 33 in the DHNT

Jeremiah 33 in the DNT

Jeremiah 33 in the ELBE

Jeremiah 33 in the EMTV

Jeremiah 33 in the ESV

Jeremiah 33 in the FBV

Jeremiah 33 in the FEB

Jeremiah 33 in the GGMNT

Jeremiah 33 in the GNT

Jeremiah 33 in the HARY

Jeremiah 33 in the HNT

Jeremiah 33 in the IRVA

Jeremiah 33 in the IRVB

Jeremiah 33 in the IRVG

Jeremiah 33 in the IRVH

Jeremiah 33 in the IRVK

Jeremiah 33 in the IRVM

Jeremiah 33 in the IRVM2

Jeremiah 33 in the IRVO

Jeremiah 33 in the IRVP

Jeremiah 33 in the IRVT

Jeremiah 33 in the IRVT2

Jeremiah 33 in the IRVU

Jeremiah 33 in the ISVN

Jeremiah 33 in the JSNT

Jeremiah 33 in the KAPI

Jeremiah 33 in the KBT1ETNIK

Jeremiah 33 in the KBV

Jeremiah 33 in the KJV

Jeremiah 33 in the KNFD

Jeremiah 33 in the LBA

Jeremiah 33 in the LBLA

Jeremiah 33 in the LNT

Jeremiah 33 in the LSV

Jeremiah 33 in the MAAL

Jeremiah 33 in the MBV

Jeremiah 33 in the MBV2

Jeremiah 33 in the MHNT

Jeremiah 33 in the MKNFD

Jeremiah 33 in the MNG

Jeremiah 33 in the MNT

Jeremiah 33 in the MNT2

Jeremiah 33 in the MRS1T

Jeremiah 33 in the NAA

Jeremiah 33 in the NASB

Jeremiah 33 in the NBLA

Jeremiah 33 in the NBS

Jeremiah 33 in the NBVTP

Jeremiah 33 in the NET2

Jeremiah 33 in the NIV11

Jeremiah 33 in the NNT

Jeremiah 33 in the NNT2

Jeremiah 33 in the NNT3

Jeremiah 33 in the PDDPT

Jeremiah 33 in the PFNT

Jeremiah 33 in the RMNT

Jeremiah 33 in the SBIAS

Jeremiah 33 in the SBIBS

Jeremiah 33 in the SBIBS2

Jeremiah 33 in the SBICS

Jeremiah 33 in the SBIDS

Jeremiah 33 in the SBIGS

Jeremiah 33 in the SBIHS

Jeremiah 33 in the SBIIS

Jeremiah 33 in the SBIIS2

Jeremiah 33 in the SBIIS3

Jeremiah 33 in the SBIKS

Jeremiah 33 in the SBIKS2

Jeremiah 33 in the SBIMS

Jeremiah 33 in the SBIOS

Jeremiah 33 in the SBIPS

Jeremiah 33 in the SBISS

Jeremiah 33 in the SBITS

Jeremiah 33 in the SBITS2

Jeremiah 33 in the SBITS3

Jeremiah 33 in the SBITS4

Jeremiah 33 in the SBIUS

Jeremiah 33 in the SBIVS

Jeremiah 33 in the SBT

Jeremiah 33 in the SBT1E

Jeremiah 33 in the SCHL

Jeremiah 33 in the SNT

Jeremiah 33 in the SUSU

Jeremiah 33 in the SUSU2

Jeremiah 33 in the SYNO

Jeremiah 33 in the TBIAOTANT

Jeremiah 33 in the TBT1E

Jeremiah 33 in the TBT1E2

Jeremiah 33 in the TFTIP

Jeremiah 33 in the TFTU

Jeremiah 33 in the TGNTATF3T

Jeremiah 33 in the THAI

Jeremiah 33 in the TNFD

Jeremiah 33 in the TNT

Jeremiah 33 in the TNTIK

Jeremiah 33 in the TNTIL

Jeremiah 33 in the TNTIN

Jeremiah 33 in the TNTIP

Jeremiah 33 in the TNTIZ

Jeremiah 33 in the TOMA

Jeremiah 33 in the TTENT

Jeremiah 33 in the UBG

Jeremiah 33 in the UGV

Jeremiah 33 in the UGV2

Jeremiah 33 in the UGV3

Jeremiah 33 in the VBL

Jeremiah 33 in the VDCC

Jeremiah 33 in the YALU

Jeremiah 33 in the YAPE

Jeremiah 33 in the YBVTP

Jeremiah 33 in the ZBP