Jeremiah 35 (BOKCV)
1 Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa BWANA, wakati wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda: 2 “Nenda kwa jamaa ya Warekabi, uwaalike waje kwenye moja ya vyumba vya pembeni vya nyumba ya BWANA, na uwape divai wanywe.” 3 Basi nikaenda kumwita Yaazania mwana wa Yeremia, mwana wa Habazinia, na ndugu zake na wanawe wote, yaani jamaa nzima ya Warekabi. 4 Nikawaleta katika nyumba ya BWANA, ndani ya chumba cha wana wa Hanani mwana wa Igdalia mtu wa Mungu. Kilikuwa karibu na chumba cha maafisa, ambacho kilikuwa juu ya kile cha Maaseya mwana wa Shalumu, aliyekuwa bawabu. 5 Kisha nikaweka mabakuli yaliyojaa divai na baadhi ya vikombe mbele ya watu wa jamaa ya Warekabi na kuwaambia, “Kunyweni divai.” 6 Lakini wao wakajibu, “Sisi hatunywi divai, kwa sababu baba yetu Yonadabu mwana wa Rekabu, alitupa agizo hili: ‘Ninyi wala wazao wenu kamwe msinywe divai. 7 Pia msijenge nyumba kamwe, wala kuotesha mbegu au kupanda mashamba ya mizabibu. Kamwe msiwe na kitu chochote katika hivi, lakini siku zote lazima muishi kwenye mahema. Ndipo mtakapoishi kwa muda mrefu katika nchi ambayo ninyi ni wahamiaji.’ 8 Tumetii kila kitu ambacho baba yetu Yonadabu mwana wa Rekabu alituamuru. Sisi wenyewe wala wake zetu wala wana wetu na binti zetu kamwe hatujanywa divai 9 wala kujenga nyumba za kuishi au kuwa na mashamba ya mizabibu, mashamba au mazao. 10 Tumeishi katika mahema na tumetii kikamilifu kila kitu alichotuamuru baba yetu Yonadabu. 11 Lakini wakati Nebukadneza mfalme wa Babeli alipoivamia nchi hii, tulisema, ‘Njooni, lazima twende Yerusalemu ili kukimbia majeshi ya Wakaldayo na ya Washamu.’ Kwa hiyo tumeishi Yerusalemu.” 12 Ndipo neno la BWANA likamjia Yeremia kusema: 13 “Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, aliye Mungu wa Israeli, asemalo: Nenda ukawaambie watu wa Yuda na watu wa Yerusalemu, ‘Je, hamwezi kujifunza kutoka kwa wana wa Rekabu, na kuyatii maneno yangu?’ asema BWANA. 14 ‘Yonadabu mwana wa Rekabu aliwaagiza wanawe wasinywe divai, na agizo hilo wamelishika mpaka leo hawanywi divai, kwa sababu wanatii amri ya baba yao. Lakini nimenena nanyi tena na tena, lakini hamkunitii mimi. 15 Tena na tena nimewatuma watumishi wangu wote manabii kwenu. Wakasema, “Kila mmoja wenu ni lazima ageuke na kuacha njia zake mbaya, na kuyatengeneza matendo yake. Msifuate miungu mingine ili kuitumikia. Ndipo mtakapoishi katika nchi niliyowapa ninyi na baba zenu.” Lakini hamkujali wala kunisikiliza. 16 Wazao wa Yonadabu mwana wa Rekabu walitimiza amri ambayo baba yao aliwapa, lakini watu hawa hawakunitii mimi.’ 17 “Kwa hiyo, hili ndilo BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Sikilizeni! Nitaleta juu ya Yuda na juu ya kila mmoja aishiye Yerusalemu kila aina ya maafa niliyotamka dhidi yao. Nilinena nao, lakini hawakusikiliza. Niliwaita, lakini hawakujibu.’ ” 18 Kisha Yeremia akaiambia jamaa ya Warekabi, “Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: ‘Mmetii amri ya baba yenu Yonadabu, na mmefuata mafundisho yake yote na mmefanya kila kitu alichowaamuru.’ 19 Kwa hiyo hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Yonadabu mwana wa Rekabu hatakosa kamwe kuwa na mtu wa kunitumikia mimi.’ ”
In Other Versions
Jeremiah 35 in the ANGEFD
Jeremiah 35 in the ANTPNG2D
Jeremiah 35 in the AS21
Jeremiah 35 in the BAGH
Jeremiah 35 in the BBPNG
Jeremiah 35 in the BBT1E
Jeremiah 35 in the BDS
Jeremiah 35 in the BEV
Jeremiah 35 in the BHAD
Jeremiah 35 in the BIB
Jeremiah 35 in the BLPT
Jeremiah 35 in the BNT
Jeremiah 35 in the BNTABOOT
Jeremiah 35 in the BNTLV
Jeremiah 35 in the BOATCB
Jeremiah 35 in the BOATCB2
Jeremiah 35 in the BOBCV
Jeremiah 35 in the BOCNT
Jeremiah 35 in the BOECS
Jeremiah 35 in the BOGWICC
Jeremiah 35 in the BOHCB
Jeremiah 35 in the BOHCV
Jeremiah 35 in the BOHLNT
Jeremiah 35 in the BOHNTLTAL
Jeremiah 35 in the BOICB
Jeremiah 35 in the BOILNTAP
Jeremiah 35 in the BOITCV
Jeremiah 35 in the BOKCV2
Jeremiah 35 in the BOKHWOG
Jeremiah 35 in the BOKSSV
Jeremiah 35 in the BOLCB
Jeremiah 35 in the BOLCB2
Jeremiah 35 in the BOMCV
Jeremiah 35 in the BONAV
Jeremiah 35 in the BONCB
Jeremiah 35 in the BONLT
Jeremiah 35 in the BONUT2
Jeremiah 35 in the BOPLNT
Jeremiah 35 in the BOSCB
Jeremiah 35 in the BOSNC
Jeremiah 35 in the BOTLNT
Jeremiah 35 in the BOVCB
Jeremiah 35 in the BOYCB
Jeremiah 35 in the BPBB
Jeremiah 35 in the BPH
Jeremiah 35 in the BSB
Jeremiah 35 in the CCB
Jeremiah 35 in the CUV
Jeremiah 35 in the CUVS
Jeremiah 35 in the DBT
Jeremiah 35 in the DGDNT
Jeremiah 35 in the DHNT
Jeremiah 35 in the DNT
Jeremiah 35 in the ELBE
Jeremiah 35 in the EMTV
Jeremiah 35 in the ESV
Jeremiah 35 in the FBV
Jeremiah 35 in the FEB
Jeremiah 35 in the GGMNT
Jeremiah 35 in the GNT
Jeremiah 35 in the HARY
Jeremiah 35 in the HNT
Jeremiah 35 in the IRVA
Jeremiah 35 in the IRVB
Jeremiah 35 in the IRVG
Jeremiah 35 in the IRVH
Jeremiah 35 in the IRVK
Jeremiah 35 in the IRVM
Jeremiah 35 in the IRVM2
Jeremiah 35 in the IRVO
Jeremiah 35 in the IRVP
Jeremiah 35 in the IRVT
Jeremiah 35 in the IRVT2
Jeremiah 35 in the IRVU
Jeremiah 35 in the ISVN
Jeremiah 35 in the JSNT
Jeremiah 35 in the KAPI
Jeremiah 35 in the KBT1ETNIK
Jeremiah 35 in the KBV
Jeremiah 35 in the KJV
Jeremiah 35 in the KNFD
Jeremiah 35 in the LBA
Jeremiah 35 in the LBLA
Jeremiah 35 in the LNT
Jeremiah 35 in the LSV
Jeremiah 35 in the MAAL
Jeremiah 35 in the MBV
Jeremiah 35 in the MBV2
Jeremiah 35 in the MHNT
Jeremiah 35 in the MKNFD
Jeremiah 35 in the MNG
Jeremiah 35 in the MNT
Jeremiah 35 in the MNT2
Jeremiah 35 in the MRS1T
Jeremiah 35 in the NAA
Jeremiah 35 in the NASB
Jeremiah 35 in the NBLA
Jeremiah 35 in the NBS
Jeremiah 35 in the NBVTP
Jeremiah 35 in the NET2
Jeremiah 35 in the NIV11
Jeremiah 35 in the NNT
Jeremiah 35 in the NNT2
Jeremiah 35 in the NNT3
Jeremiah 35 in the PDDPT
Jeremiah 35 in the PFNT
Jeremiah 35 in the RMNT
Jeremiah 35 in the SBIAS
Jeremiah 35 in the SBIBS
Jeremiah 35 in the SBIBS2
Jeremiah 35 in the SBICS
Jeremiah 35 in the SBIDS
Jeremiah 35 in the SBIGS
Jeremiah 35 in the SBIHS
Jeremiah 35 in the SBIIS
Jeremiah 35 in the SBIIS2
Jeremiah 35 in the SBIIS3
Jeremiah 35 in the SBIKS
Jeremiah 35 in the SBIKS2
Jeremiah 35 in the SBIMS
Jeremiah 35 in the SBIOS
Jeremiah 35 in the SBIPS
Jeremiah 35 in the SBISS
Jeremiah 35 in the SBITS
Jeremiah 35 in the SBITS2
Jeremiah 35 in the SBITS3
Jeremiah 35 in the SBITS4
Jeremiah 35 in the SBIUS
Jeremiah 35 in the SBIVS
Jeremiah 35 in the SBT
Jeremiah 35 in the SBT1E
Jeremiah 35 in the SCHL
Jeremiah 35 in the SNT
Jeremiah 35 in the SUSU
Jeremiah 35 in the SUSU2
Jeremiah 35 in the SYNO
Jeremiah 35 in the TBIAOTANT
Jeremiah 35 in the TBT1E
Jeremiah 35 in the TBT1E2
Jeremiah 35 in the TFTIP
Jeremiah 35 in the TFTU
Jeremiah 35 in the TGNTATF3T
Jeremiah 35 in the THAI
Jeremiah 35 in the TNFD
Jeremiah 35 in the TNT
Jeremiah 35 in the TNTIK
Jeremiah 35 in the TNTIL
Jeremiah 35 in the TNTIN
Jeremiah 35 in the TNTIP
Jeremiah 35 in the TNTIZ
Jeremiah 35 in the TOMA
Jeremiah 35 in the TTENT
Jeremiah 35 in the UBG
Jeremiah 35 in the UGV
Jeremiah 35 in the UGV2
Jeremiah 35 in the UGV3
Jeremiah 35 in the VBL
Jeremiah 35 in the VDCC
Jeremiah 35 in the YALU
Jeremiah 35 in the YAPE
Jeremiah 35 in the YBVTP
Jeremiah 35 in the ZBP