John 1 (BOKCV)

1 Hapo mwanzo alikuwako Neno, huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu. 3 Vitu vyote viliumbwa kwa yeye, wala pasipo yeye hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa. 4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu. 5 Nuru hungʼaa gizani nalo giza halikuishinda. 6 Alikuja mtu mmoja aliyetumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. 7 Alikuja kama shahidi apate kuishuhudia hiyo nuru, ili kwa kupitia kwake watu wote waweze kuamini. 8 Yeye mwenyewe hakuwa ile nuru, bali alikuja kuishuhudia hiyo nuru. 9 Kwamba nuru halisi, imwangaziayo kila mtu ilikuwa inakuja ulimwenguni. 10 Huyo Neno alikuwako ulimwenguni na ingawa ulimwengu uliumbwa kupitia kwake, haukumtambua. 11 Alikuja kwa walio wake, lakini wao hawakumpokea. 12 Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. 13 Hawa ndio wasiozaliwa kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali kwa mapenzi ya Mungu. 14 Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli. 15 Yohana alishuhudia habari zake, akapaza sauti, akisema, “Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuniliko mimi, kwa kuwa alikuwepo kabla yangu.’ ” 16 Kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema juu ya neema. 17 Kwa kuwa sheria ilitolewa kwa mkono wa Mose, lakini neema na kweli imekuja kupitia Yesu Kristo. 18 Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote, ila ni Mungu Mwana pekee, aliye kifuani mwa Baba ndiye ambaye amemdhihirisha. 19 Huu ndio ushuhuda wa Yohana wakati Wayahudi walipowatuma makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu kumuuliza, “Wewe ni nani?” 20 Yohana alikiri waziwazi pasipo kuficha akasema, “Mimi si Kristo.” 21 Wakamuuliza, “Wewe ni nani basi? Je, wewe ni Eliya?”Yeye akajibu, “Hapana, mimi siye.”“Je, wewe ni yule Nabii?”Akajibu, “Hapana.” 22 Ndipo wakasema, “Basi tuambie wewe ni nani ili tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Wewe wasemaje juu yako mwenyewe?” 23 Akawajibu kwa maneno ya nabii Isaya, akisema, “Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Yanyoosheni mapito ya Bwana.’ ” 24 Basi walikuwa wametumwa watu kutoka kwa Mafarisayo 25 wakamuuliza, “Kama wewe si Kristo, wala si Eliya na wala si yule Nabii, kwa nini basi unabatiza?” 26 Yohana akawajibu, “Mimi ninabatiza kwa maji, lakini katikati yenu yupo mtu msiyemjua. 27 Yeye ajaye baada yangu, sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake.” 28 Mambo haya yote yalitukia huko Bethania, ngʼambo ya Mto Yordani, mahali Yohana alipokuwa akibatiza. 29 Siku iliyofuata, Yohana alimwona Yesu akimjia akasema, “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 30 Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Mtu anakuja baada yangu ambaye ni mkuu kuniliko mimi, kwa kuwa alikuwepo kabla yangu.’ 31 Mimi mwenyewe sikumfahamu, lakini sababu ya kuja nikibatiza kwa maji ni ili yeye apate kufunuliwa kwa Israeli.” 32 Kisha Yohana akatoa ushuhuda huu: “Nilimwona Roho akishuka kutoka mbinguni kama hua, akakaa juu yake. 33 Mimi nisingemtambua, lakini yeye aliyenituma nibatize kwa maji alikuwa ameniambia, ‘Yule mtu utakayemwona Roho akimshukia na kukaa juu yake, huyo ndiye atakayebatiza kwa Roho Mtakatifu.’ 34 Mimi mwenyewe nimeona jambo hili na ninashuhudia kuwa huyu ndiye Mwana wa Mungu.” 35 Siku iliyofuata, Yohana alikuwa huko tena pamoja na wanafunzi wake wawili. 36 Alipomwona Yesu akipita, akasema, “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu!” 37 Wale wanafunzi wawili walipomsikia Yohana akisema haya, wakamfuata Yesu. 38 Yesu akageuka, akawaona wakimfuata akawauliza, “Mnataka nini?”Wakamwambia, “Rabi,” (maana yake Mwalimu), “Unaishi wapi?” 39 Yesu akawajibu, “Njooni, nanyi mtapaona!”Hivyo wakaenda na kupaona mahali alipokuwa anaishi, wakakaa naye siku ile, kwa kuwa ilikuwa yapata saa kumi. 40 Andrea nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliosikia yale Yohana aliyokuwa amesema, naye ndiye alimfuata Yesu. 41 Kitu cha kwanza Andrea alichofanya ni kumtafuta Simoni nduguye na kumwambia, “Tumemwona Masiya” (yaani, Kristo). 42 Naye akamleta kwa Yesu.Yesu akamwangalia na kusema, “Wewe ni Simoni mwana wa Yohana. Utaitwa Kefa” (ambalo limetafsiriwa Petro). 43 Siku iliyofuata Yesu aliamua kwenda Galilaya. Akamkuta Filipo, akamwambia, “Nifuate.” 44 Basi Filipo alikuwa mwenyeji wa Bethsaida, mji alikotoka Andrea na Petro. 45 Filipo naye akamkuta Nathanaeli na kumwambia, “Tumemwona yeye ambaye Mose aliandika habari zake katika Sheria na ambaye pia manabii waliandika kumhusu, yaani, Yesu wa Nazareti, mwana wa Yosefu.” 46 Nathanaeli akauliza, “Nazareti! Je, kitu chochote chema chaweza kutoka Nazareti?” Filipo akamwambia, “Njoo uone.” 47 Yesu alipomwona Nathanaeli anakaribia, akanena habari zake akasema, “Tazama huyu ni Mwisraeli kweli kweli; hana hila ndani yake.” 48 Nathanaeli akamuuliza, “Umenifahamuje?”Yesu akamjibu, “Nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini, kabla hata Filipo hajakuita.” 49 Nathanaeli akamwambia, “Rabi, wewe ni Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli!” 50 Yesu akamwambia, “Unaamini kwa kuwa nilikuambia nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini? Basi utaona mambo makuu zaidi kuliko hilo.” 51 Ndipo akawaambia, “Amin, amin nawaambia, ninyi mtaona mbingu ikifunguka na malaika wa Mungu wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.”

In Other Versions

John 1 in the ANGEFD

John 1 in the ANTPNG2D

John 1 in the AS21

John 1 in the BAGH

John 1 in the BBPNG

John 1 in the BBT1E

John 1 in the BDS

John 1 in the BEV

John 1 in the BHAD

John 1 in the BIB

John 1 in the BLPT

John 1 in the BNT

John 1 in the BNTABOOT

John 1 in the BNTLV

John 1 in the BOATCB

John 1 in the BOATCB2

John 1 in the BOBCV

John 1 in the BOCNT

John 1 in the BOECS

John 1 in the BOGWICC

John 1 in the BOHCB

John 1 in the BOHCV

John 1 in the BOHLNT

John 1 in the BOHNTLTAL

John 1 in the BOICB

John 1 in the BOILNTAP

John 1 in the BOITCV

John 1 in the BOKCV2

John 1 in the BOKHWOG

John 1 in the BOKSSV

John 1 in the BOLCB

John 1 in the BOLCB2

John 1 in the BOMCV

John 1 in the BONAV

John 1 in the BONCB

John 1 in the BONLT

John 1 in the BONUT2

John 1 in the BOPLNT

John 1 in the BOSCB

John 1 in the BOSNC

John 1 in the BOTLNT

John 1 in the BOVCB

John 1 in the BOYCB

John 1 in the BPBB

John 1 in the BPH

John 1 in the BSB

John 1 in the CCB

John 1 in the CUV

John 1 in the CUVS

John 1 in the DBT

John 1 in the DGDNT

John 1 in the DHNT

John 1 in the DNT

John 1 in the ELBE

John 1 in the EMTV

John 1 in the ESV

John 1 in the FBV

John 1 in the FEB

John 1 in the GGMNT

John 1 in the GNT

John 1 in the HARY

John 1 in the HNT

John 1 in the IRVA

John 1 in the IRVB

John 1 in the IRVG

John 1 in the IRVH

John 1 in the IRVK

John 1 in the IRVM

John 1 in the IRVM2

John 1 in the IRVO

John 1 in the IRVP

John 1 in the IRVT

John 1 in the IRVT2

John 1 in the IRVU

John 1 in the ISVN

John 1 in the JSNT

John 1 in the KAPI

John 1 in the KBT1ETNIK

John 1 in the KBV

John 1 in the KJV

John 1 in the KNFD

John 1 in the LBA

John 1 in the LBLA

John 1 in the LNT

John 1 in the LSV

John 1 in the MAAL

John 1 in the MBV

John 1 in the MBV2

John 1 in the MHNT

John 1 in the MKNFD

John 1 in the MNG

John 1 in the MNT

John 1 in the MNT2

John 1 in the MRS1T

John 1 in the NAA

John 1 in the NASB

John 1 in the NBLA

John 1 in the NBS

John 1 in the NBVTP

John 1 in the NET2

John 1 in the NIV11

John 1 in the NNT

John 1 in the NNT2

John 1 in the NNT3

John 1 in the PDDPT

John 1 in the PFNT

John 1 in the RMNT

John 1 in the SBIAS

John 1 in the SBIBS

John 1 in the SBIBS2

John 1 in the SBICS

John 1 in the SBIDS

John 1 in the SBIGS

John 1 in the SBIHS

John 1 in the SBIIS

John 1 in the SBIIS2

John 1 in the SBIIS3

John 1 in the SBIKS

John 1 in the SBIKS2

John 1 in the SBIMS

John 1 in the SBIOS

John 1 in the SBIPS

John 1 in the SBISS

John 1 in the SBITS

John 1 in the SBITS2

John 1 in the SBITS3

John 1 in the SBITS4

John 1 in the SBIUS

John 1 in the SBIVS

John 1 in the SBT

John 1 in the SBT1E

John 1 in the SCHL

John 1 in the SNT

John 1 in the SUSU

John 1 in the SUSU2

John 1 in the SYNO

John 1 in the TBIAOTANT

John 1 in the TBT1E

John 1 in the TBT1E2

John 1 in the TFTIP

John 1 in the TFTU

John 1 in the TGNTATF3T

John 1 in the THAI

John 1 in the TNFD

John 1 in the TNT

John 1 in the TNTIK

John 1 in the TNTIL

John 1 in the TNTIN

John 1 in the TNTIP

John 1 in the TNTIZ

John 1 in the TOMA

John 1 in the TTENT

John 1 in the UBG

John 1 in the UGV

John 1 in the UGV2

John 1 in the UGV3

John 1 in the VBL

John 1 in the VDCC

John 1 in the YALU

John 1 in the YAPE

John 1 in the YBVTP

John 1 in the ZBP