Job 9 (BOKCV)
1 Kisha Ayubu akajibu: 2 “Naam, najua hili ni kweli.Lakini mwanadamu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu? 3 Ingawa mtu angetaka kushindana naye,asingaliweza kumjibu Mungu hata mara moja miongoni mwa elfu moja. 4 Hekima yake ni kubwa sana na ana uwezo mwingi mno.Ni nani aliyempinga naye akawa salama? 5 Aiondoa milima bila yenyewe kujuana kuipindua kwa hasira yake. 6 Aitikisa dunia kutoka mahali pakena kuzifanya nguzo zake zitetemeke. 7 Husema na jua, nalo likaacha kuangaza;naye huizima mianga ya nyota. 8 Yeye peke yake huzitandaza mbinguna kuyakanyaga mawimbi ya bahari. 9 Yeye ndiye Muumba wa nyota za Dubu, na Orioni,Kilimia, na makundi ya nyota za kusini. 10 Hutenda maajabu yasiyopimika,miujiza isiyoweza kuhesabiwa. 11 Anapopita karibu nami, siwezi kumwona;apitapo mbele yangu, simtambui. 12 Anapochukua kwa ghafula, ni nani awezaye kumzuia?Ni nani awezaye kumwambia, ‘Unafanya nini?’ 13 Mungu hataizuia hasira yake;hata jeshi kubwa la Rahabu lenye nguvulinajikunyata miguuni pake. 14 “Ni vipi basi mimi nitaweza kubishana naye?Nawezaje kupata maneno ya kuhojiana naye? 15 Ingawa sikuwa na hatia, sikuweza kumjibu;ningeweza tu kumsihi Mhukumu wangu anihurumie. 16 Hata kama ningemwita kwenye shauri, naye akakubali,siamini kama angenisikiliza. 17 Yeye angeniangamiza kwa dhorubana kuongeza majeraha yangu pasipo na sababu. 18 Asingeniacha nipumuebali angenifunika kabisa na huzuni kuu. 19 Kama ni suala la nguvu, yeye ni mwenye nguvu!Kama ni suala la haki, ni nani awezaye kumwita mahakamani? 20 Hata kama sikuwa na hatia, kinywa changu kingenihukumu;kama sikuwa na kosa, kingenitangaza kuwa mwenye hatia. 21 “Ingawa mimi sina kosa,haileti tofauti katika nafsi yangu;nauchukia uhai wangu. 22 Hayo yote ni sawa; ndiyo sababu nasema,‘Yeye huwaangamiza wasio na makosa pamoja na waovu.’ 23 Wakati pigo liletapo kifo cha ghafula,yeye hudhihaki kule kukata tamaa kwa yule asiye na kosa. 24 Wakati nchi inapoangukia mikononi mwa waovu,yeye huwafunga macho mahakimu wake.Kama si yeye, basi ni nani? 25 “Siku zangu zapita mbio kuliko mkimbiaji;zinapita upesi bila kuona furaha hata kidogo. 26 Zinapita upesi kama mashua ya mafunjo,mfano wa tai ayashukiaye mawindo kwa ghafula. 27 Kama nikisema, ‘Nitayasahau malalamiko yangu,nitabadili sura ya uso wangu na kutabasamu,’ 28 bado ninahofia mateso yangu yote,kwa kuwa ninajua hutanihesabu kuwa sina hatia. 29 Kwa kuwa nimeonekana mwenye hatia,kwa nini basi nitaabishwe bure? 30 Hata kama ningejiosha kwa sabunina kutakasa mikono yangu kwa magadi, 31 wewe ungenitupa kwenye shimo la utelezikiasi kwamba hata nguo zangu zingenichukia sana. 32 “Yeye si mwanadamu kama mimi ili niweze kumjibu,ili kwamba tuweze kushindana naye mahakamani. 33 Laiti angelikuwepo mtu wa kutupatanisha kati yetu,aweke mkono wake juu yetu sote wawili, 34 mtu angeliiondoa fimbo ya Mungu juu yangu,ili utisho wake usiendelee kunitia hofu. 35 Ndipo ningenena naye, bila kumwogopa,lakini kama ilivyo kwangu sasa, sitaweza.
In Other Versions
Job 9 in the ANGEFD
Job 9 in the ANTPNG2D
Job 9 in the AS21
Job 9 in the BAGH
Job 9 in the BBPNG
Job 9 in the BBT1E
Job 9 in the BDS
Job 9 in the BEV
Job 9 in the BHAD
Job 9 in the BIB
Job 9 in the BLPT
Job 9 in the BNT
Job 9 in the BNTABOOT
Job 9 in the BNTLV
Job 9 in the BOATCB
Job 9 in the BOATCB2
Job 9 in the BOBCV
Job 9 in the BOCNT
Job 9 in the BOECS
Job 9 in the BOGWICC
Job 9 in the BOHCB
Job 9 in the BOHCV
Job 9 in the BOHLNT
Job 9 in the BOHNTLTAL
Job 9 in the BOICB
Job 9 in the BOILNTAP
Job 9 in the BOITCV
Job 9 in the BOKCV2
Job 9 in the BOKHWOG
Job 9 in the BOKSSV
Job 9 in the BOLCB
Job 9 in the BOLCB2
Job 9 in the BOMCV
Job 9 in the BONAV
Job 9 in the BONCB
Job 9 in the BONLT
Job 9 in the BONUT2
Job 9 in the BOPLNT
Job 9 in the BOSCB
Job 9 in the BOSNC
Job 9 in the BOTLNT
Job 9 in the BOVCB
Job 9 in the BOYCB
Job 9 in the BPBB
Job 9 in the BPH
Job 9 in the BSB
Job 9 in the CCB
Job 9 in the CUV
Job 9 in the CUVS
Job 9 in the DBT
Job 9 in the DGDNT
Job 9 in the DHNT
Job 9 in the DNT
Job 9 in the ELBE
Job 9 in the EMTV
Job 9 in the ESV
Job 9 in the FBV
Job 9 in the FEB
Job 9 in the GGMNT
Job 9 in the GNT
Job 9 in the HARY
Job 9 in the HNT
Job 9 in the IRVA
Job 9 in the IRVB
Job 9 in the IRVG
Job 9 in the IRVH
Job 9 in the IRVK
Job 9 in the IRVM
Job 9 in the IRVM2
Job 9 in the IRVO
Job 9 in the IRVP
Job 9 in the IRVT
Job 9 in the IRVT2
Job 9 in the IRVU
Job 9 in the ISVN
Job 9 in the JSNT
Job 9 in the KAPI
Job 9 in the KBT1ETNIK
Job 9 in the KBV
Job 9 in the KJV
Job 9 in the KNFD
Job 9 in the LBA
Job 9 in the LBLA
Job 9 in the LNT
Job 9 in the LSV
Job 9 in the MAAL
Job 9 in the MBV
Job 9 in the MBV2
Job 9 in the MHNT
Job 9 in the MKNFD
Job 9 in the MNG
Job 9 in the MNT
Job 9 in the MNT2
Job 9 in the MRS1T
Job 9 in the NAA
Job 9 in the NASB
Job 9 in the NBLA
Job 9 in the NBS
Job 9 in the NBVTP
Job 9 in the NET2
Job 9 in the NIV11
Job 9 in the NNT
Job 9 in the NNT2
Job 9 in the NNT3
Job 9 in the PDDPT
Job 9 in the PFNT
Job 9 in the RMNT
Job 9 in the SBIAS
Job 9 in the SBIBS
Job 9 in the SBIBS2
Job 9 in the SBICS
Job 9 in the SBIDS
Job 9 in the SBIGS
Job 9 in the SBIHS
Job 9 in the SBIIS
Job 9 in the SBIIS2
Job 9 in the SBIIS3
Job 9 in the SBIKS
Job 9 in the SBIKS2
Job 9 in the SBIMS
Job 9 in the SBIOS
Job 9 in the SBIPS
Job 9 in the SBISS
Job 9 in the SBITS
Job 9 in the SBITS2
Job 9 in the SBITS3
Job 9 in the SBITS4
Job 9 in the SBIUS
Job 9 in the SBIVS
Job 9 in the SBT
Job 9 in the SBT1E
Job 9 in the SCHL
Job 9 in the SNT
Job 9 in the SUSU
Job 9 in the SUSU2
Job 9 in the SYNO
Job 9 in the TBIAOTANT
Job 9 in the TBT1E
Job 9 in the TBT1E2
Job 9 in the TFTIP
Job 9 in the TFTU
Job 9 in the TGNTATF3T
Job 9 in the THAI
Job 9 in the TNFD
Job 9 in the TNT
Job 9 in the TNTIK
Job 9 in the TNTIL
Job 9 in the TNTIN
Job 9 in the TNTIP
Job 9 in the TNTIZ
Job 9 in the TOMA
Job 9 in the TTENT
Job 9 in the UBG
Job 9 in the UGV
Job 9 in the UGV2
Job 9 in the UGV3
Job 9 in the VBL
Job 9 in the VDCC
Job 9 in the YALU
Job 9 in the YAPE
Job 9 in the YBVTP
Job 9 in the ZBP