Joel 2 (BOKCV)

1 Pigeni tarumbeta katika Sayuni;pigeni mbiu katika mlima wangu mtakatifu.Wote waishio katika nchi na watetemeke,kwa kuwa siku ya BWANA inakuja. Iko karibu, 2 siku ya giza na huzuni,siku ya mawingu na utusitusi.Kama mapambazuko yasambaavyotoka upande huu wa milimahata upande mwinginejeshi kubwa na lenye nguvu linakuja.Jambo kama hili halijakuwepo tangu zamaniwala halitakuwepo tena kamwekwa vizazi vijavyo. 3 Mbele yao moto unateketeza,nyuma yao miali ya motoinawaka kwa nguvu.Mbele yao nchi iko kama bustani ya Edeni,nyuma yao ni jangwa lisilofaa:hakuna kitu kinachowaepuka. 4 Wanaonekana kama farasi;wanakwenda mbiokama askari wapanda farasi. 5 Wanatoa sauti kama magari ya vita,wanaporukaruka juu ya vilele vya milima,kama mlio wa miali ya moto ilayo mabua,kama jeshi kubwa lililojipanga kwa ajili ya vita. 6 Wanapoonekana, mataifa yanakuwa katika maumivu makuu;kila uso unabadilika rangi. 7 Wanashambulia kama wapiganaji wa vita;wanapanda kuta kama askari.Wote wanatembea katika safu,hawapotoshi safu zao. 8 Hakuna anayemsukuma mwenzake;kila mmoja anakwenda mbele moja kwa moja.Wanapita katika vizuizibila kuharibu safu zao. 9 Wanaenda kasi kuingia mjini;wanakimbia ukutani.Wanaingia ndani ya nyumba;kwa kuingilia madirishani kama wevi. 10 Mbele yao dunia inatikisika,anga linatetemeka,jua na mwezi vinatiwa giza,na nyota hazitoi mwanga wake tena. 11 BWANA anatoa mshindo wa ngurumombele ya jeshi lake;majeshi yake hayana idadi,ni wenye nguvu nyingiwale ambao hutii agizo lake.Siku ya BWANA ni kuu,ni ya kutisha.Ni nani anayeweza kuistahimili? 12 “Hata sasa,” asema BWANA,“nirudieni kwa mioyo yenu yote,kwa kufunga, kwa kulia na kuomboleza.” 13 Rarueni mioyo yenuna siyo mavazi yenu.Mrudieni BWANA, Mungu wenu,kwa maana yeye ndiye mwenye neemana mwingi wa huruma,si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo,huona huruma, hujizuia kuleta maafa. 14 Ni nani ajuaye? Yeye aweza kugeuka na kuwa na hurumana kuacha baraka nyuma yake:sadaka za nafaka na sadaka za vinywajikwa ajili ya BWANA Mungu wenu. 15 Pigeni tarumbeta katika Sayuni,tangazeni saumu takatifu,liiteni kusanyiko takatifu. 16 Wakusanyeni watu,wekeni wakfu kusanyiko;waleteni pamoja wazee,wakusanyeni watoto,wale wanyonyao maziwa.Bwana arusi na atoke chumbani mwakena bibi arusi naye atoke katika chumba chake. 17 Makuhani, ambao wanahudumu mbele za BWANA,na walie katikati ya ukumbiwa Hekalu na madhabahu.Waseme, “Wahurumie watu wako, Ee BWANA.Usifanye urithi wako kitu cha kudharauliwa,neno la dhihaka kati ya mataifa.Kwa nini wasemezane miongoni mwao,‘Yuko wapi Mungu wao?’ ” 18 Kisha BWANA atakuwa na wivu kwa ajili ya nchi yakena kuwa na huruma juu ya watu wake. 19 BWANA atawajibu:“Ninawapelekea nafaka,mvinyo mpya na mafuta,vya kuwatosha ninyihadi mridhike kabisa;kamwe sitawafanya tenakitu cha kudharauliwa na mataifa. 20 “Nitafukuza jeshi la kaskazini likae mbali nanyi,nikilisukuma ndani ya jangwa,askari wa safu za mbele wakiendandani ya bahari ya masharikina wale wa safu za nyumakatika bahari ya magharibi.Uvundo wake utapaa juu;harufu yake itapanda juu.” Hakika ametenda mambo makubwa. 21 Usiogope, ee nchi;furahi na kushangilia.Hakika BWANA ametenda mambo makubwa. 22 Msiogope, enyi wanyama pori,kwa kuwa mbuga za malisho yenuzinarudia ubichi.Miti nayo inazaa matunda,mtini na mzabibu inatoa utajiri wake. 23 Furahini, enyi watu wa Sayuni,shangilieni katika BWANA Mungu wenu,kwa kuwa amewapa mvua za vulikwa kipimo cha haki.Anawapelekea mvua nyingi,mvua ya vuli na ya masika, kama mwanzoni. 24 Sakafu za kupuria zitajaa nafaka,mapipa yatafurika mvinyo mpya na mafuta. 25 “Nitawalipa kwa ajili ya miaka ile iliyoliwa na nzige:parare, madumadu na tunutu,jeshi langu kubwa ambalonililituma katikati yenu. 26 Mtakuwa na wingi wa vyakula mpaka mshibe,na mtalisifu jina la BWANA Mungu wenu,ambaye amefanya maajabu kwa ajili yenu;kamwe watu wangu hawataaibishwa tena. 27 Ndipo mtakapojua kwamba mimi niko katika Israelikwamba mimi ndimi BWANA Mungu wenu,na kwamba hakuna mwingine;kamwe watu wangu hawataaibika tena. 28 “Hata itakuwa, baada ya hayo,nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili.Wana wenu na binti zenu watatabiri,wazee wenu wataota ndoto,na vijana wenu wataona maono. 29 Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake,katika siku zile nitamimina Roho wangu. 30 Nami nitaonyesha maajabu katika mbinguna duniani:damu, moto na mawimbi ya moshi. 31 Jua litageuzwa kuwa gizana mwezi kuwa mwekundu kama damu,kabla ya kuja siku ya BWANAile kuu na ya kutisha. 32 Na kila mtu atakayeliitiajina la BWANA ataokolewa.Kwa maana juu ya Mlima Sayuni na katika Yerusalemukutakuwepo wokovu,kama BWANA alivyosema,miongoni mwa walionusurikaambao BWANA awaita.

In Other Versions

Joel 2 in the ANGEFD

Joel 2 in the ANTPNG2D

Joel 2 in the AS21

Joel 2 in the BAGH

Joel 2 in the BBPNG

Joel 2 in the BBT1E

Joel 2 in the BDS

Joel 2 in the BEV

Joel 2 in the BHAD

Joel 2 in the BIB

Joel 2 in the BLPT

Joel 2 in the BNT

Joel 2 in the BNTABOOT

Joel 2 in the BNTLV

Joel 2 in the BOATCB

Joel 2 in the BOATCB2

Joel 2 in the BOBCV

Joel 2 in the BOCNT

Joel 2 in the BOECS

Joel 2 in the BOGWICC

Joel 2 in the BOHCB

Joel 2 in the BOHCV

Joel 2 in the BOHLNT

Joel 2 in the BOHNTLTAL

Joel 2 in the BOICB

Joel 2 in the BOILNTAP

Joel 2 in the BOITCV

Joel 2 in the BOKCV2

Joel 2 in the BOKHWOG

Joel 2 in the BOKSSV

Joel 2 in the BOLCB

Joel 2 in the BOLCB2

Joel 2 in the BOMCV

Joel 2 in the BONAV

Joel 2 in the BONCB

Joel 2 in the BONLT

Joel 2 in the BONUT2

Joel 2 in the BOPLNT

Joel 2 in the BOSCB

Joel 2 in the BOSNC

Joel 2 in the BOTLNT

Joel 2 in the BOVCB

Joel 2 in the BOYCB

Joel 2 in the BPBB

Joel 2 in the BPH

Joel 2 in the BSB

Joel 2 in the CCB

Joel 2 in the CUV

Joel 2 in the CUVS

Joel 2 in the DBT

Joel 2 in the DGDNT

Joel 2 in the DHNT

Joel 2 in the DNT

Joel 2 in the ELBE

Joel 2 in the EMTV

Joel 2 in the ESV

Joel 2 in the FBV

Joel 2 in the FEB

Joel 2 in the GGMNT

Joel 2 in the GNT

Joel 2 in the HARY

Joel 2 in the HNT

Joel 2 in the IRVA

Joel 2 in the IRVB

Joel 2 in the IRVG

Joel 2 in the IRVH

Joel 2 in the IRVK

Joel 2 in the IRVM

Joel 2 in the IRVM2

Joel 2 in the IRVO

Joel 2 in the IRVP

Joel 2 in the IRVT

Joel 2 in the IRVT2

Joel 2 in the IRVU

Joel 2 in the ISVN

Joel 2 in the JSNT

Joel 2 in the KAPI

Joel 2 in the KBT1ETNIK

Joel 2 in the KBV

Joel 2 in the KJV

Joel 2 in the KNFD

Joel 2 in the LBA

Joel 2 in the LBLA

Joel 2 in the LNT

Joel 2 in the LSV

Joel 2 in the MAAL

Joel 2 in the MBV

Joel 2 in the MBV2

Joel 2 in the MHNT

Joel 2 in the MKNFD

Joel 2 in the MNG

Joel 2 in the MNT

Joel 2 in the MNT2

Joel 2 in the MRS1T

Joel 2 in the NAA

Joel 2 in the NASB

Joel 2 in the NBLA

Joel 2 in the NBS

Joel 2 in the NBVTP

Joel 2 in the NET2

Joel 2 in the NIV11

Joel 2 in the NNT

Joel 2 in the NNT2

Joel 2 in the NNT3

Joel 2 in the PDDPT

Joel 2 in the PFNT

Joel 2 in the RMNT

Joel 2 in the SBIAS

Joel 2 in the SBIBS

Joel 2 in the SBIBS2

Joel 2 in the SBICS

Joel 2 in the SBIDS

Joel 2 in the SBIGS

Joel 2 in the SBIHS

Joel 2 in the SBIIS

Joel 2 in the SBIIS2

Joel 2 in the SBIIS3

Joel 2 in the SBIKS

Joel 2 in the SBIKS2

Joel 2 in the SBIMS

Joel 2 in the SBIOS

Joel 2 in the SBIPS

Joel 2 in the SBISS

Joel 2 in the SBITS

Joel 2 in the SBITS2

Joel 2 in the SBITS3

Joel 2 in the SBITS4

Joel 2 in the SBIUS

Joel 2 in the SBIVS

Joel 2 in the SBT

Joel 2 in the SBT1E

Joel 2 in the SCHL

Joel 2 in the SNT

Joel 2 in the SUSU

Joel 2 in the SUSU2

Joel 2 in the SYNO

Joel 2 in the TBIAOTANT

Joel 2 in the TBT1E

Joel 2 in the TBT1E2

Joel 2 in the TFTIP

Joel 2 in the TFTU

Joel 2 in the TGNTATF3T

Joel 2 in the THAI

Joel 2 in the TNFD

Joel 2 in the TNT

Joel 2 in the TNTIK

Joel 2 in the TNTIL

Joel 2 in the TNTIN

Joel 2 in the TNTIP

Joel 2 in the TNTIZ

Joel 2 in the TOMA

Joel 2 in the TTENT

Joel 2 in the UBG

Joel 2 in the UGV

Joel 2 in the UGV2

Joel 2 in the UGV3

Joel 2 in the VBL

Joel 2 in the VDCC

Joel 2 in the YALU

Joel 2 in the YAPE

Joel 2 in the YBVTP

Joel 2 in the ZBP