Nehemiah 5 (BOKCV)
1 Wakati huu wanaume na wake zao wakalia kilio kikuu dhidi ya ndugu zao Wayahudi. 2 Baadhi yao walikuwa wakisema, “Sisi na wana wetu na binti zetu tuko wengi. Ili tuweze kula na kuishi, ni lazima tupate nafaka.” 3 Wengine walikuwa wakisema, “Tunaweka rehani mashamba yetu, mashamba ya mizabibu, na nyumba zetu ili tupate nafaka wakati wa njaa.” 4 Bado kukawa na wengine waliokuwa wakisema, “Ilitubidi tukope fedha ili kulipa kodi ya mfalme kwa ajili ya mashamba yetu na mashamba yetu ya mizabibu. 5 Ingawa sisi ni mwili na damu moja sawa na watu wa nchi yetu, na ijapo wana wetu ni wazuri kama wana wao, bado inatupasa kuwatoa wana wetu na binti zetu kwenye utumwa. Baadhi ya binti zetu wameshakuwa watumwa tayari, lakini hatuna uwezo wa kuwakomboa, kwa sababu mashamba yetu na mashamba ya mizabibu yetu ni mali ya wengine.” 6 Niliposikia kilio chao na malalamiko haya, nilikasirika sana. 7 Nikayatafakari katika akili yangu, nikiwalaumu wakuu na maafisa. Nikawaambia, “Mnawaonea ndugu zenu kwa kuwatoza riba!” Basi nikaitisha mkutano mkubwa ili kuwashughulikia 8 na kusema: “Kulingana na uwezo wetu, tumewakomboa ndugu zetu Wayahudi waliokuwa wameuzwa kwa watu wasioamini. Sasa mnawauza ndugu zenu, ili wauzwe tena kwetu!” Walinyamaza kimya, kwa sababu hawakupata chochote cha kusema. 9 Basi nikaendelea kusema, “Mnachokifanya si sawa. Je, haikuwapasa kutembea katika hofu ya Mungu wetu ili tuepukane na shutuma za adui zetu wasioamini? 10 Mimi na ndugu zangu na watu wangu tunawakopesha watu fedha na nafaka. Lakini jambo hili la kutoza riba likome! 11 Warudishieni mara moja mashamba yao, mashamba yao ya mizabibu, mashamba yao ya mizeituni, na nyumba zao, pia riba yao mnayowatoza na sehemu ya fungu la mia la fedha, nafaka, divai mpya na mafuta.” 12 Wakasema, “Tutawarudishia na hatutataka kitu chochote zaidi kutoka kwao. Tutafanya kama ulivyosema.”Kisha nikawaita makuhani na kuwafanya wakuu na maafisa kuapa kufanya kile walichoahidi. 13 Pia nikakungʼuta makunjo ya vazi langu na kusema, “Kila mtu ambaye hatatimiza ahadi hii, Mungu na amkungʼute hivi kutoka nyumba yake na katika mali zake. Basi mtu wa namna hiyo akungʼutiwe nje na aachwe bila kitu!”Waliposikia hili, mkutano wote ukasema, “Amen,” na wakamtukuza BWANA. Nao watu wakafanya kama walivyokuwa wameahidi. 14 Zaidi ya hayo, kutoka mwaka wa ishirini wa Mfalme Artashasta, wakati nilipoteuliwa kuwa mtawala wao katika nchi ya Yuda, mpaka mwaka wake wa thelathini na mbili, yaani miaka kumi na miwili, mimi wala ndugu zangu hatukula chakula ambacho kwa kawaida hupewa watawala. 15 Lakini watawala wa mwanzoni, wale walionitangulia, waliwalemea watu na kuchukua kutoka kwao shekeli arobaini za fedha, pamoja na chakula na mvinyo. Wasaidizi wao pia walijifanya wakuu juu ya watu. Lakini kwa kumheshimu Mungu sikufanya hivyo. 16 Badala yake, nilijitoa kwa bidii katika kazi ya ukuta huu. Watu wangu wote walikutanika pale kwa ajili ya kazi. Hatukujipatia shamba lolote. 17 Zaidi ya hayo, Wayahudi na maafisa 150 walikula mezani pangu, pamoja na wale waliotujia kutoka mataifa jirani. 18 Kila siku niliandaliwa maksai mmoja, kondoo sita wazuri, na kuku, na mvinyo wa kila aina kwa wingi kila baada ya siku kumi. Licha ya mambo haya yote, sikudai chakula kilichokuwa fungu la mtawala, kwa sababu madai yalikuwa mazito sana kwa watu hawa. 19 Unikumbuke kwa fadhili, Ee Mungu wangu, kwa yote niliyofanya kwa ajili ya watu hawa.
In Other Versions
Nehemiah 5 in the ANGEFD
Nehemiah 5 in the ANTPNG2D
Nehemiah 5 in the AS21
Nehemiah 5 in the BAGH
Nehemiah 5 in the BBPNG
Nehemiah 5 in the BBT1E
Nehemiah 5 in the BDS
Nehemiah 5 in the BEV
Nehemiah 5 in the BHAD
Nehemiah 5 in the BIB
Nehemiah 5 in the BLPT
Nehemiah 5 in the BNT
Nehemiah 5 in the BNTABOOT
Nehemiah 5 in the BNTLV
Nehemiah 5 in the BOATCB
Nehemiah 5 in the BOATCB2
Nehemiah 5 in the BOBCV
Nehemiah 5 in the BOCNT
Nehemiah 5 in the BOECS
Nehemiah 5 in the BOGWICC
Nehemiah 5 in the BOHCB
Nehemiah 5 in the BOHCV
Nehemiah 5 in the BOHLNT
Nehemiah 5 in the BOHNTLTAL
Nehemiah 5 in the BOICB
Nehemiah 5 in the BOILNTAP
Nehemiah 5 in the BOITCV
Nehemiah 5 in the BOKCV2
Nehemiah 5 in the BOKHWOG
Nehemiah 5 in the BOKSSV
Nehemiah 5 in the BOLCB
Nehemiah 5 in the BOLCB2
Nehemiah 5 in the BOMCV
Nehemiah 5 in the BONAV
Nehemiah 5 in the BONCB
Nehemiah 5 in the BONLT
Nehemiah 5 in the BONUT2
Nehemiah 5 in the BOPLNT
Nehemiah 5 in the BOSCB
Nehemiah 5 in the BOSNC
Nehemiah 5 in the BOTLNT
Nehemiah 5 in the BOVCB
Nehemiah 5 in the BOYCB
Nehemiah 5 in the BPBB
Nehemiah 5 in the BPH
Nehemiah 5 in the BSB
Nehemiah 5 in the CCB
Nehemiah 5 in the CUV
Nehemiah 5 in the CUVS
Nehemiah 5 in the DBT
Nehemiah 5 in the DGDNT
Nehemiah 5 in the DHNT
Nehemiah 5 in the DNT
Nehemiah 5 in the ELBE
Nehemiah 5 in the EMTV
Nehemiah 5 in the ESV
Nehemiah 5 in the FBV
Nehemiah 5 in the FEB
Nehemiah 5 in the GGMNT
Nehemiah 5 in the GNT
Nehemiah 5 in the HARY
Nehemiah 5 in the HNT
Nehemiah 5 in the IRVA
Nehemiah 5 in the IRVB
Nehemiah 5 in the IRVG
Nehemiah 5 in the IRVH
Nehemiah 5 in the IRVK
Nehemiah 5 in the IRVM
Nehemiah 5 in the IRVM2
Nehemiah 5 in the IRVO
Nehemiah 5 in the IRVP
Nehemiah 5 in the IRVT
Nehemiah 5 in the IRVT2
Nehemiah 5 in the IRVU
Nehemiah 5 in the ISVN
Nehemiah 5 in the JSNT
Nehemiah 5 in the KAPI
Nehemiah 5 in the KBT1ETNIK
Nehemiah 5 in the KBV
Nehemiah 5 in the KJV
Nehemiah 5 in the KNFD
Nehemiah 5 in the LBA
Nehemiah 5 in the LBLA
Nehemiah 5 in the LNT
Nehemiah 5 in the LSV
Nehemiah 5 in the MAAL
Nehemiah 5 in the MBV
Nehemiah 5 in the MBV2
Nehemiah 5 in the MHNT
Nehemiah 5 in the MKNFD
Nehemiah 5 in the MNG
Nehemiah 5 in the MNT
Nehemiah 5 in the MNT2
Nehemiah 5 in the MRS1T
Nehemiah 5 in the NAA
Nehemiah 5 in the NASB
Nehemiah 5 in the NBLA
Nehemiah 5 in the NBS
Nehemiah 5 in the NBVTP
Nehemiah 5 in the NET2
Nehemiah 5 in the NIV11
Nehemiah 5 in the NNT
Nehemiah 5 in the NNT2
Nehemiah 5 in the NNT3
Nehemiah 5 in the PDDPT
Nehemiah 5 in the PFNT
Nehemiah 5 in the RMNT
Nehemiah 5 in the SBIAS
Nehemiah 5 in the SBIBS
Nehemiah 5 in the SBIBS2
Nehemiah 5 in the SBICS
Nehemiah 5 in the SBIDS
Nehemiah 5 in the SBIGS
Nehemiah 5 in the SBIHS
Nehemiah 5 in the SBIIS
Nehemiah 5 in the SBIIS2
Nehemiah 5 in the SBIIS3
Nehemiah 5 in the SBIKS
Nehemiah 5 in the SBIKS2
Nehemiah 5 in the SBIMS
Nehemiah 5 in the SBIOS
Nehemiah 5 in the SBIPS
Nehemiah 5 in the SBISS
Nehemiah 5 in the SBITS
Nehemiah 5 in the SBITS2
Nehemiah 5 in the SBITS3
Nehemiah 5 in the SBITS4
Nehemiah 5 in the SBIUS
Nehemiah 5 in the SBIVS
Nehemiah 5 in the SBT
Nehemiah 5 in the SBT1E
Nehemiah 5 in the SCHL
Nehemiah 5 in the SNT
Nehemiah 5 in the SUSU
Nehemiah 5 in the SUSU2
Nehemiah 5 in the SYNO
Nehemiah 5 in the TBIAOTANT
Nehemiah 5 in the TBT1E
Nehemiah 5 in the TBT1E2
Nehemiah 5 in the TFTIP
Nehemiah 5 in the TFTU
Nehemiah 5 in the TGNTATF3T
Nehemiah 5 in the THAI
Nehemiah 5 in the TNFD
Nehemiah 5 in the TNT
Nehemiah 5 in the TNTIK
Nehemiah 5 in the TNTIL
Nehemiah 5 in the TNTIN
Nehemiah 5 in the TNTIP
Nehemiah 5 in the TNTIZ
Nehemiah 5 in the TOMA
Nehemiah 5 in the TTENT
Nehemiah 5 in the UBG
Nehemiah 5 in the UGV
Nehemiah 5 in the UGV2
Nehemiah 5 in the UGV3
Nehemiah 5 in the VBL
Nehemiah 5 in the VDCC
Nehemiah 5 in the YALU
Nehemiah 5 in the YAPE
Nehemiah 5 in the YBVTP
Nehemiah 5 in the ZBP