Numbers 13 (BOKCV)
1 BWANA akamwambia Mose, 2 “Watume baadhi ya watu wakaipeleleze nchi ya Kanaani, ambayo ninawapa Waisraeli. Kutoka kwa kila kabila la baba zao, tuma mmoja wa viongozi wao.” 3 Hivyo kwa agizo la BWANA Mose akawatuma kutoka Jangwa la Parani. Wote walikuwa viongozi wa Waisraeli. 4 Haya ndiyo majina yao: kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri; 5 kutoka kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori; 6 kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune; 7 kutoka kabila la Isakari, Igali mwana wa Yosefu; 8 kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni; 9 kutoka kabila la Benyamini, Palti mwana wa Rafu; 10 kutoka kabila la Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi, 11 kutoka kabila la Manase (kabila la Yosefu), Gadi mwana wa Susi; 12 kutoka kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemali; 13 kutoka kabila la Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli; 14 kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Wofsi; 15 kutoka kabila la Gadi, Geueli mwana wa Maki. 16 Haya ndiyo majina ya watu ambao Mose aliwatuma kuipeleleza nchi. (Mose akampa Hoshea mwana wa Nuni jina Yoshua.) 17 Mose alipowatuma wakaipeleleze Kanaani, alisema, “Pandeni kupitia Negebu, mwende mpaka nchi ya vilima. 18 Mwone nchi ni ya namna gani, na kama watu waishio humo wana nguvu au ni wadhaifu, iwapo ni wachache au wengi. 19 Wanaishi katika nchi ya namna gani? Je, ni nzuri au mbaya? Wanaishi katika miji ya namna gani? Je, haina kuta au ngome? 20 Ardhi iko aje? Ina rutuba au la? Je, kuna miti ndani yake au la? Jitahidini kadiri mwezavyo kuleta baadhi ya matunda ya nchi.” (Ulikuwa msimu wa kuiva zabibu za kwanza.) 21 Hivyo wakapanda na kuipeleleza nchi kutoka Jangwa la Sini hadi Rehobu, kuelekea Lebo-Hamathi. 22 Wakapanda kupitia Negebu hadi wakafika Hebroni, mahali ambapo Ahimani, Sheshai na Talmai, wazao wa Anaki, waliishi. (Hebroni ulikuwa umejengwa miaka saba kabla ya mji wa Soani ulioko Misri.) 23 Walipofika katika Bonde la Eshkoli, walivunja tawi lililokuwa na kishada kimoja cha zabibu. Wawili wao wakalichukua lile tawi kwenye mti, pamoja na komamanga na tini. 24 Eneo lile likaitwa Bonde la Eshkoli kwa sababu ya kile kishada cha zabibu ambacho Waisraeli walikikata huko. 25 Mwishoni mwa siku arobaini wakarudi kutoka kuipeleleza nchi. 26 Wakarudi kwa Mose, Aroni na jumuiya yote ya Waisraeli huko Kadeshi kwenye Jangwa la Parani. Hapo ndipo walipotoa habari kwao na kwa kusanyiko lote na kuwaonyesha matunda ya hiyo nchi. 27 Wakampa Mose taarifa hii: “Tuliingia katika nchi uliyotutuma, nayo inatiririka maziwa na asali! Hili hapa tunda lake. 28 Lakini watu wanaoishi huko ni wenye nguvu, na miji yao ina ngome na ni mikubwa sana. Huko tuliona hata wazao wa Anaki. 29 Waamaleki wanaishi Negebu; Wahiti, Wayebusi na Waamori wanaishi katika nchi ya vilima; nao Wakanaani wanaishi karibu na bahari na kando ya Yordani.” 30 Kisha Kalebu akawanyamazisha watu mbele ya Mose na kusema, “Imetupasa kupanda na kuimiliki nchi, kwa maana hakika tunaweza kufanya hivyo.” 31 Lakini watu waliokuwa wamepanda pamoja naye wakasema, “Hatuwezi kuwashambulia wale watu; wana nguvu kutuliko sisi.” 32 Wakaeneza taarifa mbaya miongoni mwa Waisraeli kuhusu nchi waliyoipeleleza. Wakasema, “Nchi tuliyoipeleleza hula watu waishio ndani yake. Watu wote tuliowaona huko ni majitu. 33 Tuliwaona Wanefili huko (wazao wa Anaki wanatokana na Wanefili.) Tulijiona kama panzi machoni petu wenyewe, nao ndivyo walivyotuona.”
In Other Versions
Numbers 13 in the ANGEFD
Numbers 13 in the ANTPNG2D
Numbers 13 in the AS21
Numbers 13 in the BAGH
Numbers 13 in the BBPNG
Numbers 13 in the BBT1E
Numbers 13 in the BDS
Numbers 13 in the BEV
Numbers 13 in the BHAD
Numbers 13 in the BIB
Numbers 13 in the BLPT
Numbers 13 in the BNT
Numbers 13 in the BNTABOOT
Numbers 13 in the BNTLV
Numbers 13 in the BOATCB
Numbers 13 in the BOATCB2
Numbers 13 in the BOBCV
Numbers 13 in the BOCNT
Numbers 13 in the BOECS
Numbers 13 in the BOGWICC
Numbers 13 in the BOHCB
Numbers 13 in the BOHCV
Numbers 13 in the BOHLNT
Numbers 13 in the BOHNTLTAL
Numbers 13 in the BOICB
Numbers 13 in the BOILNTAP
Numbers 13 in the BOITCV
Numbers 13 in the BOKCV2
Numbers 13 in the BOKHWOG
Numbers 13 in the BOKSSV
Numbers 13 in the BOLCB
Numbers 13 in the BOLCB2
Numbers 13 in the BOMCV
Numbers 13 in the BONAV
Numbers 13 in the BONCB
Numbers 13 in the BONLT
Numbers 13 in the BONUT2
Numbers 13 in the BOPLNT
Numbers 13 in the BOSCB
Numbers 13 in the BOSNC
Numbers 13 in the BOTLNT
Numbers 13 in the BOVCB
Numbers 13 in the BOYCB
Numbers 13 in the BPBB
Numbers 13 in the BPH
Numbers 13 in the BSB
Numbers 13 in the CCB
Numbers 13 in the CUV
Numbers 13 in the CUVS
Numbers 13 in the DBT
Numbers 13 in the DGDNT
Numbers 13 in the DHNT
Numbers 13 in the DNT
Numbers 13 in the ELBE
Numbers 13 in the EMTV
Numbers 13 in the ESV
Numbers 13 in the FBV
Numbers 13 in the FEB
Numbers 13 in the GGMNT
Numbers 13 in the GNT
Numbers 13 in the HARY
Numbers 13 in the HNT
Numbers 13 in the IRVA
Numbers 13 in the IRVB
Numbers 13 in the IRVG
Numbers 13 in the IRVH
Numbers 13 in the IRVK
Numbers 13 in the IRVM
Numbers 13 in the IRVM2
Numbers 13 in the IRVO
Numbers 13 in the IRVP
Numbers 13 in the IRVT
Numbers 13 in the IRVT2
Numbers 13 in the IRVU
Numbers 13 in the ISVN
Numbers 13 in the JSNT
Numbers 13 in the KAPI
Numbers 13 in the KBT1ETNIK
Numbers 13 in the KBV
Numbers 13 in the KJV
Numbers 13 in the KNFD
Numbers 13 in the LBA
Numbers 13 in the LBLA
Numbers 13 in the LNT
Numbers 13 in the LSV
Numbers 13 in the MAAL
Numbers 13 in the MBV
Numbers 13 in the MBV2
Numbers 13 in the MHNT
Numbers 13 in the MKNFD
Numbers 13 in the MNG
Numbers 13 in the MNT
Numbers 13 in the MNT2
Numbers 13 in the MRS1T
Numbers 13 in the NAA
Numbers 13 in the NASB
Numbers 13 in the NBLA
Numbers 13 in the NBS
Numbers 13 in the NBVTP
Numbers 13 in the NET2
Numbers 13 in the NIV11
Numbers 13 in the NNT
Numbers 13 in the NNT2
Numbers 13 in the NNT3
Numbers 13 in the PDDPT
Numbers 13 in the PFNT
Numbers 13 in the RMNT
Numbers 13 in the SBIAS
Numbers 13 in the SBIBS
Numbers 13 in the SBIBS2
Numbers 13 in the SBICS
Numbers 13 in the SBIDS
Numbers 13 in the SBIGS
Numbers 13 in the SBIHS
Numbers 13 in the SBIIS
Numbers 13 in the SBIIS2
Numbers 13 in the SBIIS3
Numbers 13 in the SBIKS
Numbers 13 in the SBIKS2
Numbers 13 in the SBIMS
Numbers 13 in the SBIOS
Numbers 13 in the SBIPS
Numbers 13 in the SBISS
Numbers 13 in the SBITS
Numbers 13 in the SBITS2
Numbers 13 in the SBITS3
Numbers 13 in the SBITS4
Numbers 13 in the SBIUS
Numbers 13 in the SBIVS
Numbers 13 in the SBT
Numbers 13 in the SBT1E
Numbers 13 in the SCHL
Numbers 13 in the SNT
Numbers 13 in the SUSU
Numbers 13 in the SUSU2
Numbers 13 in the SYNO
Numbers 13 in the TBIAOTANT
Numbers 13 in the TBT1E
Numbers 13 in the TBT1E2
Numbers 13 in the TFTIP
Numbers 13 in the TFTU
Numbers 13 in the TGNTATF3T
Numbers 13 in the THAI
Numbers 13 in the TNFD
Numbers 13 in the TNT
Numbers 13 in the TNTIK
Numbers 13 in the TNTIL
Numbers 13 in the TNTIN
Numbers 13 in the TNTIP
Numbers 13 in the TNTIZ
Numbers 13 in the TOMA
Numbers 13 in the TTENT
Numbers 13 in the UBG
Numbers 13 in the UGV
Numbers 13 in the UGV2
Numbers 13 in the UGV3
Numbers 13 in the VBL
Numbers 13 in the VDCC
Numbers 13 in the YALU
Numbers 13 in the YAPE
Numbers 13 in the YBVTP
Numbers 13 in the ZBP