Numbers 33 (BOKCV)

1 Hivi ndivyo vituo katika safari ya Waisraeli walipotoka Misri kwa vikosi chini ya uongozi wa Mose na Aroni. 2 Kwa agizo la BWANA, Mose aliweka kumbukumbu ya vituo katika safari yao. Hivi ndivyo vituo katika safari yao: 3 Waisraeli walisafiri kutoka Ramesesi katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, siku iliyofuata Pasaka. Walitembea kwa ujasiri wazi mbele ya Wamisri wote, 4 waliokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza wote, ambao BWANA alikuwa amewaua katikati yao, kwa kuwa BWANA alikuwa ameleta hukumu juu ya miungu yao. 5 Waisraeli waliondoka Ramesesi na kupiga kambi huko Sukothi. 6 Wakaondoka Sukothi na kupiga kambi huko Ethamu, pembeni mwa jangwa. 7 Wakaondoka Ethamu, wakageuka wakarudi Pi-Hahirothi, hadi mashariki ya Baal-Sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli. 8 Wakaondoka Pi-Hahirothi wakapita katikati ya bahari mpaka jangwani, na baada ya kusafiri kwa siku tatu katika Jangwa la Ethamu, walipiga kambi huko Mara. 9 Wakaondoka Mara wakaenda Elimu, mahali ambapo palikuwa na chemchemi kumi na mbili na mitende sabini, huko wakapiga kambi. 10 Wakaondoka Elimu na kupiga kambi kando ya Bahari ya Shamu. 11 Wakaondoka kando ya Bahari ya Shamu na kupiga kambi katika Jangwa la Sini. 12 Wakaondoka katika Jangwa la Sini, wakapiga kambi huko Dofka. 13 Wakaondoka Dofka, wakapiga kambi huko Alushi. 14 Wakaondoka Alushi, wakapiga kambi Refidimu, mahali ambapo hapakuwa na maji kwa ajili ya watu kunywa. 15 Wakaondoka Refidimu na kupiga kambi katika Jangwa la Sinai. 16 Wakaondoka katika Jangwa la Sinai na kupiga kambi huko Kibroth-Hataava. 17 Wakaondoka Kibroth-Hataava na kupiga kambi huko Haserothi. 18 Wakaondoka Haserothi na kupiga kambi huko Rithma. 19 Wakaondoka Rithma na kupiga kambi huko Rimon-Peresi. 20 Wakaondoka Rimon-Peresi na kupiga kambi huko Libna. 21 Wakaondoka Libna na kupiga kambi huko Risa. 22 Wakaondoka Risa na kupiga kambi huko Kehelatha. 23 Wakaondoka Kehelatha na kupiga kambi kwenye mlima Sheferi. 24 Wakaondoka kwenye mlima Sheferi na kupiga kambi huko Harada. 25 Wakaondoka Harada na kupiga kambi huko Makelothi. 26 Wakaondoka Makelothi na kupiga kambi huko Tahathi. 27 Wakaondoka Tahathi na kupiga kambi huko Tera. 28 Wakaondoka Tera na kupiga kambi huko Mithka. 29 Wakaondoka Mithka na kupiga kambi huko Hashmona. 30 Wakaondoka Hashmona na kupiga kambi Moserothi. 31 Wakaondoka Moserothi na kupiga kambi huko Bene-Yakani. 32 Wakaondoka Bene-Yakani na kupiga kambi huko Hor-Hagidgadi. 33 Wakaondoka Hor-Hagidgadi na kupiga kambi huko Yotbatha. 34 Wakaondoka Yotbatha na kupiga kambi huko Abrona. 35 Wakaondoka Abrona na kupiga kambi huko Esion-Geberi. 36 Wakaondoka Esion-Geberi na kupiga kambi huko Kadeshi katika Jangwa la Sini. 37 Wakaondoka Kadeshi na kupiga kambi kwenye Mlima Hori, mpakani mwa Edomu. 38 Kwa amri ya BWANA, kuhani Aroni alipanda Mlima Hori, mahali alipofia katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano, mwaka wa arobaini baada ya Waisraeli kutoka Misri. 39 Aroni alikufa juu ya Mlima Hori akiwa na umri wa miaka 123. 40 Mfalme Mkanaani wa Aradi, ambaye aliishi huko Negebu ya Kanaani, akasikia kwamba Waisraeli wanakuja. 41 Wakaondoka kwenye mlima Hori na kupiga kambi huko Salmona. 42 Wakaondoka Salmona, wakapiga kambi huko Punoni. 43 Wakaondoka Punoni, wakapiga kambi huko Obothi. 44 Wakaondoka Obothi, wakapiga kambi huko Iye-Abarimu, mipakani mwa Moabu. 45 Wakaondoka Iye-Abarimu, wakapiga kambi huko Dibon-Gadi. 46 Wakaondoka Dibon-Gadi na kupiga kambi huko Almon-Diblathaimu. 47 Wakaondoka Almon-Diblathaimu na kupiga kambi katika milima ya Abarimu, karibu na Nebo. 48 Wakaondoka kwenye milima ya Abarimu na kupiga kambi kwenye tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko. 49 Huko kwenye tambarare za Moabu walipiga kambi kandokando ya Mto Yordani, kuanzia Beth-Yeshimothi mpaka Abel-Shitimu. 50 Katika tambarare za Moabu kando ya Yordani kuvukia Yeriko, BWANA akamwambia Mose, 51 “Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapovuka Mto Yordani kuingia Kanaani, 52 wafukuzeni wakazi wote wa nchi iliyo mbele yenu. Haribuni sanamu zao zote za kuchongwa, na sanamu zilizotengenezwa kwa kuyeyusha chuma, na kupabomoa mahali pao pa ibada. 53 Mtaimiliki nchi hiyo na kukaa huko, kwa kuwa nimewapeni ninyi kuimiliki. 54 Mtaigawanya nchi hiyo kwa kupiga kura, kufuatana na koo zenu. Kwa kundi kubwa zaidi toa urithi mkubwa zaidi, na kwa kundi dogo zaidi urithi mdogo zaidi. Chochote kinachowaangukia kwa kura kitakuwa chao. Mtaigawanya nchi kufuatana na makabila ya babu zenu. 55 “ ‘Lakini kama hamkuwafukuza wenyeji wakaao katika nchi hiyo, wale mtakaowaruhusu wabaki watakuwa kama sindano kwenye macho yenu na miiba kwenu kila upande. Watawasumbua katika nchi mtakayoishi. 56 Kisha nitawatenda ninyi kile ambacho nimepanga kuwatenda wao.’ ”

In Other Versions

Numbers 33 in the ANGEFD

Numbers 33 in the ANTPNG2D

Numbers 33 in the AS21

Numbers 33 in the BAGH

Numbers 33 in the BBPNG

Numbers 33 in the BBT1E

Numbers 33 in the BDS

Numbers 33 in the BEV

Numbers 33 in the BHAD

Numbers 33 in the BIB

Numbers 33 in the BLPT

Numbers 33 in the BNT

Numbers 33 in the BNTABOOT

Numbers 33 in the BNTLV

Numbers 33 in the BOATCB

Numbers 33 in the BOATCB2

Numbers 33 in the BOBCV

Numbers 33 in the BOCNT

Numbers 33 in the BOECS

Numbers 33 in the BOGWICC

Numbers 33 in the BOHCB

Numbers 33 in the BOHCV

Numbers 33 in the BOHLNT

Numbers 33 in the BOHNTLTAL

Numbers 33 in the BOICB

Numbers 33 in the BOILNTAP

Numbers 33 in the BOITCV

Numbers 33 in the BOKCV2

Numbers 33 in the BOKHWOG

Numbers 33 in the BOKSSV

Numbers 33 in the BOLCB

Numbers 33 in the BOLCB2

Numbers 33 in the BOMCV

Numbers 33 in the BONAV

Numbers 33 in the BONCB

Numbers 33 in the BONLT

Numbers 33 in the BONUT2

Numbers 33 in the BOPLNT

Numbers 33 in the BOSCB

Numbers 33 in the BOSNC

Numbers 33 in the BOTLNT

Numbers 33 in the BOVCB

Numbers 33 in the BOYCB

Numbers 33 in the BPBB

Numbers 33 in the BPH

Numbers 33 in the BSB

Numbers 33 in the CCB

Numbers 33 in the CUV

Numbers 33 in the CUVS

Numbers 33 in the DBT

Numbers 33 in the DGDNT

Numbers 33 in the DHNT

Numbers 33 in the DNT

Numbers 33 in the ELBE

Numbers 33 in the EMTV

Numbers 33 in the ESV

Numbers 33 in the FBV

Numbers 33 in the FEB

Numbers 33 in the GGMNT

Numbers 33 in the GNT

Numbers 33 in the HARY

Numbers 33 in the HNT

Numbers 33 in the IRVA

Numbers 33 in the IRVB

Numbers 33 in the IRVG

Numbers 33 in the IRVH

Numbers 33 in the IRVK

Numbers 33 in the IRVM

Numbers 33 in the IRVM2

Numbers 33 in the IRVO

Numbers 33 in the IRVP

Numbers 33 in the IRVT

Numbers 33 in the IRVT2

Numbers 33 in the IRVU

Numbers 33 in the ISVN

Numbers 33 in the JSNT

Numbers 33 in the KAPI

Numbers 33 in the KBT1ETNIK

Numbers 33 in the KBV

Numbers 33 in the KJV

Numbers 33 in the KNFD

Numbers 33 in the LBA

Numbers 33 in the LBLA

Numbers 33 in the LNT

Numbers 33 in the LSV

Numbers 33 in the MAAL

Numbers 33 in the MBV

Numbers 33 in the MBV2

Numbers 33 in the MHNT

Numbers 33 in the MKNFD

Numbers 33 in the MNG

Numbers 33 in the MNT

Numbers 33 in the MNT2

Numbers 33 in the MRS1T

Numbers 33 in the NAA

Numbers 33 in the NASB

Numbers 33 in the NBLA

Numbers 33 in the NBS

Numbers 33 in the NBVTP

Numbers 33 in the NET2

Numbers 33 in the NIV11

Numbers 33 in the NNT

Numbers 33 in the NNT2

Numbers 33 in the NNT3

Numbers 33 in the PDDPT

Numbers 33 in the PFNT

Numbers 33 in the RMNT

Numbers 33 in the SBIAS

Numbers 33 in the SBIBS

Numbers 33 in the SBIBS2

Numbers 33 in the SBICS

Numbers 33 in the SBIDS

Numbers 33 in the SBIGS

Numbers 33 in the SBIHS

Numbers 33 in the SBIIS

Numbers 33 in the SBIIS2

Numbers 33 in the SBIIS3

Numbers 33 in the SBIKS

Numbers 33 in the SBIKS2

Numbers 33 in the SBIMS

Numbers 33 in the SBIOS

Numbers 33 in the SBIPS

Numbers 33 in the SBISS

Numbers 33 in the SBITS

Numbers 33 in the SBITS2

Numbers 33 in the SBITS3

Numbers 33 in the SBITS4

Numbers 33 in the SBIUS

Numbers 33 in the SBIVS

Numbers 33 in the SBT

Numbers 33 in the SBT1E

Numbers 33 in the SCHL

Numbers 33 in the SNT

Numbers 33 in the SUSU

Numbers 33 in the SUSU2

Numbers 33 in the SYNO

Numbers 33 in the TBIAOTANT

Numbers 33 in the TBT1E

Numbers 33 in the TBT1E2

Numbers 33 in the TFTIP

Numbers 33 in the TFTU

Numbers 33 in the TGNTATF3T

Numbers 33 in the THAI

Numbers 33 in the TNFD

Numbers 33 in the TNT

Numbers 33 in the TNTIK

Numbers 33 in the TNTIL

Numbers 33 in the TNTIN

Numbers 33 in the TNTIP

Numbers 33 in the TNTIZ

Numbers 33 in the TOMA

Numbers 33 in the TTENT

Numbers 33 in the UBG

Numbers 33 in the UGV

Numbers 33 in the UGV2

Numbers 33 in the UGV3

Numbers 33 in the VBL

Numbers 33 in the VDCC

Numbers 33 in the YALU

Numbers 33 in the YAPE

Numbers 33 in the YBVTP

Numbers 33 in the ZBP