Psalms 1 (BOKCV)
1 Heri mtu yule ambayehaendi katika shauri la watu waovu,wala hasimami katika njia ya wenye dhambi,au kuketi katika baraza la wenye mizaha. 2 Bali huifurahia sheria ya BWANA,naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana. 3 Mtu huyo ni kama mti uliopandwakando ya vijito vya maji,ambao huzaa matunda kwa majira yakena majani yake hayanyauki.Lolote afanyalo hufanikiwa. 4 Sivyo walivyo waovu!Wao ni kama makapiyapeperushwayo na upepo. 5 Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu,wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki. 6 Kwa maana BWANA huziangalia njia za mwenye haki,bali njia ya waovu itaangamia.