Psalms 110 (BOKCV)
undefined Zaburi ya Daudi. 1 BWANA amwambia Bwana wangu:“Keti mkono wangu wa kuume,mpaka nitakapowafanya adui zakokuwa mahali pa kuweka miguu yako.” 2 BWANA ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni;utatawala katikati ya adui zako. 3 Askari wako watajitolea kwa hiarikatika siku yako ya vita.Ukiwa umevikwa fahari takatifu,kutoka tumbo la mapambazukoutapokea umande wa ujana wako. 4 BWANA ameapa,naye hatabadilisha mawazo yake:“Wewe ni kuhani milele,kwa mfano wa Melkizedeki.” 5 Bwana yuko mkono wako wa kuume,atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake. 6 Atawahukumu mataifa, akilundika mizogana kuwaponda watawala wa dunia nzima. 7 Atakunywa maji katika kijito kando ya njia,kwa hiyo atainua kichwa chake juu.